WAZIRI MASAUNI ASEMA HAKUNA SABABU VIONGOZI WA CHADEMA KUTOREJEA NCHINI, TANZANIA NI SALAMA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni amesema Tanzania ni salama na haina tishio lolote la usalama, pia Masauni amesema hakuna sababu ya Mtanzania yeyote ikiwemo viongozi wa CHADEMA waliopo nje ya nchi kutorudi Nchini ili waje kutumia fursa zilizopo za maendeleo pia kushiriki kutoa mchango wa kwa maendeleo kwani Tanzania ni nyumbani kwao.

Masauni alikuwa akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Grace Tendega aliyeuliza kuhusu wanasiasa walioenda nje ya nchi ilhali Rais Samia ameshayaweka makundi tofauti pamoja hivyo kutaka kauli ya Serikali kuwataka Watanzania waliopo nje ya nchi kurudi nchini.

Pia Masauni ametumia fursa hiyo kusema Serikali ya awamu ya sita itaendelea kusimamia vyombo vyake vya usalama kutekeleza majukumu yake kwa misingi ya kisheria ili haki sio tu itendeke lakini ionekane kuwa imetendeka.
MWISHO.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *