
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, amepokea ripoti kutoka Kwa Wabunge wawili aliowaagiza June 3, 2022 kuleta uthibitisho Kwa kile walicholalamika kuhusu wananchi wa majimboni mwao kuuawa
Dkt.Tulia amesema siku ya jumatatu Mbunge Tarime vijijini Mhe. Mwita Waitara alidai kuwa baadhi ya wananchi wake wameuawa Kwa kipigwa risasi na kuchukuliwa mifugo naye Mbunge wa Songwe Mhe. Philip Mulugo kudai wananchi wa Jimbo lake kuuawa na tembo, Simba na mamba ambapo Mhe. Dkt.Tulia aliwataka walete taatifa ya uthibitisho kuhusu masuala hayo.
Katika ripoti walizoleta Wabunge hao Mhe. Dkt.Tulia amesema ripoti hizo hazina uthibitisho wa kutosha badala yake ni malalamiko yaleyale ya wananchi ambayo Wabunge hao walichangia June 3, 2022 kwenye bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii.
Aidha, Spika ameiomba Serikali kufuatilia malalamiko hayo ili yafanyiwe kazi.

