SERIKALI YAJA NA MKAKATI KUTATUA CHANGAMOTO SKIMU ZA UMWAGILIAJI NCHINI

Na; Emmanuel Charles

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imesema kuwa Itakwenda kufanya maboresho katika Skimu mbalimbali za umwagiliaji nchini ili kuleta tija kwa Wakulima
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Kilimo Bungeni Mhe. Antony Mavunde, wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Momba Mhe. Condester Sichalwe aliyeuliza kuwa Je!ni lini Serikali itafanya maboresho ya Skimu ya umwagiliaji ya naming’ong’o iliyopo Chitete Wilayani Momba ambayo ndiyo inategemewa na Wakulima ili kulima kwa ufasaha na kuweza kuleta tija, ukizingatia Mwaka huu hakukuwa na Mvua.
“Skimu ya umwagiliaji ya naming’ong’o iliyopo Chitete Wilayani Momba ndiyo inategemewa na Wakulima ili kulima kwa ufasaha, Je!ni lini Serikali itafanya maboresho ya Skimu hiyo ili kuweza kuleta tija, ukizingatia Mwaka huu hakukuwa na Mvua na mpunga umekauka”


Mavunde amesema, Moja kati ya kazi kubwa waliyoipa Tume ya Taifa ya umwagiliaji ni kuhakikisha kuwa inafanya Stadi na kupitia skimu zote na kujua Status zake ili ziweze kufanyiwa marekebisho,
“kwahiyo nimhakikishie Mhe. Mbunge na Skimu aliyoitamka tumeiweka katika mipango yetu kwaajili ya utekelezaji ndani ya Serikali”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *