TAASISI YA ELIMU (TASESO) YAMPONGEZA RAIS SAMIA MAGEUZI MAKUBWA SEKTA YA ELIMU

HOTUBA YA TASESO KWA WANAHABARI

Ndg Wanahabari,

Awali ya yote napenda nimshukuru mwenyezi Mungu mwingi wa rehema kwa kutukutanisha leo hapa sote tukiwa wazima wa afya njema.

Nitumie pia fursa hii kuwashukuru sana nyie kama wanahabari kwa kukubali na kuitikia mwaliko huu kuja kusikiliza ili mkaujuze umma wa watanzani kuhusu mafanikio ya serikali ya awamu ya sita sekta ya elimu AMBAYO SISI KAMA Taseso imetulazimu tuyaseme na kuipongeza serikali kwa hatua hiyo.

Niwashukuru pia wadau wetu wa kielimu wote wanaojishughulisha na masuala yote ya kielimu nchini.

Kwa mkatadha huo, niwakaribishe wote ndani ya ukumbi huu ambapo Taasisi yakielimu Taseso, tukiwa hapa kuipongeza serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Sahani kwa maendeleo yaliyofanyika kupitia sekta Elimu katika kipindi cha muda mfupi toka Rais Samia Suluhu Hasani aingie madarakani.

Ndg Wanahabri ,

Kwanza ningependa mjue kuwa TASESO nikifupi cha maneno ya TANZANIA SCHOOLS EMPOWERMENT AND SERVICE ORGANIZATIO, yaani nitaasisi inayohusika na masuala ya kuimpower elimu ambapo makao makuu ya Taasisi hii yapo hapa Dodoma.

Ndg Wanahabari

Baada ya utangulizi huo sasa, Tungependa sana muufikishie umma juu ya mafanikio ya serikali ya awamu ya sita ambayo leo hii Taseso inayachambua kwenu, na kuipongeza serikali katika sekta hiyo kwa kupiga hatua kubwa sana katika kipindi kifupi toka serikali ya awamu ya sita iingie madarakani

 Ndg wanahabari.

Taseso imefanikiwa kufanya ziara Zaidi ya mikoa 23 nchi nzima na kuyaona haya ambayo leo hii serikali yapaswa kupongezwa kwa dhati kwani ndani ya uongozi wa serikali ya awmu ya sita kwa kipindi kifupi mpaka sasa ,Serika  imeweza kuongeza idadi ya walimu watakaofundisha shule za sekondari hususani wamosomo ya hisabati na sayansi kwenda kufundisha mshuleni.

Aidha utoaji wa elimu bila malipo na michango umepelekea kuongezeka kwa wanafnzi mashuleni

Ndg wanahabri

Tunaipongeza serikali kwa kukarabati takribani shule 17 kongwe ili kuboresha mazingira ya kufundishia.miongoni mwa shule zilizokarabatiwa ni pamoja na KILAKALA SEC,SHULE YA WASICHANA TABORA,PUGU,KOROGWE,SENGEREMA NA NYINGINEZO,hayo yote yamefanyikia kipindi kifupi cha Rais samia madarakani

Ndg wanahabri

Rais Samia amewezesha ujenzi wa ukarabati wa miundombinu mbalimbali katika shule hizo ikiwemo kuboresha mifumo ya maji taka,madarasa,vyoo,mambweni,nyumba za walimu pamoja na ofisi za walimu.

Ndani ya kipindi kifupi cha Mh Rais,Serikali imeweza kulipa madeni ya walimu na kupandisha madaraja na kulipa malimbikizo ya mishahara yenye thamni ya sh takribani bilioni 74.12 kwa watumishi  takribani 36126 ambapo kati ya fedha hizo Tsh takribani 32.669 bilioni zimelipwa kwa walimu takribani 11272,hii sisi Taseso kama wadau wa Elimu tunasema kwa dhati kuwa Rais Samia Suluhu Hasan anastahili pongezi na tunampongeza kwani hiyo nihatua kubwa sana katika ujenzi wa sekta ya elimu nchini.

Aidha mpaka sasa,Rais Samia akiwa madarakani amepunguza kodi (PAYE) katika mishahara kutoka asilimia 9 hadi asilimia 8,hii nihatua kubwa sana katika sekita ya elimu.

Ndg Waandishi Wa Habari

Mpaka sasa rais samia ameweza kujenga takribani madarasa 15000,na kutoa ajira za mbalimbali za walimu aidha ikumbukwe kuwa katika mafanikio ya Mh Rais samia katika awamu ya sita ongezeko la idadi ya shule za msingi zilizosajiliwa kutoka takribani shule 3,270 mwaka 1961 hadi shule takribani 18,546 mwaka 2021,kati ya  shule takribani 18,546,shule takribani 16656 niza serikali na takribani 1,890 za binafsi, aidha shule za sekondari zimeongezeka kutoka takribani shule 41 mwaka 1961 ambapo shule takribvani 2 zilikuwa za binafsi hadi kufikia takribani shule  5,460 mwaka 2021 ambapo kati ya hizo,shule takribani 3,983 nizaserikali na shule 1287 nizabinafsi,hii nikazi ya kupongezwa sana kwa jitahada inazozifanya serikali katika kuwekeza kwenye elimu

Ndg Waandishi Wa Habari

Tunaishukuru na kuipongeza serikali katika kuwapa kipaumbele wawekezaji binafsi katika sekta ya elimu,hii inasaidia kwa kiwango kikubwa kuinua kiwango cha elimu nchini na kuifanya elimu ya Tanzania iwe bora Zaidi

Ndg Waandishi Wa Habari

Kwamjibu wa takwimu za serikali,uwepo wa uwekezaji kwenye elimu katika sekta binafsi imewezesha uandikishaji wa wanafunzi wa elimu ya sekondari kuongezeka kutoka wanafunzi  wa kidato cha kwanza takribani  4,432 mwaka 1961 hadi wanafunzi takribani 803085 mwaka 2021. Ongezeko hilo limechangiwa na  mikakati mbalimbali ya serikali ikiwemo utekelezaji wa sera ya Elimu Bila Malipo ulioanza kutekelezwa mwaka 2016 chini ya serikali ya awamu ya tano na unaendelea kutekelezwa hadi sasa.

Ndg Waandishi Wa Habari.

Serikali yetu chini ya mama Samia Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imehakikisha kila mtoto anaenda shule,aidha uwekezaji uliofanyika katika elimu imeiwezesha serikali kuchukua wanafunzi zaidi ya laki tisa kwa mkupuo kuingia kidato cha kwanza.aidha serikali ya awamu ya sita imehakikisha watoto wote hata wale walioacha shule kwa sababu mbalimbali ikiwepo kupata mimba watafutiwe mkakati wa namna ya kurudi shule.

Ndg Waandishi Wa Habari

Aidha tunaishukuru na kuipongeza kwa dhati serikali ya awamu ya sita kwani kwa mwaka mmoja imeweza kuongeza fedha za mikopo kutoka Bilion takribani 464 hadi  takribani 570 na kuagiza asilimia sita iliyokuwa inatozwa  kwa ajili ya kulinda thamani ya hela iondolewe na asilimia kumi kama adhabu ya kuchelewa kulipa ifutwe,hii imepelekea wanafunzi wengi kusoma bila kikwazo hivyo kwa hatua hii yapaswa serikali ipongezwe kwa hatua inzozichukua katika elimu

ELIMU MAALUM

Ndg wanahabri.

Tunaipongeza kwa dhati serikali kwa kuona umuhimu wa engo hii katika suala la elimu,kama ambavyo sera za elimu zimekuwa zikisisitiza juu ya umuhimu wa elimu jumuishi kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu ambapo baadhi ya mafanikio yaliyopatikana ni pamoja kuongezeka kwa idadi ya shule za msingi zinazochuklua wanafunzi wenye mahitaji maalumu kutoka shule takribani nne za wamisionari  kama vile (tabora,Buigiri,Irente na Uhuru Mchanganyiko) mwaka 1961 hadi kufikia shule takribani 776 mwaka 2021.

Aidha pongezi kubwa kwani shule za serikali zimeongezeka kutoka shule moja (mpwapwa sekondari) mwaka 1960 hadi kufikia shule takribani 74 mwaka2021,kuongezeka kwa vyuo vikuu vinavyopokea wanafunzi wenye mahitaji maalum kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam mwaka 1961 hadi vyuo vikuu takriobani 11 mwaka 2021.

Ndg wanahabari.

Ongezeko hilo la vyuo kwa watu wenye mahitaji maalum tumeona likitoa fursa kwa wanafunzi kuchagua vyuo na fani wanazozitaka kusomea,kuanzishwa ya elimu maalumu mwaka 1976 ambapo wizara ya Elimu ilianza kuandaa walimu kwa wanafunzi wasioona na viziwi katika chuo cha Ualimu Tabora

Ndg wanahabari.

Kuna msemo unasema mnyonge mnyongen haki yake mpeni,nini namaanisha?

Kwa kipindi kifupi toka aingie madarakani,Mh Rais samia amefanya kazi kubwa sana katika sekta mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu,sisi Taseso tumekuwa shahidi kwa hayo kwani tumezunguka mikoa Zaidi ya 23 Tanzania bara na kuyashuhudia kwa macho haya,hivyo tunaamini kufikia 2025 tutakuwa mbali.

Nachelea kusema “mama anaupiga mwingi tumuungeni mkono” mama kaongeza 23%  mshahara kwa watumishi wa umma, hii nihatua na mafanikio sanjari na uthubutu mkubwa sana kwa Mh Rais wetu katika kuwajali watu wake

MWISHO

Tunaiomba serikali sasa kuzipa kipaumbele asasi za kiraia zinazojihusisha na masuala ya elimu kuzipatia vibali maalumu katika kuweza kutekeleza majuku mbalimbali ya kielimu sanjari na kuzishika mkono pale inapobidi ili kuendelea kuboresha elimu yetu na kuunga mkono jitihada za serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu,Vibali vya utendaji kazi katika sekta ya elimu kutoka kwa mamlaka husika vimekuwa vikicheleweshwa bila sababu.

Tunatoa rai kwa mamlaka husika kuliweka hili suala la vibali vya kitaasisi zinzojishughulisha na masuala ya elimu kupewa kipaumbele ili tuungane pamoja katika kuiinua elimu yetu ,kama ambavyo Mh Rais amekuwa akijitahidi kuboresha sekta hiyo kubwa nchini

PICHA: MKURUGENZI WA TASESO NDG; DEUS LUGAILA AKIZUNGUMZA MBELE YA WANAHABARI DODOMA LEO

MENEJA WA TASESO NDG; JULIUS SANGA AKIZUNGUMZA MBELE YA WANAHABARI DODOMA LEO JUNI 15, 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *