TAHA YAPOKEA UGENI KUTOKA SHIRIKA LA USDA

TAHA imepokea ugeni kutoka Shirika la USDA ambao umejumuisha Bi. Paige Cowie na Bi. Shoshana Griffith ambao walipokelewa na timu ya uongozi ya TAHA. Katika ziara hii ugeni huu umepata kufahamu kwa ukaribu mchango wa USAID na USDA kwa TAHA katika kukuza tasnia ya Horticulture nchini. Mbali na kufahamu shughuli za TAHA pia wametembelea mashamba ya wakulima na Kongani zilizopo Arusha ili kujionea maendeleo katika mnyororo wa thamani wa mazao ya Parachichi, Nyanya, Vitunguu, Karoti na Pilipili kisha kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea kituo cha mafunzo ya vitendo na uchakataji wa mazao cha TAHA kilichoko Tengeru.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *