NDANDA YAWEKWA SOKONI, WENYE FEDHA WAKARIBISHWA KUINUNUA

Timu ya Ndanda FC, maarufu wanakuchele ya mkoani Mtwara ambayo inashiriki Ligi daraja la kwanza rasmi imetangazwa kuuzwa.

Mkurugenzi wa bodi ya timu hiyo Said Limbega amewaambia waandishi wa habari kuwa, timu hiyo inauzwa kutokana na kukosa fedha za kujiendesha.

Limbega amesema Juni 11 mwaka huu kikao cha bodi ya Wakurugenzi kiliketi na kujadili ajenda mbalimbali ikiwa ni pamoja na mwendelezo wa timu, maendeleo na uwezo wa kujiendesha kitimu.

Amesema baada ua majadiliano hayo, ìmeamuliwa kuuzwa kwa timu hiyo kwa kuwa imekuwa na changamoto nyingi.

Timu ya Ndanda FC imedumu kwenye Ligi Kuu kwa muda wa miaka sita na ligi daraja la kwanza kwa misimu miwili.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *