Wizara ya Kilimo imegawa Mbegu za Pamba na Dawa kwa Wakulima Bure kwa Wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera


Waziri wa Kilimo Mhe. Hussein Bashe amesema Wizara ya Kilimo imegawa mbegu za Pamba na Dawa bure kwa Wakulima wa Pamba wa Wilaya ya Biharamuri mkoani Kagera.

Waziri Bashe Ameyasema hayo Leo 8,June 2022 wilayani Biharamuro mkoani Kagera katika ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Bashe amesema mbali na Serikali kutoa mbegu bure kwa Wakulima pia amewahakikishia Wananchi wa Biharamulo soko la uhakika la mazao ya Pamba, Kahawa na Tumbaku.

Amesema Wakulima watauza zao la Pamba kupitia Chama Kikuu cha Ushirika cha Chato na MBCU na Kuelekeza Bei elekezi ya zao hilo la Pamba kuwa kati ya Shilingi, 1560 mpaka 1900.

Waziri Bashe amewaambia Wakulima hakutokuwa na makato ya Aina yoyote pia Serikali imefuta tozo ya zao la Kahawa na Mkulima atauza kahawa bila makato yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *