BEI YA UMEME HAIJAPANDA, TUTAWACHUKULIA HATUA WANAOPOTOSHA MITANDAONI

Waziri wa Nishati Mhe. Januari Makamba amekataa Uvumi unaoenezwa mitandaoni juu ya kupanda kwa Bei ya Umeme nchini

Makamba ameyasema hayo Leo Juni 10, 2022 Bungeni wakati akijibu Swali la Mbunge wa Nyasa Eng. Stella Manyanya aliyeuliza Je! ni kweli Bei ya Umeme imepanda?

“Si kweli kabisa kwamba bei ya umeme imepanda, na serikali inasikitishwa na wale wanaoeneza maneno hayo na uvumi huo kwenye mitandao, na tumeomba mamlaka husika zichukue hatua kwa udanganyifu na upotofu huo unaofanywa”.amesema Waziri Makamba

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *