
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), leo Juni 17, 2022 amekutana Ofisini kwake na Angel Bukuku mwenye umri wa miaka (11), Mwanafunzi wa darasa la sita, Shule ya msingi Capital iliyopo Jijini Dodoma. Angel ni mtoto mwenye kipaji cha ubunifu wa mavazi na ushonaji nguo ambapo pia amepata fursa ya kumfanyia vipimo vya nguo Mhe. Spika.

Angel mwenye ndoto ya kufika mbali kwenye Sanaa ya ubunifu wa mavazi aliambatana na Mama yake mzazi Joyce Bukuku

