USHURU WA FORODHA WAONGEZWA KWENYE MAWIGI

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba amesema Nchi Wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki zimekubaliana kuongeza Ushuru wa Forodha kutoka
asilimia 25 hadi asilimia 35 kwenye nywele bandia zinazotambulika kwa
Heading 6704.

Ameyasema hayo leo Juni 14, Jijini Dodoma wakati akisoma Hotuba ya Mapendekezo ya Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 ambapo amesema Hatua hii inalenga kulinda wazalishaji wa ndani wa bidhaa hizo, kuongeza ajira pamoja na
kuongeza mapato ya Serikali;

Aidha, Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zimekubaliana
kupunguza Ushuru wa Forodha kutoka asilimia 25 hadi asilimia 10 kwenye
mafuta mengineyo ya petroli
yanayotambulika kwa HS Code
2710.19.10.

“Lengo la hatua hii ni kutoa
unafuu na kulinda watumiaji wa
bidhaa hii”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *