VIWANJA VITANO KUWEKEWA NYASI BANDIA NCHINI

Akisoma Bungeni Hotuba ya Mapendekezo na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023 Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba amesema Serikali itarejesha bahati nasibu ya taifa kwa utaratibu wa kutumia
Sekta Binafsi.

Sambamba na hiyo Serikali kupitia
Bodi ya Michezo ya kubahatisha, TRA na Sekta
Binafsi wataanza kuendesha bahati nasibu kwa
kupitia risiti za EFD ili kuchochea wananchi
kudai risiti wanaponunua bidhaa.

Aidha amesema, Serikali
itatumia sehemu ya Mchango wa Wajibu wa Kampuni kwa Jamii (Corporate Social Responsibity) kwa kiwango kisichozidi asilimia 2 kwa ridhaa ya Waziri mwenye dhamana ya masuala ya fedha ili kuendeleza michezo nchini ambapo makampuni yataruhusiwa kukitambua
kiasi hicho kwenye mapato yanayostahili kutozwa
kodi.

“Nitumie nafasi hii kuwahakikishia
watanzania kuwa tutaweka nyasi bandia kwenye
viwanja vitano kwa kuanzia Mwanza, Arusha,
Tanga, Dodoma na Mbeya ili kukuza mchezo hapa
nchini. Katika mwaka wa fedha wa 2022/2023
76
msamaha wa kodi kwenye nyasi bandia na vifaa
ambata vyake utakwenda mpaka ngazi ya
Halmashauri.”

Nitumie fursa hii kuzipongeza timu
zetu za Serengeti Girls na Tembo Warriors
zilizokata tiketi za kuiwakilisha nchi kwenye
mashindano ya Dunia. Niitakie kila la heri timu
yetu ya Taifa Stars ambayo bado iko kwenye
kampeni za kutafuta tiketi ya mashindano ya
kimataifa.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *