HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO MWAKA WA FEDHA 2022/2023

    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA  

WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO

HOTUBA YA     WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO, MHESHIMIWA DKT.  MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU (MB.), AKIWASILISHA

 BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA 

YA FEDHA NA MIPANGO KWA MWAKA 2022/23

DODOMA                    JUNI 2022

i  

ii

        1.0       UTANGULIZI

 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2021/22 na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya mafungu nane (8) ya Wizara, pamoja na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa Mwaka 2022/23.
 • Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya njema, na kutuwezesha kukutana kwa mara nyingine tena kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa Mwaka 2021/22 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2022/23. 
 • Mheshimiwa Spika, kipekee, napenda kutumia fursa hii kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini kuongoza Wizara ya Fedha na Mipango. Napenda kumhakikishia, kwa mara nyingine kuwa nitaendelea kutumikia dhamana aliyonipa kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa. Ni dhahiri kwamba, katika kipindi cha takribani mwaka mmoja na miezi mitatu (3) ya uongozi wake, nchi yetu imepata mafanikio mengi ambayo kila mmoja wetu anapaswa kujivunia. Mwenyezi Mungu amjalie afya njema, hekima na busara katika kuliongoza Taifa letu.
 • Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii adhimu kukupongezawewe binafsi na Naibu Spika, Mheshimiwa Mussa A. Zungu (Mb) kwa kuchaguliwa kwa kishindo na waheshimiwa wabunge kuliongoza Bunge letu Tukufu. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu awajalie afya njema na hekima ili kutekeleza majukumu yenu ya kibunge kwa ufanisi. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha kwa kuteuliwa kwake na Mheshiwa Rais kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pamoja na pongezi hizo, natoa pole kwa Bunge lako Tukufu kwa kuondokewa na Mheshimiwa Irene A. Ndyamukama, Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa, ambaye ametangulia mbele ya haki. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
 • Mheshimiwa Spika, kwa muktadha wa tukio la leo, naomba kutoa pongezi zangu za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, chini ya Mwenyekiti wake Mhe. Daniel Baran Sillo – Mbunge wa Babati Vijijini pamoja na Makamu Mwenyekiti, Mhe. Omari Mohamed Kigua – Mbunge wa Kilindi kwa maoni na ushauri wao mzuri katika kuboresha utendaji wa Wizara pamoja na maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/23. Kwa niaba ya Wizara na taasisi zake, napenda kuihakikishia Kamati kuwa tutaendelea kushirikiana kwa karibu ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi waliotupa dhamana ya kusimamia masuala ya mipango, uchumi na fedha kwa Taifa letu.
 • Mheshimiwa Spika, baada ya utangulizi huo, sasa naomba nijielekeze katika hoja yangu yenye maeneo makuu manne (4) ambayo ni: majukumu ya Wizara; mapitio ya utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2021/22; vipaumbele vya Wizara na taasisi zake kwa Mwaka 2022/23; na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2022/23. 

        2.0       MAJUKUMU YA WIZARA 

7. Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa tangazo la Serikali Na. 534 la tarehe 02 Julai 2021, majukumu ya kisera na kiutendaji ya Wizara ya Fedha na Mipango ni pamoja na:

 1. usimamizi wa sera za uchumi jumla, fedha, ununuzi wa umma na ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi:
  1. usimamizi mipango, mikakati na miongozo ya kitaifa ya maendeleo;
  1. usimamizi wa bajeti ya Serikali;
  1. kuratibu upatikanaji wa fedha kutoka taasisi za fedha za kikanda na kimataifa kwa ajili ya utekelezaji wa Bajeti ya

Serikali;

 • udhibiti utakasishaji wa fedha haramu, ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi; 
  • usimamizi na udhibiti wa mali za umma;
  • usimamizi uendeshaji wa Mashirika ya Umma pamoja na vitega uchumi vya Serikali; 
  • usimamizi wa masuala ya pamoja ya fedha kati ya

Tanzania Bara na Zanzibar; ix) usimamizi wa mafao na pensheni kwa wastaafu wasio wanachama wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii;

x)     usimamizi wa Deni la Serikali; xi)    usimamizi wa michezo ya kubahatisha ; xii) usimamizi wa maendeleo ya Sekta ya Fedha; na xiii) usimamizi wa takwimu rasmi za kitaifa.

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2021/22  

3.1 Mapitio ya Mapato na Matumizi  

3.1.1 Mapato

8. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilipanga kukusanya maduhuli ya shilingi bilioni 920.38 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo gawio, michango kutoka katika taasisi na mashirika ya umma, marejesho ya mikopo, kodi za pango, mauzo ya leseni za udalali na nyaraka za zabuni. Hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kukusanya jumla ya shilingi bilioni 689.5, sawa na asilimia 74.9 ya lengo la mwaka. Mchanganuo wa mwenendo wa ukusanyaji wa maduhuli ni kama inavyoonekana katika Jedwali Na.1.

Jedwali Na.1: Mwenendo wa Ukusanyaji wa Maduhuli kati ya Julai 2021 na Aprili 2022

FunguJina la FunguKiasi
7Ofisi ya Msajili wa Hazina629,041,408,131.00
23Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali60,126,687,875.95
50Wizara ya Fedha na Mipango396,549,202.00
 JUMLA689,564,645,208.95

          Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango

3.1.2 Matumizi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ya Fedha na Mipango iliidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 13.26 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo kwa mafungu yake saba (7) ya kibajeti pamoja na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 11.99 ni matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.27 ni matumizi ya maendeleo. 
 1. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, mafungu ya Wizara pamoja na Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi yametumia jumla ya shilingi trilioni 9.64 sawa na asilimia 72.6  ya bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 9.04 ni matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 597.55 ni matumizi ya maendeleo. Mchanganuo wa fedha zilizotumika kwa kila Fungu ni kama inavyoonekana katika kiambatisho Na. 1– 3.

3.2  Utekelezaji wa Majukumu

11. Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa mwaka 2021/22 unaendelea kwa kuzingatia vipaumbele vifuatavyo: 

 1. kufanya mapitio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mpango Elekezi wa Miaka 15 (2011/12 – 2025/26) na kuanza maandalizi ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050; 
 2. kufanya tafiti za kiuchumi na modeli za fedha ili kubaini fursa fiche za uwekezaji na vyanzo vipya vya mapato, ikiwa ni pamoja na mapato ya kugharamia shughuli za

Muungano; iii) kufanya tathmini ya kina ya mfumo wa mapato na matumizi ya Serikali ili kubaini maeneo yenye upungufu au changamoto na kupendekeza hatua stahiki za kuchukua; 

 1. kufanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali; 
 2. kuratibu mipango na mikakati ya upatikanaji wa misaada, mikopo yenye masharti nafuu pamoja na mikopo yenye masharti ya kibiashara kwa ajili ya kugharamia bajeti ya

Serikali; vi) kutunga Sera ya Maendeleo ya Sekta ya Benki na Mkakati wake;

 • kuandaa Mwongozo wa Usimamizi, Tathmini na Ufuatiliaji wa Uwekezaji katika Taasisi na Mashirika ya Umma; 
 • kufanya ufuatiliaji, tathmini, ukaguzi, udhibiti na uhakiki wa mapato, matumizi, miradi ya maendeleo,mali za umma; na miamala ya utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi; 
 • kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya PPP;
 • kukamilisha maandalizi ya Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Programu na Miradi ya

Maendeleo;  xi) kufanya maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya

Mwaka 2022;  xii) kuhuisha Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu na Mkakati wa utekelezaji wake;

xiii) kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Uchumi wa Bahari

(National Strategy for Blue Economy);  xiv) kuwajengea uwezo watumishi kutoka Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala za Serikali, Taasisi na Mashirika ya Umma, Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhusu matumizi ya mifumo ya usimamizi na udhibiti wa mapato, matumizi na mali za Serikali, hususan MUSE, GEPG na GAMIS;

 • kuimarisha usalama na ulinzi wa mifumo ya TEHAMA pamoja na mifumo ya usimamizi na udhibiti wa mapato, matumizi na mali za Serikali; na
 • ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa Magufuli pamoja na maandalizi ya ujenzi wa jengo la Ofisi ya Usimamizi wa Mali za Serikali, Geita.

12. Mheshimiwa Spika, kati ya Julai 2021 na Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:- 

3.2.1 Usimamizi wa Sera za Uchumi Jumla 

 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara iliweka malengo na shabaha za uchumi jumla kama msingi wa kubuni na kutunga sera zenye mwelekeo wa kujenga uchumi jumuishi, himilivu na endelevu. Ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa mwaka 2021 ulikua kwa asilimia 4.9 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2020. Ongezeko la ukuaji wa uchumi limetokana na jitihada mbalimbali zinazoendelea kuchukuliwa na Wizara ikiwemo: Kuwezesha shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii kurejea katika hali ya kawaida baada ya kuathirika na UVIKO -19; na kuwezesha upatikanaji wa mkopo nafuu usio na masharti kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) wa shilingi trilioni 1.3 kwa ajili ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi UVIKO-19. 
 1. Mheshimiwa Spika, mfumuko wa bei umeendelea kubaki chini ya asilimia 5.0 kama ilivyotarajiwa katika kipindi cha muda wa kati. Mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 3.7 mwaka 2021 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3

mwaka 2020. Aidha, katika kipindi cha Julai 2021 hadi Aprili 2022, mfumuko wa bei ulikuwa wa wastani wa asilimia 3.9 ikilinganishwa na asilimia 3.3 katika kipindi kama hicho mwaka 2020/21. Ongezeko la mfumuko wa bei limetokana na: kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia kutokana na athari za UVIKO-19 na vita baina ya Urusi na Ukraine; kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma, hususan bidhaa ya petroli, mafuta ya kula, mbolea, chuma na malighafi za viwandani katika soko la dunia; na kupungua kwa upatikanaji wa mazao ya chakula katika baadhi ya masoko ya ndani kutokana na mabadiliko ya tabia ya nchi.  Pamoja na ongezeko hilo, kiwango hicho bado kipo ndani ya matarajio ya wigo wa nchi wa kati ya asilimia 3.0 – 5.0 na lengo la nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki la asilimia 8.0.

3.2.2 Usimamizi wa Mpango na Bajeti ya Serikali

3.2.2.1 Mpango wa Maendeleo wa Taifa

 1. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 ambao uliidhinishwa na Bunge lako Tukufu Aprili 2021. Mpango huo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 pamoja na mipango na mikakati ya maendeleo ya kikanda na kimataifa.
 1. Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:  (i)  kukamilisha maandalizi ya nyaraka za mapitio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 (ii) kuandaa Mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2022/23 ambao uliwasilishwa katika Bunge lako Tukufu Machi 2022, na baadaye utawasilishwa tena mbele ya Bunge lako Juni 2022 kwa idhini (iii) kufanya uchambuzi wa maombi ya fedha kwa miradi ya kimkakati 38 kutoka halmashauri 28 yenye thamani ya  shilingi bilioni 288.06, ambapo Wizara iliridhia maombi ya shilingi bilioni 201.80 yaliyokidhi vigezo (iv) kukamilisha na kusambaza Mwongozo wa Kitaifa wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi na Programu za Maendeleo (v) kufanya ufuatiliaji na tathmini ya ujenzi wa madarasa 15,000 na mabweni 50 yaliyojengwa chini ya Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya athari za Kiuchumi na Kijamii za UVIKO-19, mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kati kwa Standard Gauge, mradi waUjenzi wa Daraja la Kigongo – Busisi (M 3,200) na Barabara Unganishi (Km 1.66), Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) na mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115 na (vi) kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi 173 ya maendeleo katika sekta za; Kilimo, Viwanda, Utawala bora, Ujenzi, Uchukuzi, Maji, Elimu, Afya, Biashara na Mifugo katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Geita, Kagera, Mara na Simiyu. Sekta hizo zimepewa kipaumbele kwa kuwa sehemu kubwa ya fedha za maendeleo zimeelekezwa katika maeneo hayo.

3.2.2.2 Usimamizi wa Bajeti ya Serikali

3.2.2.2.1 Mapato ya ndani

17. Mheshimiwa  Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilikadiriwa  kuwezesha na kukusanya mapato ya  kodi na yasiyo  ya kodi  ya jumla ya shilingi trilioni 25.69, ikijumuisha  mapato ya  Mamlaka za Serikali za Mitaa.  Hadi Aprili 2022, ukusanyaji wa mapato ya Serikali umefikia shilingi trilioni 19.99, sawa na asilimia 93.3 ya makadirio ya kukusanya shilingi trilioni 21.42 katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, mapato ya kodi yamefikia shilingi trilioni 17.20, sawa na asilimia 94.5 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 18.2. Aidha, Wizara imewezesha Wizara, Idara Zinazojitegemea, Wakala na Taasisi za Serikali kukusanya mapato yasiyo ya kodi ya jumla ya shilingi trilioni 2.03, sawa na asilimia 81.2 ya lengo la kukusanya shilingi trilioni 2.5 na Mamlaka za Serikali za Mitaa shilingi bilioni 759.0, ikiwa ni asilimia 104.8 ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 724.1 katika kipindi hicho.

3.2.2.2.2 . Misaada na Mikopo

 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilipanga kuratibu upatikanaji wa mikopo ya jumla ya shilingi trilioni 4.99 kutoka katika soko la fedha la ndani na shilingi trilioni 3.05 kutoka katika masoko ya nje yenye masharti ya kibiashara ili kuziba nakisi ya bajeti. Hadi Aprili 2022, Wizara imefanikisha upatikanaji wa mikopo ya jumla ya shilingi trilioni

4.12 kutoka katika soko la fedha la ndani, sawa na asilimia 98.11 ya makadirio ya kukopa shilingi trilioni 4.20 katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 2.63 zimegharamia mikopo ya ndani iliyoiva na shilingi trilioni 1.49 zimegharamia miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara imefanikisha upatikanaji wa mikopo ya jumla ya shilingi trilioni 1.81 kutoka katika masoko ya nje yenye masharti ya kibiashara, sawa na asilimia 79 ya makadirio ya kukopa shilingi trilioni 2.28 katika kipindi hicho.

 1. Mheshimiwa Spika, Washirika wa Maendeleo waliahidi kuchangia katika bajeti ya Serikali ya mwaka 2021/22 shilingi trilioni 4.25, ikijumuisha misaada shilingi trilioni 1.14 na mikopo nafuu shilingi trilioni 3.11. Aidha, kati ya shilingi trilioni 4.25 zilizoahidiwa, misaada na mikopo nafuu ya kibajeti ni shilingi trilioni 1.31, Mifuko ya Pamoja ya Kisekta ni shilingi bilioni 270.4; na miradi ya maendeleo ni shilingi trilioni 2.67. 
 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, shilingi trilioni 3.93 zimepokelewa kutoka kwa Washirika wa Maendeleo, sawa na asilimia 106.1 ya makadirio ya kupokea shilingi trilioni 3.70 katika kipindi hicho. Kati ya kiasi hicho, misaada na mikopo nafuu ya bajeti ni shilingi trilioni 1.36, sawa na ufanisi wa asilimia 104.0, misaada na mikopo nafuu ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta ni shilingi bilioni 92.4, sawa na ufanisi wa asilimia 34.8 na misaada na mikopo nafuu kwa ajili ya kugharamia miradi ya maendeleo ni shilingi trilioni 2.47, sawa na ufanisi wa asilimia 116.3 ya makadirio ya kipindi hicho. Aidha, misaada na mikopo nafuu ya Mifuko ya Pamoja ya Kisekta haikufikia lengo kutokana na kutokamilika kwa wakati kwa taratibu za utoaji fedha kwa baadhi ya Washirika wa Maendeleo, kuchelewa kukamilika kwa taratibu za ununuzi kwa baadhi ya programu na baadhi ya Washirika wa Maendelo kubadilisha taratibu za utoaji fedha.  

3.2.2.2.3 Utoaji fedha, ufuatiliaji na uhakiki wa malipo, madai, malimbikizo ya mishahara na madeni 

 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, jumla ya shilingi trilioni 29.40 zimetolewa kwa ajili ya kugharamia utekelezaji wa

Mpango na Bajeti ya Serikali. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 10.61 zimetolewa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, shilingi trilioni 7.27 kwa ajili ya kuhudumia deni la Serikali, shilingi trilioni 6.73 kwa ajili ya mishahara na shilingi trilioni 4.79 kwa ajili ya matumizi mengineyo.  

 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Wizara imefanya ufuatiliaji na uhakiki wa matumizi ya fedha zilizovuka mwaka 2020/21 katika maeneo yafuatayo: Sekretarieti za Mikoa tisa (9) na Halmashauri 36; Bohari Kuu ya Dawa (MSD); Miradi ya Maji inayotekelezwa na RUWASA na Ofisi za Mamlaka za Maji za Mikoa ya Mwanza, Mbeya, Dar-es-Salaam, Shinyanga, Kagera, Arusha, Manyara na Songwe; vyuo vya kilimo; na fidia ya  Bararaba ya Mzunguko Dodoma,  Reli ya kisasa (SGR) katika njia ya kuingia Bandarini, Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Awamu ya Pili – Barabara ya Kilwa na Kiwanja cha Ndege Shinyanga, Tanga na Manyara, Kituo cha Kitaifa cha Maafa, na maeneo yanayotwaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania Kaboya (Muleba), Nyamisangura (Tarime),  Usule (Tabora) na Nyangungulu (Mwanza).
 • Mheshimiwa Spika, kati ya Julai 2021 na Aprili 2022, Wizara imefanya uhakiki wa taarifa mbalimbali za malimbikizo ya mishahara ya watumishi wa umma 76,404 ambapo  kati ya hao, 74,670 utumishi wao haujakoma na 1,734 ni wale ambao utumishi wao umekoma. Baada ya uhakiki kukamilika, jumla ya shilingi bilioni 124.32 zimelipwa kwa watumishi ambao utumishi wao haujakoma na shilingi bilioni 5.98 kwa watumishi waliostaafu. Vilevile, madeni ya jumla ya shilingi bilioni 772.87 yalihakikiwa na kulipwa. Kati ya kiasi hicho, madai ya wakandarasi ni shilingi bilioni 4.24, wazabuni shilingi bilioni 81.67, watumishi (yasiyo ya kimshahara) shilingi bilioni 25.71, watoa huduma shilingi bilioni 52.74 na madeni mengineyo shilingi bilioni 608.51.

3.2.3 Usimamizi wa Deni la Serikali

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia deni la Serikali kwa mujibu wa Sheria ya Mikopo, Dhamana na Misaada, SURA 134. Kati ya Julai 2021 na Aprili 2022, Wizara imelipa deni lote lililoiva katika kipindi hicho la jumla ya shilingi trilioni 6.81. Kati ya kiasi hicho, deni la ndani ni shilingi trilioni

4.21, ikijumuisha riba shilingi trilioni 1.72 na mtaji shiling trilioni 2.49. Aidha, deni la nje ni shilingi trilioni 2.60, ikijumuisha riba shilingi trilioni 0.572 na mtaji shilingi trilioni 2.02.

 • Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika ni kufanya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali kwa miaka 20 ijayo, kuanzia 2021/22 hadi 2040/41. Matokeo ya tathmini yanaonesha kuwa, deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda mfupi, wakati na mrefu. Aidha, Taarifa inaonesha kuwa thamani ya sasa ya deni la Serikali kwa Pato la Taifa ni asilimia 31.8 ikilinganishwa na ukomo wa asilimia 55. Napenda kuliarifu Bunge lako Tukufu, wananchi na wadau wote wa maendeleo kuwa Taarifa kamili ya tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali inapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni www.mof.go.tz.

3.2.4 Usimamizi wa Mafao ya Wastaafu na Mirathi

26. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha mfumo wa huduma ya pensheni, mirathi, utunzaji wa kumbukumbu, uhakiki wa wastaafu na ulipaji wa mafao na pensheni kwa watumishi wa Serikali ambao siyo wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii, pamoja na mirathi na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi wa Serikali walio katika mikataba na viongozi wa kisiasa. Hadi Aprili 2022, Wizara imelipa mafao na pensheni kwa wastani wa wastaafu 59,825 kila mwezi, mirathi kwa warithi 1,038, malipo ya malezi kwa walezi 1,246 na malipo ya kiinua mgongo kwa watumishi wa Serikali walio kwenye mikataba 500. Aidha, Wizara inaendelea kufanya uhakiki wa wastaafu wote wanaopata malipo ya pensheni kupitia Hazina

3.2.5 Usimamizi wa Mifumo ya Fedha na Mali za Serikali 

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilipanga kuhuisha na kufungamanisha mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha na mali za Serikali ili kudhibiti upotevu wa mapato na matumizi yasiyo ya lazima pamoja na kurahisisha upatikanaji na usuluhishi wa taarifa za fedha kwa wakati. Aidha, Wizara ilipanga kuimarisha usalama na ulinzi wa mifumo ya TEHAMA pamoja na mifumo ya usimamizi wa mapato, matumizi na mali za Serikali na kufanya uhakiki wa mali katika vituo 180 katika Taasisi za Umma, Wizara, Idara zinazojitegemea na Wakala wa Serikali, Sekretarieti za Mikoa na Serikali za Mitaa.
 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kuhuisha na kufungamanisha Mfumo wa Ulipaji Serikalini (MUSE) na mifumo ya PlanRep I (TAMISEMI), PlanRep II (Msajili wa Hazina) na GePG. Mafanikio mengine ni kufungamanisha mfumo wa GAMIS na GePG na kuunganisha watoa huduma za malipo 853, benki 28 na mitandao saba ya simu katika mfumo wa GePG.  Aidha, Wizara inaendelea kuimarisha usalama na ulinzi wa mifumo ya TEHAMA kwa kuanzisha kituo cha utafiti na usimamizi wa usalama wa mifumo ya fedha.  
 • Mheshimiwa Spika,  mafanikio mengine ni pamoja na: kufanya  ukaguzi wa mali za Serikali katika vituo 126 kwa lengo la kudhibiti na kuimarisha matumizi ya mali husika; uhakiki maalumu wa  mali na madeni ya Hospitali ya DAR Group ili kurejesha hospitali hiyo serikalini; na ukaguzi wa mali za mradi wa ECO – Village adaptation of Climatic Change in Central Zone (Eco ACT) zenye thamani ya shilingi bilioni 1.033, ikijumuisha ardhi ekari 270, majengo mawili, vyombo vya moto, mitambo na vifaa 256 ili kuzitambua na kuzigawanya kwa matumizi mengine baada ya mradi kukamilika.

3.2.6 Usimamizi wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta binafsi

30. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/22, Wizara ilipanga kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Ubia 2021/22-2025/26, kutoa ushauri wa kitaalamu kuhusu miradi inayoibuliwa na kuandaliwa na Mamlaka za Serikali na kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Mamlaka za Serikali.  Hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kuandaa Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Ubia kama ilivyopangwa na ushauri wa kitaalamu kwa miradi ya PPP 32 iliyowasilishwa na Mamlaka za Serikali za Mitaa na taasisi mbalimbali za Serikali.  Kati ya miradi hiyo, mradi wa Uendeshaji wa Mabasi Yaendayo Haraka Awamu ya Kwanza umepata mbia na maandalizi ya majadiliano ya uendeshaji wa mradi yanaendelea. Aidha, miradi minne (4) ambayo ni Ujenzi wa Hoteli ya Nyota Nne, ujenzi wa Jengo la biashara katika Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere, Ujenzi wa Kiwanda cha kuzalisha Dawa na Vifaa Tiba na Kiwanda cha Kutengeneza Simu ipo katika hatua za ununuzi; mradi mmoja (1) upo kwenye hatua ya mwisho ya upembuzi yakinifu; miradi saba (7) ipo kwenye hatua ya upembuzi yakinifu wa awali; na miradi 19 ipo katika hatua ya andiko dhana. 

3.2.7 Usimamizi wa Taasisi na Mashirika ya Umma

31. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilipanga kufanya ufuatiliaji na tathmini ya uendeshaji wa kampuni tanzu za mashirika na taasisi za umma pamoja na mashirika 120 yaliyobinafsishwa. Hadi Aprili 2022, ufuatiliaji umefanyika na kubaini kuwa mashirika na taasisi zote za Serikali zina miliki jumla ya kampuni tanzu 57. Aidha, Mfumo wa Taarifa za Fedha wa Ofisi ya Msajili wa Hazina (OTRMIS) umeboreshwa ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa za kifedha za kampuni tanzu na kurahisisha usimamizi wake. Vilevile, Mwongozo wa uanzishaji, uendeshaji na usimamizi wa kampuni tanzu za Taasisi na Mashirika ya Umma umekamilika na kuanza kutumika. Pia, ufuatiliaji na tathmini imefanyika katika mashirika 98 yaliyobinafsishwa, ikijumuisha hoteli 10, kampuni 31, mashamba 15 na viwanda 42. Matokeo ya ufuatiliaji huo yamebaini kiwango kidogo cha uzalishaji wa zao la mkonge, baadhi ya mashamba kutoendelezwa na mengine kutelekezwa. 

3.2.8 Usimamizi wa Sekta ya Fedha 

3.2.8.1 Mifumo ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha   

 • Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana na taasisi na mamlaka za usimamizi na udhibiti katika kusimamia na kuendeleza sekta ya fedha. Hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kuhuisha rasimu ya Sera ya Taifa ya Bima; kuzindua Mpango wa Kutoa Elimu ya Fedha kwa Umma wa mwaka 2020/21 – 2024/25 pamoja na nyenzo ya kufundishia; kuandaa wiki ya Huduma za Fedha kitaifa kwa lengo la kutoa elimu ya fedha kwa umma; kuandaa rasimu ya Sera ya Maendeleo ya Sekta ya Benki na Mkakati wake; kuandaa Mkakati wa Upatikanaji wa Fedha kwa

Wajasiriamali Wadogo na wa Kati; na kuzindua Mkakati wa Ugharamiaji wa Miradi ya Maendeleo kwa Njia Mbadala (Alternative Project Financing – APF Strategy).

 • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni kuandaa mapendekezo ya mabadiliko ya Sheria ya Mali

Zinazohamishika Sura 210, kwa lengo la kujumuisha masuala ya mikopo salama na masijala ya dhamana pamoja na mapendekezo ya uendelevu wa Mifuko ya Dhamana kwa Wajasiriamali Wadogo na Mauzo Nje ya Nchi (SME na Export Credit Guarantee Scheme).

3.2.8.2 Masoko ya Mitaji, Dhamana na Bidhaa

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara kupitia Masoko ya Mitaji na Dhamana ilipanga kuongeza bidhaa 38 ili kuimarisha ukwasi katika masoko ya mitaji; kuboresha kanuni za soko la hisa; kutoa leseni 150 kwa watendaji na washauri wa uwekezaji katika masoko ya mitaji; kuongeza idadi ya wataalamu wa masoko ya mitaji wanaokidhi viwango vya kimataifa kutoka 601 hadi 650; na kutoa elimu kwa umma.Hadi Aprili 2022, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana imefanikiwa kutoa leseni 154 ikilinganishwa na leseni 144 zilizotolewa katika kipindi kama hicho mwaka 2021, ikiwa ni ongezeko la asilimia 7 na kuongeza idadi ya watendaji wa masoko ya mitaji wanaotambulika kimataifa kutoka 601 hadi 667, sawa na ongezeko la asilimia 11. Aidha, idadi ya bidhaa katika masoko ya mitaji ambazo zinajumuisha hisa; hatifungani; na mifuko ya uwekezaji wa pamoja zimeongezeka kutoka 599 na kufikia 637, sawa na ongezeko la asilimia 6.
 • Mheshimiwa Spika, Soko la BidhaaTanzania – TMX lilipanga kuboresha Mfumo wa Uuzaji na Malipo kwa Njia ya

Kielektroniki, kuandaa Sera ya TEHAMA,  Sera ya usalama wa Mifumo ya TEHAMA na kuandaa miongozo ya mauzo ya bidhaa. Hadi Aprili 2022, imefanikiwa kuboresha Mfumo wa Mauzo kwa Njia ya Kielektroniki na hivyo kuwa na uwezo wa kuuza mazao zaidi ya saba; kuandaa Sera ya TEHAMA na Sera ya Usalama ya TEHAMA kama sehemu ya kulinda mifumo inayotumika katika soko la bidhaa kwa ujumla; na kuandaa miongozo ya  mauzo ya zao la chai, mifugo hai, ngozi, viazi, vitunguu na pilipili manga ambayo itaanza kutumika kuuza mazao hayo kupitia Soko la bidhaa mara baada ya maandalizi ya Stakabadhi za Ghala kukamilika.

3.2.8.3 Taasisi za Benki

36. Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusimamia taasisi za benki ili kukuza mitaji, amana na ukwasi na hivyo kuchochea kasi ya utoaji wa mikopo kwa ajili ya uwekezaji na biashara katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu kama ifuatavyo:

3.2.8.3.1 Benki Kuu ya Tanzania

 • Mheshimiwa Spika, shabaha ya ukuaji wa Pato la Taifa ilikuwa ni asilimia 5.0 mwaka 2021 na mfumuko wa bei kubaki ndani ya wigo wa kati ya asilimia 3.0 na 5.0. Ili kufikia azma hiyo, Benki Kuu ilipanga kukuza wastani wa ukuaji wa ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) kwa asilimia 10.0; ukuaji wa fedha taslimu (M0) wa wastani wa asilimia 9.9; wastani wa ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi kwa asilimia 10.6; na kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosha kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi  minne.
 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili  2022wastani wa fedha taslimu uliongezeka kwa asilimia 13.8 ikilinganishwa na asilimia 2.7 katika kipindi kama hicho mwaka 2021;  ujazi  wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ulikua kwa wastani wa asilimia 13.1 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 6.8 katika kipindi kama hicho mwaka 2021; na ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi uliongezeka na kufikia wastani wa asilimia 8.4 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.3 kwa mwaka 2021.

Aidha, akiba za fedha za kigeni ilifikia dola za Marekani bilioni 5.46 kiasi ambacho kinatosheleza uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi cha miezi 4.8 ikilinganishwa na lengo la nchi la miezi 4.0 na miezi isiyopungua 4.5 kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

3.2.8.3.2 Benki za Maendeleo

 • Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamiabenki mbili (2) za maendeleo ambazo ni Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania – TADB na Benki ya Maendeleo TIB.  Kwa mwaka 2021/22, TADB ilipanga kutoa mikopo ya kiasi cha shilingi bilioni 203.50 kwa miradi ya uchakataji wa mazao, ununuzi wa mazao, ununuzi wa pembejeo, uwezeshaji wa wakulima wadogo kupitia vyama vya msingi (AMCOS); ununuzi wa zana za kilimo; kutoa dhamana kwa wakulima wadogo na SMEs; na kufungua Ofisi ya Kanda ya kusini na ofisi ndogo Morogoro. Hadi Aprili 2022, TADB imetoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 116.36 kwa miradi 181 iliyowanufaisha wakulima wadogo, wa kati na wakubwa 1,527,175 na kufanya jumla ya mikopo iliyotolewa toka benki ilipoanza kufikia shilingi bilioni 364.50. 
 • Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa na TADB ni pamoja na: kutoa mikopo ya shilingi bilioni 54.37 kupitia Mfuko wa Dhamana kwa Wakulima Wadogo (SCGS) na kufanya mikopo iliyotolewa na mfuko huo kufikia shilingi bilioni 144.04 tangu ulipoanza rasmi udhamini wa mikopo mwaka 2018. Mikopo hiyo imewanufaisha wakulima 987, biashara ndogo na za kati za kilimo (SMEs), na vyama vya msingi (AMCOS) katika mikoa 26 nchini. Vilevile, TADB imefungua Ofisi ya kanda ya Kusini iliyopo mkoani Mtwara na Ofisi ndogo Mkoani Morogoro. Ofisi ya Kanda ya Kusini itahudumia Mikoa ya Mtwara, Lindi na Ruvuma.
 • Mheshimiwa Spika, benki ya Maendeleo TIB  ilipanga kutoa mikopo ya shilingi bilioni 54.59 katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, nishati, utalii, na elimu; na kukuza mizania ya benki kufikia shilingi 775.5. Hadi Aprili 2022, Benki ya Maendeleo TIB imefanikiwa kutoa mikopo ya jumla ya shilingi bilioni 17.91. Sekta zilizonufaika na mikopo hiyo ni maji, utalii, madini ya dhahabu na ujenzi. Aidha mizania ya benki ilikua na kufikia shilingi bilioni 625.78.

3.2.8.3.3 Benki ya TCB

42. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Benki ya TCB ilipanga kuboresha mifumo ya benki ya kuzalisha mapato na utoaji huduma. Hadi Aprili 2022, benki imefungua akaunti 29,488 za vikundi vya kawaida na kusajili vikundi 43,236 kupitia simu za mkononi kwa kushirikiana na Vodacom.  Aidha, benki imebuni mradi wa vikundi vilivyombali na huduma za kifedha, ambapo jumla ya akaunti 16,558 zimefunguliwa. Vilevile, benki imefanikiwa kukusanya amana zenye thamani ya shilingi bilioni 937 na kutoa mikopo ya shilingi bilioni 736, ambapo shilingi bilioni 1.4 ni mikopo kwa vikundi vya wajasiriamali.

3.2.8.3.4 Taasisi za Bima

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bima – TIRA ilipanga kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kusimamia vipindi 10 vya redio vya utoaji elimu na kutoa elimu kwa makundi maalumu ya Bodaboda, Bajaji, Vyama vya wafanyabiashara, vyama vya wasafirishaji pamoja na Jeshi la Polisi. Hadi Aprili 2022,TIRA imefanya ukaguzi wa vyombo vya moto barabarani 19,221;  kutoa elimu ya bima kwa umma kupitia vipindi 9 vya redio na luninga na makundi mbalimbali ya kijamii ambapo zaidi ya wananchi 514,112 wamefikiwa. Kati ya hao,  3,214 ni askari polisi wa usalama barabarani, 344 watumishi wa Serikali, 75 waandishi wa habari na watumishi wa vyombo vya Habari na 510,479 madereva wa bodaboda, watu wenye ulemavu wa usikivu, wakulima na vyama vya ushirika.
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Shirika la Bima la Taifa lilipanga kujenga mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Taarifa za Bima ili kuweka mazingira wezeshi na shindani. Hadi Aprili 2022, Shirika limefanikiwa kuanza kuunda na kujenga Mfumo wa Kielektroniki wa Usimamizi wa Taarifa za Bima na kuanza kusimika mfumo wa Enterprise Resource Management System (ERMS) kwa ajili ya kusimamia taarifa za kihasibu. Mifumo hiyo kwa pamoja inatarajiwa kuongeza ufanisi na uwazi katika utunzaji wa taarifa za wateja, ulipaji wa madai, utunzaji sahihi wa taarifa za kihasibu pamoja na kuwezesha wateja kukata bima na kuwasilisha madai yao kwa njia ya kielektroniki.

3.2.8.3.5 Taasisi za Uwekezaji na Uwezeshaji

 • Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia taasisi mbili (2) za Uwekezaji na Uwezeshaji ambazo ni Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja – UTT AMIS na Mfuko wa Huduma Ndogo za Fedha (Self Microfinace Fund). Katika mwaka 2021/22, UTT AMIS ilipanga kuongeza rasilimali za mifuko kwa asilimia 15, kuongeza idadi ya wawekezaji kwa asilimia tano (5) na kutoa huduma kwa wawekezaji kwa kutumia mifumo ya kidijitali. Hadi Aprili 2022, UTT AMIS ilifanikiwa kuongeza rasilimali za mifuko pamoja na huduma ya usimamizi wa mitaji binafsi kutoka shilingi bilioni 619.57 mwezi Julai 2021 hadi shilingi bilioni 927.45 mwezi Aprili 2022, sawa na ongezeko la asilimia 49.69. Katika kipindi hicho, idadi ya wawekezaji katika mifuko iliongezeka kutoka 172,242 hadi 194,632, sawa na ongezeko la asilimia 12.99. Kutokana na maboresho ya mifumo ya TEHAMA, asilimia 46.10 ya mauzo ya vipande katika  kipindi hicho yalifanyika kwa njia ya kidijitali.
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Mfuko wa  Huduma Ndogo za Fedha – SELF ulipanga kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 34.32 kwa wajasiriamali wadogo 17,852 na kutoa mafunzo kwa wajasiriamali wadogo wapatao 265. Hadi Aprili 2021, Mfuko umetoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 32.97, sawa na asilimia 96 ya lengo na kunufaisha wajasiriamali wadogo 13,744 na kutoa mafunzo kwa  wajasiriamli wadogo 2,397.

3.2.6     Taasisi za Mafunzo, Elimu ya Juu na Bodi za Kitaaluma

47. Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia Taasisi za mafunzo ya elimu ya juu na bodi za kitaaluma kwa lengo la kuendeleza wataalamu na kufanya tafiti katika fani ya fedha na uhasibu, mipango, takwimu, ununuzi na ugavi na kutoa ushauri wa kitaalamu katika masuala yanayohusu fani hizo. Taasisi hizo ni: Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP; Chuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM; Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC; Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA; Chuo cha Uhasibu Arusha – IAA; Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi – PSPTB na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA.

3.2.6.1 Taasisi za Mfunzo na Elimu ya Juu

3.2.6.1.1 Chuo cha Usimamizi wa Fedha

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Chuo cha Usimamizi wa Fedha kilipanga kutekeleza yafuatayo: Kudahili wanafunzi 14,500; kujenga uwezo wa Chuo wa kutoa huduma elekezi; kuendelea na ujenzi wa Kampasi za Kanda ya Ziwa – Simiyu na Chato na kuendeleza kampasi ya Mwanza. Hadi Aprili 2022, Chuo kimedahili wanafunzi 15,528, sawa na asilimia 107 ya lengo; kuwezesha wahadhiri kuchapisha jumla ya tafiti 18; na kutoa huduma elekezi nne (4) zenye thamani ya shilingi milioni 136.50 kwa taasisi mbalimbali, ikiwemo taasisi za Serikali. 
 • Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo,Chuo kimekamilisha ujenzi wa majengo manne (4) katika Kampasi ya Chato mkoani Geita, ikiwemo Jengo la Utawala, Madarasa, Bwalo la Chakula na Ukumbi wa Mihadhara, ambapo ujenzi wa kampasi hiyo umefikia asilimia 78. Aidha, Chuo kimefanikiwa kununua ekari 37.42 katika eneo la Kiseke kwa ajili ya kampasi ya Mwanza, ambapo ujenzi umeanza kwa jengo la ghorofa nne (4) litakalokuwa na ofisi, madarasa, maabara ya kompyuta na maktaba.

3.2.6.1.2  Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini kilipanga kudahili wanafunzi 15,011 katika kozi 27 za muda mrefu; kutoa udhamini wa masomo kwa watumishi katika ngazi ya uzamili na uzamivu; na kuanza ujenzi wa jengo la ukumbi wa mihadhara na bweni la wanafunzi katika kampasi ya Kanda ya Ziwa (Kisesa) – Mwanza. Hadi Aprili 2022, Chuo kimefanikiwa kudahili jumla ya wanafunzi 14,417, sawa na asilimia 96 ya lengo. Aidha, Chuo kimetoa udhamini wa masomo kwa watumishi 62 ambapo kati ya hao, 34 ni ngazi ya uzamivu, 16 uzamili, nane (8) shahada na wanne (4) stashahada. Vilevile, Chuo kimefanikiwa kufanya tafiti 7 katika masuala ya ukuaji wa uchumi na hali ya umaskini; usambazaji wa umeme vijijini na maendeleo ya viwanda vidogo; mchango na uhusiano wa kijinsia katika upatikanaji wa maji vijijini; na shughuli za ujasiliamali vijijini. 
 • Mheshimiwa Spika, kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Chuo kinaendelea na ujenzi wa ukumbi wa mihadhara na bweni la wanafunzi katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa (Kisesa) – Mwanza. Hadi Aprili 2022, ujenzi wa ukumbi wa mihadhara umefikia asilimia 80 na bweni la wanafunzi asilimia 20. Aidha, katika kipindi hicho, Chuo kimekamilisha ujenzi wa jengo la maktaba, jengo la utawala na bwalo la chakula katika Kampasi ya Kanda ya Ziwa, Kisesa.

3.2.6.1.3    Chuo cha Uhasibu Arusha – IAA

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Chuo cha Uhasibu Arusha- IAA kilipanga kudahili jumla ya wanafunzi 9,870, ikiwemo ngazi ya cheti 2,646, stashahada 2,678, shahada 3,767 na uzamili 779. Aidha, Chuo kilipanga kuendeleza shughuli za utafiti pamoja na mafunzo kwa watumishi, kutoa huduma za ushauri wa kitaalamu na

kukamilisha ujenzi wa vyumba vya   madarasa   vyenye   uwezo   wa   kuhudumia wanafunzi 4,800 katika kampasi kuu Arusha, mabweni manne (4), jengo la uzamili, ujenzi wa madarasa na jengo la utawala katika kampasi ya Babati.

 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 7,483, sawa na ufanisi wa asilimia 75.8, ambapo ngazi ya cheti wamedahiliwa wanafunzi 2,646, stashahada wanafunzi 1,762, shahada wanafunzi 2,160 na shahada ya uzamili 915. Kuhusu utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Chuo kimekamilisha ujenzi wa madarasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 4,800 katika kampasi kuu Arusha. 

3.2.6.1.4  Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Taasisi ya Uhasibu Tanzania ilipanga kudahili jumla ya wanafunzi 24,866 na kuendeleza ujenzi na ukarabati wa majengo mbalimbali ya Taasisi katika kampasi kuu Dar es Salaam, Mtwara, Mbeya na Mwanza. Hadi Aprili 2022, Taasisi imefanikiwa kudahili jumla ya wanafunzi 23,621, sawa na ufanisi wa asilimia 95, ambapo ngazi ya cheti wamedahiliwa wanafunzi 4,954, ngazi ya stashahada 7,499, shahada11,106, stashahada ya uzamili 10 na shahada ya uzamili 52. 
 • Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Taasisi imekamilisha ujenzi wa jengo la taaluma na kuendelea na ukarabati wa jengo la utawala kampasi ya Makao Makuu, Dar es salaam, kuendelea na ujenzi wa hosteli mbili (2), vyumba vinne (4) vya madarasa, nyumba moja (1) ya wafanyakazi, maktaba moja (1) na maabara moja (1) ya kompyuta katika kampasi ya Mtwara na kuanza ujenzi wa jengo la taaluma linalojumuisha maabara ya kompyuta, maktaba na ofisi za utawala katika kampasi ya Mwanza. 

3.2.6.1.5  Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika – EASTC

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika kilipanga kudahili jumla ya wanafunzi 500, kuendeleza wahadhiri 37, kutoa mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji ya wadau, kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunza, kupitia upya na kutengeneza mitaala mipya ya programu za chuo na kuboresha mfumo wa kutoa mafunzo kwa njia ya masafa au kidijitali.  
 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Chuo kimefanikiwa kudahili jumla ya wanafunzi 439, sawa na ufanisi wa asilimia 88, ambapo ngazi ya astashahada wamedahiliwa wanafunzi 38, stashahada 106, shahada 267 na 26 katika ngazi ya uzamili. Aidha, katika kipindi hicho, Chuo kimetoa udhamini wa masomo kwa wahadhiri 37, kuboresha miundombinu ya madarasa kwa kufunga viti vyenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 180 badala ya wanafunzi 80 wa awali, kukamilisha maandalizi ya mitaala mipya kwa ngazi ya cheti, Stashahada na Shahada ili kukidhi mahitaji ya muda wa kati na mrefu ya wataalamu wa fani ya takwimu rasmi, uchumi na TEHAMA na kuanza kutoa mafunzo kwa njia ya mtandao kwa waalimu na wanafunzi.

3.2.6.2  Bodi za Kitaaluma na Kitaalamu

 • Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia Bodi mbili (2) za kitaaluma na kitaalamu ambazo ni Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi – PSPTB naBodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA. Katika mwaka 2021/22, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi ilipanga kudahili watahiniwa 4,000 na kuendesha mitihani ya kitaaluma na kitaalamu, kujenga uwezo wa wataalamu, kutoa ushauri elekezi na huduma za kiufundi, kusimamia ubora wa kazi za wataalamu na wanataaluma pamoja na kufanya usajili wa wataalamu wa fani ya Ununuzi na Ugavi. Hadi Aprili 2022, PSPTB imefanikiwa kudahili watahiniwa 1,376 katika ngazi mbalimbali za mitihani, kuwajengea uwezo wataalamu 1,185 katika fani ya ununuzi na ugavi na kusajili wataalamu 1,444 wa ununuzi na ugavi katika ngazi mbalimbali za kitaalamu.
 • Mheshimiwa Spika, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu – NBAA ilipanga kudahili watahiniwa 11,720, kufanya ukaguzi kwa taasisi 75 kuhusu uandaaji wa taarifa za fedha, kuendesha semina 30 na kutoa mafunzo ya diploma ya viwango vya uandaaji wa taarifa kwa watahiniwa 460. Hadi Aprili 2022, Bodi ilifanya ukaguzi wa ubora wa uandaaji wa taarifa za fedha katika taasisi 81, kuendesha semina 21 kwa taasisi za Serikali, asasi za kiraia na sekta binafsi kuhusu matumizi vya viwango vya kimataifa (IPSAS na IFRS) katika utayarishaji na ukaguzi wa taarifa za fedha, kutunga, kusimamia na kusahihisha mitihani kwa watahiniwa 7,008, ambapo 44 walifaulu mitihani ya Cheti cha Utunzaji wa Hesabu na 428 Shahada ya Juu ya Uhasibu na kutoa mafunzo ya diploma ya viwango vya uandaaji wa taarifa za fedha serikalini kwa wahitimu 178.
 • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ya NBAA ni pamoja na: Kutoa ushauri elekezi na huduma za kiufundi kwa taasisi za umma na binafsi 12 Tanzania Bara; kufanya ukaguzi wa kampuni 50 za uandaaji na ukaguzi wa hesabu; na kusajili watunza vitabu wawili (2), wahasibu wahitimu 622 waliopata uzoefu wa kazi, wahasibu 85 ngazi ya ACPA, wakaguzi hesabu 36 katika ngazi ya CPA-PP, kampuni tatu (3) za ukaguzi wa hesabu na kampuni moja (1) ya uhasibu.

           3.2.7         Usimamizi wa Kodi na Rufaa za kodi

61. Mheshimiwa Spika, Wizara inasimamia taasisi moja (1) ya ukusanyaji wa mapato ya kodi na taasisi mbili (2) za usimamizi na utatuzi wa mashauri ya kodi. Taasisi hizo ni Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA, Bodi ya Rufaa za Kodi- TRAB na Baraza la Rufaa za Kodi-TRAT.

3.2.7.1     Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania ilipanga kuanzisha mfumo wa ukaguzi wa mizigo uliofungamanishwa wa

“Scanner”, kujenga Mfumo wa Kielektroniki wa Dirisha Moja la Forodha, kujenga Mfumo Unganifu wa Kusimamia Mapato ya Ndani na kujenga Mfumo wa Utoaji Taarifa za Mrejesho kwa Walipakodi.

 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, TRA imefanikiwa kujenga mfumo uliofungamanishwa na Scanner na kuunganishwa na mfumo wa TANCIS. Mfumo huo unatumika katika uondoshaji wa mizigo katika bandari ya Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.  Aidha, scanner nne (4) zimesimikwa katika Bandari ya Dar es Salaam na mbili (2) katika Bandari ya Tanga. Vilevile, Mamlaka imefanikiwa kujenga Mfumo wa Kielektroniki wa Dirisha Moja na kuunganisha mawakala wa forodha 545 pamoja na Taasisi za Udhibiti nne (4), ambapo hadi sasa unatumika katika Bandari ya Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere. 
 • Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizotekelezwa na TRA ni pamoja na: Kuendelea na ujenzi wa mfumo Unganifu wa Kusimamia Mapato ya Ndani (Integrated Domestic Tax Administration System – IDRAS) ili kurahisisha au kuwezesha uwasilishaji wa ritani za kodi, makisio ya kodi na malipo ya kodi.  Aidha, moduli za Usimamizi wa Madeni na Kodi ya Ongezeko la Thamani -VAT ziko katika hatua mbalimbali za uundwaji. Vilevile, Mfumo wa Utoaji Taarifa za Mrejesho kwa Walipakodi umekamilika na mafunzo yametolewa kwa wataalamu 201 kuhusu matumizi ya mfumo huo. Mfumo huo umeonesha mafanikio makubwa baada ya kufanyiwa majaribio katika Mikoa ya Geita na Njombe.

 3.2.7.2 Bodi ya Rufaa za Kodi – TRAB

65. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Bodi ya Rufaa za Kodi ilipanga kusikiliza mashauri ya kodi kwa wakati ili kuiwezesha Serikali kufanikisha azma yake ya kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara. Hadi Aprili 2022, Bodi imesajili maombi mapya 36 na mashauri mapya 394. Aidha, katika kipindi hicho, Bodi imesikiliza na kutolea maamuzi jumla ya maombi 65 na mashauri 510. 

3.2.7.3 Baraza la Rufani za Kodi – TRAT

66. Mheshimiwa Spika,Baraza la Rufani za Kodi – TRAT lilipanga kusikiliza na kutolea maamuzi rufaa zote za kodi, kuandaa Mfumo wa Takwimu za Mashauri na kuchapisha vitabu vya rejea kwa kesi zilizoamuliwa kuanzia mwaka 2013 hadi 2020. Hadi Aprili, 2022, Baraza limefanikiwa kusikiliza mashauri 161 na kutolea maamuzi mashauri 142.  Aidha, Mfumo wa Takwimu za Mashauri umekamilika na zoezi la kuchambua takwimu kwa ajili ya kuziingiza kwenye mfumo linaendelea. Vilevile, uchambuzi wa mashauri yaliyotolewa maamuzi mwaka 2013 umekamilika na kupelekwa kwa Mhariri kwa hatua ya uchapishaji.

3.2.8 Usimamizi wa Masuala ya Pamoja ya Fedha kati ya Tanzania Bara na Zanzibar

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Tume ya Pamoja ya Fedha ilipanga kufanya stadi za masuala ya fedha ya pamoja kati ya Tanzania Bara na Zanzibar na kutoa ushauri stahiki kwa pande zote za Muungano. Hadi Aprili 2022, Wizara kupitia Tume imefanya Stadi kuhusu ukusanyaji wa mapato ya Muungano katika huduma za mawasiliano ya simu, fedha na bima kwa kampuni zilizosajiliwa upande mmoja wa Muungano na kufanya biashara katika pande mbili za Muungano. 
 • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni pamoja na uchambuzi wa takwimu za mapato na matumizi yanayohusu utekelezaji wa shughuli za Muungano kwa kipindi cha mwaka 2012/13 hadi 2021/22. Uchambuzi huo umeonesha kuwa, matumizi ya Muungano yalikuwa ya wastani wa asilimia 25.4 ikilinganishwa na matumizi ya Serikali (SMT). Aidha, uwiano wa mapato ya Muungano na mapato ya ndani ya SMT kwa kipindi cha kuanzia 2012/13 hadi 2021/22 yalikuwa ya wastani wa asilimia 49.8 na asilimia 35.8 kwa SMZ. Vilevile, Tume imetoa elimu kwa wadau kuhusu masuala ya uhusiano wa kifedha kati ya SMT na SMZ. Wadau waliopewa elimu hiyo ni wataalamu kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ya SMT na wajumbe wa Baraza la Mapinduzi la Zanzibar, Makatibu Wakuu wa Wizara na Wakuu wa Taasisi za SMZ.

3.2.9 Michezo ya kubahatisha

69. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha ilipanga kutoa leseni 11,367 kwa waendesha michezo ya kubahatisha, ambapo kati ya hizo 7,408 ni leseni mpya na 3,959 ni leseni zitakazohuishwa na kufanya ukaguzi kwa waendesha michezo ya kubahatisha 76  waliosajiliwa ili kudhibiti uvunjifu wa sheria na taratibu. Hadi Aprili 2022, Bodi imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 6,974, ambapo leseni 4,799 ni mpya na 2,175 zimehuishwa. Vilevile, Bodi imeweza kufanya ukaguzi kwa waendesha michezo ya kubahatisha 65 na kuunganisha mifumo ya michezo ya kubahatisha na mfumo wa GEPG, BRELA na mifumo ya Mamlaka ya Mapato Tanzania -TRA.

3.2.10 Udhibiti wa Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi  

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara kupitiaKitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi ilipanga kuendelea kupokea na kuchambua taarifa za miamala shuku, fedha taslimu, utumaji na upokeaji wa fedha kwa njia za kielektroniki, usafirishaji wa fedha taslimu na hati za malipo kutoka na kuingia nchini kupitia mipakani, kuwasilisha taarifa fiche kwenye vyombo vinavyosimamia utekelezaji wa sheria na kushirikiana na wadau katika kuimarisha mifumo ya kupambana na utakasishaji wa fedha haramu na ufadhili wa ugaidi na ufadhili wa silaha za maangamizi. Hadi Aprili 2022, Kitengo kilipokea na kuchambua taarifa fiche 658 za miamala shuku yenye thamani ya shilingi trilioni 1.568, taarifa 4,301 za fedha taslimu zenye thamani ya shilingi trilioni 36.15, taarifa 8,350 za usafirishaji fedha kwa njia ya kielektroniki zenye thamani ya shilingi trilioni 86.35 na taarifa 2,332 zenye thamani ya shilingi trilioni 2.482 zinazohusu usafirishaji wa fedha taslimu na hati za malipo kupitia mipakani. Aidha, taarifa fiche 32 ziliwasilishwa kwenye taasisi za utekelezaji wa sheria.
 • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni pamoja na: Kukamilisha marekebisho ya Sheria ya Kudhibiti Fedha Haramu, SURA 423; kufanya ukaguzi kwa waendesha michezo ya kubahatisha 8 na Kasino 4 juu ya utekelezaji wa matakwa ya Sheria ya Udhibiti Utakasishaji Fedha Haramu na Ufadhili wa Ugaidi; kuandaa miongozo ya usimamizi wa sekta ya bima na sekta ya masoko na mitaji ya dhamana; na kuunganisha server za Mamlaka ya Usajili wa Matukio ya Kijamii ya Zanzibar na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa ili kubadilishana taarifa kwa urahisi na uharaka.

            3.2.11        Taasisi za Ununuzi wa Umma 

 • Mheshimiwa Spika, Wizara inajukumu la kusimamia na kudhibiti tasnia ya Ununuzi wa Umma na Ugavi kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Ununuzi wa Umma – PPRA, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini – GPSA na  Mamlaka ya Rufaa za Zabuni za Umma – PPAA.
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini ulipanga kusimika Mfumo wa Kielektroniki wa Uratibu wa Ununuzi wa Magari ya Serikali na kujenga matenki manne katika mikoa ya Shinyanga, Tabora, Kagera na Morogoro na kukarabati matenki mawili katika mikoa ya Mwanza na Tanga. Hadi Aprili 2022, Wakala umefanikiwa kuunda Mfumo wa Kielektroniki wa Uratibu wa Ununuzi wa Magari ya Serikali, ugomboaji na uondoshwaji, pamoja na mfumo wa utoaji wa hati za madai, usimamizi na udhibiti wa vifaa na maghala (GIMIS), ambao umeanza kutumika rasmi Machi 2022. Aidha, Wakala umekamilisha Ujenzi wa matanki mawili (2) yenye uwezo wa kuhifadhi lita 40,000 za mafuta kila moja katika mikoa ya Tabora na Kagera na ujenzi unaendelea katika mikoa ya Lindi, Geita na Morogoro. Vilevile, wakala umekarabati matanki mawili katika mikoa ya Tanga na Mwanza.
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ilipanga kufanya ukaguzi wa ununuzi katika taasisi 180, kutoa mafunzo kwa watumishi 1,200 kutoka kwa taasisi nunuzi 300 ambao wamesajiliwa katika mfumo wa ununuzi (TANePS) na kufuatilia uzingatiaji kwa taasisi nunuzi 120. Hadi Aprili 2022, PPRA imetoa mafunzo ya matumizi ya mfumo kwa watumishi 736, ambapo jumla ya Taasisi Nunuzi 530 zimeunganishwa na mfumo, kuunganisha wazabuni 26,691 kwenye Mfumo wa TANePS, kutoa mafunzo maalumu ya Sheria ya Ununuzi, SURA 410 kwa watumishi 346 kutoka Taasisi  Nunuzi 11 na kuandaa warsha saba (7) kuhusu ununuzi wa umma, ambapo jumla ya washiriki 575 kutoka Taasisi Nunuzi walihudhuria. Aidha, Mamlaka ilifanya kaguzi za ununuzi kwa Taasisi Nunuzi 105 kwa miamala iliyofanyika mwaka 2020/21. 
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Mamlaka ya Rufaa za Zabuni – PPAA ilipanga kusikiliza na kutolea maamuzi rufaa 30 pamoja na kuendelea kuimarisha utawala bora katika masuala ya ununuzi wa umma. Hadi Aprili 2022, Mamlaka imepokea jumla ya mashauri 30 ambayo ni sawa na asilimia 100 ya rufaa zilizokadiriwa kwa mwaka. Mashauri 22 yaliyowasilishwa yamesikilizwa na kutolewa maamuzi ndani ya kipindi cha siku 45 zilizowekwa kisheria, mashauri manne (4) yako katika hatua ya kusikilizwa na mashauri manne (4) yaliondolewa na walalamikaji. 

            3.2.12        Usimamizi wa Takwimu Rasmi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Ofisi ya Taifa ya Takwimu ilipanga kuendelea na zoezi la kutenga maeneo ya kuhesabia watu wakati wa Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 2022. Shabaha nyingine ni kutoa takwimu za Pato la Taifa za robo mwaka na takwimu za mfumuko wa bei kila mwezi. Hadi Aprili 2022, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imefanikiwa kuandaa na kutoa takwimu za Pato la Taifa za mwezi Julai hadi Desemba 2021 na mfumuko wa bei hadi Machi 2022.  
 • Mheshimiwa Spika, Ofisi ya Taifa ya Takwimu imekamilisha kazi ya kutenga maeneo ya kuhesabia watu kwa Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar ambapo vitongoji vyote 64,318 na mitaa 4,670 Tanzania Bara imetengwa, ikiwa ni ufanisi wa asilimia 100. Aidha, jumla ya maeneo ya kuhesabia watu 4,313 kutoka katika Shehia zote 388 yametengwa kwa upande wa Zanzibar, sawa na asilimia 100 ya lengo. Kazi nyingine zilizokamilika ni kuandaa madodoso ya Sensa ya Watu na Makazi, Sensa ya Majengo na Sensa ya Anwani za Makazi, miongozo na fomu za kudhibiti ubora; kuandaa mfumo wa ufuatiliaji (census Dash Board), kufanya Sensa ya Majaribio Agosti, 2021 katika mikoa 18 ya Tanzania Bara na Zanzibar na kuendelea na taratibu za ununuzi wa vifaa vya Sensa.

                3.2.6     Utekelezaji wa Maagizo ya Serikali

78. Mheshimiwa Spika, kama utakavyokumbuka, Serikali ilitoa maagizo kwa Wizara na taasisi za kisekta kutafsiri sheria zote katika lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wa kawaida kusoma na kushiriki ipasavyo katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa. Hadi Aprili 2022, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imefanikiwa kutafsiri jumla ya sheria 20 zinazohusiana na masuala ya fedha, takwimu, ununuzi na ugavi, kodi, bima, michezo ya kubahatisha, ukaguzi, masoko ya mitaji na dhamana, forodha na mafunzo kwa taasisi za elimu za Wizara. 

3.2.7    Usimamizi wa Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma

79. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22, Wizara ilipanga kufanya tathmini ya utekelezaji wa Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma Awamu ya Tano -PFMRP V inayotarajiwa kufikia ukomo Juni 30, 2022 na kuandaa Mpango Mkakati wa Awamu ya Sita. Hadi Aprili 2022, Wizara imefanikiwa kukamilisha tathmini ya Programu na kuandaa Mpango Mkakati wa Awamu ya Sita ambao utekelezaji wake unatarajiwa kuanza mwaka 2022/23. Aidha, katika kipindi hicho, Wizara  kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo imefanikiwa kuratibu zoezi la Tathmini ya Nchi kuhusu Uwajibikaji katika Usimamizi wa Fedha za Umma. Matokeo ya tathmini hiyo yanaonesha kuimarika kwa mifumo ya usimamizi wa fedha za umma, hususan katika eneo la uchambuzi, udhibiti, utekelezaji na usimamizi wa bajeti na mali za Serikali.

                3.2.8    Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi ilipanga kukagua mapato na matumizi ya mafungu yote ya Serikali Kuu, ikiwemo mafungu 66, wakala 31 na balozi 42. Kazi nyingine ni kufanya ukaguzi wa Mamlaka ya Serikali za Mitaa 185, Mikoa 26 na Mashirika ya Umma 192, kufanya kaguzi za Ufanisi 12 na kaguzi 8 za kiufundi, kufanya ukaguzi wa kina wa usimamizi wa Mikataba ya ujenzi katika Mamlaka 37 za Serikali za Mitaa, kukagua Miradi ya Maendeleo 442 inayotekelezwa kwa fedha za ndani pamoja na Washirika wa Maendeleo na kufanya kaguzi maalumu 15 katika maeneo au miradi mahsusi.
 • Mheshimiwa Spika, hadi Aprili 2022, Ofisi ya Taifa ya

Ukaguzi imefanikiwa kufanya ukaguzi kwa Wizara, Idara za Zinazojitegemea 66; Wakala 31; Hospitali za Rufaa na Maalumu 33; Mifuko Maalumu ya Serikali 17; Mamlaka za Maji (Daraja C) pamoja na mabonde ya maji 29; Taasisi za Serikali 64; Balozi 43; Mikoa 26; Mamlaka 185 za Serikali za Mitaa; Mashirika ya Umma 195; na ukaguzi wa Vyama vya Siasa 19 vyenye usajili wa kudumu. Aidha, Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi imefanikiwa kufanya kaguzi 12 za ufanisi na 8 za kiufundi. Pia, jumla ya kaguzi maalum 56 zimefanyika, ambapo 37 ni kwenye Mamlaka ya Serikali za Mitaa, 12 Serikali Kuu, 6 Mashirika ya Umma na Moja kwenye Mifumo ya Tehama. 

 • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ni kufanya ukaguzi kwa Miradi ya Maendeleo 302, ikijumuisha Miradi 199 chini ya Sekta ya Afya, 11 Sekta ya Elimu, 16 Sekta ya Usafirishaji, 19 Sekta ya Nishati na Madini, 14 Sekta ya Jamii, 11 Sekta ya Maji na 32 kutoka katika sekta nyingine. Aidha, ulifanyika ukaguzi wa kina wa usimamizi wa mikataba ya RUWASA katika Mikoa 25.

3.3 Changamoto na Mikakati ya Kukabiliana nazo

3.3.1 Changamoto

83. Mheshimiwa Spika, pamoja mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara pamoja na taasisi zake, changamoto zifuatazo zilijitokeza:

 1. kuvurugika kwa mfumo na mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia kutokana na athari za UVIKO-19 na vita baina ya Urusi na Ukraine na hivyo kusababisha ongezeko la mfumuko wa bei katika soko la ndani pamoja na kasi ndogo ya ukuaji wa Pato la Taifa;  
 2. kusitishwa kwa baadhi ya mikataba ya ununuzi na ugavi wa vitendea kazi, hususan magari kutokana na athari za

UVIKO – 19; iii) kasi kubwa ya mabadiliko ya teknolojia ya habari na mawasiliano ikilinganishwa na uwezo wa ndani wa kuimarisha na kujenga mifumo ya TEHAMA pamoja na mifumo ya kielektroniki ya usimamizi wa fedha; na

iv) kuongezeka kwa gharama za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ununuzi wa vitendea kazi kutokana na athari za mfumuko wa bei na hivyo kuathiri utekelezaji wa Mpango na Bajeti iliyoidhinishwa na Bunge.

3.3.2 Mikakati ya Kukabiliana na Changamoto

84. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea kuchukua hatua zifuatazo katika kukabiliana na changamoto zilizojitokeza:

 1. kuchukua hatua za kisera, hususan kutoa ruzuku kwa bidhaa za petroli ili kupunguza kasi ya ongezeko la mfumuko wa bei na gharama za maisha;
 1. kuhamasisha uzalishaji na matumizi ya baadhi ya mazao kama njia mbadala kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, hususan ngano na mafuta ya kula ili kudhibiti msukumo wa mfumuko wa bei kutoka nje;
 1. kufanya mazungumzo na wazalishaji na wauzaji mbalimbali wa magari na mitambo ili kuepuka au kupunguza athari zinazoweza kujitokeza; 
 1. kuongeza uwekezaji katika ujuzi na utafiti wa masuala ya TEHAMA na mifumo ya kielektroniki ili kupunguza athari za utegemezi wa mifumo ya nje; na
 • kutoa kipaumbele kwa majukumu au kazi zenye maslahi mapana kwa Taifa, hususan miradi ya maendeleo na matumizi yaliyolindwa.

4.0 VIPAUMBELE KWA MWAKA 2022/23

4.1 Vipaumbele vya Wizara

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Wizara ya Fedha na Mipango kupitia mafungu yake nane (8) inatarajia kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia malengo, shabaha na vipaumbele vilivyoainishwa katika Mpango wa Matumizi wa Muda wa Kati (MTEF) wa kila Fungu na Taasisi zake. Aidha, malengo, shabaha na vipaumbele vya Mpango na Bajeti ya mwaka 2022/23 vimeibuliwa kutoka kwenye Mpango Mkakati wa Wizara 2021/22 – 2025/26, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26 na Ilani ya Chama Tawala – CCM kama ifuatavyo:
  • kukusanya, kutafuta na kudhibiti mapato na

matumizi ya Serikali;

 1. kuhudumia kwa wakati deni la Serikali pindi

linapoiva; 

 1. kufanya tathmini ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 ikiwa ni maandalizi mahsusi ya Dira Mpya ya

Taifa ya Maendeleo 2050; iv) kufanya tathmini ya mfumo na muundo wa ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa miradi ya Maendeleo ili kuwezesha kutungwa kwa Sera ya Taifa ya

Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi ya Maendeleo;

 • kurejesha Bahati Nasibu ya Taifa;
  • kufanya tafiti katika sekta za uzalishaji ili kuibua fursa za uwekezaji, uwezeshaji na vyanzo vya mapato ya Serikali katika muda mfupi, kati na mrefu; 
  • kuendelea kutekeleza maagizo ya Serikali ya kutafsiri sheria za Wizara na taasisi zake kwa lugha ya Kiswahili; na
  • kuhuisha Mwongozo wa Taifa wa Usimamizi wa

Viashiria Hatarishi.

 • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa matumizi ya maendeleo, Wizara inatarajia kujielekeza katika maeneo yafuatayo: 
  • kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kupitia Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa

Fedha za Umma Awamu ya Sita (PFMRP VI); ii) kuandaa na kujenga ghala la takwimu (Data warehouse);

iii) kuratibu na kusimamia zoezi la Sensa ya Watu na

Makazi; iv) kuziwezesha taasisi za Wizara, hususan taasisi za elimu na mafunzo kuboresha miundombinu ya

kujifunza na kufundishia;

v) kuendelea na ujenzi wa jengo la Wizara katika Mji wa

Magufuli, Mtumba Dodoma; vi) ujenzi wa jengo la Ofisi ya Mhakikimali na Hazina

Ndogo katika mkoa wa Geita, Njombe na Songwe; na vii) ukarabati wa jengo la Wizara lililopo Jijini Dar es Salaam, Hazina Ndogo Morogoro, Kigoma na Ruvuma.

4.2 Vipaumbele vya Taasisi 

87. Mheshimiwa Spika, Wizara inatekeleza baadhi ya majukumu yake kupitia taasisi za elimu na mafunzo na elimu ya juu, bodi za kitaalamu na kitaaluma, usimamizi wa fedha, kodi, bima, ununuzi na ugavi, michezo ya kubahatisha, uwekezaji na uwezeshaji pamoja na takwimu.

        Taasisi za Mafunzo ya Elimu ya Juu

 • Mheshimiwa Spika, taasisi za Mafunzo ya Elimu ya Juu zinatarajia kudahili jumla ya wanafunzi 73,074, ikiwemo ngazi ya cheti 14,017, stashahada 19,427, shahada 37,450 na uzamili 2,180.  Aidha, Chuo kinatarajia kuendeleza wahadhiri 196, ambapo ngazi ya uzamivu ni 158 na Uzamili 38 pamoja na kuendeleza shughuli za ushauri na utafiti. 
 • Mheshimiwa Spika, shabaha zaChuo cha Usimamizi wa Fedha – IFM ni pamoja na: Kukamilisha ujenzi wa mabweni manne (4) yenye ghorofa moja moja yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 400, nyumba nne (4) zenye uwezo wa kuhudumia familia nane (4) za wafanyakazi pamoja na maktaba moja (1) katika kampasi ya Gieta; kuendelea na ukarabati wa miundombinu katika kampasi ya Dar es Salaam na ujenzi wa jengo la taaluma likijumuisha ofisi zenye uwezo wa kuhudumia wahadhiri 40 na madarasa yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,520 kwa wakati mmoja katika kampasi ya Mwanza.
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Chuo cha Uhasibu Arusha – IAA kinatarajia kutekeleza yafuatayo: kukamilisha ujenzi wa mabweni manne (4) yenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 2,000 katika kampasi kuu Arusha; kukamilisha ujenzi wa jengo la utawala linalojumuisha madarasa 16, mabweni mawili yenye uwezo wa wakuchukua wanafunzi 1,000 na jengo moja (1) la utawala katika kampasi ya Babati; na kufanya mapitio ya mitaala kumi (10). 
 • Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2022/23, Chuo cha

Mipango ya Maendeleo Vijijini – IRDP kimepanga kufanya tafiti saba (7) na kutoa huduma za ushauri elekezi kwa kuzingatia mahitaji ya wadau; kuwezesha mafunzo kwa watumishi 396; kukarabati nyumba 13 za watumishi katika kampasi kuu ya Dodoma; na kuendelea na ujenzi wa bweni la wanafunzi na Maktaba katika Kituo cha Mafunzo, Kanda ya Ziwa Mwanza.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Taasisi ya Uhasibu Tanzania – TIA imepanga kujenga jengo moja la utawala katika kampasi ya Misungwi, Mwanza na kampasi ya Kigoma; kujenga ukumbi moja (1) wa mihadhara, maabara ya Kompyuta moja (1) na Maktaba moja (1) katika Kampasi ya Mbeya; na kuboresha miundombinu na huduma mtandao

(internet service) katika maktaba za kampasi zote.

 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika – EASTC kipanga kuendelea na ujenzi wa jengo la utawala, kuendeleza wahadhiri 28 na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 20. 

                                                  Bodi za Kitaaluma na Kitaalamu

94. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi inatarajia kusajili wataalamu 3,500 wa ununuzi na ugavi, kuendesha mafunzo na ushauri wa kitaalamu kwa wataalamu 6,500 na kuendesha mitihani ya kitaaluma kwa watahiniwa 4,000. Aidha, Bodi ya NBAA inatarajia kusajili wahasibu 1,125 katika ngazi mbalimbali, kuanza ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu Jijini Dodoma, kufanya ukaguzi wa ubora wa uandaaji wa taarifa za fedha kwa taasisi 75 na kutoa mafunzo ya diploma ya viwango vya uandaaji wa taarifa za fedha serikalini kwa wahitimu 500.

                        Taasisi za Usimamizi wa Kodi na Rufaa za Kodi 

95. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Mamlaka ya Mapato Tanzania – TRA inatarajiwa kufanya yafuatayo: Kuhuisha Mkakati wa Muda wa Kati na Mrefu wa Ukusanyaji Mapato; kutunga upya Sheria na Kanuni za Ushuru wa Stempu na Bidhaa; kuanzisha Maabara ya Forodha; kutengeneza na kutekeleza Mfumo Unganifu wa Kusimamia Mapato ya Ndani na kuboresha Kituo cha Udhibiti na Ufuatiliaji wa Mifumo. Aidha, taasisi za rufaa za kodi zitaendelea kusajili, kusikiliza na kutoa maamuzi ya maombi, mashauri na rufaa za kodi ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara nchini.

                                                 Bodi ya Michezo ya kubahatisha

96. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Bodi ya Michezo ya Kubahatisha inatarajia kutoa leseni 7,697 kwa waendesha michezo ya kubahatisha, ambapo 1,923 ni leseni mpya na 5,774 ni leseni zitakazohuishwa; kufanya ukaguzi kwa waendesha michezo ya kubahatisha 83; kufanya mapitio ya Sheria na Kanuni za Michezo ya kubahatisha; na kurejesha Bahati Nasibu ya Taifa.

                                        Masoko ya Mitaji, Dhamana na Bidhaa

97. Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2022/23, Mamlaka ya Mosoko ya Mitaji na Dhamana – CMSA inatarajia kuanza kusimamia masoko ya mitaji kwa kutumia mfumo wa vihatarishi (Risk Based Supervision), kupanua wigo wa elimu kwa umma kuhusu masoko ya mitaji, dhamana na bidhaa pamoja na kuongeza idadi ya bidhaa katika soko, hususan hisa, hatifungani na vipande katika Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja.  

                                                                             Taasisi za Benki

 • Mheshimiwa Spika, ili kuchochea na kudhibiti ustawi wa viashiria vya uchumi jumla, Benki Kuu ya Tanzania imepanga katika mwaka 2022/23 kukuza wastani wa ukuaji wa ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3) ili kuendana na mahitaji ya shughuli za kiuchumi, kuchochea ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, kudhibiti na kupunguza kiwango cha mikopo chechefu pamoja na kuwa na akiba ya fedha za kigeni inayotosheleza mahitaji ya kuagiza bidhaa na huduma kutoka nje ya nchi kwa kipindi kisichopungua miezi minne (4).
 • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Benki ya TADB imepanga kutoa mikopo ya takribani shilingi bilioni 78 kwa sekta ya viwanda, hususan viwanda vya mafuta ya kula na sukari katika mkoa wa Kigoma, Shinyanga na Manyara. Mikopo hiyo inatarajia kupunguza upungufu wa mafuta ya kula na sukari hapa nchini. Aidha, benki imepanga kutoa mkopo wa takribani shilingi bilioni 130 kwa ajili ya ununuzi wa pamba na kahawa.  
 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Benki ya TIB imepanga kutoa mikopo ya takribani shilingi bilioni 47 kwa sekta ya viwanda, maji, nishati, madini, mafuta na gesi, huduma na utalii pamoja na kilimo; kukuza mizania ya benki kufikia shilingi billioni 902.63; kupunguza ukwasi kwa kuongeza mtaji wa benki kwa shilingi billioni 373; na kuuza hati fungani zenye thamani ya shilingi billioni 300.
 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Benki ya Biashara Tanzania – TCB imepanga pamoja na mambo mengine: Kuboresha uwezo wa benki wa kuzalisha mapato ili kufikia shilingi bilioni 185.6; kukuza faida ya benki kabla ya kodi ili kufikia shilingi bilioni 21.4; kutoa mikopo salama ya shilingi bilioni 709; kukusanya amana za wateja shilingi bilioni 974; kukuza mali za benki ili kufikia shilingi bilioni 1,257; na kukuza thamani ya hisa na kufikia shilingi bilioni 128. 

                                                                              Taasisi za Bima

 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23,  Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania- TIRA inatarajia kutekeleza yafuatayo: Kufanya uchambuzi wa mikataba ya bima mtawanyo kwa kampuni 30 za bima nchini; kufanya ukaguzi wa kampuni 30 za bima, madalali 70, benki wakala 26 na mawakala 278; kufanya upekuzi wa kina  ili kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato kwa kampuni 10; kutoa elimu ya bima kwa watu takribani milioni 1.5 kuhusu huduma za bima; na kuhamasisha kampuni za bima kuandaa bidhaa za bima kwenye sekta ya kilimo.
 1. Mheshimiwa Spika, Shirika la Taifa la Bima linatarajia kupanua wigo wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa huduma za bima; kubuni bidhaa mpya nne (4) za bima; kuhamasisha na kufuatilia uandikishaji wa bima kwa Taasisi za Umma 100 ambazo hazijakata bima na NIC na kuandaa Mfumo wa Usimamizi wa Vihatarishi (Enterprise Risk Management Framework). 

       Taasisi za Uwekezaji na Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi

104. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Kampuni ya Uwekezaji wa Pamoja – UTT AMIS inatarajia kutekeleza yafuatayo: Kuongeza rasilimali za mifuko kwa kiwango cha asilimia 15; kuongeza idadi ya wawekezaji kwa asilimia 5;  na kuhamasisha Taasisi za Serikali, Mifuko ya Hifadhi za Jamii, Mashirika na vikundi mbalimbali vya kijamii kama vile SACCOS kujiunga na mifuko ya UTT AMIS. Aidha, Mfuko wa SELF unatarajia kutoa mikopo yenye masharti nafuu ya shillingi bilioni 43.5 kwa wajasiriamali 28,255 na kuhakikisha kiwango cha urejeshaji wa mikopo kinafikia asilimia 95; na kutoa mafunzo ya ujasiriamali kwa walengwa 4,000.

               Usimamizi wa Takwimu Rasmi

105. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inatarajia kuratibu na kuwezesha Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022, kufanya utafiti wa Sekta isiyo rasmi na utafiti wa Afya ya Mama na Mtoto na kuendelea kutoa takwimu za msingi za uchumi kila mwezi, robo mwaka na nusu mwaka kulingana na aina ya takwimu.  

Usimamizi na Udhibiti wa Ununuzi wa Umma

 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/23, Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma – PPRA inatarajia kuanza ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu Jijini Dodoma na ofisi ya kanda Jijini Dar es Salaam, kuwezesha mafunzo kwa watumishi 940 kutoka katika Taasisi Nunuzi 170 na wazabuni 1,200 ambao wamejisajili katika mfumo wa TANePS, kufanya mapitio na ujenzi wa mfumo mpya wa usimamizi wa ununuzi wa umma na kufuatilia utekelezaji wa Mikataba ya Ununuzi katika Taasisi Nunuzi 530.
 1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23,Wakala waHuduma ya Ununuzi Serikalini – GPSA unatarajia kukamilisha ujenzi wa Ofisi ya Mkoa wa Kigoma, kituo cha mafuta katika mikoa ya Njombe, Pwani, Arusha na Wilaya ya Kahama na ujenzi wa ghala katika Wilaya ya Korogwe, Masasi na Dodoma. Aidha, PPAA imepanga kuandaa mfumo wa kielektroniki wa usajili na usimamizi wa rufaa za ununuzi wa umma na kufanya mapitio ya kanuni za rufaa.

5.0 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA KWA MWAKA 2022/23

Maduhuli

108. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23, Wizara inakadiria kukusanya maduhuli ya jumla ya shilingi trilioni 1.05 kutoka katika vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na gawio, kodi za pango, marejesho ya mikopo, michango kutoka katika taasisi na mashirika ya umma na mauzo ya leseni za udalali. Mchanganuo wa maduhuli yanayokadiriwa kukusanywa kwa mafungu ni kama inavyoonekana katika Jedwali Na. 2.

Jedwali Na.2: Maduhuli Yanayokadiriwa Kukusanywa na

Mafungu ya Wizara kwa mwaka 2022/23

FunguJina la FunguKiasi
7Ofisi ya Msajili wa Hazina      988,254,978,000.00
23Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali        60,100,000,000.00
50Wizara ya Fedha na Mipango          1,000,000,000.00
JUMLA   1,049,354,978,000.00

           Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango

      Matumizi

109. Mheshimiwa Spika,Wizara ya Fedha na Mipango inawasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, maombi ya kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 14.94 kwa mafungu yake nane (8), ili kugharamia matumuzi ya kawaida na maendeleo kwa mwaka 2022/23. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 13.62 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi trilioni 1.32 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo.Aidha,naliomba Bunge lako Tukufu kuidhinisha jumla ya shilingi bilioni 85.52 kwa ajili ya Fungu 45 – Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Kati ya kiasi hicho, shilingi bilioni 74.59 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 10.93 ni kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Mchanganuo wa kiasi kinachoombwa kwa kila fungu umeainishwa katika Jedwali Na.3.

Jedwali Na. 3: Mchanganuo wa Bajeti ya Mafungu ya Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa mwaka 2022/23.

                                                             MATUMIZI YA KAWAIDA  MATUMIZI YA MAENDELEO

                                                                             MATUMIZI  MATUMIZI YA

    FUNGU JINA LA FUNGU MISHAHARA     MENGINEYO KAWAIDA           NDANI        NJE     JUMLA-MAENDELEO JUMLA KUU

     1 Deni la Serikali                               –     9,093,984,694,000     9,093,984,694,000                            –                            –                                    –      9,093,984,694,000

7 Ofisi ya Msajili wa Hazina         5,142,226,000         37,229,786,000         42,372,012,000            940,000,000       650,000,000              1,590,000,000          43,962,012,000 10 Tume ya Pamoja ya Fedha            934,163,000           2,048,142,000           2,982,305,000                      –                                   –              2,982,305,000

13 Kitengo cha Udhibiti wa Fedha Haramu                            –            2,915,586,000            2,915,586,000                             –                  470,000,000                  470,000,000            3,385,586,000

 • HAZINA               945,178,117,000        1,181,695,401,000      2,126,873,518,000  1,257,970,257,000      29,784,942,000                 1,287,755,199,000    3,414,628,717,000
 • Huduma Nyinginezo         9,452,132,000    2,214,379,800,000    2,223,831,932,000                           –                      –                                   –      2,223,831,932,000 23 Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali         6,361,101,000         39,551,734,000         45,912,835,000         1,880,000,000      964,792,000               2,844,792,000         48,757,627,000

50 Wizara ya Fedha na Mipango        48,267,019,000          40,657,910,000          88,924,929,000         22,118,347,000               4,640,863,000            26,759,210,000        115,684,139,000

  JUMLA – MAFUNGU YOTE 1,015,334,758,000   12,612,463,053,000   13,627,797,811,000        1,282,908,604,000        36,510,597,000       1,319,419,201,000   14,947,217,012,000

45 Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi        14,757,479,000          59,838,739,000          74,596,218,000          7,828,000,000                 3,098,935,000            10,926,935,000          85,523,153,000

       Chanzo: Wizara ya Fedha na Mipango

     5.0 HITIMISHO.

 1. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuhitimisha hoja yangu, napenda kumshukuru Mheshimiwa Hamad Hassan Chande (Mb), kwa ushauri na ushirikiano anaoendelea kunipatia katika kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Aidha, nawashukuru watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi zake wakiongozwa na Bw. Emmanuel M. Tutuba, Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Naibu Makatibu Wakuu Bi. Amina Kh. Shaaban, Bw. Lawrence N. Mafuru na Bi. Jenifa C. Omolo kwa ushauri na usimamizi thabiti majukumu na kazi za kila siku za Wizara na Taasisi zake. Vilevile, nawashukuru wakuu wa Idara, vitengo na wafanyakazi wote wa Wizara na Taasisi zake kwa utekelezaji mzuri wa mikakati ya maendeleo, ushauri pamoja na ushirikiano wao mahiri katika kufanikisha majukumu yangu ya kila siku. Asanteni sana na Kazi Iendelee.
 1. Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha hotuba yangu kwa kuliarifu Bunge lako Tukufu kuwa, Serikali inaendelea na maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022. Zoezi hili ni muhimu kwa nchi ili kupata taarifa za msingi zitakazosaidia katika uandaaji na utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo kwa Taifa letu. Hivyo, napenda kutoa wito kwa waheshimiwa wabunge wenzangu kuwa tuendelea kuelimisha na kuhamasisha wapiga kura wetu na watanzania wote kwa ujumla kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23, 2022.
 1. Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda nikushukuru tena pamoja na waheshimiwa wabunge kwa kunipa nafasi ya kuwasilisha hoja hii mbele yenu na umma wa watanzania kwa ujumla. Hotuba hii inapatikana katika tovuti ya Wizara ambayo ni www.mof.go.tz.
 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

Kiambatisho Na.1: Fedha zilizotumika kwa Mishahara hadi Aprili 2022

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *