CAPITAL CITY MARATHON WATETA NA WAZIRI MKUU

Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Capital City Evening Run leo wamepata wasaa kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaliko wa Mhe. Tulia Ackson – Spika. Pia wamefanya mazungumzo na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa – Waziri Mkuu kuhusu jitihada zetu kwenye sekta ya mchezo hususani riadha. Siku ya kesho wanatarajia kufanya Capital City Evening Run kwa 5km na 15km itakayofanyika katika mji wa Serikali Mtumba.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amekutana na kufanya mazungumzo na Kamati ya Waandaaji wa Capital City Marathon Wakiongozwa na Bw. Nsolo Mlonzi walipomtembelea Ofisini kwake Bungeni Jijini Dodoma leo Juni 10, 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *