SERIKALI YAFUTA ADA KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO NA SITA

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba amependekeza kufuta Ada kwa Wanafunzi wa Kidato cha Tano na Sita ili kuwapunguzia gharama watoto hao

Waziri Dkt. Mwigulu ametoa kauli hiyo leo Juni 14, 2022 Bungeni Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023

Waziri Mwigulu amesema, kwa sasa wanafunzi wa
kidato cha tano ni takriban 90,825 na kidato cha
sita ni 56,880. Mahitaji ya fedha ni shilingi
10,339,350,000.

“Ili kuwapunguzia gharama
watoto hao kama Mheshimiwa Rais alivyoielekeza
Wizara, napendekeza kufuta ADA kwa
wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa
hatua hiyo, Elimu bila Ada ni kuanzia shule za
msingi mpaka kidato cha sita. Serikali
itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya
kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa.
Nani kama SAMIA? Nani kama Mama? Nani kama
CCM? CCM ni Na 1.”

Aidha, Serikali imewezesha
ujenzi wa madarasa 15,000 katika shule za
sekondari na vituo shikizi na mabweni 50 kwa ajili
ya wanafunzi wenye mahitaji maalum.

“Ujenzi wa
miundombinu hii umewezesha wanafunzi wote
907,803 waliofaulu mtihani wa darasa la saba
50 mwaka 2021 kupata nafasi ya kuanza kidato cha
kwanza Januari 2022 bila kusubiri chaguo la pili.”

Kadhalika, Serikali imekamilisha maboma 560 ya
vyumba vya madarasa katika shule za sekondari
kutokana na tozo za miamala ya simu ambapo
shilingi bilioni 7.0 zilitolewa; Aidha, Serikali
imetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni
569 kwa wanafunzi 177,777 wa elimu ya juu.

Ameongeza kuwa katika mwaka 2022/23 Serikali itaenda kutekeleza mradi wa “Higher Education for Economic Transformation” (HEET)
wenye thamani ya dola za Marekani milioni 425. ambapo Mradi huu utahusisha ujenzi wa miundombinu
katika vyuo vikuu mama na katika mikoa kadhaa ambayo haina vyuo vikuu ikiwemo Lindi, Kagera,
Rukwa, Katavi, Manyara na kukamilisha ujenzi
wa Institute of Marine Science Zanzibar na kujenga chuo kipya cha TEHAMA Dodoma

Serikali imeendelea kugharamia programu ya elimumsingi bila ada ambapo hadi Aprili 2022, jumla ya shilingi bilioni
244.5 zilitolewa.

Amesema, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Mungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa CCM ameguswa sana
na watoto kukatisha masomo kwa ajili ya sababu
mbalimbali

. Miongoni mwa sababu
zinazosababisha kukatisha masomo ni umaskini
wa kipato kwenye familia zetu, mimba za utotoni,
mwamko duni wa elimu kwa baadhi ya jamii na
utoro na wale wasioendelea kufuatana kwa
mujibu wa sheria (Ufaulu).

“Ili kukabiliana na
utoro (drop out) wa wanafunzi wanaotoka
familia maskini, bado tuna watoto
wanaoshindwa kumudu mahitaji ya lazima licha
ya kuwepo kwa programu ya elimu bila malipo na
hivyo wanasaidiwa na wabunge, madiwani na
wengine kuchangiwa na wasamaria wema.
Napendekeza kuanzisha dirisha maalum
(Special Fund) kupitia TASAF itakayosaidia
watoto wanaotokea familia maskini. Kwa msingi
huo napendekeza kuanza na bilion 8 kwa ajili ya
watoto masikini watakaopatikana kwenye
database ya TASAF na taarifa za wabunge na
madiwani.”

Pia, ili kukabiliana na mimba za utotoni, Serikali itaendelea kujenga mabweni kwenye maeneo hatari kwa watoto wa kike.

Aidha, ili kutoa fursa kwa watoto
wasioendelea na vidato na vyuo, Serikali itaendelea kuimarisha elimu ya ufundi hususan katika vyuo vya kati kwa lengo la kuwajengea
uwezo wa kujiajiri ama kuajiriwa. Mpaka sasa Wilaya 77 zina vyuo vya Ufundi VETA kati ya
Wilaya 138 nchini kote.

“Tuna mikoa 25 ina Vyuo
vya Ufundi kati ya mikoa 26. Bado mkoa wa
Songwe hauna kabisa Chuo cha VETA na
wabunge wa mkoa wa Songwe wamekuwa
wakishinda Ofisini wakifuatilia ahadi waliopewa
na Mheshimiwa Rais. Bado kuna wilaya 36
ambazo hazina vyuo wala vyuo vya Mkoa.
Napendekeza kutoa bilioni 100 kwa ajili ya ujezi
wa vyuo vya ufundi kwa Mkoa wa Songwe na
wilaya 36 ambazo hazina vyuo ili kufanya wilaya
zote 138 kuwa na chuo cha Ufundi (VETA).
Waheshimiwa wabunge, Huyo ndio SAMIA.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *