
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Mtwara kutomfumbia macho na mfanyabiashara wa pembejeo anayetumia vibaya jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika biashara yake ya pembejeo feki za kilimo.
Shaka ameyasema hayo wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya kikazi mkoani Mtwara, ambapo amesema mfanyabiashara huyo anauza pembejeo zisizokidhi viwango huku akidai ni mali ya Waziri Mkuu Majaliwa jambo ambalo sio kweli.
Amesema mfanyabiashara huyo anafanya hujuma dhidi ya juhudi za rais Samia Suluhu Hassan kuwasaidia wakulima ambapo serikali inagawa bure pembejeo hizo.
“Na bahati mbaya sana mfanyabiashara huyo anatumia jina la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwamba eti hiyo ni mali ya Waziri Mkuu na yeye amepewa uwakala na Waziri Mkuu. Vyombo vya ulinzi na usalama huyo mtu bado yupo tu mtaani kweli!.
“Kweli huyo mtu bado yupo tu mtaani, sijui kwa sababu ana nguvu ya fedha sijui kwa kweli, na bahati nzuri nilipopata taarifa na nikapata ushahidi nilimtafuta waziri Mkuu, nikamwambia mheshimiwa waziri Mkuu, akaniambia katika hili huyo mtu aje athibitishe.

“Sijawahi kufanya biashara ya pembejeo si Mtwara, sio sehemu yoyote sihusiki na hilo jambo na mie nashangaa vyombo vya ulinzi na usalama havijamtia mkononi bado, na anasambaa ndani ya Mkoa huu wa Mtwara,” amesema.
Kwa mujibu wa Shaka ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, amesema miongoni mwa wahusika wa mchezo huo mchafu wa biashara ya pembejeo feki, wamo baadhi ya madiwani ambapo ameisitiza kuwa Chama hakitamvumilia kiongozi yeyote atakayethibitika kufanya uhalifu.
Aidha Shaka amewataka viongozi wa chama cha mapinduzi mkoani huko kuhakikisha wanasimamia zoezi la usambazaji wa pembejeo hizo na kutekeleza dhamira njema ya Rais Samia kwa wananchi.
Angela Msimbira ARUSHA
Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Dunia imezindua program ya kuimarisha ujifunzaji wa wanafunzi wa elimu ya awali na Msingi (BOOST wenye thamani ya shilingi trilioni 1.15 utakaosaidia kuboresha mazingira ya ujifunzaji na ufundishaji, kuboresha ujuzi na ubora walimu katika ufundishaji darasani na kuimarisha upatikanaji wa rasilimali wa kuwezesha utoaji wa huduma katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
Akizindua proramu hiyo leo tarehe 6 June, 2022 , Jijini Arusha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adalf Mkenda amesema program hiyo itatekelezwa katika Mikoa yote ya Tanzania Bara baada ya kusaini rasmi tarehe 17 Disemba, 2021 na kuanza utekelezaji wake mnamo tarehe 24 April, 2022
Amesema Programu itajikita katika afua za kuboresha miundombinu ya shule za msingi kwa kuzingatia mahitaji hususani ujenzi wa madarasa, uimarishaji wa mpango wa shule salama, kuimarisha uwiano wa uandikishwaji wa wanafunzi kwenye elimu ya awali, kuboresha vifaa vya ufundishaji katika madarasa ya elimu ya awali, uimarishaji na uendelezaji mpango wa mafunzo ya walimu kazini na kuimarisha vituo vya walimu wa shule za msingi na kuendeleza utengaji wa bajeti
Prof Mkenda amesema program hiyo itatekelezwa kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026 na unathamani ya dola za kimerikani shilingi bilioni 500 ambazo ni sawa na takribani shilingi trioni 1.15 za kitanzania na afua zote zitatekelezwa kwa utaratibu wa lipa kulingana na matokeo.
Aidha amesema matokeo yanayotarajiwa kupatikana katika utekelezaji program hiyo ni vyumba vya madarasa 12,000 kujengwa ambapo lengo ni ni kujenga vyumba vya madarasa 3000 kila mwaka kuanzia mwaka wa fedha 2022/2023, shule 600 kutekeleza mpango wa shule salama, vituo vya walimu shule za msingi 800 kuwekewa vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kujifunza na utoaji wamafunzo endelevu kwa walimu, madarasa 12,000 ya awali kuboreshwa na uandikishwaji wa wanafunzi wa Elimu ya awali kuongezeka, kuimarikakwa utawala katika ngazi ya shule za msingi na kuimarika kwa ubora wa walimu katika ufundishaji kutokana na mafunzo ya walimu kazini.

Wakati huohuo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mhe. David Silinde amesema serikaliimepanga kuwajengea uwezo Makatibu Tawala wa Mkoa, Maafisa elimu Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa elimu wa Halmashauri, Maafisa elimu kata, wakuu wa shule na waalimu juu ya utekelezaji wa programu ya kuimarisha ujifunzaji wa wanafunzi wa Elimu ya Awali na Msingi
Naye Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Charles Msonde amesema serikali imechukua hatua mbalimbali katika kuhakikisha inaimarisha sekta ya elimu nchini kwa kujiwekea mikakati madhubuti katika utekelezaji wa afua za elimi nchini.