
Serikali ya Tanzania kupitia TANROADS imetangaza tender ya ujenzi wa Barabara ya njia nne kutoka IGAWA – UYOLE – SONGWE – TUNDUMA, Tenda namba AE/001/2021-22/HQ/W/54 ili kupata mzabuni kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Hatua hii inakuja ikiwa ni sehemu ya kutumiza ahadi iliyotolewa na Serikali ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikipigiwa kelele na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson.
