WAZIRI BASHE ASISITIZA HATOFUNGA MIPAKA KUWAZUIA WAKULIMA

Waziri wa Kilimo Mhe.Hussein Bashe ameendelea kusisitiza kuwa hatofunga mipaka kuwazuia wakulima wa Tanzania kuuza mazao yao nje ya nchi.

Waziri Bashe amesema hayo jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Nane la Mwaka la Wadau wa Sekta ya Mazao,Mifugo na Uvuvi.

Waziri Bashe ameongeza kuwa kumzuia mkulima kupeleka sokoni mazao aliyovuna ni kumrudisha nyuma mkulima na kumtia umasikini.

Waziri Bashe ametumia fursa hiyo kusisitiza kuwa Kilimo ni Biashara kama zilivyo Biashara zingine hivyo mkulima anastahili kupata faida baada ya kuvuna.


“Hakuna mazao ya chakula na mazao ya biashara kwani chakula ndio biashara kubwa hivyo mkulima ana haki ya kuuza chochote anachuvuna”. Amesema Waziri Bashe.

Mhe. Bashe amfafanua kuwa ingawa mavuno ya msimu huu yameshuka ikilinganishwa na msimu uliopita hali ya chakula nchini ni nzuri.

Ameongeza kuwa Mamlaka ya Hifadhi ya Chakula (NFRA) inanunua mahindi kutoka kwa wakulima kwa bei ya kushindana na wafanyabiashara na itapeleka chakula katika maeneo ambayo yatakuwa na upungufu wa chakula kwa bei ambayo kila Mwananchi ataimudu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *