DAWA ZA KULEVYA ZILIZOKAMATWA ZAVUNJA REKODI TANGU UHURU

Na; Emmanuel Charles

Imeelezwa kuwa Dawa za Kulevya zinazozalishwa Viwandani, Mwaka 2021 jumla ya tani 1.13 za heroin zilikamatwa ikiwa ni Kiasi Kikubwa kuwahi Kukamatwa kwa Mwaka mmoja katika Historia ya Nchi ambapo Kiasi hicho ni mara tatu ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2022 pamoja na Kiasi cha gramu 811.30 za Cocain zilikamatwa

Hayo yamethibitishwa na Waziri wa Nchi-Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene Wakati akizungumza na Wanahabari katika Ukumbi wa Idara ya Habari Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 10, 2022

Ameeleza kuwa kwa mara ya kwanza Mwaka 2022, katika Historia ya mapambano dhidi ya Dawa za kulevya nchini, Shehena kubwa ya kilo 430.77 za Dawa za kulevya aina ya metamphetamine inayotengenezwa na kemikali bashirifu ilikamatwa, ikihusisha watuhumiwa tisa raia wa Iran wote wakiwa wanaume

“Katika Kukabiliana na tatizo hilo, Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uingizwaji na matumizi ya Madawa hayo pamoja na kemikali bashirifu ambazo hutumika kutengeneza dawa hizo”

Simbachawene ameongeza kuwa, Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya nchini limeendelea kuwepo pamoja na juhudi za udhibiti zinazofanywa na Serikali.ambapo hadi kufikia mwezi Desemba 2021, waraibu wa dawa mbalimbali za kulevya pamoja na vilevi vingine wapatao 905, 902 walijitokeza kupata tiba katika hospitali za Wilaya na Mikoa nchini.

Kwa Upande mwingine amesema Serikali imeendelea kupambana na tatizo la uzalishaji, matumizi na biashara ya dawa za kulevya Nchini.kama ilivyokuwa katika kipindi kilichopita Uzalishaji, matumizi, biashara ya dawa za kulevya imeendelea kuwa tatizo duniani na kuleta athari za kiuchumi, kijamii na masuala ya ulinzi na usalama.

“Bangi na mirungi zimeendelea kuwa tatizo Nchini ambapo katika mwaka 2021, jumla ya tani 22.74 za bangi zilikamatwa, ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2020”

Ukamataji huo ulihusisha jumla ya watuhumiwa 9,484. mirungi iliyokamatwa katika kipindi hicho ilifikia tani 10.93 zikihusisha watuhumiwa 1,395.

Aidha, ameeleza kuwa Serikali imeendelea kupanua wigo wa matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya ambapo hadi kufikia mwezi Desemba, 2021 huduma za tiba ya uraibu zilikuwa zikipatikana kwenye vituo 15 vya kutolea tiba kwa waraibu wa heroini(MAT Clinics) na vituo hivyo kwa pamoja vilikuwa vimesajili waraibu 11,650.

Vituo hivyo vinapatikana katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga, Mbeya, Songwe, Dodoma, Mwanza na Arusha.

“Serikali imeendelea kufanya usimamizi katika nyumba 44 za upataji Nafuu(Sober House) nchini.
Wakati huo huo Mhe. Simbachawene ameipongeza Mamlaka ya kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya pamoja na wadau wote kwa ushirikiano uliowezesha udhibiti na mapambano dhidi ya dawa za kulevya katika mwaka 2021 pamoja na kuhamasisha jamii kukabiliana na tatizo hilo ambalo ni hatari.

“Napenda kuwahimiza wananchi wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali katika kupambana na tatizo la dawa za kulevya kwa manufaa yetu sote, ikiwemo kutumia Simu ya Bure namba 119 ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *