CAPITAL CITY MARATHON YAPAMBANA KUISAPOTI SERIKALI MAGONJWA YASIYO YA KUAMBUKIZA

Capital City Marathon wameandaa Capital City Evening Run iliyofanyika katika Mji wa Magufuli Mtumba, Dodoma Juni 11, 2022 ambapo watu mbalimbali wamejitokeza kushiriki akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.

Akizungumza na Uhondo Tv Baada ya kumalizika kwa Mbio hizo Mratibu wa Capital City Evening Run Bw. Nsolo Mlozi amesema lengo la kufanya mbio hizo katika Mji wa Magufuli Mtumba, Dodoma ni kujiandaa na mbio kubwa za Capital City Marathon zinazotarajiwa kufanyika Mwezi Oktoba, 2022.

Pia lengo lingine ni Kutalii na kujionea Muundo wa Mji huo wa Magufuli ambao umejengwa kisasa na wenye kuvutia.

Ameongeza kuwa kama lilivyo lengo la Capital City Marathon ni kusapoti juhudi za Serikali katika kujikinga na Magonjwa yasiyoambukiza kwa kufanya Mazoezi.

hivyo, wanaishukuru Serikali na wote Waliojitokeza kushiriki.

“Niishukuru sana Serikali na wote Waliojitokeza hapa.ninyi wenyewe mmeona watu ni wengi wamekuja, Pia niwashukuru sana wadau wote waliotuunga mkono”amesema Nsolo

Baadhi ya Washiriki wakikimbia Mbio za Capital City Evening Run wakiwemo Watoto

Mbio hizo zimefanyika kuanzia Majira ya Saa 10:00

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *