LUDEWA THE ROYAL TOUR MBIONI KUANZA

Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ameungana na wananchi wa Ludewa mjini majira ya saa mbili usiku, katika eneo la stendi kuu kuitazama filamu ya The Royal Tour iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa lengo la kuvitangaza vivutio mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

Akiwa katika eneo hilo mkuu huyo ametangaza rasmi kufuata nyayo za Rais Samia kwa kutengeneza filamu itakayo vitangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya wilaya ya Ludewa itakayotambulika kwa jina la The Ludewa Royal Tour.

“Ludewa kuna vivutio vingi sana ambavyo watu hawavifahamu, hivyo wilaya hii itaandaa filamu itakayoitwa The Ludewa Royal Tour ambayo itaongozwa na mimi mwenyewe”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *