MAAGIZO YA WAZIRI MKUU PIKIPIKI ZA WIZARA YA KILIMO YAANZA KUTEKELEZWA

Juni 9,2022 Naibu Waziri wa Kilimo nchini Mhe. Antony Mavunde ameongoza zoezi la ugawaji wa pikipiki kwa wakurugenzi wa Halmashauri Iliziende kwa maafisa ugani kote nchini

Hatua hiyo imekuja Baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Juni 8, 2022 kuagiza Wizara hiyo kukabidhi Pikipiki hizo kwa Maafisa Ugani ndani ya Siku Tano.

Waziri Mkuu alisema, tayari Mheshimiwa Rais Samia alishazikabidhi kwa ajili ya kupelekwa kwa maafisa ugani, hivyo kitendo cha pikipiki hizo kuendelea kubaki katika eneo hilo hakikubaliki.

Akizungumza Baada ya Zoezi hilo Naibu Waziri Mavunde amesema Wizara ya kilimo imehakikisha inasimamia zoezi hilo kama Waziri Mkuu alivyoelekeza

Mavunde amesema zoezi hilo litakamilika kwa 90% ifikapo tarehe 10,6,2022 kwa sababu viongozi wote wa mikoa wapo njiani kwenda kuchukua pikipiki hizo

“Kama ambavyo ameelekeza Waziri Mkuu vifaa hivyo vitakapopokelewa viende moja kwa moja Kufanya kazi iliyo kusudiwa” Amesema Mavunde

Mnamo Aprili 4, 2022 Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan alizindua ugawaji wa vitendea kazi vilivyoandaliwa na Wizara ya Kilimo kwa ajili ya Maafisa Ugani wote nchini ambapo Vifaa hivyo ni Pamoja na Pikipiki.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *