
Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) imenunua mita (dira) za maji 14,000 za nusu inchi zenye gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.2.
Mita hizi zimepokelewa leo Ijumaa kwa ajili maunganisho kwa wateja wapya na kubadilisha mita chakavu. Kabla ya kufungwa mita hizi zitapimwa na Wakala wa Vipimo Tanzania kuhakiki ufanisi wake.
Mita hizi zinatoka kampuni ya B- Meter ya nchini Italia.


