DENI LA TAIFA LAONGEZEKA KWA ASILIMIA 14.4

Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba amesema hadi Aprili 2022, deni la
Serikali lilikuwa shilingi trilioni 69.44, sawa na
ongezeko la asilimia 14.4 ikilinganishwa na
shilingi trilioni 60.72 Aprili 2021. Kati ya kiasi
hicho, deni la ndani ni shilingi trilioni 22.37, sawa
na asilimia 32.2 na deni la nje ni shilingi trilioni
47.07, sawa na asilimia 67.8.

Waziri Mwigulu ameyasema hayo leo Juni 14, 2022 Bungeni Jijini Dodoma wakati akiwasilisha Mapendekezo ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/ 2023

amesema Kati ya deni la nje,
deni lenye masharti ya kibiashara ni shilingi
trilioni 14.27, sawa na asilimia 30.3. Hivyo,
sehemu kubwa ya deni la nje ni mikopo yenye
masharti nafuu

“Mheshimiwa Spika, tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Novemba 2021 kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada Sura 134 ilionesha kuwa viashiria vya deni la Serikali viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu. Katika Tathmini hiyo,viashiria vinaonesha kuwa: uwiano wa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.0 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55; uwiano wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa Pato la Taifa ni 18.8 ikilinganishwa na ukomo wa
asilimia 40; na uwiano wa thamani ya sasa ya
deni la nje kwa mauzo ya nje ni asilimia 142.4
6 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 180. Tathmini ya Kukopesheka kwa Nchi (Credit
Rating)”

ameongeza kuwa katika mwaka
2021/22, zoezi la tathmini na ukadiriaji wa kukopesheka kwa nchi (credit rating) ambalo lilisimama hapo awali lilianza tena kupitia benki ya Citibank ambayo ilikuwa mshauri wa Serikali. Hadi kufikia mwezi Mei 2022, Serikali imefikia hatua za mwisho za kukamilisha taratibu za ununuzi ambapo imefanikiwa kuchagua kampuni mbili ambazo zinatambulika kimataifa na kupitia mikataba yao.

Aidha, Serikali inaendelea na mazungumzo na kampuni hizo pamoja na kuandaa takwimu mbalimbali ambazo zitatumika katika zoezi la tathmini na ukadiriaji wa
kukopesheka.

ameeleza kuwa, Serikali inategemea kukamilisha
zoezi hili ndani ya mwaka 2022/23. Naomba
nichukue fursa hii kuziomba taasisi za Serikali, za
binafsi na benki zitakazopata nafasi ya kuhojiwa
na wataalamu wa Kampuni hizo kutoa ushirikiano
kwa kuzingatia maslahi mapana ya nchi.
Kukamilika kwa zoezi hili kutatuwezesha
kuongeza wigo wa wakopeshaji kwa Serikali na
makampuni binafsi hususan katika masoko ya
mitaji ya kimataifa (International Capital Markets).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *