
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Wawakilishi wa Kampuni ya Silent Ocean waliofika Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 16, 2022 kwa lengo la kujitambulisha na kuelezea shughuli wanazozifanya ikiwemo usafirishaji wa mizigo kutoka nje ya nchi ikiwemo China, Dubai, Uturuki na Marekani Kuja Tanzania.
