MCHECHU AENDELEA KUIPAISHA NHC, RAIS SAMIA ATAJWA KINARA WA MCHEZO

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Bw. Nehemiah Mchechu, amewasilisha kwenye Menejimenti ya Wizara ya Utumishi na Utawala Bora Mpango wa Uendelezaji wa sekta ya nyumba nchini unaoenda kutekelezwa na NHC. Ameelezea manufaa makubwa ya sekta ya nyumba katika kuchangia ukuaji wa uchumi na maisha ya watanzania.

Akiongea baada ya mawasilisho ya Mpango huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Dkt. Damas Ndumbaro, amempongeza Bw. Mchechu kwa kuaminiwa tena na Serikali na mikakati yake mikubwa ya ujenzi wa nyumba ambazo zitawanufaisha pia Watumishi wa Umma. Amesema wizara yake italiunga mkono Shirika la Nyumba la Taifa katika kufanikisha ndoto zake za kuwapàtia watanzania makazi bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *