WAZIRI DKT. ASHATU KIJAJI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA RAIS WA IFC BW. SERGIO PIMENTA

Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa katika picha na Makamu wa Rais wa Taasisi ya International Finance Corporation (IFC) mara baada ya kumaliza kikao chao walipokutana kwa ajili ya kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya IFC na Tanzania katika kusaidia kwenye Uwekezaji kwa kutoa Mikopo yenye masharti nafuua kwenye Miradi mbalimbali ya kimkakati.

IFC ni Taasisi ya Benki ya Dunia ambayo hutoa Mikopo nafuu kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya Miundombinu, Kilimo, Huduma Jumuishi za Kifedha, Utalii, Afya, Elimu, n.k.

Mkutano huo kati ya Mheshimiwa Waziri Dkt. Kijaji na Makamu wa Rais, Bw. Pimenta ulifanyika Jijini, Abidjan nchini Ivory Coast jana tarehe 14 Juni, 2022 mara baada ya kumalizika Kongamano la Wakuu wa Taasisi na Mashirika Barani Afrika (Africa CEO Forum) uliofanyika kwa siku mbili kuanzia tarehe 13-14, Juni, 2022 katika Hotel ya Sofitel, Abidjan.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *