MANARA ATANGAZA USAJILI WA WACHEZAJI WAPYA YANGA KIMATAIFA

Klabu ya Yanga ikiwa inajiandaa kumaliza Msimu huku kukiwa na matumaini ya kutwaa mataji mawili yaliyosalia mbele yao ikiwa ni NBC PREMIERE LEAGUE na AZAM SPORTS FEDERATION CUP

Tayari tambo za Usajili zimeanza na baadhi ya Wachezaji wakitajwa kusajiliwa hususani wa Kimataifa

Leo Juni 13, 2022 Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari Jijini Dar es salaam, Msemaji wa Klabu hiyo Ndg. Haji Manara ametaja aina ya wachezaji ambao Yanga itakwenda kuwasajili

“Yanga msimu huu tutasajili Wachezaji wanne hadi watano wa kimataifa. Na hatuna tetesi tena. Yanga tutakwenda kwenye nchi hizi;”

1 – Yanga tutamsajili mchezaji ambaye anatoka Afrika magharibi na anacheza ligi ya Ivorycoast 🇨🇮”

2 – Yanga tutasajili mchezaji anayetoka Afrika mashariki na kati”

3 – Yanga tutasajili mchezaji ambaye amecheza ligi kuu ya Afrika kusini”

4 – Yanga tutasajili mchezaji kutoka Angola”
.
.
“Yanga tuko katika mazungumzo na bodi ya ligi kuwaomba kama itawapendeza, tukabidhiwe kombe letu la ligi kuu Jijini Mbeya July 25, 2022 …. Wananchi wanataka kombe lao lipande ndege kuja Dar”
.
.
“Sisi Yanga hatuchukui pesa za NANI ZAIDI kwenda kununua cement au tofali …. Nimesikia habari kuna jamaa yao amechukua fungu la pesa kisha akaweka kwenye NANI ZAIDI ili waonekane wakubwa Ameniambia Bumbuli”

“Tunawaheshimu Coastal Union ila tunakwenda kutwaa UBINGWA Jumatano, mashabiki mjitokeze kwa wingi, wale ambao mko mbali muangalie kwenye TV”

Miongoni mwa Majina yanayotajwa kusajiliwa Yanga ni Mchezaji Stephane Ki Aziz ambaye ni Raia wa Ivory Coast

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *