PADRE AUAWA KIKATILI MBEYA, KICHWA NA KIWILIWILI VYATENGANISHWA.

Padre wa kanisa katoliki Jimbo kuu la Mbeya Michael Samsoni ameuawa kikatili na watu wasio julikana Kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwili kisha kuutupa mwili wake Katika mto meta chini ya daraja la jakalanda Jijini Mbeya.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishina msaidizi mwandamizi wa Jeshi Hilo Ulrich Matei, amesema mwili wa Padre huyo Raia wa Malawi ulikutwa siku ya Jana ukiwa umevilingishwa kwenye duveti na blanket kisha kutupwa eneo Hilo.

Padre Michael alikua akihudumu katika Shirika la Missionaries of Africa (WHITE FATHER’S) ambapo alitoweka jioni ya tarehe 10 mwezi huu baada ya kuwaaga wenzie kua anaenda kufanya mazoezi na hakurejea Hadi mwili wake ulipo kutwa siku ya Jana majira ya asubuhi

Kamanda Urlich Matei amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kifo cha padre huyo

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *