MNDOLWA AONGOZA MAPITIO YA MPANGO MKAKATI WA MIAKA MITANO WA TUME YA TAIFA YA UMWAGILIAJI

Na; Mwandishi Wetu – Dodoma

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Bw. Raymond Mndolwa, ameongoza kikaokazi  cha mapitio ya mpango mkakati wa miaka mitano wa Tume ya Taifa ya umwagiliaji, uliohusisha wataalam na wahandisi wa Umwagiliaji nchini, mapema leo Jijini Dodoma.

 Bw. Mndolwa alisema kuwa, kuna umuhimu wa kufanya mapitio ya mpango mkakati huo kwa pamoja  tofauti kwakuwa Mpango mkakati huo ni Dira ya Taasisi, hivyo ni muhimu kila mtumishi katika taasisi anatakiwa kuifahamu kwani ndiyo zana inayotumika katika utekelezaji  wa kazi za kila siku.

“Nimeona kuna Umuhimu wa kupitia kwa pamoja ili pale ambapo patakuwa na marekebisho turekebishe kwa pamoja, na kuwe na ushiriki kwa hoja katika kazi hii.” Alifafanua Mndolwa.

Kwa upande wake Mhandisi wa Umwagiliaji wa MKoa wa Singida William Kadinda amesema, kikao kazi hiki kinatoa fursa ya mpango wa miaka mitano ambao unajumuisha shughuli zinazofanyika, pia kinaangalia maslahi ya watumishi katika upande wa mafunzo na kuona mahitaji yao, na kuweza kuwaongezea uwezo kiutendaji.

Kukamilika kwa mpango mkakati huo ni hatua muhimu kwa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji wakati huu, ikiwa na jukumu kubwa la ukarabati na ujenzi wa Skimu za umwagiliaji pamoja na Mabwawa kwaajili ya umwagiliaji. Lengo la serikali ni kufikia Hekta 1,200,000 za umwagiliaji mwaka 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *