YANGA YANG’ARA BUNGENI, WAZIRI MWIGULU AMUOMBA MSAMAHA WAZIRI MKUU KWA WALICHOFANYIWA SIMBA NA FEI TOTO

Waziri wa Fedha na Mipango nchini Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba Akiwasilisha Bungeni Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 ameipongeza Timu ya Yanga kwa kufanya vizuri kwenye Mashindano mbalimbali msimu huu

“nitumie fursa hii kuipongeza sana
timu ya Yanga kwa mwenendo wao mzuri sana mwaka huu na nitumie fursa hii kumwomba radhi Bosi wangu Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kitendo alichowafanyia mwanangu FEI TOTO kule
Mwanza. Mniwie radhi, nilipompeleka FEI TOTO Yanga sikujua atakuja kuwafanyia kitumbaya hivi, mpaka nasikia anatafutwa maliasili eti kaua mnyama bila kibali. Nakupongeza Mheshimiwa Anthony Mavunde wewe ndio ulikuwa Mwenyekiti wa kuisaidia Yanga ikiwa na mapito. Nampongeza
GSM kwa kurejesha furaha ya wananchi hasahasa kwa usajili wa Fiston Mayele. Mayele amekuwa maarufu kuliko Makatibu wenezi wa baadhi ya vyama vya Siasa. Nawapongeza sana na marafiki zangu klabu ya Simba kwa kuwakilisha vyema kwenye mashindano ya Kimataifa, wananijua mara zote kimataifa tuko pamoja,
siwezi kukana Bendera ya Taifa langu kwa ajili ya
utani wa jadi.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *