YANGA YAMWONGEZEA MKATABA FARID MUSSA, KUSHEREHEKEA UBINGWA WIKI HII

Klabu ya Yanga leo hii imetangaza kumwongezea Mkataba Kiungo Mshambuliaji Farid Mussa kwa Kipindi cha Miaka Miwili
Farid Mussa ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akitumika kama Beki wa kushoto na amekuwa akionesha kiwango maradufu, hivyo atasalia jangwani mpaka 2024.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram wa Mchezaji huyo amepost Picha aliyoambatanisha maneno Alhamdulillah 💚💛👉2024

Kwa Upande mwingine leo hii Msemaji wa Yanga Haji Manara amesema kuwa nafasi ya Ubingwa wa NBC PREMIERE LEAGUE kwa Yanga ni Asilimia 99 mpaka sasa japo hawajatangaza Ubingwa
Manara ameyasema hayo katika Mkutano na Wanahabari leo Juni 13, Jijini Dar es salaam.
“Nafasi yetu ya kushinda ubingwa ni kubwa sana kama 99%, bado hatujashinda ubingwa lakini nafasi ya sisi kuwa mabingwa ni kubwa sana, kwa mujibu ya msimamo wa ligi tunaitaji alama 3 ili tutawazwe kuwa mabingwa wa msimu huu” Amesema Manara


Aidha, ametamba kuwa Mpaka sasa Yanga inadaiwa Ushindi wa Mechi zote Nne zilizosalia ili kuweka rekodi ya kutokupoteza Mchezo Duru hili la Pili kama ilivyokuwa kwenye Mzunguko wa Kwanza wa Ligi
“Tumebakiza michezo minne (4) ya ligi kuu ya Tanzania NBC, katika michezo 26 tuliyocheza tumekusanya alama 66, tukishinda michezo 20 na sare 6, kwenye mzunguko wa kwanza tulishinda michezo 12 na sare 3 pia kwenye mzunguko wa pili tumeshatoka sare michezo mitatu (3) na tunadaiwa ushindi wa michezo 4 ili tukusanye alama sawa na mzunguko wa kwanza”

Pia Manara ametamba kuwa “Huu ndiyo msimu wetu bora zaidi katika kipindi cha miaka 10 nyuma, baada ya kupoteza michezo miwili ya #cafclcc na ule mchezo wa Wiki ya Wananchi kutokea hapo utajapoteza mchezo wowote ndani ya dakika 90’ mpaka hivi sasa”
Yanga inatarajia kushuka Dimbani Jumatano ya Wiki hii kumenyana na Wagosi wa Kaya Coastal Union katika Dimba la Mkapa, Dar es salaam na iwapo wakishinda watatawazwa Rasmi kuwa Mabingwa wapya wa NBPL Msimu wa 2021/2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *