TANZANIA YAOMBA KUCHAGULIWA UJUMBE WA BARAZA

Katibu Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Duniani Bw. Houlin Zhao akiwahutubia washiriki wa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022) katika dhifa fupi ya chakula cha mchana, iliyolenga kuendeleza ushirikiano na wadau wa mawasiliano, pembezoni mwa Mkutano Mkuu wa Maendeleo ya Mawasiliano Duniani wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU-WTDC-2022), tarehe 14 Juni, 2022, jijini Kigali- Rwanda.

Tanzania imetumia fursa hiyo kuomba uungwaji mkono ili kuchaguliwa kuwa mjumbe wa Baraza-Tendaji la ITU kwenye Mkutano Mkuu wa Shirika hilo unaotarajiwa kufanyika Septemba 2022 jijini Bucharest, Romania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *