HOTUBA YA BAJETI WIZARA YA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023

                                                                                                         1

YALIYOMO

ORODHA YA VIFUPISHO……………………………………. iii

1.0 UTANGULIZI………………………………………………… 1

2.0 MAJUKUMU, MISINGI YA MWELEKEO, NA VIPAUMBELE VYA WIZARA…………………………………………………… 12

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2021/22………………………………………. 16

4.0 CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA KUKABILIANA NAZO……………… 86

5.0 MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23   88

5.1 SEKTA YA MAENDELEO YA   UTAMADUNI……….. 88

5.1.1 IDARA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI………. 88

5.1.2 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)……. 89

5.2 SEKTA YA MAENDELEO YA SANAA………………… 90

5.2.1 IDARA YA MAENDELEO YA SANAA………………. 90

5.2.2 BODI YA FILAMU TANZANIA……………………….. 93

5.2.3 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)…………. 93

5.2.4 TAASISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA)… 94

5.2.5 TAASISI  YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)…………………………………………………………………….. 95

5.3 SEKTA YA MAENDELEO YA MICHEZO…………….. 95

5.3.1 IDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO………….. 95

5.3.2 BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT)…………. 98

5.4 MIRADI YA MAENDELEO………………………………. 99

5.5 KUIMARISHA UTENDAJI WA WIZARA……………. 102

7.0 MAOMBI YA FEDHA KWA  AJILI YA KUTEKELEZA MPANGO WA MWAKA 2022/23………………………………………. 104

8.0 MWISHO NA SHUKRANI……………………………… 105

VIAMBATISHO……………………………………………………………………………… 109

Kiambatisho Na.1A………………………………………………………………………… 109

Kiambatisho Na.1B………………………………………………………………………… 110

Kiambatisho Na. 2………………………………………………………………………….. 111

Kiambatisho Na.3……………………………………………………………………………. 112

Kiambatisho Na.4A………………………………………………………………………… 113

Kiambatisho Na.4B…………………………………………………………………. 113

Kiambatisho Na.4C…………………………………………………………………. 114

Kiambatisho Na. 5…………………………………………………………………… 115

Kiambatisho Na.6…………………………………………………………………….. 121

Kiambatisho Na.7…………………………………………………………………….. 122

Kiambatisho Na.8A…………………………………………………………………. 123

Kiambatisho Na.8B…………………………………………………………………. 124

Kiambatisho Na.9A…………………………………………………………………. 125

Kiambatisho Na.9B…………………………………………………………………. 127

Kiambatisho Na.9C…………………………………………………………………. 129

ORODHA YA VIFUPISHO

AMIS        AFCONArtist Management Information System (Mfumo wa njia ya kieletroniki wa usajili na utoaji leseni kwa watumiaji wa kazi za ubunifu African Cup of Nations (Kombe la Mataifa ya Afrika)
BAKITABaraza la Kiswahili la Taifa
BASATA BASSFU Baraza la Sanaa la Taifa Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni
BMTBaraza la Michezo la Taifa
CHANChampionnat D’Afrique Des Nations (Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani)
CHANETA  COSAFAChama cha Netiboli Tanzania  Council of Southern Africa Football Associations (Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Kusini mwa Afrika)
COSOTACopyright Society of Tanzania (Taasisi ya Hakimiliki Tanzania)
e-GA JAMAFESTe-Government Authority  (Mamlaka ya Serikali Mtandao) Jumuiya ya Afrika Mashariki Festival(Tamasha la Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki)
MAKISATUMashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu
MUSEMfumo wa Ulipaji Serikalini
NACTENational Council for Technical Education (Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi) 
NADONational Anti-Doping Organization (Taasisi ya Kitaifa ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa na Mbinu Haramu Michezoni)  
NCAANgorongoro Conservation Area Authority (Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) 
NSSFNational Social Security Fund (Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii) 
OAUOrganisation of African Union (Umoja wa Nchi Huru za Afrika) 

Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa

OR- TAMISEMI

na Serikali za Mitaa

SADC       TAFFSouthern  African   Development   Community (Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika) Shirikisho la Filamu Tanzania  
TaSUBaTaasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo 
TBCTanzania Broadcasting Corporation (Shirika la Utangazaji Tanzania) 
TFBTanzania Film Board (Bodi ya Filamu Tanzania) 
TFFTanzania Football Federation (Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania) 
TOCTanzania Olympic Committee (Kamati ya Olimpiki Tanzania)
TOT TPA Tanzania One Theatre Tanzania Ports Authority (Mamlaka ya Bandari Tanzania)
TRATanzania Revenue Authority (Mamlaka ya Mapato Tanzania)
TSNTanzania Standard Newspapers (Kampuni ya Magazeti ya Serikali)
TTCLTanzania Telecommunications Corporation Limited (Shirika la Mawasiliano  Tanzania)
UCSAFUniversal Communications Service Access Fund (Mfuko wa  Mawasiliano kwa  Wote)
UMISSETAUmoja wa Michezo ya Shule za Sekondari Tanzania

UMITASHUMTA Umoja wa Michezo na Taaluma

 kwa Shule za Msingi Tanzania
UNESCOUnited Nations, Educational, Scientific and Cultural Organization  (Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa)
UVIKO-19Ugonjwa wa Virusi vya Korona19

HOTUBA YA  WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA

NA MICHEZO, MHE. MOHAMED OMARY

MCHENGERWA (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI

MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/23

1.0 UTANGULIZI

  1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii  leo katika Bunge lako Tukufu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 
  2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutuwezesha kukutana tena hapa Bungeni tukiwa buheri wa afya, na kuendelea kuijalia nchi yetu amani, utulivu, mshikamano na upendo. Aidha, nikushukuru wewe binafsi Mheshimiwa Spika na Waheshimiwa Wabunge wote kwa ushirikiano mnaonipa, unaoniwezesha kutekeleza kwa ufanisi mkubwa majukumu niliyokabidhiwa.
  3. Mheshimiwa Spika, pianitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Awamu ya Sita (6) wa

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama kwa kutimiza mwaka mmoja hivi karibuni katika uongozi wa Taifa letu tangu alipoapishwa kushika nafasi hiyo mwezi Machi mwaka 2021. Aidha, nimpongeze kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi chake kifupi cha uongozi katika  sekta zetu yaliyo shahir na dhahir yaliyotokana na kuliongoza Taifa letu kwa umahiri, weledi, umakini na upeo mkubwa unaoendelea kulishamirisha Taifa letu ndani na nje ya nchi. Sisi na wadau wetu wote wa sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo tunamuahidi kuendelea kuchapa kazi kwa bidii na kwa weledi ili kuendana na fikra, maono, na falsafa yake ya kazi iendelee lakini pia tunaendelea kumuombea dua njema kila uchao kwani Waswahili husema: “Dua njema ya msafiri ndilo tairi salama”. 

  • Mheshimiwa Spika, sambamba na pongezi hizo, nimpongeze sana Mheshimiwa Rais,   kwa kutawazwa Septemba 8, 2021, kuwa Chifu wa Machifu Tanzania, Chifu “Hangaya.” Pia, tunampongeza kwa namna alivyo mstari wa mbele kuhimiza masuala ya Utamaduni na Sanaa pamoja na kusimamia na kuendeleza Michezo nchini hususan Michezo kwa Wanawake kupitia maagizo na maelekezo yake  aliyoyatoa kwa nyakati mbalimbali. Nasi tupo mstari wa mbele kutekeleza maagizo na maelekezo yote ya Mheshimiwa Rais anayotoa katika Sekta ninazozisimamia. Tunamuahidi kuendelea kuutengeneza mwingi, ili aweze kuupiga mwingi.
  • Mheshimiwa Spika, baadhi ya maelekezo ya  Mheshimiwa Rais na ambayo yanaendelea kuwa Dira Kuu kwetu ni pamoja na: kufanyika kwa matamasha ya utamaduni yatakayoshirikisha mikoa yote kwa kushindanishwa ili kumpata mshindi mmoja; Kufufua  mashindano ya Taifa Cup,  michezo iliyositishwa kwa muda mrefu. Vilevile, kuboresha michezo kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kuwaelimisha wanawake kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika michezo, ikizingatiwa wanawake wamekuwa wakifanya vizuri katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa kila wanapopata nafasi.
  • Mheshimiwa Spika, maelekezo mengine ya Mheshimiwa Rais nikurejesha Tuzo mbalimbali; kutoa mirabaha kwa wasanii; na kuhakikisha Timu zetu za Taifa zinafanya vyema ndani na nje ya nchi yetu kwa kuandaa timu bora za Taifa zitakazoundwa na vijana watakaopatikana kupitia programu ya kusaka na kuibua vipaji vya vijana nchi nzima itakayoitwa michezo Mtaa kwa Mtaa. 
  • Mheshimiwa Spika, Halikadhalika, nawapongeza sana Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri

ya Muungano wa Tanzania, na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kwa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi mkubwa katika kumsadia Mheshimiwa Rais kutekeleza majukumu yake. Kipekee, viongozi hawa wasiochoka, wamekuwa wadau mahiri wa sekta zetu ambapo katika kipindi hiki viongozi hawa wabobezi hapa nchini wameshirikiana nasi kuzindua au kufunga matukio mbalimbali ya kimichezo, kiutamaduni na sanaa na kutupatia maelekezo ya kuboresha sekta hizi. Tunawashukuru sana. 

  • Mheshimiwa Spika, naomba nitambue pia na kumpongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, kiongozi mwingine galacha ambaye Taifa hili limebarikiwa kuwa naye, kwa juhudi zake thabiti za kuendeleza Kiswahili na hasa msisitizo anaoutoa mara kwa mara katika mikutano yake, kutumia Kiswahili fasaha na sanifu kwa kiasi cha kutambuliwa mchango wake kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na kukabidhiwa Tuzo ya Heshima wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani lililofanyika Jijini Arusha tarehe 14 hadi 18 Machi, 2022. Dkt. Hussein Ali Mwinyi pia si mchache wa mengi katika maeneo na mawanda mengine nje ya Kiswahili; tunampongeza kwa jitihada kubwa, mahiri na za kimkakati anazochukua katika kuleta ufanisi kwenye sekta za utamaduni, sanaa na michezo kwa upande wa Zanzibar na Tanzania kwa ujumla. 
  • Mheshimiwa Spika, Waswahili wanasema: “Mwenda tezi na omo, marejeo ngamani,” sasa nitambue na kukupongeza wewe binafsi  kwa kuchaguliwa kwa kishindo na Waheshimiwa wabunge wote kuwa Spika wa Saba wa Bunge la Jamhuri  ya  Muungano  wa Tanzania. Kuchaguliwa kwako kumeendeleza historia adhimu katika nchi yetu kwani umekuwa mwanamke wa pili kuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia umeshika madaraka haya ukiwa ni Spika kijana kabisa katika historia ya Bunge la Vyama Vingi. Sisi tuna imani kubwa na wewe kuwa Bunge letu litaendelea kutekeleza wajibu wake kwa kasi na umakini mkubwa. Hili tayari limedhihirika katika vikao ambavyo umeviongoza kwa kipindi hiki. “Jina jema hung’ara gizani.” Hongera sana!  
  • Mheshimiwa Spika, pianitumie fursa hii kumpongeza Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mbunge wa Ilala kwa  kuchaguliwa kwake kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri  ya Muungano wa Tanzania. Ni matumaini yangu kuwa uzoefu wake wa muda mrefu akiwa Mwenyekiti wa Bunge, utamwezesha kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa na kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuisimamia Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo. “Kwa hakika ya kale ni dhahabu”. 
  • Mheshimiwa      Spika,   niwapongeze

Waheshimiwa Wabunge wote waliochaguliwa kujiunga na Bunge lako Tukufu kwa lengo la kuwawakilisha wananchi katika majimbo yao. Waheshimiwa hao ni pamoja na: Mheshimiwa Emmanuel Peter Cherehani kutoka Jimbo la Ushetu; Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai wa Jimbo la Ngorongoro; na Mheshimiwa Mohamed Said Issa kutoka Jimbo la Konde. Aidha, nitumie fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 

  1. Mheshimiwa Spika, nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipomshukuru tena kipekee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuniamini kwa mara nyingine tena na kuniteua kusimamia Wizara hii kubwa yenye dhamana ya kuratibu na kuendeleza Sekta za Kimkakati za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambazo ndio Nguvu Shawishi ya Taifa (Soft Power). Natoa shukrani hizo kwanza kwa kuteuliwa mara ya pili ndani ya kipindi kifupi cha mwaka mmoja nikitumikia nafasi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na sasa ni Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. 
  2. Mheshimiwa Spika, sambamba na teuzi hizo, Mheshimiwa Rais ameniweka kwenye historia mpya inayonifanya niwe  miongoni mwa mawaziri wachache hapa nchini waliopata bahati ya kulitumikia Taifa katika mihimili yote mitatu ya Dola katika nafasi andamizi. Nimekuwa kwenye mhimili wa Mahakama nikitumikia nafasi mbalimbali andamizi za uongozi kwa takribani miaka 20, nimekuwa kwenye Bunge nikitumikia nafasi ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kwa vipindi viwili mfululizo, na sasa naitumikia Serikali katika chombo cha juu kabisa cha ushauri na maamuzi (Baraza la Mawaziri) nikiwa Waziri kamili. 
  3. Mheshimiwa Spika, Wizara hii ni kubwa na muhimu kwani ina nguvu ya kujenga ushawishi (soft power) kwa nchi kwa sababu inakusanya watu wote na inagusa maisha ya Watanzania wengi wapenda michezo na burudani katika nchi hii kupitia sekta zetu za Utamaduni, Sanaa na Michezo ambao wanakadiriwa kuwa takribani asilimia 90 ya Watanzania. Kila mtu katika nchi hii anaguswa ama kwa michezo, utamaduni au sanaa. Naomba kumhakikishia Mheshimiwa Rais utendaji bora na uliotukuka katika utekelezaji wa majukumu niliyokabidhiwa ili kutimiza adhima yake ya kuiunda upya

Wizara hii.

  1. Mheshimiwa Spika, naishukuru kwa dhati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki, kwa maelekezo, ushauri, michango na maoni yao kwa Wizara yangu ambayo yametusaidia sana katika kuboresha utendaji kazi. Aidha, ushauri, maoni na maelekezo hayo yamesaidia kwa kiwango kikubwa katika uwasilishaji wa hotuba hii mbele ya Bunge lako Tukufu. Wizara itaendelea kuzingatia ushauri, maoni, mapendekezo na maelekezo yanayotolewa na Kamati kwa maendeleo ya Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka 2022/23.
  2. Mheshimiwa Spika, chambilecho wahenga, “Mcheza kwao hutuzwa na mfukua lake halimchafui ukucha” nawashukuru wananchi wa Jimbo  langu la Rufiji kwa ushirikiano mkubwa wanaonipa wakati wa  kukabiliana na changamoto mbalimbali katika Jimbo letu kwa lengo la kuwaletea maendeleo wana Rufiji. Ninawaahidi utumishi uliotukuka pamoja na ushirikiano wa dhati katika kipindi chote nitakachokuwa nikiwawakilisha katika Bunge hili Tukufu. 
  3. Mheshimiwa Spika, “Jifya moja haliinjiki chungu”natambua mchango mkubwa wa viongozi wenzangu wa Wizara wakati wa kufanikisha utekelezaji wa majukumu na mageuzi makubwa tunayoendelea nayo wizarani na katika sekta zetu. Nianze kwa kumshukuru kwa dhati kabisa Mheshimiwa Pauline P. Gekul (Mb.), Naibu Waziri makini wa Wizara yangu kwa msaada mkubwa anaonipa katika kutekeleza majukumu ya Wizara. Aidha, nimshukuru Dkt. Hassan S. Abbasi, Katibu Mkuu anayehakikisha mambo yanakwenda na mageuzi yanatokea; Saidi O. Yakubu, Naibu Katibu Mkuu anayehakikisha katika mageuzi haya hatukati tamaa wala kurudi nyuma; Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Wakuu wa Vitengo na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara wasiolala kuhakikisha mambo yanatokea na mipango inakua kweli. 
  4. Mheshimiwa Spika, pia, niwashukuru kwa dhati Watumishi wote wa Wizara na Taasisi zake kwa kutekeleza kikamilifu majukumu yao kwa kujituma ili hatimaye kuleta tija na ufanisi kwa Wizara. Wadau wa maendeleo na wadau wengine kama mashirikisho, vyama, vilabu na kila mdau mmoja mmoja wa sekta za sanaa, utamaduni na michezo ninyi nyote mmekuwa msukumo mkubwa katika kuhakikisha hatukati tamaa, haturudi nyuma. Mmetushamirisha!. 
  5. Mheshimiwa Spika, ni masikitiko yetu tunapobaini kwamba katika kipindi hiki Bunge lako Tukufu lilipatwa na misiba kwa kuwapoteza Waheshimiwa Wabunge wenzetu waliokuwa wawakilishi wa wananchi katika majimbo yao. Wabunge hao ni Mheshimiwa Elias John Kwandikwa wa Jimbo la Ushetu; Mheshimiwa William Tate Ole Nasha wa Jimbo la Ngorongoro; Mheshimiwa Khatib

Said Haji wa Jimbo la Konde; na Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Rukwa. Kwa niaba yangu binafsi, Wizara na wadau wetu, tunatoa pole kwako Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa Wabunge, Familia za Marehemu, Ndugu, jamaa na marafiki na wananchi wote wa majimbo ya Ushetu, Ngorongoro, Konde na Rukwa. Nawaombea kwa Mungu azipokee na kuzilaza roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

  • Mheshimiwa  Spika,  nikifanya dhukuru ya mwaka huu mmoja pia kwa masikitiko natambua kuwa katika  kipindi  cha  Julai, 2021 hadi Mei, 2022 Taifa letu pia limepoteza wadau mahiri na wa kutegemewa wakiwemo wanamichezo na wasanii mbalimbali. Nitumie fursa hii  kutoa  pole kwa familia za marehemu wote, ndugu, jamaa na marafiki kwa kuwapoteza wapendwa wao “Hakika sote tu wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea”. Hapa pia natambua tunao wadau wetu ambao wamepatwa na maradhi na wanaendelea kupigania afya zao akiwemo msanii mahiri kupata kutokea katika kizazi cha awali cha muziki wa kizazi kipya na Mbunge mwenzetu wa zamani Joseph Haule, Profesa Jay, ambaye anaendelea kupigania afya yake katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam kwa miezi kadhaa sasa. Wizara na wadau tunaendelea kumuombea lakini pia kwa kushirikiana na Wizara ya Afya tunaendelea kusimamia kwa uthabiti ahadi ya Mhe Rais ya kuhakikisha Serikali inabeba matibabu yake kwa hatua zake zote na mpaka sasa hakuna lililokwama. 
  • Mheshimiwa Spika, hotuba hii  imeandaliwa kwa   kuzingatia maudhui ya Hotuba ya Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Mapitio ya

Utekelezaji wa  Kazi za Serikali  kwa Mwaka  2021/22 na Mwelekeo wa Kazi za Serikali kwa Mwaka 2022/23 aliyoiwasilisha hapa Bungeni. Aidha, hotuba hii imezingatia Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano 2021/22 – 2025/26; Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 – 2025; Mpango Mkakati wa

Wizara 2021/22 – 2025/26; na maelekezo mbalimbali ya viongozi wa kitaifa. 

  • Mheshimiwa Spika, hotuba yangu imegawanyika katika sehemu nane: Sehemu  ya  Kwanza  ni  Utangulizi;  Sehemu ya Pili  ni  Majukumu, Misingi ya Mwelekeo, na Vipaumbele vya Wizara; Sehemu ya Tatu inaelezea Mapitio ya Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara kwa kipindi cha Mwaka 2021/22 na Sehemu ya Nne inaelezea changamoto  zilizojitokeza na hatua  zilizochukuliwa ili kuzipatia ufumbuzi. Aidha, Sehemu ya Tano ni Mpango na Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2022/23; Sehemu ya Sita ni Makadirio ya Bajeti kwa Mwaka 2022/23; Sehemu ya Saba ni Maombi ya

Fedha kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa 

Mwaka 2022/23; na mwisho Sehemu ya Nane ni shukurani kwa wadau mbalimbali wa Wizara. 

2.0 MAJUKUMU, MISINGI YA MWELEKEO, NA VIPAUMBELE VYA WIZARA

  • Mheshimiwa Spika, ili kufikia Dira ya Wizara, majukumu ya Wizara ni pamoja na kuandaa na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Mipango, Miradi na Programu mbalimbali katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo; kuendeleza shughuli za utamaduni, sanaa na michezo na kusimamia shughuli za filamu na michezo ya kuigiza. Majukumu mengine ni kuimarisha utendaji

na Rasilimali watu Wizarani na kusimamia utendaji wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ambazo ni Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu Tanzania (TFB), Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa), Taasisi ya Hakimiliki na Hakishiriki Tanzania (COSOTA), Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya. Pia, Wizara inaratibu Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika na Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa wenye jukumu la kuwajengea uwezo wadau wa utamaduni na sanaa nchini kwa kuwapatia mafunzo na mikopo yenye riba nafuu. 

  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza na kuimarisha utendaji kazi, Wizara inaongozwa na misingi mitano ya kimkakati na kimageuzi ambayo ni Kuwafikia Wadau (Outreach Programmes); Maboresho ya

Taasisi (Institutional Reforms); Utawala Bora

(Good Governance); Uendelezaji wa Miundombinu (Infrastructure Development); na Utafutaji wa Rasilimali (Resources

Mobilization).

  • Mheshimiwa Spika, chini ya misingi hiyo, katika mwaka 2022/23 Wizara imejipanga kutekeleza maeneo saba ya kipaumbele. Maeneo hayo ni pamoja na kujenga, kukarabati na kuboresha miundombinu ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ikiwemo viwanja na kumbi za kisasa za sanaa na michezo; kuratibu, kuendesha na kusimamia matamasha, shughuli na matukio makubwa ya Utamaduni, Sanaa na Michezo; na kuimarisha, kuwezesha na kufanikisha ushiriki wa Timu za Taifa katika michezo na michuano mbalimbali. Vilevile, kuhamasisha wadau kusaidia timu, vilabu na wawakilishi mbalimbali wa kitaifa katika ushiriki wa michezo na michuano ya kimataifa. 
  • Mheshimiwa Spika, maeneo mengine ni kukamilisha mikakati, miongozo na kanuni mbalimbali za kisera na kisheria katika kuimarisha usimamizi na utendaji katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo; kuimarisha na kuongeza uwezo wa kitaasisi katika usimamizi na utekelezaji wa masuala ya Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo. Masuala mengine ni kuimarisha ushirikiano na Wizara nyingine katika utendaji kazi hususani zile zinazohusika na masuala ya Kazi na Ajira, TAMISEMI, Elimu, Afya, Maliasili na Utalii; Mambo ya Nje na Ushiriano wa Afrika Mashariki na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo Sekta Binafsi katika maendeleo kwa kufadhili na kusukuma mbele gurudumu la Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo.
  • Mheshimiwa Spika, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ni mpya lakini iliyosheheni uzoefu mkubwa katika maendeleo ya nchi hii. Wizara hii iliundwa na Mhe. Rais tarehe 13 Septemba, 2021 kwa Tangazo la Serikali Na. 782 lililochapishwa katika Gazeti la Serikali la tarehe 22 Novemba, 2021 kufuatia kutenganishwa kwa iliyokuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na kuitoa Idara ya Habari na kuipeleka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari.  
  • Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki kifupi cha uwepo wake na kwa misingi iliyowekwa nyuma na Wizara mtangulizi wake, kati ya Julai, 2021 hadi Mei, 2022, Wizara hii imepata mafanikio mbalimbali na imeweka misingi muhimu ya mafanikio zaidi katika miaka ijayo, na kubwa linaloiangaza nchi na dunia ni kwa Wizara  kujiimarisha na kuwa sehemu ya nguvu ya kujenga ushawishi (Soft Power) kwa Taifa Letu. Sekta hizi tatu zimesaidia kutengeneza ajira kwa vijana wengi na watu wa rika mbalimbali; zimewezesha kujenga afya ya akili na mwili kwa wananchi kupitia michezo. Aidha, ni sehemu ya kimkakati ya kuitangaza nchi yetu kupitia utamaduni, sanaa na michezo na hata utalii wetu ili mataifa mengine yaifahamu Tanzania na utamaduni wake.
  • Mheshimiwa Spika, naomba nirudie kusisitiza, sekta hizi zina mchango mkubwa na wa kimkakati kwa Taifa letu na hapa nimshukuru tena Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa maono na uamuzi wake wa kuiunda upya Wizara hii ili ipate nguvu ya kusimamia kwa karibu zaidi sekta hizi za ubunifu na burudani kwa Taifa. Umuhimu wa sekta hizi unadhihirishwa na maono na kauli ya zamani ya Mwasisi wa Taifa letu Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipokuwa akianzisha Wizara ya Utamaduni na Vijana, wakati akihutubia Bunge tarehe 10 Desemba, 1962 aliposema na ninukuu sehemu ya hotuba yake, “Mabadiliko makubwa niliyofanya ni kuunda Wizara mpya; Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana. Nimefanya mabadiliko hayo kwa sababu ninaamini kuwa utamaduni ni kielelezo na roho ya Taifa lolote. Nchi isiyo kuwa na utamaduni wake ni sawa na mkusanyiko wa watu pasipo kuwa na roho inayowafanya kuwa Taifa”. Mwisho wa kunukuu.

3.0 MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU KWA KIPINDI CHA MWAKA 2021/22

3.1 MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA

3.1.1 Makusanyo ya Maduhuli

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22 Wizara ilikadiria kukusanya Shilingi Milioni Mia Tisa Sitini (Sh.960,000,000). Baada ya Idara ya Habari ambayo awali ilikuwa imekadiriwa kukusanya jumla ya Shilingi Milioni Mia Moja Sabini na Saba, Mia Saba Tisini na Nane Elfu (Sh.177,798,000) kuhamishiwa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Wizara ilibaki na makadirio ya jumla ya Shilingi Milioni Mia Saba Themanini na Mbili, Mia Mbili na Mbili Elfu (Sh.782,202,000) zilizokadiriwa kwa ajili ya Idara ya Maendeleo ya Michezo. Hadi kufika mwezi Mei, 2022 Shilingi Milioni Mia Tano Kumi na Tatu, Mia Mbili Kumi na Sita

Elfu, Mia Nane Tisini na Tano (Sh.513,216,895) sawa na asilimia 65.6 ya lengo zilikuwa zimekusanywa. 

  • Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Taasisi zilizo chini ya Wizara, kiasi kilichokadiriwa kukusanywa ni Shilingi Bilioni Thelathini na Tatu, Milioni Mia Nane Sitini na Sita, Mia

                   Nne        Arobaini        na         Nne           Elfu

(Sh.33,866,444,000) baada ya kuhama kwa Taasisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Taasisi zilizobaki wizarani zilibaki na makadirio ya Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia Nne Sabini na Nane, Mia Moja Ishirini na Moja Elfu (Sh.5,478,121,000), ambapo Shilingi Bilioni Mbili, Milioni Mia Tisa Themanini na Mbili, Mia Saba Sitini na Sita Elfu, Mia Mbili na Sita (Sh.2,982,766,206) sawa na asilimia 54.4 ya lengo zilikuwa zimekusanywa hadi kufikia mwezi Mei, 2022. 

3.1.2 Bajeti ya Matumizi ya Wizara na Mtiririko wa Fedha

  • Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22 iliyokuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iliidhinishiwa Shilingi Bilioni Hamsini na Nne, Milioni Mia Saba Arobaini na Moja, Mia Nane na Mbili Elfu (Sh.54,741,802,000). Kati ya fedha hizo Mishahara ilikuwa Shilingi Bilioni Kumi na Tisa, Milioni Mia Moja Arobaini na Sita, Mia

                   Sita        Hamsini        na        Tatu           Elfu

(Sh.19,146,653,000), Matumizi Mengineyo Shilingi Bilioni Kumi na Nne, Milioni Mia Nane Themanini, Mia Moja Arobaini na Tisa Elfu (Sh.14,880,149,000) na Miradi ya

Maendeleo ni Shilingi Bilioni Ishirini, Milioni Mia Saba Kumi na Tano (Sh.20,715,000,000). 

  • Mheshimiwa Spika, kufuatia kuundwa kwa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo bajeti iliyobaki ni Shilingi Bilioni Arobaini, na Milioni Tisini na Mbili, Mia Tano na Mbili Elfu, Mia Mbili Arobaini (Sh.40,092,502,240) ambapo Mishahara ni Shilingi Bilioni Kumi na Mbili, Milioni Mia Tano Tisini na Nane, Mia Tatu Hamsini na Tatu Elfu, Mia Mbili Arobaini (Sh.12,598,353,240); Matumizi Mengineyo Shilingi Bilioni Kumi na Mbili, Milioni Mia Saba Themanini, Mia Moja Arobaini na Tisa Elfu (Sh.12,780,149,000); na Miradi ya Maendeleo Shilingi Bilioni Kumi na Nne, Milioni Mia Saba Kumi na Nne (Sh.14,714,000,000).  
  • Mheshimiwa Spika,  kufikia mwezi Mei, 2022 Wizara ilipokea jumla ya Shilingi Bilioni Ishirini na Tisa, Milioni Mia Nne na Nne, Mia Sita Arobaini na Tatu Elfu, Mia Mbili Thelathini na Saba (Sh.34,349,718,436) sawa na asilimia 85.6 ya bajeti yote, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango ambapo kati ya fedha hizo Matumizi Mengineyo ni Shilingi Bilioni Kumi na Mbili, Milioni Mia Tano Hamsini na Tatu, Mia Sita Sitini na Sita Mia Sita Tisini na Tisa (Sh.12,553,466,699); Mishahara Shilingi Bilioni Kumi na Moja, Milioni Mia Tisa Sabini na Tatu, Mia Moja Sabini na Tatu Elfu, Mia Tano na Tatu (Sh.11,973,173,503) na Miradi ya Maendeleo Shilingi Bilioni Tisa, Milioni Mia Nane Ishirini na Tatu, na Sabini na Nane Elfu, Mia Mbili Thelathini na Nne (Sh.9,823,078,234).  Fedha hizi zimekuwa chachu ya utendaji wizarani na katika Taasisi na msingi muhimu wa kufikiwa mafanikio mbalimbali ambayo tunayaeleza kwa kina katika hotuba hii. 

3.2 UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA WIZARA KWA MWAKA 2021/22

3.2.1                SEKTA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI

3.2.1.1 IDARA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI

  • Mheshimiwa Spika, Sekta ya utamaduni ina majukumu ya kuhifadhi na kuendeleza urithi na utamaduni, lugha na maadili ya Taifa; kuendeleza utambulisho wa Taifa letu; kuhimiza na  kukuza utaifa kwa vijana wetu na wananchi kwa ujumla; kukuza lugha ya Kiswahili ambayo ni lugha ya Taifa kupitia Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA); kufanya tafiti katika uga wa sekta na kuratibu na kusimamia shughuli za Programu ya Ukombozi wa Bara la Afrika na Mfuko wa Utamaduni na Sanaa.
  • Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Sekta ya Utamaduni kuendana na mabadiliko yanayoendelea kutokea duniani kote,  Wizara imeendelea kuhuisha Sera ya Taifa ya Utamaduni ya Mwaka 1997 ili iweze kukidhi mahitaji na kuendana na wakati kwa kupokea maoni kutoka kwa wadau mbalimbali wakiwemo wasanii, maafisa utamaduni, na maafisa sanaa, Machifu na Viongozi wa Kimila. Kupitia vikao mbalimbali mathalani, kikao cha Machifu na viongozi wa kimila kilichofanyika tarehe 5 Oktoba, 2021 Jijini Dodoma, Rasimu ya Kwanza ya Sera hii sasa imekamilika na muelekeo katika mwaka ujao wa fedha ni kuiwasilisha katika Mkutano wa wadau wote na kuendelea na hatua zinazofuata za kuiidhinisha.  
  • Mheshimiwa Spika, halikadhalika katika kuhakikisha kuwa Wizara inakutana na kuweka mikakati madhubuti na wadau wake, iliratibu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo wa mikoa na Halmashauri za Wilaya zote nchini kilichofanyika tarehe 04 hadi 06 Aprili, 2022 Jijini Dodoma. Kikao hicho kililenga kuibua fursa zilizopo, changamoto na kupendekeza njia madhubuti za utatuzi wa changamoto hizo. Moja ya mafanikio ya vikao hivi ni kutambuliwa kwa Kada ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwenye Muundo wa TAMISEMI ambapo sasa kimeanzishwa Kitengo kipya kinachojitegemea cha Utamaduni, Sanaa na Michezo badala ya kuwa chini ya Idara ya Elimu kama ilivyokuwa hapo awali. Muundo huo utakaochagiza mafanikio mengi kiutendaji tayari umesainiwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuanza kutumika. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais na ni matarajio yangu kuwa huko tuendako sasa kutakuwa na utekelezaji wenye tija zaidi wa majukumu ya Wizara katika ngazi ya Halmashauri.
  • Mheshimiwa Spika, vilevile,Wizara kwa kushirikiana na wadau wa utamaduni, imeendelea kuratibu na kuandaa matamasha ya kiutamaduni kwa lengo la kudumisha urithi wa utamaduni. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022, miongoni mwa matamasha yaliyoratibiwa ni pamoja na Tamasha la Utamaduni la lililohusisha jamii ya Wasukuma na Wanyamwezi lililofanyika katika Uwanja wa Red Cross, Kisesa Jijini Mwanza, tarehe 07 – 08 Septemba, 2021; Tamasha la Utamaduni

Mkoa wa Kilimanjaro lililohusisha jamii za Wachaga, Wapare na Wamasai lililofanyika katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika katika Manispaa ya Moshi tarehe 22 Januari, 2022. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliratibu Tamasha la Tambiko la Kimila la Jamii ya Waluguru lililofanyika katika Himaya ya Chifu Kingalu Mwanabanzi wa XV, tarehe 16 – 17 Oktoba, 2021 katika Kijiji cha Kinole, Wilaya ya Morogoro Vijijini. Lengo la tambiko lilikuwa kuombea Taifa letu dhidi ya majanga mbalimbali ikiwemo homa inayosababishwa na virusi vya Korona (UVIKO-19), kukosekana kwa mvua na maradhi mengine. 

  • Mheshimiwa Spika, Matamasha mengine yaliyoratibiwa ni pamoja na Tamasha la Kumbukizi ya Vita vya Maji Maji lililofanyika Mkoani Ruvuma tarehe 24 hadi 27 Februari, 2022; Tamasha la Siku ya Utamaduni  lililofanyika tarehe 09 Oktoba, 2021 Jijini Dar es Salaam katika Shule ya Awali na Msingi ya Mt. Joseph na Tamasha la Mawasiliano, Utalii na Utamaduni lililofanyika Jijini Mwanza terehe 23 Novemba, 2021. Kutokana na uzoefu wa Matamasha haya kwa sasa, Wizara inaratibu Tamasha kubwa na la Kitaifa la Utamaduni litakalofanyika kuanzia tarehe 01 Julai, 2022 Jijini Dar es Salaam na kushirikisha mikoa yote; 
  • Mheshimiwa Spika, pia, kimataifa, Wizara ilishiriki katika Maadhimisho ya miaka 25 ya Jumuiya ya Nchi zilizo katika Mwambao wa Bahari ya Hindi (Indian Ocean Rim Association – IORA). Maadhimisho hayo yalifanyika katika mji wa Mapou, Mauritius tarehe 7 Machi, 2022.  Katika Maadhimisho hayo, Serikali ilipeleka kikundi cha utamaduni (Tasting Corner and Cultural Perfomance) kwa lengo la kutangaza utamaduni wetu, ambacho kilihusika pia na maandalizi ya chakula cha asili. Hii ilikuwa fursa adhimu ya kuutangaza utamaduni wetu nje ya nchi.  
  • Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na suala  la mmomonyoko wa maadili nchini, Wizara imekamilisha Kitabu cha Mwongozo

cha Maadili na Utamaduni wa Mtanzania. Mwongozo huo umejumuisha maoni ya wadau yaliyokusanywa kupitia vikao mbalimbali na unatarajiwa kuzinduliwa wakati wa Tamasha la Kitaifa la Kiutamaduni linalotarajia kufanyika mwanzoni mwa mwezi Julai, 2022. 

3.2.1.2  BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
  • Mheshimiwa Spika, majukumu ya Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni pamoja na kuendeleza, kustawisha na kuimarisha lugha ya Kiswahili nchini na kufuatilia maendeleo yake nje ya nchi; kuhimiza matumizi ya lugha ya Kiswahili katika shughuli za Serikali na umma; kuratibu utafiti wa Kiswahili kwa kushirikiana na wadau na kuhimiza matumizi fasaha na sanifu ya lugha ya Kiswahili na kuzuia upotoshaji wake. Katika kipindi hiki mafanikio lukuki yamepatikana kama ifuatavyo: 
  • Mheshimiwa Spika, naweza kujinasibu kuwa matumizi ya Kiswahili yanazidi kukubalika kitaifa, kikanda na kimataifa ambapo jitihada hizo kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 zimezaa matunda kwa Kiswahili kuvishwa joho jipya  kuwa lugha ya kazi katika Umoja wa Afrika. Kiswahili kilipitishwa kuwa Lugha ya Kazi ya Umoja wa Afrika katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali uliofanyika Jijini Addis Ababa, Ethiopia tarehe 5 – 6 Februari, 2022

Kiambatisho Na.1A  Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwasilisha hoja ya Kiswahili kutumika kama lugha ya kazi katika Umoja wa Afrika.Hatua hii ni fursa muhimu kwa Wataalamu wetu wa Tafsiri na Ukalimani nchini ambao katika muda mfupi tu tayari Watanzania 65 wamesajiliwa kupata fursa za ajira za muda na za kudumu katika Umoja wa Afrika na Kamisheni zake. Aidha, nyaraka muhimu za Umoja wa Afrika ikiwa ni pamoja na Itifaki zitatafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili na kutoa ajira zaidi kwa wataalamu wetu.

  • Mheshimiwa Spika, tukirejelea fursa nyingine zilizoainishwa hapo juu, tayari Watanzania saba (7) wamepata nafasi ya kuhudumu katika mikutano mbalimbali ya Umoja wa Afrika na Kamisheni zake ambapo wakalimani wawili (2) walihudumu katika Mkutano wa Kawaida wa 35 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika  uliofanyika Februari, 2022 na wakalimani watatu (3)  pamoja na wafasiri wawili (2) walihudumu katika Mkutano wa 71 wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Afrika uliomalizika tarehe 13 Mei, 2022. 
  • Mheshimiwa Spika, pia, kutokana na nafasi ya Kiswahili kwa sasa, lugha hii inaendelea kushamiri, ambapo baadhi ya vyuo vikuu vya nje ya Tanzania ambavyo awali havikuwa na programu za Kiswahili vimeanza harakati za kuingiza Kiswahili katika programu zao ambapo tayari kuna makubaliano ya awali ya kushirikiana kati ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo Kikuu cha Ethiopia, Chuo Kikuu cha Port Harcourt (Nigeria) na Chuo Kikuu cha Joachim Chisano (Msumbiji) katika kufundisha Kiswahili. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara inafahamu, kunufaika zaidi kwa Watanzania katika fursa hizi za Kiswahili kutahitaji mikakati zaidi na nchi yetu kuwekeza katika kuieneza na utafiti wa lugha hii. Hivyo, moja ya mafanikio muhimu katika kipindi hiki ni Serikali kupitia Wizara hii katika kulisukuma mbele zao jipya na diplomasia mpya ya Kiswahili, Wizara kupitia BAKITA imekamilisha maandalizi ya Mkakati wa Taifa wa Kubidhaisha Kiswahili wa Miaka 10 (20222032) ambapo miongoni mwa maazimio yake makubwa unalenga kuwasajili  wataalamu wa Kiswahili na kuimarisha stadi zao. 
  • Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa lengo hili umeanza na tayari wakalimani 65 wamesajiliwa na Baraza na kupatiwa mafunzo ya kuwaimarisha katika uga huo. Vilevile, wataalamu 1,130 wamepatiwa mafunzo ya kufundisha Kiswahili kwa wageni ambapo miongoni mwao kuna walimu 2 wamekwenda kufundisha nchini Uingereza, 1 Ujerumani, 1 Polandi, 5 Afrika Kusini na 1 Uganda. Aidha, miongoni mwa wahitimu hao wapo walioanzisha madarasa ya ana kwa ana ya kufundisha Kiswahili kwa wageni na wengine wanafundisha kwa njia ya mtandao. Kwa ujumla Kiswahili kwa sasa ni bidhaa na ni ajira. 
  • Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia BAKITA inaendelea kusajili wataalamu wa Kiswahili katika kanzidata ili Watanzania wengi zaidi watambulike utaalamu wao ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 Baraza limesajili wataalamu 19 ambapo wanaume ni 13 na wanawake 6. Jumla ya wataalamu waliosajiliwa hadi sasa ni 1,325.  Tunawaalika Watanzania wote wanaojiamini kuwa na utaalamu mahsusi katika Kiswahili kutumia dirisha hili la BAKITA kujisajili ili wapate vyeti vitakavyowapa ajira duniani. 
  • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine ya kihistoria yaliyopatikana kwa juhudi za Serikali pamoja na wadau wa Kiswahili ni kupitishwa kwa tarehe 7 Julai ya kila mwaka, kuwa ya Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani. Kiambatisho Na.1B, ni nembo ya Kiswahili iliyotumika wakati wa Mkutano wa UNESCO kupitisha tarehe 7 Julai ya kila mwaka kuwa siku ya kuadhimisha Kiswahili Kimataifa.  Tarehe hii ilipitishwa rasmi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) tarehe 23 Novemba 2021. Tarehe hii ilipendekezwa kutokana na ukweli kuwa tarehe 7 Julai, 1954 Mkutano Mkuu wa TANU chini ya Uenyekiti wa Baba wa Taifa letu, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere uliamua kwa kauli moja kutumia Kiswahili kwa lengo la kuleta umoja kwa Watanganyika wote katika harakati za ukombozi. Hivyo, si kujinasibu bali ni kueleza ukweli wa dhahiri shahiri kwamba msingi wa uamuzi huu ni kutokana na mchango mkubwa wa Tanzania katika kukiasisi na kukiendeleza Kiswahili. 
  • Mheshimiwa Spika, nimesema uamuzi huu ni wa kihistoria; kwani kwa mafanikio haya Kiswahili ni lugha ya kwanza ya Kiafrika ambayo imepangiwa siku maalumu ya kusherehekewa na kuadhimishwa Kimataifa. “Chanda chema huvishwa pete”. Licha ya kuwa lugha ya kwanza kutoka Bara la Afrika, pia ni lugha yenye wazungumzaji wengi, wanaozidi milioni 200 duniani kote. 
  • Mheshimiwa Spika, ni kwa kutambua umuhimu wa johari hii ya thamani na furaha yetu kwa mafanikio haya, Serikali ya Tanzania kupitia Wizara hii inaendelea na mikakati ya kuiongoza Dunia kuadhimisha

Siku hii kwa mara ya kwanza Julai 7, 2022.

Tayari Kamati ya Kitaifa ya Kuratibu Maadhimisho ya siku hii inaendelea na kazi. Kama wasemavyo Waswahili “Hamadi ni ilio kibindoni, na silaha ni iliyo mkononi” Kiswahili ndiyo silaha yetu. 

  • Mheshimiwa Spika, kutokana na kutambuliwa huku kwa Kiswahili kimataifa Baraza limeendeleakwa kasikutangaza Kiswahili kupitia mafunzo mbalimbali yanayotolewa kwa njia ya mtandao kwa kuanzisha mfumo maalumu wa kufundisha Kiswahili kwa wageni (Swahili Prime), kutambua vituo vinavyofundisha Kiswahili nje ya nchi kikiwemo Ethiopian Swahili Community na Kituo cha Utamaduni Tanzania Seoul ambapo hadi mwezi Aprili, 2022 jumla ya vituo 17 vya kufundisha Kiswahili kwa wageni ndani na nje ya nchi vilitambuliwa rasmi na miongoni mwa vituo hivyo, vituo vinne (4) viko nje ya nchi. Vilevile, kwa kushirikiana na Balozi zetu nje ya nchi Serikali imeweza kufungua vituo vya kufundisha Kiswahili ambapo hadi mwezi Aprili, 2022, Balozi zetu nchini Korea Kusini, Ufaransa na Nigeria zinafundisha lugha ya Kiswahili. 
  • Mheshimiwa Spika, sambamba na jitihada hizi, Balozi nyingine zikiwemo Afrika Kusini, Namibia, Zimbabwe na Msumbiji zimeanza harakati za kufungua madarasa ya kufundishia Kiswahili. Pia, Ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani unakusudia kufungua maktaba na Ubalozi wa Namibia unakusudia pia kufungua Klabu za Kiswahili nchini humo. Aidha, Serikali katika kuchagiza harakati hizi imesambaza vitabu vya Mwongozo wa Taifa wa Kufundisha Kiswahili kwa Wageni katika Balozi mbalimbali zikiwemo Ubalozi wa Uholanzi, Burundi, Namibia, Afrika Kusini, Zimbabwe, Ethiopia na Nigeria. Vilevile, ilipeleka vitabu 65 vya kujifunza Kiswahili Hatua ya Kwanza  katika maonesho ya Dubai Expo 2022, ambavyo viligawiwa bure kwa lengo la kuhamasisha ujifunzaji wa lugha ya

Kiswahili kwa wageni. 

  • Mheshimiwa Spika, halikadhalikaBAKITA imeendelea kuelimisha umma kuhusu matumizi fasaha na sanifu ya Kiswahili kwa jamii ndani na nje ya nchi kwa kutumia njia mbalimbali zikiwemo vyombo vya habari. Katika kutekeleza jukumu hili, jumla ya vipindi 679 vilirushwa hewani kupitia redio na televisheni. Vipindi hivi vililenga kuuelimisha umma kuhusu matumizi fasaha na sanifu ya Kiswahili pamoja na isimu na fasihi ya lugha ya Kiswahili. Aidha, makala 32 zilichapishwa kupitia gazeti la HabariLeo; na Makala 4 katika magazeti mengine. Pia, gazeti la mtandaoni la Lugha Yetu lilitolewa mara 7. Baraza limekamilisha maandalizi ya

Jarida la Lugha Yetu Toleo Na. 40 ambapo nakala 5,000 zimechapishwa na zitasambazwa kwa shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuimarisha matumizi ya Kiswahili. Fauka ya hayo, elimu ya matumizi ya lugha ilitolewa kupitia mabango ya msamiati na misemo ya busara iliyotolewa kupitia akaunti za Baraza za mitandao ya kijamii za Facebook, Twitter na YouTube.  

  • Mheshimiwa Spika, vilevile, Baraza liliendesha mafunzo katika Mkoa wa Tanga kuimarisha ujenzi wa kada muhimu ya uandishi wa habari ambapo jumla ya waandishi na watangazaji wa vyombo vya habari 22 walipatiwa mafunzo ya matumizi fasaha na sanifu ya lugha ya Kiswahili. Aidha, Baraza liliandaa Kongamano la Waandishi na Watangazaji wa Idhaa za Kiswahili Duniani tarehe 14 – 18 Machi, 2022 lililofanyika Jijini Arusha na kufunguliwa na Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kufungwa na Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambapo washiriki takribani 250 kutoka redio na televisheni za ndani na nje ya nchi walishiriki. Kongamano hili litaendelea kila mwaka. 
  • Mheshimiwa Spika, katika jitihada hizohizo za nchi kujiimarisha kwa upande wa

Kiswahili, tayari Sheria na Kanuni ishirini na

sita (26)  za Wizara na Taasisi mbalimbali zimetafsiriwa kwa Kiswahili kwa kushirikisha wataalamu wa Baraza. Fauka ya hayo, BAKITA lilitafsiri nyaraka mbalimbali 743 kutoka katika asasi, mashirika, taasisi za serikali na watu binafsi na kuthibitisha tafsiri 2,550 zilizofanywa na wakala wake.

3.2.1.3 PROGRAMU YA URITHI WA  UKOMBOZI WA  BARA LA AFRIKA 
  • Mheshimiwa Spika, nchi yetu haitasahaulika kwa historia yake ya ushujaa na uthubutu; nguzo muhimu inayoendelea kutuongoza hadi sasa kwa jinsi tulivyoongoza huko nyuma mapambano ya ukombozi wa Bara la Afrika.Na kama unavyofahamu, kwa heshima hiyo Umoja wa Afrika (AU) uliipa Tanzania jukumu la kuwa Makao Makuu ya Programu ya Ukombozi wa Bara la Afrika, programu inayosimamiwa na Wizara hii.
  • Mheshimiwa Spika, kama walivyojitoa wazee wetu, nasi pia katika kuendeleza historia hizo tumeendelea kuratibu utekelezaji wa majukumu ya Programu, ambapo, katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022, tumeendelea kukamilisha ukarabati wa jengo lililotumiwa na Kamati ya Ukombozi ya Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) ambapo Makao Makuu yake yalikuwa Jijini Dar es Salaam kuanzia mwaka 1963 hadi 1994. Jengo hilo ambalo ni kielelezo cha Ukombozi wa Bara la Afrika lilikuwa kuukuu na wakati wowote lingebomoka na kufuta kumbukumbu hiyo muhimu.
  • Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Wizara hii imekamilisha ukarabati huo kwa asilimia 85 kufikia Mei, 2022 na baada ya kukamilika eneo hilo litakuwa Makumbusho ya Afrika ya Historia ya Ukombozi ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Umoja wa Afrika ya mwaka 2011. Aidha, katika kipindi hiki Programu hii pia imefanya utafiti na kukusanya taarifa za maeneo 15 yenye historia ya Ukombozi yaliyopo Dar es Salaam na Zanzibar; pamoja na kufanya mahojiano na mashuhuda 20 wa Harakati za Ukombozi wa Afrika ili kutunza historia hiyo. 
  • Mheshimiwa Spika, majukumu mengine yaliyotekelezwa na Programu ni pamoja na kutambua  na kukusanya nyaraka za picha na magazeti yenye taarifa za harakati za Ukombozi wa Bara la Afrika ambapo jumla ya nyaraka na magazeti 150 yamekusanywa; kufanya maonesho ya historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika; kuratibu ziara ya Mheshimiwa Monica Mutsvangwa (Mb.), Waziri wa Habari na Utangazaji kutoka Jamhuri ya Zimbabwe ya kutembelea maeneo ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika Novemba, 2021 katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Lindi, Morogoro, na Pwani; na kuratibu Maadhimisho ya Siku ya Ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika yaliyofanyika Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma tarehe 23 Machi, 2022 ambapo takribani  washiriki 700 walihudhuria maadhimisho hayo wakiwemo wanafunzi. 
  • Mheshimiwa Spika, programu iliendelea kuweka mabango ya utambulisho wa maeneo yenye urithi wa Ukombozi wa Afrika katika mikoa ya Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara, Ruvuma na Zanzibar kwa ajili ya kuyatambulisha na kuyalinda maeneo hayo; kuanzisha Maktaba ya Programu ya Ukombozi yenye vitabu 1,000 vyenye maudhui ya historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika; pamoja na kuandaa makala maalumu kuhusu mchango wa Tanzania katika Ukombozi wa Bara la Afrika. Nawaomba vijana wa Kitanzania kutembelea vituo vya Programu hii ili kujikumbusha na kujifunza uzalendo mkubwa waliouonesha wazee wetu katika kuipigania Afrika huru. 

3.2.1.4 MFUKO WA UTAMADUNI NA SANAA

  • Mheshimiwa SpikaSekta ya Utamaduni na Sanaa imekuwa muhimu siyo tu katika kukuza na kuendeleza mila, desturi, lugha na sanaa zetu bali pia ni chanzo cha ajira na maendeleo ya uchumi kwa Taifa. Sekta hii imekuwa kimbilio la kundi kubwa la vijana kwa kuwapatia ajira kupitia shughuli za kiutamaduni na sanaa kama vile ususi, ufinyanzi, uchongaji, utengenezaji wa batiki, muziki na filamu. Hata hivyo, ili kuzalisha ajira, sekta hii imekuwa ikisuasua kutokana na kukosekana mitaji na utaalamu. 
  • Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu huo, leo ninayo furaha kuliambia Bunge lako Tukufu kuwa Serikali imefanikiwa kufanya jambo jingine la kihistoria katika mageuzi ya kiutendaji kwa kuhuisha Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa uliokuwa umekwama kufanya kazi tangu mwaka 2013. Mfuko huu sasa utakuwa chachu ya ukuaji wa sekta za Utamaduni na Sanaa kupitia utoaji wa mikopo, ruzuku na kuwajengea uwezo kwa kuwapa mafunzo waandaaji wa kazi za Utamaduni na Sanaa. Hongera Mheshimiwa Samia Suluhu Hasaan kwa kufanikisha hili.
  • Mheshimiwa Spika, ili kuanza mchakato wa utoaji mikopo, tayari Serikali imeshatoa kiasi cha Shilingi Milioni Mia Tano (Sh.500,000,000) kwa Mfuko huu kati ya bajeti ya Shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Tano (Sh.1,500,000,000) ili kutimiza malengo yaliyotajwa hapo juu. Mikopo hiyo itaanza kutolewa kwa wadau wa utamaduni na sanaa mara Sekretarieti itakapokamilisha uundaji wa Kanuni za kutoa mikopo hiyo, ambapo kwa sasa ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji. Aidha, kutokana na umuhimu wa Mfuko huu, kwa mwaka 2022/23 Serikali imeongeza bajeti hadi

Shilingi Bilioni Mbili, Milioni Mia Nne (Sh.2,400,000,000) kutoka Shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Tano (Sh.1,500,000,000) kwa mwaka 2021/22. Niwaombe wabia wa maendeleo wengine kuunga mkono juhudi hizi za Mheshimiwa Rais katika kuchangia Mfuko huu.   

3.2.2 SEKTA YA MAENDELEO YA SANAA

3.2.2.1 IDARA YA MAENDELEO YA SANAA

  • Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maendeleo ya Sanaa ni eneo jingine muhimu katika maendeleo ya nchi yetu na inahusisha Idara ya Maendeleo ya Sanaa, Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza (TFB), Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) na Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa). 
  • Mheshimiwa Spika, kwa kuwa moja ya majukumu ya sekta hii ni kuwapa vijana fursa za kuonesha vipaji vyao na pia kupata ajira, Wizara katika kipindi cha kuanzia Julai, 2021 hadi Aprili, 2022, imeendelea kuandaa matukio makubwa na ya kimkakati ikiwemo Tamasha kubwa la Kitaifa la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival). Tamasha hili lilifanyika kwa siku mbili mfululizo Jijini Dodoma tarehe 12 na 13 Machi, 2022  ambapo wasanii mbalimbali zaidi ya 250 walipata fursa ya kushiriki huku wananchi zaidi ya 12,000 wakihudhuria tamasha hili na wengine wakinufaika kiuchumi kupitia malipo ya malazi katika hoteli na nyumba za wageni, chakula, usafiri na huduma nyingine mbalimbali. Aidha, watu wengi zaidi walifuatilia mubashara kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, Tamasha hili ambalo tayari ni maarufu nchini kwa kushirikisha wasanii wengi zaidi litaendelea kufanyika kila mwaka kwa malengo yaliyoainishwa kama alivyoelekeza Mheshimiwa Rais wakati wa Tamasha la “Dream Concert” lililoandaliwa na Msanii Joseph Mbilinyi (Sugu) Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.   
  • Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa, Sensa ya Filamu na Utamaduni (BASSFU) la Zanzibar na Ofisi ya Waziri Mkuu iliratibu ushiriki wa vikundi vya burudani katika Sherehe za Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Ili kuhakikisha ujumbe katika Kaulimbiu ya Maadhimisho unawafikia wananchi wengi zaidi, kwaya 10 zilishindanishwa ambapo Kwaya ya Chuo

cha Utumishi wa Umma Magogoni iliibuka kidedea na kutumbuiza katika sherehe hizo. Aidha, Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya na vikundi 8 vya burudani kutoka Bagamoyo, Zanzibar na Dar es Salaam walishiriki. Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ni Mjumbe wa kudumu katika maadhimisho ya Kitaifa katika Kamati Ndogo ya Itifaki, Mialiko na Sherehe. 

  • Mheshimiwa Spika, Serikali ilifanya kwa ufanisi mkubwa maandalizi na ushiriki wa nchi katika maonesho ya Sanaa na Utamaduni duniani wakati wa maonesho ya Dubai Expo2020 tarehe 21 hadi 27 Februari, 2022. Katika maonesho hayo, makundi ya kimkakati yaliiwakilisha nchi katika ngoma za asili na za kisasa, muziki wa Singeli, muziki wa Kizazi Kipya na Sanaa za Ufundi. Vilevile, kulikuwa na kikundi cha muziki wa Taarab kutoka Zanzibar. Vikundi vyote vilifanikiwa kuitangaza nchi katika majukwaa mbalimbali wakati wa maonesho hayo ambapo Msanii Mrisho Mpoto kupitia maonesho hayo amepata mwaliko katika maonesho ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yatakayofanyika nchini Ufaransa tarehe 1 – 8 Julai, 2022.  
  • Mheshimiwa Spika, kufuatia Rais wetu mpendwa Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kuona umuhimu wa yeye binafsi kutumia Sanaa kuitangaza nchi yetu kimataifa, kikundi cha Sanaa kutoka TaSUBa kilipata fursa ya kufanya maonesho nchini Marekani katika Jiji la New York tarehe  18 Aprili, 2022 na Los Angeles tarehe 21 Aprili, 2022 wakati wa uzinduzi wa Filamu maarufu ya Tanzania: “The Royal Tour”. Kutokana na mvuto mkubwa wa utamaduni na sanaa ya Tanzania kwa jamii ya kimataifa maonesho hayo ni kati ya matukio yaliyofuatiliwa sana na kusambazwa na watu wengi kupitia mitandao ya kijamii ndani na nje ya Marekani wakati na baada ya uzinduzi wa “Royal Tour”. Wizara itaendelea kutoa mchango wake wa kuwatafutia wasanii wengi zaidi fursa ya kwenda nje kuitangaza nchi yetu.
  • Mheshimiwa Spika, katika ngazi ya Afrika, Wizara kwa kushirikiana na Kituo cha Sanaa na Utamaduni kwa Viziwi Tanzania

(KISUVITA) iliratibu kwa mafanikio makubwa mashindano ya urembo, utanashati na mitindo kwa Viziwi tarehe 14 Agosti 2021 Jijini Dar es Salaam ambapo jumla ya warembo, watanashati na wanamitindo 74 kutoka nchi 14 za Afrika walishiriki. Kati ya hao, Watanzania sita (6) wakiongozwa na Mtanzania mrembo kiziwi namba mbili Afrika walifuzu kushiriki mashindano kama hayo ngazi ya Dunia yaliyotarajiwa kufanyika nchini Brazil mwezi Aprili, 2022.

  • Mheshimiwa Spika, hata hivyo, ninayofuraha kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba kutokana na ufanisi uliooneshwa na Tanzania katika maandalizi ya mashindano hayo ngazi ya Afrika, Bodi ya Wakurugenzi ya mashindano hayo Duniani (The Executive Board of Directors for Miss and Mr. Deaf Internaltional) wameiteua rasmi Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo na kukubaliana yafanyike Jijini Dar es Salaam mwezi Oktoba, 2022. Hii ni heshima nyingine kubwa kwa nchi yetu na katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuwa na zaidi ya washiriki 300 kutoka nchi mbalimbali duniani, tayari maandalizi yameanza na tutayaandaa kwa ubora wa Dunia. Pia Tanzania imevutia Taasisi mbalimbali  Duniani na sasa matukio makubwa yanaendelea kuletwa nchini, ambayo ni pamoja na MTV Africa Music Awards, Mkutano wa wadau wa mziki Afrika na Mashindano ya AFCON yatakayofanyika mwaka 2027.
3.2.2.2 BARAZA LA SANAA LA TAIFA

(BASATA)

  • Mheshimiwa Spika, majukumu ya Baraza la Sanaa la Taifa ni pamoja na kukuza na kuendeleza sanaa nchini; kufanya tafiti za fursa za masoko na masuala mbalimbali yanayohusu sanaa; kuandaa Kanuni za kusimamia ubora wa kazi za sanaa, na kuandaa na kuendesha maonesho, mashindano, matamasha na biashara za sanaa.
  • Mheshimiwa Spika, baada ya kipindi kirefu tangu mwaka 2015 cha kutokuwa na Tuzo za Muziki nchini, Wizara kupitia BASATA pamoja na wadau wengine wa sekta ya Sanaa nchini tumezirejesha tuzo hizi.  Serikali ya Awamu ya Sita imezisimamia na kuzigharamia tuzo hizi kwa lengo la kuhamasisha, kuchochea ushindani ili kuzalisha kazi bora na kuendeleza ubunifu kwenye tasnia ya Muziki nchini. Tuzo hizi zilizinduliwa tarehe 28 Januari, 2022 na kutolewa rasmi tarehe 02 Aprili, 2022 ambapo zilikuwa na jumla ya vipengele (categories) 19, na kwamba tuzo zilizoshindaniwa zilikuwa (47) na tuzo za heshima zilikuwa (4) na Tuzo Maalumu moja (1) kama alivyoeleza Mheshimiwa Rais wakati wa Tamasha la “Dream Concert” tarehe 31 Mei, 2022. Tuzo hizi zimeamsha ari na kujituma kwa wasanii. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kuonesha jinsi wasanii wetu walivyokuwa na ukame wa kupata Tuzo, na kwamba Serikali yao ilikuwa imefanya jambo jema kuzirejesha, jumla ya kazi za muziki zilizopokelewa zilikuwa 1,360 kutoka kwa wasanii wapatao 536 waliojisajili na kuwasilisha kazi zao ili kushindania tuzo hizi. Aidha, katika kuhakikisha haki inatendeka mazoezi ya uwasilishaji wa kazi kutoka kwa wasanii pamoja na zoezi la wananchi kupiga kura vilifanyika kupitia mfumo maalumu `wa kielektroni na kusimamiwa na majaji na wakaguzi wabobezi wakiongozwa na mwanamuziki nguli nchini John Kitime. Tuzo hizi zitaendelea kutolewa kila mwaka na Serikali itapanua wigo kwa kuandaa tuzo katika Sanaa nyingine zikiwemo Sanaa za Maonesho na Ufundi. Aidha, Serikali kwa sasa inafanya tathmini na kukusanya maoni kutoka kwa wadau kuhusiana na tuzo hizi ili kuziboresha zaidi katika miaka inayofuata. “Pole pole ndio mwendo”. 
  • Mheshimiwa Spika, mageuzi mengine muhimu ni katika kuwaondolea adha wadau wa Sanaa kwani kwamara ya kwanza imeanzishwa mifumo ya kielektroni ya usajili na utoaji wa vibali mtandaoni. Kwa sasa baada ya kero ya muda mrefu ya wasanii kutoka mikoa yote nchini kulazimika kusafiri kwenda ofisi za BASATA Dar es Salaam, kwa mifumo hii, wasanii wanaweza kujisajili mtandaoni na kupata vyeti na vibali vyao ambavyo vinatumika kuwatambulisha katika mamlaka na taasisi mbalimbali ili wapate huduma wanazohitaji. Mfumo huu unaojulikana kwa jina la Artist Managenment

Information System (AMIS), vibali vyote hutolewa bila ya wasanii kufika katika ofisi za BASATA na hivyo kuwapunguzia gharama. Mathalani, kutokana na matumizi ya mfumo huu muda wa msanii kupata huduma za usajili na vibali umepungua kutoka siku 3 hadi nusu saa tu. Pia, idadi ya wasanii binafsi wanaojisajili imeongezeka toka wasanii 65 kwa mwezi hadi wasanii 200 kwa mwezi. Mfumo huu unapatikana kwenye mtandao kwa kiunganishi (link) cha https://sanaa.go.tz/login.   

  • Mheshimiwa Spika, Baraza pia limeimarisha utendaji wake kwa kuendeleza na kuimarisha utaratibu wa kukutana na kuwashirikisha wasanii na wadau wa Sanaa katika masuala mbalimbali ikiwemo utatuzi wa changamoto zilizopo. Baraza limefanikiwa kushirikiana na wasanii na wadau wa Sanaa katika zoezi la marekebisho ya Kanuni zake Na. 43 za mwaka 2018 pamoja na maandalizi ya Mwongozo wa Usimamizi wa Maadili katika tasnia ya Muziki nchini. Wasanii na wadau wa sanaa zaidi ya 341 walishirikishwa kutoa maoni yao juu ya marekebisho ya Kanuni za BASATA pamoja na Mwongozo tajwa hapo juu. 
  • Mheshimiwa Spika, vilevile, Baraza limefanikiwa kuweka utaratibu wa kuwa na Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa wa mwaka (Annual Art Sector Conference) ambapo wasanii na wadau mbalimbali wa Sekta hii wanashiriki. Lengo la mikutano hii ni kujadili kwa pamoja masuala yanayohusu maendeleo ya Sekta ya Sanaa nchini kati ya Serikali, wasanii na wadau wa sekta hii. 

Katika mwaka 2021/22 mkutano huu ulifanyika katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam, tarehe 29 Septemba, 2021. Baraza litaendelea kuimarisha utendaji wake ili kuongeza tija na ufanisi katika kutoa huduma kwa wasanii na wadau wa sekta ya Sanaa nchini kwa kuendeleza mageuzi ya kulifanya lihamasishe zaidi maendeleo ya Sanaa kuliko kudhibiti zaidi kama zamani. Pamoja na nia hiyo Wizara kupitia Baraza itaendelea kama alivyoagiza Mheshimiwa Rais wakati wa Tamasha la “Dream Concert” tarehe 31 Mei, 2022 kuwakumbusha wasanii kuzingatia maadili.

3.2.2.3 BODI YA FILAMU TANZANIA

(TFB)

  • Mheshimiwa Spika, majukumu ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ni pamoja na kusimamia na kuratibu kazi za filamu ikiwemo kuhakiki na kuzipanga katika madaraja; kutoa vibali vya usambazaji, maonesho ya filamu, michezo ya kuigiza, kampuni za usambazaji wa filamu, kumbi za maonesho ya filamu, maktaba za picha za filamu, studio za uandaaji wa filamu; pamoja na kujenga uwezo wa wadau wa kazi za filamu.
  • Mheshimiwa Spika, kama ilivyokuwa kwa suala la kihistoria la kurejesha Tuzo za Muziki, kwa upande wa filamu, Serikali ya Awamu ya Sita, imefanya mageuzi ya kukumbukwa kwa kuanzisha (haijapata kuwepo) kwa mara ya kwanza Tuzo za Kitaifa za Filamu. Tuzo hizi zilizotolewa Jijini Mbeya mwezi Desemba, 2021, zilishuhudia hamasa kubwa ambapo jumla ya filamu 638 ziliwasilishwa na kupatikana washindi 30 waliopata tuzo na fedha taslimu. 
  • Mheshimiwa Spika, Wizara inapoziangalia tuzo hizi inaona maendeleo ya sekta tena ya kasi kwani tuzo hizi zimewajengea ujasiri na uthubutu wadau wa filamu kushiriki katika tuzo mbalimbali duniani na kupata ushindi. Mathalani, filamu ya Obambo na Safari ya Kifo zilizoibuka na ushindi katika tuzo hizi, zilishiriki na kushinda tuzo ya  kimataifa nchini Marekani na Nigeria. 
  • Mheshimiwa Spika, Bodi ya Filamu Tanzania imeendelea kuwezesha matamasha mbalimbali yanayoanzishwa na wadau wa filamu ambapo  katika kipindi hiki imesaidia kuratibu maandalizi na kufanyika kwa tamasha la tuzo kwa wanafunzi wa Vyuo Vikuu (UNI AWARDS) lililofanyika tarehe 3 Julai, 2021 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (JINCC) Jijini Dar es Salaam. Kupitia tamasha hilo, tuzo 21 zilitolewa kwa wanafunzi waliofanya vizuri katika fani mbalimbali ikiwemo za filamu zilizohusisha washiriki 187. 
  • Mheshimiwa Spika, halikadhalika, Bodi ya Filamu inaratibu programu mbalimbali za mafunzo. Moja ya mafunzo yaliyoratibiwa ni mafunzo kwa njia ya Semina, ambapo Bodi kwa kushirikiana na Kamati Maalumu ya Rais, iliratibu mafunzo ambayo ni mafanikio ya awali kabisa ya Filamu ya Royal Tour. Aidha, mafunzo yaliyoratibiwa ni kuwakutanisha wadau wa filamu na Bw. John Feist, mtayarishaji wa Royal Tour, kutoka Hollywood, nchini Marekani, ambaye alitoa semina hiyo tarehe 29 Aprili, 2022 katika ukumbi wa JNICC Jijini Dar es Salaam kwa wadau takribani 300. 
  • Mheshimiwa Spika, semina hiyo imetoa fursa ya mafunzo mengine kwa wadau wa filamu, ambapo mapendekezo zaidi huko mbele yatahusu namna ya utengenezaji wa mawazo ya kibiashara katika uandaaji wa filamu (Elevator Pitch), matumizi ya teknolojia ya utengenezaji wa filamu yakiwemo matumizi sahihi ya teknolojia ya simu mtelezo (smart phone film), uandishi wa miswada na hadithi za filamu (Script na Story Writing) pamoja na kuwaunganisha waandaaji wa filamu kutoka Tanzania na Marekani (Hollywood). Tunamshukuru Mheshimiwa Rais kwa kushiriki Royal Tour kwani nasi katika sekta zetu tumeanza kuona mafanikio hayo.
  • Mheshimiwa Spika, vilevile, kwa upande mwingine Wizara kwa maguezi yanayoendelea inazidi kuona umahiri wa wanatasnia ya filamu hapa nchini ukiongezeka katika uzalishaji wa filamu bora zinazopata nafasi katika majukwaa ya kimataifa. Mathalani, filamu ya Vuta N’kuvuteiliyoandaliwa mwaka 2021 na inayotoa uhalisia wa hadithi ya Vuta N’kuvute iliyoko kwenye riwaya ya Adam Shaffi, imepata nafasi ya kuzinduliwa katika Tamasha la

Toronto International Film Festival (TIFF) nchini Kanada ambalo ni tamasha kubwa katika matamasha 5 makubwa Ulimwenguni, na ilishinda tuzo ya FESPACO ambayo inashindanishwa nchini Bukinafaso. Filamu hii imeendelea kuoneshwa kwenye matamasha mengi zaidi ya kimataifa na kuendelea kushinda tuzo kadhaa ulimwenguni. Aidha, filamu ya BINTI ambayo tarehe 7 Januari 2022 iliingia katika moja ya majukwaa maarufu zaidi ya usambazaji wa filamu ulimwenguni lijulikanalo kama NETFLIX, inakuza ari ya wadau wa filamu kutengeneza filamu zilizo bora na zenye viwango vya Kimataifa, inatangaza utamaduni wa nchi ikiwemo lugha ya Kiswahili, inaongeza kipato cha wadau wa filamu na Serikali, na inafungua fursa ya washiriki wa filamu wa Kitanzania kwa kampuni za nje na kuwapatia ajira zaidi. 

  • Mheshimiwa Spika, jitihada mbalimbali zimefanyika pia katika kutatua changamoto ya masoko na kuongeza fursa za ajira kwenye tasnia ya filamu nchini. Baadhi ya jitihada hizo ni pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo wenye kampuni za utangazaji kama vile DSTV, Azam, Startimes na wengineo kuweka mazingira rafiki kwa wadau kuuza kazi zao. Kampuni hizo zimeendelea kuongeza uwekezaji, kuongeza idadi ya chaneli zinazoonesha filamu za Kitanzania kwa saa 24, siku 7 za wiki pamoja na kuboresha malipo ya filamu zinazonunuliwa kutoka kwa wadau wa filamu nchini.  
  • Mheshimiwa Spika, vilevile, Serikali imeendelea kuvutia wadau wenye kampuni za usambazaji wa filamu kidijiti kupitia Programu Tumizi kama vile Starmedia, VidoApp, Airtel, Swahiliflix, Kipaji App, Nilipe App, Mambo TV na Noela TV inayotoka nchini Uholanzi. Katika hatua nyingine ya kuwaongezea masoko wadau wake, Bodi ya Filamu imeendelea kuweka mazingira mazuri kwa kushirikiana na wadau kuhamasisha Watanzania kuangalia filamu kwenye kumbi za sinema zinazopatikana kwenye maeneo mbalimbali hapa Tanzania. Mageuzi na hamasa yote hii kwa ujumla, kwa upande wa sanaa ya filamu tu, katika kipindi hiki, tunakadiria kuwa takribani ajira 30,000 zimezalishwa kwenye tasnia ya filamu kupitia filamu 1,713 zilizowasilishwa Bodi ya Filamu kwa ajili ya uhakiki na kupangiwa madaraja.
  • Mheshimiwa Spika, Bodi ilitoa leseni 31 za uendeshaji wa shughuli na biashara za Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini. Leseni hizo zilitolewa ikiwa ni hatua za urasimishaji wa shughuli na biashara ya filamu nchini. Aidha, vitambulisho 125 vilitolewa kwa wadau wanaojihusisha na shughuli za Filamu na Michezo ya Kuigiza. Vilevile, kufikia mwishoni mwa mwezi Aprili, 2022 filamu 1,751 zilipokelewa kwa ajili ya uhakiki na kupangiwa madaraja; na filamu zote zilihakikiwa na kupangiwa madaraja sawa na asilimia 194.5 ya lengo la filamu 900 zilizopangwa kuhakikiwa katika kipindi hicho. Kati ya filamu hizo, za ndani zilikuwa 1,713 na za nje ni 38. Kiambatisho Na.2. Pia, katika kipindi hicho miswada na maombi ya vibali vya kutayarisha filamu 150 imechambuliwa ambapo kati yake, maombi 71 yalikuwa ya watayarishaji kutoka nje ya nchi na maombi 79 kutoka ndani ya nchi. Maombi ya utayarishaji wa filamu nchini hushughulikiwa na Bodi ya Filamu kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya Vibali vya Filamu. Aidha, katika kipindi hiki maombi yote yalipatiwa vibali. Kiambatisho Na.3.
  • Mheshimiwa Spika, Serikalikupitia Bodi ya Filamu Tanzania imeendelea kulinda haki za wasanii kwa kushughulikia malalamiko ya wadau, kutatua migogoro kati yao na kukabiliana na watu wanaofanya shughuli za filamu bila kufuata Sheria hasa kwa upande wa usambazaji filamu. Wadau wa filamu nchini wameendelea kusaidiwa katika upatikanaji wa haki zao ambapo kupitia Kamati ya Kutetea Haki za Wasanii inayoratibiwa na Bodi ya Filamu, malalamiko 12 yalipokelewa. Kati ya malalamiko hayo, malalamiko tisa (9) yalisuluhishwa na malalamiko matatu (3) yanaendelea katika hatua mbalimbali za usuluhishi. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na wasambazaji wasiofuata Sheria, Bodi imefanya operesheni 38 katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam na Mwanza ambapo hatua mbalimbali zilichukuliwa kwa wahusika ikiwemo kuwafikisha mahakamani. Juhudi hizi za kulinda haki za wasanii dhidi ya maharamia wa kazi zao zitaendelea. Ni azma ya Serikali kuona sekta hii ndogo ya filamu katika sekta pana ya sanaa inaendelea kuimarika na hatimaye kufikia azma yetu mpya ya kuanzisha kiwanda kikubwa cha filamu yaani

“Swahiliwood.”

3.2.2.4 TAASISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA).

  • Mheshimiwa Spika, majukumu ya Taasisi ya COSOTA  inayosimamia haki za kiuchumi za wasanii wetu ni pamoja na kukuza na kulinda maslahi ya watunzi, waandishi, wasanii, wafasiri, watayarishaji wa kurekodi sauti, watangazaji, na wachapishaji, hususan kukusanya na kugawa mirabaha au ujira unaotolewa kulingana na haki zao zilizofafanuliwa katika Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7 ya Mwaka 1999.  Aidha, COSOTA ina jukumu la kutunza rejesta za kazi, usanii na vyama vya watunzi, wasanii, wafasiri, watayarishaji wa sauti zilizorekodiwa, watangazaji na wachapishaji. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha haki za wasanii zinapiganiwa, utendaji na usimamizi wa COSOTA uliimarishwa na kuweka rekodi ya ukusanyaji wa mirabaha ambapo kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2021 hadi 31 Desemba, 2021 jumla ya Shilingi 312,290,259 zilikusanywa na kugawanywa kwa wasanii wa muziki ambapo jumla ya wanufaika 1,123 wenye kazi 5,924 walipata mirabaha. Gawio hilo lililotangazwa tarehe 28 Januari, 2022 ni kubwa zaidi kuwahi kukusanywa tangu Taasisi hiyo ilipoanza kutoa mirabaha. Hii ni kutokana na agizo la Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuelekeza vyombo vya Habari (Televisheni na Redio) ambao ni wadau wakubwa wanaotumia kazi za muziki kulipia mirabaha. Mgao huo ni ongezeko la asilimia 58 ukilinganisha na gawio lililofanyika kwa mara ya mwisho mwaka 2019 ambapo lilikuwa la jumla ya Shilingi 183,588,000 tu. Ongezeko hili limetokana na jitihada  za Taasisi za kufikia maeneo mbalimbali yanayotakiwa kulipia, na kuongezeka kwa rasilimali fedha za usimamizi wa majukumu ya Taasisi. Kutokana na jitihada hizi, COSOTA katika kipindi hiki imeweza kugawa mirabaha mikubwa zaidi hadi kiasi cha Shilingi Milioni 8.7 kwa wasanii wa kwaya; na Shilingi Milioni 7.6 kwa msanii binafsi. Mgao kama huu utaendelea kutolewa kila baada ya miezi sita huku Serikali ikiendelea kuboresha mifumo ya ukusanyaji na ugawaji sambamba na kutatua changamoto zilizopo. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza dhamira ya Serikali ya kusimamia haki za wabunifu, COSOTA imefanya mapitio ya Kanuni za leseni na utangazaji za mwaka 2003 zinazotumika kukusanya mirabaha na kuja na  Kanuni mpya za Leseni na Haki ya Kunufaika na Mauzo Endelevu ya Mwaka 2022 zilizoanza kutumika kuanzia tarehe 18 Machi, 2022 baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali kupitia Tangazo Na.137 la mwaka 2022. Kanuni hiyo imeweka viwango rafiki vinavyolipika katika maeneo mbalimbali yanayotumia kazi za muziki na filamu ikiwemo Vyombo vya Usafiri, Redio na Televisheni pamoja na maeneo mengine yanayotumia kazi hizo. Kupitia Kanuni hii, kutakuwa na ongezeko la makusanyo ya mirabaha. Vilevile, itasaidia wasanii wa sanaa za ufundi kunufaika na haki ya mauzo endelevu. 
  • Mheshimiwa Spika, Serikali pia, imefanya marekebisho ya Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Sura ya 218 Toleo la Mwaka 2002 kwa kuingiza vifungu vya Mkataba wa Marrakesh na kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari, 2022. Hii imetoa fursa kwa Watu Wenye Ulemavu wa Macho au uoni hafifu kuchapisha machapisho mbalimbali katika maandishi yanayoshikika pasipo kuomba ridhaa ya mmiliki wa chapisho husika. Vilevile, Serikali kupitia COSOTA, imeanza mchakato wa kupitia Kanuni ya usajili wa wanachama na kazi zao kupitia Tangazo la Serikali Na. 18/2006 na tayari rasimu ya Kanuni hiyo imeandaliwa kwa lengo la kuwasilishwa kwa wadau ili kupata maoni yao. Fauka ya hayo, Taasisi imepitia na kuhuisha Kanuni zake za Utumishi ili kuongeza ufanisi katika Usimamizi wa Rasilimali Watu na kuongeza tija.
  • Mheshimiwa Spika, COSOTA kama ilivyokuwa kwa BASATA na Taasisi nyingine, nayo imeboresha mfumo wa kuwahudumia wanachama wake kidigitali ambapo ilikamilisha uboreshaji wa mfumo wa usajili na utoaji wa Leseni kwa Watumiaji wa Kazi za Ubunifu kwa njia ya kielektroniki (AMIS) uliozinduliwa rasmi tarehe 22 Novemba, 2021. Mfumo huu unawezesha  kutambua wabunifu

na kazi zao lakini pia kutambua watumiaji wa kazi za sanaa bila ya wao kutembelea ofisi za COSOTA zilizopo Dar  es Salaam au Dodoma. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 COSOTA imesajili jumla ya Wabunifu 444na kazi zao 3,021. 

  • Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza jukumu la kutoa elimu ya masuala ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa Wabunifu ilikuelewa wajibu na haki zao, COSOTA imetoa elimu kupitia njia mbalimbali ikiwemo vyombo vya habari ambapo zaidi ya vipindi 55 vimefanyika kupitia Redio na Televisheni. Aidha, kwa upande wa mitandao ya kijamii, zaidi ya taarifa 95 ziliwekwa kwenye mitandao ya Instagram, Twitter,  Facebook na Youtube. Pia, Taasisi imetoa elimu kwa makundi mbalimbali ya wadau kupitia Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Shirikisho la Muziki Tanzania, Shirikisho la Sanaa za Maonesho, Shirikisho la Sanaa za Ufundi, Watayarishaji wa Muziki, Chama cha Tanzania Producers and Composers Association (TPCA), Wasanii wa Muziki wa Injili kupitia Shirika la Tanzania Music Foundation (TAMUFO), Waandishi wa Vitabu, Wasanii wa Muziki wa Dansi, Wamiliki wa Vyombo vya Habari, Wahariri kwa kushirikiana na Kampuni ya Multichoice Tanzania na Mafunzo kwa Mahakimu kwa kushirikiana na Chuo cha Mahakama Lushoto na Mahakama ya Tanzania na Kampuni ya Azam Media.
  • Mheshimiwa Spika, kwa kufahamu kwamba Sheria ya Hakimiliki ina mipaka na kazi za wasanii wetu zinatumika  sehemu mbalimbali duniani COSOTA imeingia makubaliano na Taasisi mbalimbali duniani zinazofanya kazi kama za COSOTA. Makubaliano hayo yanawezesha usimamizi wa haki za wasanii wetu katika nchi hizo ambapo inawezesha pia wao kunufaika na mirabaha inayokusanywa na taasisi hizo. Taasisi ambazo tayari tuna makubaliano ni pamoja na CAPASSO

(Composers Authors and Publishers Association of South Africa) ya Afrika Kusini ambayo husimamia matumizi ya kazi za wasanii kwenye mitandao ya  kijamii. Aidha, kutokana na makubaliano haya mwezi Aprili, 2022 wataalamu kutoka nchini Afrika Kusini walikuja nchini kutoa elimu kwa wataalam wa COSOTA kuhusu matumizi ya mfumo wa CAPASSO-Portal unaowezesha wasanii wetu kujisajili pamoja na kazi zao ili wanufaike na mirabaha wanayoikusanya

  • Mheshimiwa Spika, pia, COSOTA ina makubaliano na mashirikisho mengine ya kimataifa kama vile The International Federation of Reproduction Rights Organizations, GHAMRO – Ghana, SAMPRO –

Afrika Kusini, RSAU – Rwanda, COSOZA –

Zanzibar, NASCAM – Namibia, COSOMA – Malawi, UPRS – Uganda, ZAMCOPS – Zambia, IPRS – India, TEOSTO – Finland, SPA – Ureno, MASA – Mauritania na AGADU – Uruguay. Halikadhalika, majadiliano yanaendelea ili kushirikiana na vyama na mashirikisho mengine. Ushirikiano huu ni mkakati mwingine muhimu wa kuhakikisha COSOTA inatoka kuwa na uwezo wa ndani tu wa kukusanya haki za wasanii hadi kujijengea wigo wa kufuatilia na kukusanya haki za wasanii wetu popote kazi zao zinakotumika nje ya nchi. Huu ndio mwelekeo tunaokwenda kuuimarisha katika mwaka ujao wa fedha, sanaa ni ajira, sanaa ni biashara na hakika sanaa ni uchumi.

3.2.2.5 TAASISI YA SANAA NA

UTAMADUNI   BAGAMOYO     

(TaSUBa)

  • Mheshimiwa Spika, hatuwezi kuendeleza sanaa bila kuwekeza katika utaalamu na utafiti; TaSUBa ni Taasisi inayotoa mafunzo ya aina mbalimbali kuhusiana na masuala ya Sanaa na Utamaduni nchini. Mwaka 2012 TaSUBa iliteuliwa kuwa Kituo cha Jumuiya ya Afrika Mashariki chenye Ubora Uliotukuka katika ufundishaji wa fani za utamaduni na sanaa hivyo ni kituo chenye hadhi ya kimataifa. 
  • Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu huo, Wizara kwa kushirikiana na uongozi wa chuo imeweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha na kuongeza udahili ambapo mwaka 2021/22 TaSUBa ilipanga kudahili wanafunzi 600 katika programu za Astashahada na Stashahada ambapo hadi mwezi Aprili, 2022 ilidahili jumla ya wanachuo 695 na walioendelea na masomo ni wanachuo 533 ukilinganisha na usajili wa Mwaka 2020/21 ambapo wanafunzi 300 pekee walisajiliwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 78. Sambamba na hilo, TaSUBa inafanya juhudi za ufundishaji wa kozi fupi ili kuwafikia vijana wengi zaidi. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 TaSUBa iliendesha mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 275. 
  • Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa mafunzo na kuongeza nafasi zaidi kwa vijana wa Kitanzania kujiunga na sekta ya ubunifu, Taasisi imejipanga kuongeza mitaala mipya zaidi ya iliyopo sasa. Hatua hii itasaidia kutoa wigo mpana kwa wanafunzi kuwa na uchaguzi wa  masomo. Mitaala mipya ni pamoja na Uongozi wa Sanaa na Masoko; Urithi wa Utamaduni na Utalii; na Muziki. Katika kutekeleza hilo, Taasisi inafanyia kazi marekebisho yaliyoagizwa na NACTE ili kukidhi vigezo vya kupatiwa ithibati.
  • Mheshimiwa Spika, Taasisi iliendesha Tamasha la 40 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo lililofanyika tarehe 28-30 Oktoba, 2021 na kuhudhuriwa na watazamaji wapatao 75,000 kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi. Tamasha hilo pia lilirushwa mubashara kupitia televisioni  mbalimbali ndani na nje ya nchi. Jumla ya vikundi 79 vilishiriki kufanya maonesho ya sanaa za jukwaani ambapo vikundi 75 vilitoka nchini (Tanzania Bara na Zanzibar) na vikundi vinne (4) vilitoka nje ya Tanzania; Mayotte na India. Wakati wa maonesho hayo, Sanaa mbalimbali zilioneshwa zikiwemo ngoma, muziki, maigizo, sarakasi, vichekesho na mazingaombwe. Aidha, Vyombo vya Habari 25 vikiwemo redio, runinga, magazeti na blogu vilishiriki kutangaza shughuli mbalimbali za Tamasha. Matarajio ni kuongeza ushiriki wa vikundi kutoka nje katika tamasha lijalo.
  • Mheshimiwa Spika, ikiwa ni kuendeleza na kupima uwezo wa Taasisi kwa kuwatofautisha na vijana wengine wenye vipaji bila elimu, wanachuo wa Taasisi hii wamekuwa wakishiriki mashindano mbalimbali ya Sanaa ya Kitaifa ya kuibua vipaji mbalimbali kwa kufanya vizuri. Mashindano haya yanasadia kuhamasisha vijana katika kufanya kazi zao kwa weledi, bidii na maarifa na kutambua umuhimu wa elimu. Vijana kutoka TaSUBa wameendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali kama inavyobainishwa  katika  jedwali lifuatalo: 

Mashindano Yaliyoshirikisha Wanafunzi wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo Katika Mwaka 2021/22 na Hatua

Waliyofikia

NaAina ya ShindanoMwakaKundi (Category)Hatua Waliyofikia
1UN-Awards2021KuimbaNusu Fainali
2UN-Talents2021KuimbaFainali
3Taifa Cup2021Mziki           wa Bongo      Flava (Kuimba)Nafasi    ya Kwanza
4UN-Talents2022KuimbaNafasi    ya Kwanza

Chanzo: Taasisi ya Sanaa na Utamaduni 

Bagamoyo, 2022

3.2.3 SEKTA YA MAENDELEO YA MICHEZO 

3.2.3.1 IDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO 
  1. Mheshimiwa Spika, Sekta ya Maendeleo ya Michezo ni mhimili mwingine muhimu wa ajira na siha za watu wetu hapa nchini na inahusisha Idara ya Maendeleo ya Michezo, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu, kazi kubwa ya kupigiwa mfano iliyoanza kufanyika ni kuanza kushughulikia tatizo sugu la miundombinu ya michezo ambayo kwa muda mrefu imekuwa na changamoto au kuanzisha mipya inayoendana na matakwa ya sasa. Serikali ya Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuja na mtazamo mpya katika eneo hili  na imetekeleza miradi kadhaa ya kihistoria kama ifuatavyo:

Mosi,uamuzi wa kimkakati wa kujenga viwanja changamani vya michezo na sanaa (Sports and Arts Arena) katika mikoa ya Dodoma na Dar es salaam, umefikia hatua muhimu ambapo usanifu wa michoro

(Architectural Design) umekamilika na sasa Serikali imetenga fedha za kuanza ujenzi lakini pia inazungumza na wadau wa sekta binafsi ili kutekeleza kwa pamoja ambapo sasa Tanzania inakwenda kuwa na Arena ya kwanza nchini zitakazokuwa na uwezo wa kuchukua wastani wa watu 16,000 kwa wakati mmoja kila moja. Kiambatisho Na.4A muonekano wa uwanja wa Sports

and Arts Arena;  

Pili,Tumeanza hatua za ujenzi wa Viwanja vya mazoezi na mapumziko (Recreational and Leisure Centres) vitatu katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Geita ambapo hatua zote za usanifu zimekamilika na sasa ujenzi utaanza mara moja na tayari Wizara imeshapokea Shilingi Bilioni Tatu (Sh.3,000,000,000) kuanza ujenzi huo. Kiambatisho Na.4B muonekano wa maeneo ya kupumzikia wananchi;  

Tatu, Ujenzi wa Kiwanja kikubwa cha michezo Jijini Dodoma nao umeendelea katika hatua za kutafuta mkandarasi baada ya upembuzi na hatua zote za maandalizi kukamilika. Kiambatisho Na.4C muonekano wa uwanja wa mpira wa miguu utakaojengwa Dodoma;

Nne, Mkakati mwingine ni ujenzi wa Kituo cha Umahiri katika michezo (Center of

Excellence) katika Chuo cha maendeleo ya Michezo Malya na hosteli mpya ya wanafunzi ambapo kwa upande wa Kituo cha Umahiri, hatua zote za usanifu zimekamilika huku ujenzi wa hosteli ukifikia asilimia 40. Vituo hivi vitakigeuza kilichokuwa chuo cha kawaida cha michezo Malya sasa kuwa na taswira mpya na kuwa Kituo cha Kimataifa kitakacholea watoto wenye vipaji kutoka mitaani huku kikiendelea kutoa mafunzo kwa vijana waliotoka mashuleni. Mwelekeo huu utasaidia kuzalisha wasomi wa michezo lakini pia na wanamichezo mbalimbali waliopikwa wakiwa wadogo. 

  1. Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine katika miundombinu ni pamoja na Serikali kutoa fedha za ukarabati na hatimaye kuurejesha uwanja wa michezo wa ndani wa Taifa uliokuwa umesitishwa kutumika kutokana na uchakavu na hii ilihusisha pia kuweka vifaa vya kisasa vya mazoezi (gym) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam. Mafanikio ya kuurejesha tu uwanja wa ndani wa michezo tayari yameamsha ari ya michezo ya ndani na pia nchi imekuwa mwenyeji wa mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo ya mpira wa mikono, mpira wa pete, mpira wa kikapu na mashindano ya ngumi yaliyomalizika hivi karibuni na kuhusisha nchi zaidi ya tano za Afrika.
  2. Mheshimiwa Spika, pamoja na hatua hizi muhimu, lakini ni ukweli ulio wazi kuwa kwa mujibu wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 na mantiki tu, suala la miundombinu haliwezi kubaki kwa Serikali peke yake bali linahusu wadau mbalimbali wa michezo kuwekeza katika maeneo mengine. Hapa niwapongeze wadau wote waliofanya jambo moja au jingine katika kuwekeza katika miundombinu ya kisasa na wanaoendelea kufanya hivyo. Mathalani, nakipongeza Chama cha Mapinduzi (CCM) na wadau wake kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan na ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa aliyoyatoa Jijini Mwanza mwaka jana, Chama hicho kimeendelea na mkakati wa kuboresha viwanja vyake hasa vya soka vinavyotumika kwenye ligi mbalimbali nchini na sasa vimeanza kuwa na sura mpya.
  3. Mheshimiwa Spika, siwezi pia kuishiwa wingi wa shukrani kwa baadhi ya Halmashauri kama Geita, Ruangwa; na majiji kama Arusha na Mwanza, Manispaa za Temeke na

Kinondoni kwa viongozi wao kuona umuhimu wa michezo na kutumia fedha zao wenyewe kufanya ukarabati wa viwanja vyao au kuanza miradi ya ujenzi mpya wa viwanja huku wataalamu wa Wizara wakisaidia kutoa ushauri wa kiufundi. Hapa pia tutambue uwekezaji muhimu wa Jiji la Dodoma katika eneo la Chinangali lenye viwanja vingi vya michezo ikiwemo mpira wa kikapu, mpira wa pete, mpira wa mikono na michezo mingine. Nitumie fursa hii kuwaomba Wakurugenzi wengine nchini kufuata nyayo hizi kwani Sera ya Michezo inatupa hamasa hizo. 

  1. Mheshimiwa Spika, vilevile, mashirikisho mbalimbali ya michezo nchini nayo yamewekeza katika ujenzi na ukarabati wa miradi ikiwemo Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) wanaojenga vituo viwili vya michezo katika miji ya Dar es salaam na Tanga ambavyo viko katika hatua za mwisho za ujenzi. Hatua hii itasaidia kuboresha timu zetu kwa kuwa na vituo maalumu vya kukuzia michezo, kambi maalum na zenye utulivu za timu za Taifa kama ilivyo kwa nchi nyingine zilizoendelea katika sekta ya michezo ili nasi tuendelee kushiriki kisayansi zaidi katika mashindano yenye ushindani. 
  2. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua umuhimu wa kuanza kuendeleza vipaji vya michezo katika hatua ya awali kwa kufuata misingi ya kisayansi ya uendelezaji na uibuaji wa vipaji, Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia tumekamilisha utekelezaji wa maelekezo ya Mheshimiwa Rais kwa hatua ya kwanza ya kuteua jumla ya shule 56 kuwa shule maalumu za Michezo nchini ikiwa ni shule mbili (2) za Sekondari kila Mkoa isipokuwa mikoa minne ya Iringa, Ruvuma, Morogoro na Mwanza ambayo itakuwa na shule tatu (3) ili kuwapokea watoto wenye mahitaji maalumu. Shule hizi zitakuwa kwenye uangalizi na mkakati kabambe ambapo zitakarabatiwa miundombinu yake na kupangiwa walimu na vifaa vya kufundishia. Katika mwaka ujao wa fedha Serikali imetenga Shilingi Bilioni Mbili kuanza kazi hii. Kiambatisho Na.5: Shule 56 zilizoteuliwa kuwa shule maalumu za michezo nchini kwa kuzingatia vigezo mbalimbali ikiwemo uwepo wa viwanja kwa sasa, miundombinu mingine na jiografia.  
  3. Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mkakati huu utakaohitaji takribani Shilingi Bilioni 19 za kuanzia, tayari Wizara yangu kwa kushirikiana na OR-TAMISEMI tumeanza ukarabati wa Shule za Tabora Wavulana na Wasichana mkoani Tabora zitakazotumika wakati wa mashindano ya Shule za Sekondari (UMISSETA) na Shule za Msingi

(UMITASHUMTA) kitaifa mwezi Agosti, 2022. 

  1. Mheshimiwa Spika, hapa pia nieleze kuwa tumeendelea kuboresha michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA ambayo huko nyuma ilififia. Zoezi la uratibu mpya na wa pamoja chini ya Wizara tatu (3) za Utamaduni, Sanaa na Michezo; Elimu, Sayansi na Teknolojia; na OR-TAMISEMI lilifanyika vizuri katika michezo ya mwaka 2021 iliyofanyika mkoani Mtwara. Maandalizi ya vikao na ukarabati wa miundombinu ya michezo katika shule hizo unaendelea vizuri. Michezo hii ni muhimu na imekuwa chachu kubwa ya kuibuwa wachezaji mbalimbali wanaocheza katika timu zetu za Taifa za vijana zinazofanya vizuri katika ukanda wetu wa Afrika. Wizara itaendelea kuisimamia michezo hii ili izidi kuwa chemchem ya kuzalisha vipaji. 
  2. Mheshimiwa Spika, kufanikisha michezo hakuwezi kwenda bila kuwa na mikakati Madhubuti, katika kipindi hiki, Serikali imekamilisha Mkakati wa Maendeleo ya Michezo nchini wa mwaka 2022-2032.Mkakati huu umeandaliwa ili kuhakikisha Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995 inatekelezwa kwa ufanisi ukilenga kuzipatia ufumbuzi changamoto zilizojitokeza katika kipindi cha miaka 27 ya utekelezaji wake. Mambo muhimu yaliyozingatiwa katika Mkakati huo ni pamoja na kuongeza ushiriki wa wananchi katika michezo na mazoezi ya viungo; kuwa na miundombinu na vifaa vya michezo vinavyoendana na mahitaji; kuimarisha uteuzi na malezi ya timu za Taifa na kuwa na michezo ya kipaumbele Kitaifa. 
  3. Mheshimiwa Spika, masuala mengine ni kuimarisha upatikanaji wa wataalamu wa michezo; ugharimiaji wa shughuli za michezo pamoja na kuimarisha utalii wa michezo. Aidha, Mkakati unabainisha mgawanyo wa majukumu kwa wadau mbalimbali ili kuwezesha malengo kufikiwa na Mfumo wa Ufuatiliaji na Tathmini. Mkakati ulizinduliwa na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo kilichofanyika Jijini Dodoma tarehe 4 hadi 6 Aprili, 2022.  
  1. Mheshimiwa Spika, ili kulinda wanamichezo wetu na kutoruhusu matumizi ya dawa haramu michezoni, Serikali imeendelea na zoezi la kuandaa Sheria ya Kudhibiti Matumizi ya Dawa na Mbinu Haramu Michezoni inayolenga kuanzisha chombo cha kitaifa cha kuratibu na kusimamia masuala ya Matumizi ya Dawa na Mbinu Haramu Michezoni (National AntiDoping Organization-NADO). Sheria hiyo inahitajika kwa ajili ya kudhibiti uzalishaji, usafirishaji, uagizaji, usambazaji, uuzaji na utumiaji wa dawa na mbinu haramu michezoni; kuweka utaratibu utakaowataka wazalishaji na wasambazaji wa virutubisho (nutritional supplements) kuwa na mfumo bora wa uuzaji na usambazaji wa bidhaa hizo; na kuhakikisha watendaji ikiwemo mameneja, madaktari, makocha, waamuzi na wachezaji hawajihusishi na vitendo vya matumizi ya dawa na mbinu haramu michezoni. 
  2. Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu  wa malezi ya timu zetu  za Taifa ili kuziwezesha kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa, Serikali ilifanya uamuzi mwingine mgumu na muhimu katika miaka ya karibuni wa nayo kutobaki mtazamaji bali kurejea kutenga fedha kwa ajili ya walau, kwa kuanzia kusaidia timu za Taifa. Mathalani, kuanzia mwaka 2019/20 Serikali ilitenga jumla ya Shilingi 270,000,000; mwaka 2020/21 Shilingi 431,000,000 lakini ikaongeza kiasi hicho hadi Shilingi 1,320,000,000 mwaka 2021/22. Usaidizi wa Timu za Taifa kutoka Serikalini na wadau mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo umekuwa ukiongezeka kwa kasi kubwa ambapo mwaka 2022/23 Serikali imeongeza bajeti kutoka Sh.1,320,000,000 za mwaka 2021/22 hadi Sh.1,446,900,000 mwaka 2022/23 sawa na ongezeko la asilimia 9.6.
  3. Mheshiwa Spika, ikiwa ni juhudi za kuimarisha ushirikiano na wadau, Serikali kupitia Wizara ninayoisimamia, iliratibu Kikao Kazi cha Maafisa Utamaduni na Michezo nchini kilichofanyika katika ukumbi wa Mtakatifu Gasper Jijini Dodoma tarehe  04 – 06 Aprili, 2022. Katika kikao hicho mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwa ni pamoja na Programu maalumu ya michezo Mtaa kwa Mtaa ambayo itazinduliwa hivi karibuni ikiwa ni  mashindano yanayolenga kuhamasisha umma kushiriki katika michezo tangu ngazi za awali; kuibua vipaji vya michezo katika ngazi ya mitaa, vijiji, Kata, Tarafa, Wilaya na mikoa na hatimaye Taifa (Taifa Cup). Pia, Mashindano haya yanalenga kuunganisha na kujenga mshikamano katika jamii kwa kupitia michezo na kuifanya jamii kuelewa umuhimu wa Michezo katika ujenzi wa uchumi binafsi na nchi kwa ujumla.  
  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na programu ya michezo ya mtaa kwa mtaa inatarajiwa vijana kati ya 50-100 kutoka mikoani watapata nafasi ya kushiriki michezo ya kitaifa. Halikadhalika, inatarajiwa jumla ya washiriki 724,370 watashiriki/watapata ajira katika michezo kwa mchanganuo ufuatao: mpira wa miguu (255,780); netibali (42,630); riadha (127,810); mpira wa wavu (127,810); mpira wa kikapu (127,710); na ngumi

(42,630).  

  1. Mheshimiwa Spika; uwekezaji wa serikali na wadau wengine katika michezo, ikiwemo Serikali kuendelea kuimarisha bajeti za michezo, vimeleta mwanga mpya wa matumaini, huku pia siri nyingine kubwa ikiwa ni umoja na ushirikiano kati ya wadau na Serikali na vyombo vyake kama BMT. Tumeona na sasa tumejifunza, pale ambapo kuna ushirikiano wa dhati na mikakati ya pamoja timu zetu zinapata morali na zinafanya vyema. Hapa naomba kulishirikisha Bunge lako tukufu katika baadhi ya mafanikio kwa baadhi ya michezo katika kipindi hiki kama ifuatavyo:

Kwa upande wa mchezo wa ngumi; Tanzania imeendelea kufanya vizuri kimataifa, mabondia mbalimbali wamefanikiwa kushinda mataji kadhaa ya kimataifa ikiwemo: 

  1. Bondia Twaha Kiduku alimchapa Alex

                                         Kabangu       kutoka       Jamhuri       ya

Kidemokrasia ya Congo (DRC) katika pambano lililofanyika tarehe 26 Machi, 2022, Tanzanite Hall, Morogoro na kutwaa ubingwa wa UBO Africa katika uzito wa kilogramu. 76; 

  • Bondia Tony Rashid alimtwanga Bongani Mahlangu kutoka nchini Afrika ya Kusini katika pambano lililofanyika tarehe 25 Februari, 2022, Kilimanjaro Hall, Ubungo Plaza na kutwaa ubingwa wa ABU uzito wa kilogramu 55; na
    • Bondia Hassan Mwakinyo alimtandika Julius Indongo kutoka Namibia kwa Kock Out (KO), katika pambano lililofanyika tarehe 3 Septemba, 2021, Kilimanjaro Hall, Ubungo Plaza na kutwaa ubingwa wa ABU Superwelter uzito wa kilogramu 69; Aidha, Bondia Hassan Mwakinyo anashikilia nafasi ya 8/2144 kwa mabondia wa Afrika kwa uzito tofauti tofauti. Aidha, anashikilia nafasi ya 1/172 kwa mabondia wa Afrika kwa uzito wake; na anashikilia nafasi ya 15/1898 kwa mabondia wa duniani wa uzito wake.
  1. Mheshimiwa Spika, Timu yetu ya Taifa ya Soka la Walemavu (Tembo Warriors), ilitutoa kimasomaso baada ya mwezi Novemba, 2021 kufuzu kwenda kucheza Kombe la Dunia nchini Uturuki Oktoba, 2022 kufuatia Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano yaliyoshirikisha zaidi ya nchi 13 za Afrika na kufanyika Dar es Salaam, Tanzania. Itakumbukwa ili kuchagiza ushindi huo Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  alimtuma Mheshimiwa Waziri Mkuu kwenda kambini na kutoa kiasi cha Shilingi milioni 150 zilizosaidia kuitunza timu yetu ya Taifa na maandalizi mengine. Haikuwa kazi rahisi kwa Tembo Warriors kwani  ili kupata nafasi hiyo walifanya yafuatayo: 
    1. Waliichabanga timu ya Morocco mabao

2-1; 

  • Waliicharaza timu Sierra Leone mabao

1-0; pia, 

  • Waliibugiza timu ya Cameroon kwa mabao 5-0.
  • Mheshimiwa Spika, timu hiyo kwa sasa  ipo kambini tangu mwezi Februari, 2022 kwa maandalizi ya mashindano ya Kombe la Dunia ambapo Serikali ndio inagharimia kambi hiyo kwa matumizi yote ikiwemo malazi,  chakula, ufundi, usafiri wa ndani na nje pamoja na posho za wachezaji na benchi lao la ufundi.
  • Mheshimiwa Spika, mafanikio mengine makubwa ni kwa Timu zetu za Taifa za wanawake ambazo nazo zimeendelea kufanya vyema kimataifa ikiwemo Twiga Stars iliyotwaa Kombe la COSAFA mara tatu mfululizo na Timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya U17 ya Serengeti Girls ambayo inafanya vizuri katika mashindano ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa Wanawake. Hadi kufikia tarehe 03 Juni, 2022, Serengeti Girls ilifanikiwa kuzifunga timu zifuatazo:
    • Iliibugiza Timu ya Taifa ya Botswana kwa jumla ya magoli 11-0; 
    • Ikaibamiza timu ya Burundi kwa jumla ya magoli 5-2 na 
    • Iliichabanga timu ya Cameroon kwa magoli 4-1 ugenini kabla ya kurudiana hapa nyumbani.
  • Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) itahakikisha kuwa timu hiyo inapatiwa malezi na mafunzo yanayostahili ili iweze kuendelea kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali Duniani. Aidha, nazipongeza sana timu zetu zote kwa hatua kubwa zilizofikia.
  • Mheshimiwa Spika, Tanzania pia katika kipindi hiki imefanya vyema katika mchezo wa Kabaddi Afrika mashindano yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo nchi za Misri, Cameroon, Kenya na Tanzania zilishiriki, katika mashindano hayo Tanzania ilishika nafasi ya pili kwa timu ya wanawake na wanaume na wachezaji wawili  (2) walipata ajira ya kucheza mchezo wa kulipwa nchini India. Kwa upande wa mchezo wa Karatetimu ya Taifa ya mchezo wa Shotokhan karate  ilitwaa medali 27 (7 za dhahabu, 8 za fedha na 12 za shaba) katika mshindano yaliyofanyika nchini Congo (Congo DRC). Kati ya medali hizo 27, medali 13 zilitwaliwa na wachezaji wanawake na zilizobaki 14 zilitwaliwa na wanaume.
  • Mheshimiwa Spika, jambo jingine la kihistoria katika mageuzi kwenye michezo ni maandalizi ya kimkakati ya Timu za Taifa ambapokwa mara ya kwanza Serikali imeweza kugharimia maandalizi ya  timu za Taifa zinazojiandaa na mashindano ya Michezo ya Jumuiya ya Madola itakayofanyika nchini Uingereza katika jiji la Birmigham na maandalizi ya Tembo Warriors kwenda Kombe la Dunia Uturuki Oktoba mwaka huu. Timu hizo za michezo ya Ridhaa, Ngumi, Judo, Mchezo wa kuogelea pamoja na kunyanyua vitu vizito (Powerlifting) kwa watu wenye ulemavu ambapo timu zote kama ilivyoelezwa hapo awali zipo kambini tangu mwezi Februari, 2022 na zinaendelea na mechi au mapambano ya kirafiki. 
  1. Mheshimiwa Spika, Serikali imegharimia kambi hizo kwa kulipa malazi, chakula, mavazi, huduma za afya na wachezaji wamelipiwa bima za afya, posho za kujikimu na kulipa benchi la ufundi kwa kambi zote. Lengo letu ni kuhakikisha kuwa timu zetu zinapata malezi bora ili wachezaji watimize majukumu yao kimichezo na kuliletea ushindi Taifa letu kimataifa. Huu ndio utakuwa mwelekeo wetu mpya kama Serikali kuhakikisha Timu za Taifa hazibaki tu mikononi mwa vyama na mashirikisho,

Serikali nayo inashiriki kuweka mchango wake na kwa pamoja si tu, tutashinda, bali uzoefu wa miaka miwili hii unaonesha kabisa umoja huu ni ushindi. 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2019/20 si kambi ya Jumuiya ya Madola tu na ushiriki wa Tembo Warriors Uturuki, bali pia, Timu mbalimbali za Taifa zilizofuzu kuiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya Kimataifa zilipatiwa usaidizi. Miongoni mwa timu hizo ni pamoja na timu ya wachezaji watatu (3) wa riadha walioshiriki michezo ya Tokyo-Japan mwaka 2021 iliyofanyika mwezi Julai – Agosti, 2021 ambapo Mtanzania Alphonce Felix Simbu alishika Nafasi ya saba (7), Failuna Abdi Matanga Nafasi ya 22 na Gabriel Gerald Geay alishindwa kumaliza baada ya kupata ajali akiwa katika mashindano hayo. Aidha, mwezi Mei, 2022 mwanariadha Emanuel Giniki Gisamoda alishika nafasi ya kwanza katika mashindano ya Generali Geneve Marathon yaliyofanyika nchini Uswisi na katika mashindano ya Generali Milan Marathon yaliyofanyika mwezi Machi, 2022 katika Jiji la Milan Italia, mwanariadha Alphonce Felix Simbu alishika nafasi ya tatu (3). Pamoja na wanariadha hao, Timu 12 za Taifa ziliwezeshwa kushiriki mashindano ya Kimataifa. Mafanikio mengine nitayaeleza kwa kina katika eneo la Baraza la Michezo la Taifa (BMT). 
  2. Mheshimiwa Spika katika kuhakikisha kuwa sekta ya michezo kwa kutumia Utalii wa michezo inalitangaza Taifa letu, Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Coca-Cola walishirikiana kuleta Kombe la Dunia litakaloshindaniwa Nchini Qatar mwezi Novemba, 2022 katika mashindano ya Kombe la Dunia kwa mchezo wa mpira wa miguu.

Kombe hili liliwasili nchini tarehe 31 Mei, 2022 na kupokelewa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ikulu ya Dar es Salaam na baadae wananchi kupata fursa ya kuliona kombe hilo tarehe 01 Juni, 2022 katika uwanja wa Benjamin Mkapa. 

  1. Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ipo kwenye maandalizi ya kuwa wenyeji wa Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) utakaofanyika katika Jiji la Arusha mwezi Agosti, 2022. Kikao hicho kitahudhuriwa na wawakilishi kutoka katika nchi 54 za Bara la Afrika pamoja na viongozi wa juu wa Shirikisho la Mpira Duniani (FIFA) wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Gianni Infantino. Inakadiriwa kuwa zaidi ya washiriki 300 watahudhuria. Hii itakuwa ni fursa muhimu kwa nchi yetu kuendelea kujitangaza duniani kiutalii, kiuchumi na kiutamaduni.
  2. Mheshimiwa Spika, sambamba na jitihada hizo, Wizara imeendelea kuhamasisha matumizi ya vivutio mbalimbali vilivyopo nchini kwa kutumia michezo, sanaa na utamaduni ili kuvutia uwekezaji zaidi nchini pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa. Katika kufanikisha hilo, Wizara kwa kushirikiana na wadau iliandaa maonesho ya mechi ya fainali ya Kombe la UEFA kati ya Timu ya Real Madrid na Liverpool iliyofanyika tarehe 28 Mei, 2022 juu ya Daraja la Tanzanite Jijini Dar es Salaam.

3.2.3.2 BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA

(BMT)

  1. Mheshimiwa Spika, majukumu ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ni pamoja na kuendeleza, kustawisha na kusimamia aina zote za michezo ya ridhaa na kulipwa kwa kushirikiana na Vyama na Mashirikisho ya Michezo; kuhimiza na kutoa fursa za ushirikiano miongoni mwa Vyama vya Michezo; kuidhinisha mashindano na matamasha ya Kitaifa na Kimataifa yanayoandaliwa na Mashirikisho au Vyama vya Michezo na kuamsha ari ya wananchi kupenda aina zote za michezo.
  2. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha shughuli za michezo zinafanyika kwa ufanisi mkubwa Serikali katika kipindi hiki kwa mara ya kwanza imeridhia kutoa asilimia tano (5) ya kodi ya michezo ya kubashiri matokeo kupitia BMT kama chanzo cha mapato katika Mfuko wa Maendeleo ya Michezo nchini ikiwa ni juhudi za kimkakati za kusaidia maendeleo ya michezo nchini.  Serikali imetekeleza hilo na hadi sasa tayari kiasi cha Sh.

2,049,614,866.20 zimepokelewa. 

  1. Mheshimiwa Spika, kazi zilizofanyika kutokana na fedha hizo ni pamoja na kuandaa mashindano ya Taifa Cup Desemba, 2021, kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana wa kitanzania ambapo mashindano haya yalihusisha mikoa 30 ya Tanzania Bara na Zanzibar na yalirejea baada ya miaka mingi ya kutofanyika; kuratibu mashindano ya Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu Barani Afrika (CANAF) ambapo nchi 13 zilishiriki ikiwemo mwenyeji Tanzania, Uganda, Kenya, Angola, Nigeria,

Cameroon, Misri, Morocco, Liberia, SierraLeone, Zanzibar, Ghana na Gambia. Aidha, mashindano hayo kama nilivyoeleza awali Tanzania sasa itashiriki Kombe la Dunia nchini Uturuki mwezi Septemba – Oktoba, 2022. 

  1. Mheshimiwa Spika, fedha hizo pia zimetumika kugharamia timu mbalimbali za taifa ambazo zimeshiriki mashindano mbalimbali ya Kimataifa kama ifuatavyo: 
    1. Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya

Wanaume (Taifa Stars); 

  • Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu kwa

Wanawake (Twiga Stars); 

  • Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya

Wanawake chini ya Umri wa miaka 20

(Tanzanite); 

  • Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya

Wasichana chini ya umri wa miaka 17

(Serengeti Girls);

  • Timu za Taifa ya Mchezo wa Netiboli;
    • Timu ya Taifa ya Riadha;
    • Timu ya Taifa ya Judo;
    • Timu ya Taifa ya Shotokan Karate;
    • Timu ya Taifa ya Baseball;
    • Timu ya Taifa ya mchezo wa Ngumi;
    • Timu ya Taifa ya Riadha kwa watu wenye Ulemavu;
    • Timu ya Taifa ya mchezo wa Kuogelea; na
    • Timu ya Taifa mpira wa miguu kwa

Watu wenye ulemavu (Tembo Warriors). 

  1. Mheshimiwa Spika, halikadhalika fedha hizi zinatumika kusaidia uwezo wa Taasisi ya BMT kuvihudumia vyama vyote vya michezo nchini ikiwemo kununua vitendea kazi ikiwemo gari maalumu aina ya “Coaster” ambalo litatumiwa na Timu za Taifa zinapokuwa katika mashindano mbalimbali ikiwa ni pamoja na safari za kimichezo ndani ya nchi na nchi za jirani. Katika mwaka ujao wa fedha, mapato haya yataendelea kusaidia maeneo ya kimkakati zaidi ikiwemo miundombinu ya michezo na mafunzo kwa wataalamu wetu. 
  2. Mheshimiwa Spika, aidha, uwezeshaji huo na namna ulivyosaidia timu zetu za taifa kushiriki mashindano mengi, umesaidia vijana wa Kitanzania kupata fursa za ajira nje ya nchi katika michezo ya kulipwa ikiwemo wachezaji wanne (4) wa timu ya mpira wa miguu kwa watu wenye ulemavu Frank Ngairro, Ramadhan Chomelo, Alfan Kiyanga na

Shadrack Hebron waliopata nafasi katika timu mbalimbali nchini Uturuki. Kwa upande wa Mpira wa Miguu kwa Wanawake wachezaji waliopata fursa za ajira nje ya nchi ni Aisha Masaka – Sweden, Mwanahamisi Omari –- Morocco, Enekia Kasongo – Morocco, Opa Clement – Uturuki na Diana Lucas – Morocco.

  1. Mheshimiwa Spika, kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali, Sekta ya michezo imeendelea kukua katika eneo la michezo ya kulipwa ambapo katika kipindi cha mwaka 2021/22 idadi ya wachezaji wa kulipwa imeongezeka kwa wachezaji wa

Tanzania kupata nafasi ya  kucheza katika Ligi za nchi mbalimbali. Jumla ya wachezaji 11 wa kiume wa mpira wa miguu walijiunga na vilabu mbalimbali wakiwemo David Uromi (Al Hilal – Sudan), Kelvin Pius John (KRC Genk-

Belgium), Mourice Abraham (FK Spartak-

Serbia), Abdul Yusuph Haule (FK AtmosferLithunia), Alphonce Mabula (FK Spartak- Serbia), Omary Marungu (Hapoel Kfar- Israel), Shabani Mrope (Hahaya Fc- Comoros), Adam Salamba (JS Soura-Algeria), Shabani Ningazi (MFK-Czech), Dulla Hilka (Port Darwin-

Australia), na Julius Hamis (Hahaya FcComoros). 

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika Michezo na kutekeleza maelekezo ya Mheshimiwa Rais aliyoyatoa katika Bunge hili wakati wa hotuba yake ya kwanza, Wizara iliandaa Tamasha la michezo kwa wanawake (Tanzanite) ambapo jumla ya wanamichezo 350 walishiriki katika tamasha hilo lililohusisha shughuli mbalimbali ikiwemo mashindano ya michezo ya Netiboli, Mpira wa Miguu, Riadha, Ngumi, Karate na Michezo ya jadi. Shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na Kongamano la Elimu kuhusu fursa za Michezo kwa wanawake na maonesho ya shughuli za ujasiriamali zinazofanywa na wanawake. Lengo la Tamasha hilo lilikuwa kuhamasisha ushiriki wa wanawake katika michezo na kuonesha vipaji vya Michezo kwa wanawake na kuwaelimisha wanawake kuhusu fursa za kiuchumi zilizopo katika michezo, hasa ikizingatiwa kuwa Timu za Wanawake ndiyo zinazofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa. Kama alivyoelekeza Mhe. Rais, Tamasha hili litaendelea kila mwaka. 
  2. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha dhana ya utawala bora inasimamiwa, BMT kwa kushirikiana na Vyama na Mashirikisho ya Michezo  kwa mujibu wa Katiba zao limehakikisha uratibu wa  uchaguzi wa viongozi wa Vyama na Mashirikisho kumi (10) unafanyika ikiwemo Chama cha Netiboli Tanzania (CHANETA), Shirikisho la Michezo ya Mashirika ya Umma Tanzania (SHIMMUTA), Chama cha Mchezo wa Judo Tanzania (JATA), Chama cha Mpira wa Wavu Tanzania (TAVA), Shirikisho la  Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC), Chama cha Makocha, Waamuzi, Wakuzaji, Mawakala na Mabondia wa Ngumi za Kulipwa Tanzania. Aidha, Baraza linaendelea kufuatilia ili kuhakikisha kuwa vyama vya michezo vyote ambavyo havijafanya chaguzi zao vinafanya chaguzi haraka iwezekanavyo ikiwemo Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake Tanzania (TWFA).

Chaguzi hizi ni muhimu kwa vyama ili kujiongoza kwa kufuata dhana ya utawala bora kwani inapunguza kwa kiasi kikubwa migogoro ya kiuongozi ndani ya vyama na mashirikisho ya Michezo nchini.

  1. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia BMT imeendelea kuhamasisha wananchi kushiriki katika michezo kwa kusajili vyama, vilabu, vituo, wakuzaji na Taasisi za michezo. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 Baraza lilisajili Vyama 16, Vilabu 150, Taasisi 13 za Michezo, Wakuzaji Vipaji vya Michezo 20, Vituo vya Michezo 9 na Mawakala wa Michezo 23. Rejea Kiambatisho Na.6. Aidha, marekebisho ya Katiba za Vyama 12, Vilabu saba (7) na Akademia za michezo tatu (3) yamefanyika na kuidhinishwa na Msajili wa Vyama na Vilabu vya Michezo nchini. Katiba za Vyama vilivyofanyiwa marekebisho hayo ni pamoja na Shirikisho la Michezo la SHIMIWI, Tanzania Professional Golfers Association, Katavi Regional Football Association na Mwanga District Football Association.
  2. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuimarisha michezo katika jamii na kupunguza tatizo la uhaba wa wataalamu wa michezo, mafunzo kwa walimu na makocha wa michezo 64 yalitolewa katika Mkoa wa Mara.  Mafunzo hayo yalihusu uratibu wa matukio ya kimichezo, sheria za mchezo wa netiboli, mpira wa Wavu, mchezo wa riadha na namna ya uendeshaji wa mazoezi ya viungo vya mwili (aerobics). Lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo walimu na makocha wa Shule za Msingi na Sekondari ili kuwawezesha kufundisha masuala hayo kwa wanafunzi, jamii na wadau wengine. Mafunzo yalifanyika kuanzia tarehe 22 Februari, hadi tarehe 04 Machi, 2022. 

3.2.3.3 CHUO CHA MAENDELEO YA MICHEZO MALYA

  1. Mheshimiwa Spika, jukumu kuu la Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ni kufundisha taaluma ya michezo, kutafiti na kutoa ushauri kuhusu masuala ya maendeleo ya michezo.
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na upanuzi wa miundombinu katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ambapo inajengwa Hosteli mpya na ya kisasa kwa ajili ya makazi ya wanachuo, ujenzi huu kwa sasa umefikia asilimia 40. Hosteli inayojengwa itakuwa na uwezo wa kuchukua wanafunzi 192 hivyo, itasaidia katika kuongeza udahili wa wanachuo. Aidha, Wizara imekamilisha taratibu za awali za ujenzi wa shule maalumu ya michezo (Sports Academy) ambazo ni kupatikana kwa mshauri mwelekezi ambaye ni Chuo Kikuu cha Ardhi, na ameshakamilisha michoro inayopaswa kujengwa, hatua inayofuata ni kuanza kumtafuta mjenzi (Mkandarasi). Miundombinu hii itakifanya chuo kuwa kituo mahiri kilichotukuka katika utoaji wa mafunzo ya michezo nchini.
  3. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2021/22 chuo kimeendelea na jukumu la kutoa mafunzo ya muda mrefu kwa wanachuo 221 katika kozi za Uongozi na Utawala katika Michezo, Elimu ya Ufundishaji Michezo na Elimu ya Viungo vya Mwili katika Michezo. Kati ya wanachuo hao, wanachuo waliosajiliwa katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 walikuwa 130. Kiambatisho Na.7. Chuo kinatarajia kuongeza idadi ya usajili wa wanachuo kufikia 210 kwa mwaka 2022/23. Kutokana na malengo hayo, juhudi zinazofanywa kuongeza udahili ni pamoja na kuzishawishi Halmashauri na Sekretarieti za mikoa kupeleka watumishi hususan walimu kupata mafunzo katika chuo hiki, ambapo hadi kufikia Mei, 2022 Chuo kimefanikiwa kupangiwa wanafunzi 79 wa moja kwa moja kutoka OR – TAMISEMI ambao wanatarajiwa kuanza masomo mwezi Septemba, 2022.
  4. Mheshimiwa Spika, pia, chuo kimeendelea kutoa mafunzo ya muda mfupi katika Halmashauri na Sekretarieti za mikoa mbalimbali nchini zikiwemo Halmashauri za Kalambo (Rukwa), Ngara (Kagera) na Handeni (Tanga) ambapo jumla ya washiriki 236 walinufaika na mafunzo hayo. Aidha, mafunzo yameendelea kufanyika katika Kituo kipya cha kampasi ya Chuo Dar es Salaam ambapo jumla ya washiriki 116 walipatiwa mafunzo hayo kwa kipindi cha mwezi Julai, 2021 hadi Aprili 2022. Vilevile, Chuo kinaendelea kutoa mafunzo katika mikoa ya Mbeya na Tabora. Katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 jumla ya washiriki 352 wamepatiwa mafunzo hayo ikilinganishwa na lengo la kuwafikia washiriki 300 kwa mwaka ikiwa ni sawa na asilimia 117. 

3.2.4  KUIMARISHA UTENDAJI WA

WIZARA NA  RASILIMALI WATU 

  1. Mheshimiwa  Spika, Wizara imeendelea kuweka mazingira bora ya utendaji kazi kwa watumishi ikiwa ni pamoja na ununuzi wa vitendea kazi vikiwemo magari mapya; kuanza ujenzi wa majengo ya kudumu ya ofisi za Wizara katika eneo la Mtumba, Dodoma; kupandisha watumishi vyeo ambapo katika kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022 watumishi 87 walipandishwa vyeo; kutoa mafunzo kwa watumishi ambapo jumla ya watumishi 11 walishiriki mafunzo ya muda mrefu na watumishi 9 walishiriki  mafunzo ya muda mfupi. Aidha, katika kuimarisha ushiriki wa watumishi katika kupanga na kutekeleza majukumu ya Wizara, jumla ya mikutano miwili ya Baraza la Wafanyakazi ilifanyika. Pia, Wizara iliendelea kushiriki katika mikutano, matamasha, mashindano na matukio mbalimbali ya kitaifa ikiwa ni pamoja na Sherehe za Siku ya Wanawake Duniani zilizofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kondoa; Michezo ya SHIMIWI Kitaifa iliyofanyika mkoani Morogoro na michezo na Sherehe za Wafanyakazi (Mei Mosi). Vilevile, katika kuhakikisha watumishi wanakuwa na afya na ari ya kazi hushiriki mazoezi ya jioni mara mbili kwa wiki na asubuhi kwa siku za mwisho wa wiki.

4.0 CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA NA HATUA ZILIZOCHUKULIWA KUKABILIANA NAZO

146. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikana mwaka 2021/22, changamoto katika utekelezaji wa majukumu hazikosekani. Changamoto hizo na hatua zilizochukuliwa na Serikali ni kama ifuatavyo:

  1. Ufinyu wa Bajeti ya kutekeleza majukumu ya Wizara na Taasisi zake ikiwemo ya kugharamia maandalizi na ushiriki wa timu za Taifa katika mashindano ya kimataifa na ununuzi wa vitendea kazi muhimu vya kutekeleza majukumu ya Wizara ikiwemo magari; kompyuta; na printa. Katika kukabiliana na changamoto hii, Wizara imeendelea kujadiliana na Wizara ya Fedha na Mipango ili bajeti yake iweze kuimarishwa kila mwaka pamoja na kushirikisha wadau katika utekelezaji wa majukumu. Sambamba na jitihada hizo ambapo nyongeza kadhaa zimepatikana kupitia bajeti ijayo, Wizara imeendelea kufanya mazungumzo na Balozi mbalimbali nchini zikiwemo za China, Qatar, Falme za Kiarabu (UAE), Morocco na Uturuki ili kushirikiana katika maeneo mahsusi. Tayari mkataba wa ushirikiano na China umetiwa saini Mei 26, 2022 ambao utasaidia mafunzo na ujenzi wa miundombinu ya michezo. 
  • Athari za Ugonjwa wa Virusi vya Corona (UVIKO-19) katika Sekta za Utamaduni, Sanaa na Michezo hususan sanaa ambapo watayarishaji wa picha za filamu na wasanii kutoka nje ya nchi walizuiliwa kusafiri kuja nchini kwa ajili ya shughuli za sanaa na hivyo kuathiri mapato. Aidha, wasanii wetu walikosa fursa ya kufanya matamasha katika nchi mbalimbali kutokana na nchi hizo kutoruhusu watu kuingia na pia kuzuia mikusanyiko  kutokana na ugonjwa huo. Katika kukabiliana na changamoto hizo, Serikali iliruhusu matamasha ndani ya nchi ili kuwapa wasanii fursa za kujiendeleza na kuwatia moyo. Aidha, Serikali inaendelea na juhudi za kuwahamasisha wananchi na wasanii kuzipenda kazi zinazozalishwa na wasanii wa ndani.   

5.0 MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23

147. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2022/23 Wizara na Taasisi zake kwa kushirikiana na wadau itatekeleza majukumu mbalimbali kwa kuzingatia maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-25; ahadi na maelekezo mbalimbali ya Viongozi wa Kitaifa; Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2021/22 – 2025/26; na Mpango Mkakati wa Wizara wa Mwaka 2021/22 – 2025/26. Aidha, utekelezaji wa majukumu utazingatia pia malengo ya Umoja wa Mataifa kuhusu Maendeleo Endelevu ya  Mwaka  2030 katika maeneo yanayohitaji kuchukuliwa hatua na Wizara.

5.1 SEKTA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI

5.1.1 IDARA YA MAENDELEO YA UTAMADUNI

148. Mheshimiwa Spika, malengo yaliyopangwa kutekelezwa ni kukamilisha uhuishaji wa Sera ya Taifa ya Utamaduni ya Mwaka 1997 pamoja na kuandaa mkakati wa utekelezaji; kuratibu Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani; kuratibu vikao viwili (2) vya Machifu na Viongozi wa Kimila kwa ajili ya kukabiliana na changamoto ya mmomonyoko wa maadili nchini; kuratibu na Kuendesha Matamasha sita (6) ya Utamaduni katika mikoa 26 ya Tanzania Bara na Tamasha moja (1) la Kitaifa ili kusherehekea uanuwai wa Kiutamaduni na kukuza utalii wa Kiutamaduni; kuratibu ukuzaji na uendelezaji wa Lugha ya Kiswahili Kitaifa na Kimataifa; kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa nchini; kuratibu Kikao kazi cha Mwaka cha Maafisa Utamaduni nchini; kuratibu na Kushiriki katika Matamasha matano (5) ya Utamaduni ya Kitaifa, Kikanda na Kimataifa yanayoandaliwa na wadau wengine; kuratibu utekelezaji wa majukumu ya Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika; na kufanya utafiti na kuhifadhi nyaraka na kumbukumbu za Urithi wa Utamaduni Usioshikika na kuandaa kanzidata ya maeneo ya kihistoria na kiutamaduni nchini.

5.1.2 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)

  1. Mheshimiwa Spika, BAKITA litaratibu maadhimisho ya kwanza ya Siku ya Kiswahili Duniani; kuimarisha Kiswahili nchini na kukitangaza kimataifa; kutoa elimu ya matumizi fasaha na sanifu ya lugha ya Kiswahili kwa kuandaa na kurusha hewani jumla ya vipindi 650 kupitia redio na televisheni. Pia, makala 30 zitachapishwa katika magazeti na maudhui mbalimbali kuhusu Kiswahili yatatolewa kupitia mitandao ya kijamii ambayo ni YouTube, Facebook na Twitter; kukamilisha kupitia Sheria ya BAKITA ya Mwaka 1967; kutoa mafunzo ya kuimarisha stadi za kufundisha Kiswahili kwa wageni kwa wataalamu 50 kutoka katika mikoa mbalimbali ya Tanzania; na kutoa semina kuhusu matumizi bora ya Kiswahili kwa waandishi na watangazaji kutoka vyombo vya habari vya Mkoa wa Dar es Salaam.  
  2. Mheshimiwa Spika, BAKITA pia itaendelea kutoa ithibati kwa miswada 100 ya vitabu vya kiada na ziada; kuendesha mafunzo kwa wakalimani 50; kutoa huduma ya tafsiri kwa nyaraka 200 na kuthibitisha tafsiri 3,000 zinazofanywa na wakala wake; kutambua na kusajili jumla ya wataalamu 40 katika kanzidata ya wataalamu wa Kiswahili; kutambua na kutoa ithibati ya vituo 2 vya kufundisha Kiswahili kwa wageni; na kutoa mafunzo na kutahini kiwango cha ujuzi wa lugha ya Kiswahili kwa wageni 10 kupitia Kituo kilichopo Makao Makuu. 

5.2 SEKTA YA MAENDELEO YA SANAA

5.2.1 IDARA YA MAENDELEO YA SANAA

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023 Tanzania imepanga kushirikiana na Asasi ya Viacom CBS Network Africa and Peer Lead BET International katika maandalizi ya Tuzo maarufu za Muziki Barani Afrika zinazojulikana kama MTV Africa Music Awards kwa mwaka 2023 kwa muda utakaokubalika. Tuzo hizi kawaida huvutia watu zaidi ya 10,000 mashuhuri duniani katika Sekta ya Sanaa na hufuatiliwa na watu zaidi ya 1,000,000,000 kwenye televisheni zinazopewa haki ya kuonesha tukio hili mubashara. Tafiti zinabainisha kuwa nchi wenyeji wa Tuzo hizi hunufaika kiuchumi hadi kufikia thamani ya Dola za Marekani (US$ 25,000,000) sambamba na manufaa mengine ya kiutamaduni, kiutalii na Sanaa. 
  2. Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Asasi ya Music in Africa Conference for Collaborations, Exchange, and Showcases (ACCES) yenye Makao Makuu yake nchini Afrika Kusini inaandaa Mkutano wa Wadau wa Muziki Afrika utakaofanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Novemba, 2022. Uzoefu wa Mkutano huo katika nchi nyingine unaonesha kuwa watu kati ya 600 – 1,000 kutoka zaidi ya nchi 40 duniani hushiriki, na watu milioni 72 watafikiwa kupitia Mkutano huo. Kupitia Mkutano huo, pamoja na manufaa mengine ajira 247 za moja kwa moja zitapatikana kwa watanzania wakati wa maandalizi na uendeshaji wa kikao. Aidha, wadau wetu wa muziki watapatiwa mafunzo katika masuala ya tasnia ya muziki na Hakimiliki na Hakishiriki. 
  3. Mheshimiwa Spika, majukumu mengine ni kuratibu Vikundi nane (8) vya Burudani katika Maadhimisho ya Miaka 61 ya Uhuru wa Tanzania Bara na vikundi nane (8) katika maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano; kuratibu maandalizi ya mashindano ya urembo na Mitindo kwa Viziwi Duniani (Miss & Mr. Deaf International); kuratibu na kuandaa Tamasha la Muziki la Serengeti (Serengeti Music Festival), matamasha saba (7) ya Kitaifa na Kimataifa, kusimamia programu ya Sanaa Mtaa kwa Mtaa; kuandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Sanaa; kuratibu uanzishwaji wa kikundi cha Sanaa cha Taifa kwa kushirikiana na BASATA; kuratibu Ujenzi wa Sanamu ya Mwalimu Nyerere katika Jiji la Addis Ababa nchini Ethiopia; kuratibu mashindano ya Sanaa kwa vijana kupitia UMISSETA, UMITASHUMTA, Taifa Cup Music Challenge na Vyuo mbalimbali;  kuratibu Mafunzo ya maadili kwa wasanii na wadau wa Sanaa; kuratibu ushiriki wa nchi katika Tamasha la JAMAFEST; na kuunda Mfumo wa kupokea taarifa kutoka BASATA, BFT na COSOTA za usajili wa Wasanii, vibali vya kuendesha shughuli za Sanaa nchini, leseni za kutumia kazi za Sanaa pamoja na makusanyo na ugawaji wa mirabaha ili kuwa na kanzidata ya kisekta. 

5.2.2 BODI YA FILAMU TANZANIA

154. Mheshimiwa Spika, majukumu yatakayotekelezwa ni pamoja na kufanya operesheni 48 ili kudhibiti uendeshaji wa shughuli za filamu usiozingatia Sheria na Taratibu; kutoa ithibati na leseni 60 za uendeshaji wa shughuli za filamu na kutoa vitambulisho 1,200 kwa wadau wa filamu; kuhakiki, kupanga katika madaraja na kutoa vibali 1,500 vya uoneshaji wa filamu kwa umma; kupitia na kuchambua maombi 1,500 ya utayarishaji wa filamu na Michezo ya Kuigiza pamoja na kutoa vibali; kuwajengea uwezo wadau kwa kuanzisha/kuendeleza programu za ukuzaji na uendelezaji wa tasnia ya filamu; kuratibu na kuwezesha uendeshaji wa semina/vikao vinne (4) vya wadau, kongamano moja (1), na matamasha matano (5); kuratibu na kuandaa Tuzo za Filamu; kutangaza huduma na kazi za Bodi ili kuongeza uelewa na kuimarisha elimu kwa umma; na kubaini na kuyatangaza maeneo 15 ya upigaji picha za filamu.

5.2.3 BARAZA LA SANAA LA TAIFA (BASATA)

155. Mheshimiwa Spika, majukumu yatakayotekelezwa ni  kukuza ubunifu na utengenezaji wa sanaa bora; kuongeza ushiriki wa jamii katika shughuli za sanaa; kuimarisha  shughuli za sanaa katika shule tano (5) za msingi na shule tano (5) za sekondari; kuhabarisha umma na wadau wa sanaa juu ya masuala ya sanaa nchini; kusimamia matumizi ya sanaa za jadi nchini; kuratibu na kushiriki matamasha ndani na nje ya nchi; kuweka misingi na miongozo ya maslahi ya wasanii yasiyo ya hakimiliki au hakishiriki; kuratibu na kuandaa Tuzo za muziki; kuongeza rasilimali za Baraza na kudhibiti matumizi yake; na kusimamia Utawala Bora na masuala ya maadili katika kutekeleza shughuli za Baraza na uendeshaji wa sekta ya sanaa. 

5.2.4 TAASISI YA HAKIMILIKI TANZANIA (COSOTA)

156. Mheshimiwa  Spika,  majukumu  yatakayotekelezwa  ni kukusanya mirabaha yenye thamani ya Sh.1,350,000,000 na kuigawa kwa wabunifu na kutoa leseni 1,490; kufanya usajili wa kazi zisizopungua 2,500 na wabunifu 500; kusuluhisha migogoro ya hakimiliki; kutoa elimu ya masuala ya hakimiliki na hakishiriki kwa wabunifu na wadau mbalimbali wa Hakimiliki; kuboresha mazingira ya kazi na maslahi kwa watumishi 27 wa Taasisi; kuboresha kanzidata ya kazi za hakimiliki zilizosajiliwa kidijitali; na kuendelea kufanya operesheni moja kila robo mwaka za kupambana na uharamia wa miliki bunifu.

5.2.5 TAASISI YA SANAA NA UTAMADUNI BAGAMOYO (TaSUBa)

157. Mheshimiwa  Spika,  TaSUBaitaendelea kudahili wanachuo wapatao 600 katika kozi ndefu na 150 kwa kozi fupi; kuendelea na ukarabati wa mabweni, ukumbi mkuu, ukumbi wa “flexible” na ujenzi wa uzio kuzunguka chuo; kuendesha semina 6, warsha 8 na makongamano 3; kuandika mitaala mipya mitatu (3); kujenga studio ya kisasa ya kurekodi na kutengeneza filamu na kuandaa maandalizi ya Kituo cha Redio na TV; kufanya tathmini ya uwezekano wa kuanzisha kampasi moja ya mafunzo nje ya Bagamoyo; kuendesha Tamasha la 41 la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo; kuimarisha mfumo wa TEHAMA; kupitia upya Mpango Mkakati wa Taasisi unaoisha muda wake katika mwaka 2022/23; na kuimarisha mtandao (Networks) kati ya Taasisi na wadau wa sanaa nje na ndani ya nchi.

5.3 SEKTA YA MAENDELEO YA MICHEZO

5.3.1 IDARA YA MAENDELEO YA MICHEZO

  1. Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha Tanzania inakidhi vigezo vya kuandaa mashindano ya Kimataifa na Kikanda, Serikali katika mwaka 2022/23 imetenga kiasi cha Shilingi Billioni 10 kwa ajili ya Ukarabati wa viwanja. Kwa hatua ya kwanza vitaanza viwanja saba (7) vilivyopo katika Majiji, ambavyo ni Jamhuri – Dodoma, Sheikh Amri Abeid – Arusha, Sokoine – Mbeya, CCM Kirumba – Mwanza, na Mkwakwani – Tanga.

Aidha, ukarabati huo utavihusisha viwanja vya Uhuru na Benjamina Mkapa Jijini Dar es Salaam. Hatua ya pili ni kukarabati viwanja vingine ikiwa ni pamoja na kuweka nyasi bandia na majukwaa katika mikoa ya Kigoma, Rukwa, Mtwara, Iringa, Tabora na Shinyanga baada ya kujadiliana na wamiliki wa viwanja hivyo. Mkakati huu utaiwezesha Tanzania kufanikisha maandalizi ya kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON ambayo tayari Tanzania imependekezwa kwa mwaka 2027 ambayo ni ndoto ya Rais, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ya kuandaa mashindano makubwa ya michezo. 

  1. Mheshimiwa Spika, Wizara vilevile itashirikiana na OR-TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuratibu na kusimamia mashindano ya michezo ya Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na ya Sekondari (UMISSETA); kuratibu usimamizi na uendeshaji wa Shule 56 maalumu za michezo nchini kwa kukarabati miundombinu ya michezo na upatikanaji wa vifaa vya michezo; kuongeza ushiriki wa wananchi katika mazoezi ya viungo na michezo kwa kuongeza usajili wa vikundi kutoka 290, mwezi Februari, 2022 hadi 305, mwezi Juni, 2023; kusimamia uendelezaji wa  Michezo ya Kipaumbele ambayo ni Mpira wa Miguu, Netiboli, Mpira wa Kikapu, Mpira wa Wavu, Riadha na Mpira wa Mikono ili kufanya vyema katika mashindano ya kimataifa; kuongeza idadi ya wataalamu wa michezo wanaokidhi viwango na mahitaji; kuimarisha udhibiti wa matumizi ya dawa na mbinu haramu michezoni na dawa za kulevya katika michezo; kuimarisha ushiriki wa watu wenye mahitaji maalumu katika michezo na mazoezi ya viungo vya mwili; kutumia fursa ya ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa kwa maendeleo ya michezo, wanamichezo na Taifa kwa ujumla; na kuzingatia masuala mtambuka  (VVU na UKIMWI, utunzaji wa mazingira, utawala bora na jinsia)  katika michezo.
  2. Mheshimiwa Spika, majukumu yatayotekelezwa ni kutoa elimu na kusambaza Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995; kuimarisha uteuzi, maandalizi na ugharamiaji wa Timu za Taifa kwa kuongeza bajeti na kushirikiana na wadau wa michezo; kuratibu maandalizi na ushiriki wa Timu za Taifa katika mashindano ya Kombe la Dunia Mpira wa Miguu kwa Watu wenye Ulemavu na ushiriki wa michezo ya Jumuiya ya Madola; kusimamia ujenzi wa Miundombinu ya Michezo inayotarajiwa kujengwa ikiwa ni pamoja na Kituo maalumu

cha Michezo katika Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya; kujenga maeneo ya michezo na kupumzikia wananchi (Recreational and Sports Centres); Viwanja vya Michezo na Maonesho ya Sanaa (Sports and Arts Arena); na Uwanja Changamani wa Michezo Dodoma.

5.3.2 BARAZA LA MICHEZO LA TAIFA (BMT)

161. Mheshimiwa Spika, BMT itaendelea kusaidia vyama vya michezo 7 na kugharimia Timu za Taifa 34 katika mashindano ya Kimataifa; kutoa mafunzo ya utawala bora katika michezo kwa viongozi na makocha 100 kutoka Vyama vya Michezo 54; kufuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa shughuli za michezo katika Mikoa 26, Wilaya 52, Vyama vya Michezo 54 na Taasisi za Michezo 15; kuandaa Tamasha la Wanawake kuhamasisha ushiriki wao katika michezo na maonesho ya wanawake (Women Tanzanite Festival); kutoa tuzo kwa wanamichezo  Mahiri; na kuandaa na kuratibu Mashindano ya Taifa Cup; kusajili vyama vya Kitaifa vinne (4), Mkoa 40, Wilaya 100, Wakuzaji na Mawakala 20, vilabu 150 na Vituo na shule za michezo 70; kuendelea kuhamasisha ushiriki wa jamii katika michezo  kwa kuzingatia programu za mazoezi ya viungo kwa kila mwisho wa wiki; na kushirikiana na vyama/mashirikisho ya michezo katika kuratibu na kugharimia mafunzo ya wataalamu wa michezo katika ngazi ya kitaifa

na kimataifa. 

5.4 MIRADI YA MAENDELEO

  1. Mheshimiwa Spika, kuhusu Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kufanya utambuzi, ukusanyaji na uhifadhi wa taarifa, masimulizi na nyaraka zinazohusu historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika; kukamilisha ukarabati wa jengo lililotumiwa na Kamati ya Ukombozi Kusini mwa Afrika na kuanzisha makumbusho ya kisasa kuhusu historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika katika jengo hilo;  kuandaa filamu (Documentary) kuhusu mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Afrika; kukarabati nyumba za Viongozi Wakuu wa Vyama vya Ukombozi kutoka nchi za Afrika walizokaa wakati wa harakati za ukombozi ili zitumike kwa utalii na utafiti; kuandaa makongamano na maonesho kuhusu historia ya harakati za  ukombozi wa Bara la Afrika na kuhuisha Mkakati wa Kitaifa na Kikanda wa Miaka Mitano wa Utekelezaji wa Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika.
  2. Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania, katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli 

zitakazotekelezwa ni kuratibu uendeshaji wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wasanii 2,000 na vikundi 25; na kuimarisha mitaji kwa kutoa mikopo nafuu kwa wasanii 500 wa Utamaduni na Sanaa pamoja na kuanza taratibu za kujenga ofisi za Mfuko Jijini Dodoma;.

  1. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Ukarabati wa Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo, katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia; kukarabati miundombinu ambayo ni mabweni, ukumbi mkuu, “Flexible hall”, Jengo la Utawala, maji safi na maji taka, umeme, na TEHAMA; kununua vifaa vya kuendeshea Tamasha; kuanza ujenzi wa uzio kuzunguka chuo; na kujenga studio ya kisasa za kurekodi filamu, na kituo cha redio na TV.
  2. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa

2022/23 Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) limejipanga kutoa mafunzo elekezi kwa diaspora wanaofundisha Kiswahili kwa wageni katika nchi za Namibia, Malaysia, Komoro na Sudani Kusini; kutoa mafunzo kwa Walimu wa Walimu wa Kiswahili kwa wageni namna ya kutumia mwongozo wa Taifa wa kufundisha Kiswahili kwa wageni; na kuandaa machapisho kwa ajili ya kuwezesha ufundishaji na ujifunzaji wa Kiswahili kama lugha ya kigeni.

  1. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dodoma, katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kumpata mkandarasi wa mradi; kusafisha eneo la mradi; kufanya maandalizi ya upatikanaji wa rasilimali na kuanza ujenzi wa uwanja mkubwa.
  2. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Ujenzi wa Vituo vya Mazoezi na Kupumnzika Wananchi katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kumpata mshauri mwelekezi wa mradi; kumpata mkandarasi wa mradi; kusafisha eneo la mradi na kuanza ujenzi wa vituo husika.
  3. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dar es Salaam katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea kuboresha kumbi za mikutano kwa kununua samani pamoja na kuweka miundombinu bora zikiwemo “projector” pamoja na vipaza sauti (spika); kukamilisha ukarabati eneo la kufanyia mazoezi ya viungo (Gym) na kumpata mzabuni wa kuendesha GYM hiyo; kukarabati eneo la kukimbilia (Track) kwa kuweka zulia jipya (Tartan) la kisasa; na kukarabati eneo la Big screen.
  4. Mheshimiwa Spika, kuhusiana na ujenzi wa Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya, katika mwaka wa fedha 2022/23 shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na ujenzi wa kituo cha kukuza na kuendeleza vipaji (Sports Academy); na kuendelea na ujenzi wa hosteli

ya wanafunzi.

5.5 KUIMARISHA UTENDAJI WA WIZARA

  1. Mheshimiwa Spika,Wizara itaendelea kuratibu na kuwezesha uendeshaji wa shughuli za ofisi ikiwemo matengenezo na mafuta ya magari, huduma za usafi na ulinzi, kulipa pango la ofisi, umeme na simu pamoja na ununuzi wa vitendea kazi mbalimbali na samani za ofisi; kuratibu na kuwezesha mazoezi ya wafanyakazi wote wa Wizara kila wiki mara moja; kuwezesha upatikanaji wa stahili mbalimbali za wafanyakazi ikiwemo uhamisho, likizo, safari n.k.; kuendesha vikao viwili vya Baraza la Wafanyakazi; kuratibu ushiriki wa Wizara katika sherehe za Mei Mosi, Siku ya Wanawake Duniani, Wiki ya Utumishi wa Umma na Michezo ya SHIMIWI; na kuratibu mafunzo, ajira na upandishwaji vyeo kwa watumishi.
  2. Mheshimiwa Spika, piakuratibu uandaaji wa Bajeti ya Wizara ya Mwaka 2023/24; kuratibu na kuandaa utafutaji wa rasilimali fedha nje ya bajeti ya Serikali; kuratibu vikao vinne (4) vya ushirikiano baina ya Wizara zenye dhamana ya Utamaduni, Sanaa na Michezo za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar; kufanya mazoezi ya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa Sera, Miradi na Programu mbalimbali za Wizara; kuratibu maandalizi ya taarifa mbalimbali ikiwemo za utekelezaji wa Bajeti na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2020-2025; na kutoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja za kutangaza shughuli za Wizara, uzingatiwaji wa Sheria za fedha na ununuzi katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara, matumizi ya TEHAMA na ushauri wa kisheria.  
    1. MAKADIRIO YA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/23
    1. MAPATO
  3. Mheshimiwa       Spika, mwaka 2022/23

Wizara inatarajia kukusanya jumla ya Shilingi Milioni Mia Tisa   (Sh.900,000,000)  kupitia Idara ya Maendeleo ya Michezo. Vyanzo vya mapato hayo ni pamoja na viingilio katika matukio ya michezo yanayofanyika katika viwanja vya Benjamin Mkapa na Uhuru, kukodisha kumbi na gym zilizopo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa na ada za mafunzo kutoka Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya. Aidha, kwa upande wa Taasisi sita (6) zilizo chini ya Wizara kiasi kinachokadiriwa kukusanywa ni Shilingi Bilioni Tano, Milioni Mia Tatu Tisini na Sita,

                   Mia      Nne      Hamsini      na      Tano      Elfu

(Sh.5,396,455,000). Rejea Kiambatisho Na.8A na B ni mchanganuo wa mapato yanayotarajiwa kukusanywa na Wizara na Taasisi zake kwa mwaka 2022/23.

6.2 MATUMIZI YA KAWAIDA NA MIRADI YA MAENDELEO

  1. Mheshimiwa       Spika, mwaka 2022/23

Wizara imetengewa bajeti ya Shilingi Bilioni Thelathini na Tano, Milioni Mia Nne Ishirini na Tano, Mia Tisa Tisini na Moja Elfu (Sh.35,425,991,000). Kati ya fedha hizo Mishahara ni Shilingi Bilioni Nane, Milioni Mia Mbili na Moja, Mia Nane Themanini na Mbili Elfu (Sh.8,201,882,000), Matumizi Mengineyo ni Shilingi Bilioni Kumi na Moja, Milioni Mia Tatu Tisini na Mbili, Mia Tisa Arobaini na Tisa Elfu (Sh.11,392,949,000) na Miradi ya Maendeleo ni Shilingi Bilioni Kumi na Tano, Milioni Mia Nane Thelatini na

                   Moja,        Mia        Moja        Sitini        Elfu

(Sh.15,831,160,000). Kiambatisho Na.10A, B na C kinaonesha mgawanyo wa Bajeti ya Wizara kwa Idara na Vitengo, Taasisi zilizo chini ya Wizara na Miradi ya Maendeleo.

7.0 MAOMBI     YA FEDHA KWA      AJILI  YA KUTEKELEZA MPANGO WA  MWAKA 2022/23

174. Mheshimiwa Spika, ili kutekeleza majukumu ya Wizara katika mwaka 2022/23 naomba sasa niliombe  Bunge  lako  Tukufu  liridhie na kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka 2022/23 yenye jumla ya Shilingi Bilioni Thelathini na Tano, Milioni Mia Nne Ishirini

na Tano, Mia Tisa Tisini na Moja Elfu (Sh.35,425,991,000). Kati ya fedha hizo Mishahara ni Shilingi Bilioni Nane, Milioni Mia Mbili na Moja, Mia Nane Themanini na Mbili Elfu (Sh.8,201,882,000), Matumizi Mengineyo ni Shilingi Bilioni Kumi na Moja, Milioni Mia Tatu Tisini na Mbili, Mia Tisa Arobaini na Tisa Elfu (Sh. 11,392,949,000) na Miradi ya Maendeleo ni Shilingi Bilioni Kumi na Tano, Milioni Mia Nane Thelathini na Moja, Mia Moja Sitini Elfu

(Sh.15,831,160,000).

8.0 MWISHO NA SHUKRANI

  1. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2022/23 Wizara yangu inakusudia kufanya mageuzi makubwa katika kuendeleza Sekta zake na kuimarisha mchango wake katika Pato la Taifa, kuongeza ajira hususan kwa vijana na kuimarisha michezo nchini. Aidha, kama nilivyobainisha hapo awali, Wizara itawajengea uwezo wasanii wetu kimitaji na mafunzo kupitia Mfuko wa Utamaduni na Sanaa, hatua ambayo itaongeza tija, ubora na ushindani wa kazi za sanaa na wabunifu wetu kitaifa na kimataifa. Pia, Wizara itaboresha matumizi ya mifumo mbalimbali ya kielektroniki ya kuwahudumia wasanii na wadau wengine wa sanaa ili kuimarisha ufanisi katika utoaji wa huduma, kurahisisha urasimishaji wa Sekta ya Sanaa na shughuli za ubunifu na kubwa zaidi, kuongeza mapato ya wasanii na Serikali kupitia ukusanyaji wa mirabaha. Mifumo hiyo ni pamoja na ya kufuatilia matumizi ya kazi za sanaa hususani muziki na filamu katika vyombo vya habari, mfumo wa kusambaza kazi za wasanii kama ilivyo Netflix na mfumo wa usajili na usimamizi wa taarifa za wasanii na wadau wa sanaa.
  2. Mheshimiwa Spika, ili kuhakikisha mifumo hiyo inafanya kazi vizuri, Wizara itaweka mazingira bora ya Kisheria ikiwa ni pamoja na kukamilisha marekebisho ya Kanuni za Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki Na. 7 ya Mwaka 1999, Sheria Na. 27 ya Mwaka 1967 iliyoanzisha BAKITA pamoja na Kutunga Sheria ya Kusimamia Matumizi ya Dawa na Mbinu Haramu katika Michezo. 
  3. Mheshimiwa Spika, mafanikio yaliyopatikana katika mwaka 2021/22 yamechangiwa pia na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Shukrani zangu za dhati kama nilivyodokeza katika utangulizi wa hotuba yangu ziende kwa Viongozi Wakuu wa Nchi yetu yaani Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Viongozi wengine wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kwa upande wa wadau siyo rahisi kuwataja wote kwa majina, nitawataja wachache nikianza na wadau wa nje, nazishukuru nchi za China, Japan, Korea Kusini, Uswisi na Ujerumani, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na    Shirika la   Maendeleo   la

Kimataifa la Japan (JICA). 

  1. Mheshimiwa Spika, kwa wadau wa ndani, naomba nianze na mashirikisho na vyama vyote vya kisekta katika utamaduni, sanaa na michezo, vyombo vyote vya habari, wasambazaji wa kazi za  sanaa, filamu na michezo ya kuigiza, kampuni za Azam TV, DSTV, Startimes, Mamlaka ya Bandari (TPA), TANAPA, HEINEKEN Tanzania limited, Coca Cola, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, na Shirika la Ndege Tanzania (ATC). Nawapongeza na kuwashukuru wadau wote wakiwemo wachezaji, wasanii mbalimbali na wanautamaduni. Hakika katika mwaka huu tumeweza, tuweze na kutekeleza zaidi katika mwaka ujao. 
  2. Mheshimiwa Spika, nafahamu Bunge lako Tukufu linajua kwamba kauli ya “Anaupiga Mwingi” inatokana na lugha ya kimichezo. Nihitimishe kwa kuthibitisha kauli hiyo kwa mambo haya kumi (10):
    1. Mheshimiwa Rais ndani ya mwaka  mmoja karejesha Tuzo za Filamu;
    1. Ndani ya mwaka mmoja karejesha Tuzo za Muziki;
    1. Ndani ya   mwaka mmoja karejesha mirabaha;
    1. Ndani ya mwaka mmoja Tembo Worriors imeshiriki Kombe la Dunia;
    1. Ndani ya mwaka mmoja Serengeti Girls wanafika hatua ya juu Kimpira;
    1. Ndani ya mwaka mmoja Twiga Stars mabigwa COSAFA;
    1. Ndani ya mwaka mmoja amekamilisha usanifu wa “Sports and Arts Arena”;
    1. Ndani ya mwaka mmoja ameanzisha shule 56 maalumu za michezo;
    1. Ndani ya mwaka mmoja ametoka ofisini na kuigiza filamu ya “Royal Tour” na  
    1. Ndani ya mwaka mmoja ametoa asilimia 5 ya michezo ya kubahatisha kusaidia michezo.
  3. Mheshimiwa Spika, huku ni zaidi ya kuupiga mwingi. 
  4. Mheshimiwa  Spika, natoa  shukrani   zangu za dhati kwako binafsi na kwa Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza. Hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara kwa anwani ya www.michezo.go.tz.na kupitia mitandao ya kijamii. 
  5. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.

VIAMBATISHO

Kiambatisho Na.1A

Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango akiwasilisha hoja ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya Kazi katika Mkutano wa 35 wa Umoja wa Afrika wa Wakuu wa Nchi na Serikali, ambapo hoja hiyo ilikubaliwa na kupitishwa na Umoja huo.

                                                                                                  109

Kiambatisho Na.1B

Mkutano Mkuu wa 41 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), umepitisha Julai 7 ya kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.

                                                                                                  110

Kiambatisho Na. 2

          FILAMU     ZILIZOHAKIKIWA     NA     KUPEWA

VIBALI MWAKA     2011/12 – 2021/22 

MwakaFilamu  za  KitanzaniaFilamu  za KigeniJumla  kwa Mwaka
2011/1220612218
2012/1341412426
2013/141,181581,239
2014/151,339611,400
2015/16653114767
2016/1770692798
2017/18762148910
2018/19832158990
2019/20686119805
2020/211,388681,456
2021/221,713381,751
Jumla9,88088010,760

  Chanzo: Bodi ya Filamu Tanzania

Kiambatisho Na.3

VIBALI VYA UTAYARISHAJI WA FILAMU NA PICHA JONGEVU VILIVYOTOLEWA MWAKA

2011/12 – 2021/22

  MwakaKampuni za KitanzaniaKampuni za WageniJumla
2011/122184105
2012/1330123153
2013/1433125158
2014/1536133169
2015/1631137168
2016/1730123153
2017/1846137183
2018/1938133171
2019/202484108
2020/214662108
2021/227971150
Jumla4141,2121,626

Chanzo: Bodi ya Filamu Tanzania

Kiambatisho Na.4A

MUONEKANO WA UWANJA  WA “SPORTS AND

ARTS ARENA” 

Sports and Arts Arena ya Dar Es Salaam

Kiambatisho Na.4B

MUONEKANO WA VIWANJA NA MAENEO YA KUPUMZIKIA (SPORTS RECREATIONAL AND

LEISURE AREAS)

Recreational Centre Geita

Kiambatisho Na.4C

MUONEKANO WA UWANJA WA MPIRA WA MIGUU

UTAKAOJENGWA JIJINI DODOMA

Dodoma Sports Complex

                                              Kiambatisho Na. 5

JEDWALI LA ORODHA YA SHULE TEULE 56 ZA MICHEZO

NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
1ARUSHAMONDULI DCShule ya Sekondari ENGUTOTO SECONDARY SCHOOL
LONGIDO DCLONGIDO SECONDARY SCHOOL
2DAR ES SALAAMILALA MCPUGU SECONDARY SCHOOL
TEMEKE MCKIBASILA SECONDARY SCHOOL
3DODOMADODOMA MCDODOMA SECONDARY SCHOOL
MPWAPWA DCMPWAPWA SECONDARY SCHHOL
4GEITAGEITA TCKALANGALALA SECONDARY SCHOOL
GEITA DCKATORO SECONDARY
NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
   SCHOOL
5IRINGAIRINGA MCLUGALO SECONDARY SCHOOL
IRINGA DCIFUNDA SECONDARY SCHOOL
MUFINDI DCMALANGALI SECONDARY SCHOOL
6KAGERABUKOBA MCNYAKATO SECONDARY SCHOOL
KARAGWE DCKANONO SECONDARY SCHOOL
7KATAVINSIMBOKATUMBA SECONDARY SCHOOL
MPANDA MCMIZENGO PINDA SECONDARY SCHOOL
8KILIMANJAROMOSHI MCMOSHI TECHNICAL SEC.SCHOOL
ROMBO DCHOROMBO SECONDARY SCHOOL
NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
9KIGOMABUHIGWE DCMNANILA SECONDARY SCHOOL
KIGOMA UJIJI MC KIGOMA SECONDARY SCHOOL
10LINDIRUANGWA DCNKOWE SECONDARY SCHOOL
LINDI DCMAHIWA SECONDARY SCHOOL
11MANYARABABATI TCBABATI DAY SECONDARY SCHOOL
MBULU TCCHIEF SARWATT SECONDARY SCHHOL
12MARAMUSOMA MCMARA SECONDARY SCHOOL
TARIME TCTARIME SECONDARY SCHOOL
13MBEYAKYELA DCIKIMBA SECONDARY SCHOOL
MBEYA CCIYUNGA SECONDARY SCHOOL
14MWANZAMWANZA CCNSUMBA SECONDARY SCHOOL
SENGEREMA DC SENGEREMA SECONDARY
NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
   SCHOOL
KWIMBA DCNYAMILAMA SECONDARY SCHOOL
15MOROGOROMOROGORO MCMOROGORO SECONDARY SCHOOL
MVOMERO DCLUSANGA SECONDARY SCHOOL
KILOSA DCMAZINYUNGU SECONDARY SCHOOL
16MTWARAMTWARA DCMTWARA TECH. SECONDARY SCHOOL
MASASI DCNDANDA SECONDARY SCHOOL
17NJOMBEMAKAMBAKO TCMAKAMBAKO SECONDARY SCHOOL
NJOMBE TCMATOLA SECONDARY SCHOOL
18PWANIRUFIJI DCIKWIRIRI SECONDARY
NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
   SCHOOL
KIBAHA TCZOGOWALE SECONDARY SCHOOL
19RUKWASUMBAWANGA MCKANTALAMBA SECONDARY SCHOOL
KALAMBO DCMATAI SECONDARY SCHOOL
20RUVUMASONGEA MCSONGEA BOYS SECONDARY SCHOOL
MADABA DCMAHANJE SECONDARY SCHOOL
SONGEA DCMAPOSENI SECONDARY SCHOOL
21SHINYANGAKAHAMA MCMWENDAKULIMA SECONDARY SCHOOL
SHINYANGA MCRAJANI SECONDARY SCHOOL
22SINGIDAIKUNGIUNYAHATI SECONDARY SCHOOL
SINGIDA MCMANDEWA SECONDARY
NAMKOAHALMASHAURIJINA LA SHULE
   SCHOOL
23SIMIYUBARIADI TCBARIADI SECONDARY SCHOOL
MASWA DCBINZA SECONDARY SCHOOL
24SONGWEMBOZI DCVWAWA SECONDARY SCHOOL
TUNDUMA TC MWL. NYERERE SECONDARY SCHOOL
25TABORATABORA MCUKOMBOZI SECONDARY SCHOOL   
TABORA BOYS SECONDARY SCHOOL
26TANGATANGA CCTANGA TECHNICAL SECONDARY SCHOOL
KOROGWE TCNYERERE MEMORIAL SECONDARY SCHOOL

Kiambatisho Na.6

VYAMA, VILABU, VITUO VYA MICHEZO NA WAKUZAJI/MAWAKALA WA

MICHEZO WALIOSAJILIWA KUANZIA MWAKA 2010 – 2022

MwakaVilabu vya MichezoVyama vya MichezoVituo vya MichezoWakuzaji/ Mawakala wa Michezo
20102729
20111685
2012339
20132853712
2014464177
20152241512
2016331915
2017288291314
2018212231829
2019231182119
202011012526
2021216152260
2022119923

Chanzo: Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo (BMT)

1 Ni kwa kipindi cha Julai, 2021 hadi Aprili, 2022

                                                                                                                                                    121

Kiambatisho Na.7

WANAFUNZI WALIOSAJILIWA KATIKA CHUO CHA MAENDELEO YA

MICHEZO MALYA 2010 – 2021

MwakaWanaumeWanawakeJumla
2010NANANA
2011251439
2012NANANA
2013261440
2014NANANA
2015292453
2016311546
20179431125
201811031141
20199122113
2020702696
20219931130

Chanzo: Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya

122

Kiambatisho Na.8A

MADUHULI YANAYOTARAJIWA  KUKUSANYWA  NA  WIZARA  NA 

TAASISI ZAKE KWA MWAKA 2022/23

a) Maduhuli Yatakayokusanywa na Wizara Idara ya Maendeleo ya Michezo

KijifunguMaelezoMakadirio ya Mapato 
 Mwaka 2021/22 (Sh.) Mwaka 2022/23 (Sh.)
  140259Mapato      ya   Viwanja vya Michezo (Uhuru na Benjamin Mkapa)470,200,000640,000,000
140315Ada za Mafunzo312,000,000259,998,000
140368Mapato kutoka vyanzo mbalimbali1,0001,000
140370Marejesho ya fedha za Umma1,0001,000
Jumla Ndogo782,202,000900,000,000
JUMLA KUU782,202,000900,000,000

123

Kiambatisho Na.8B

b) Mapato Yatakayokusanywa na Taasisi Zilizo Chini ya Wizara

  NaJina la TaasisiMakadirio ya Mapato 2021/22 (Sh.)Makadirio ya Mapato 2022/23 (Sh.)
1.Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)558,630,000416,750,000
2.Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa)700,000,000720,000,000
3.Bodi ya Filamu Tanzania1,413,572,0001,359,642,000
4.Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)1,480,919,000865,063,000
5.Baraza la Michezo la Taifa (BMT)300,000,000685,000,000
6.Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)1,025,000,0001,350,000,000
 JUMLA5,478,121,0005,396,455,000

124

Kiambatisho Na.9A

MGAWANYO WA BAJETI YA WIZARA YA MWAKA 2022/23 KWA IDARA

NA VITENGO, TAASISI ZILIZO CHINI YA WIZARA NA MIRADI YA MAENDELEO

a) Mgawanyo wa Bajeti ya Wizara kwa Idara na Vitengo

Kifungu      Idara/ KitengoMakisio ya Bajeti Mwaka 2022/23
Mishahara (PE) (Sh.)Matumizi Mengineyo (Sh.)Jumla (Sh.)
  1001Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu810,024,000 4,882,223,000    5,692,247,000
1002Fedha na Uhasibu259,788,000     181,600,000       441,388,000
1003Sera na Mipango270,254,000     297,645,000       567,909,000
1004Mawasiliano124,521,000     147,356,000       271,877,000
 Serikalini   
1005Ununuzi na Ugavi184,536,000     114,080,000       293,616,000
1006Ukaguzi wa Ndani67,980,000       85,550,000       153,530,000
1007TEHAMA127,966,000     219,578,000       347,534,000
1008Huduma za Sheria52,020,000       65,882,000       117,902,000
6001Maendeleo ya Utamaduni205,298,000     517,309,000       722,607,000
6004Maendeleo ya Michezo756,360,000 1,113,897,000    1,870,257,000
6005Maendeleo ya Sanaa467,574,000     709,251,000    1,176,825,000
JUMLA3,326,321,000 8,334,371,000 11,660,692,000

Kiambatisho Na.9B

b) Mgawanyo wa Bajeti kwa Taasisi Zilizo Chini ya Wizara

    Jina la TaasisiMakisio ya Bajeti Mwaka 2022/23
Mishahara (PE) (Sh.)Matumizi Mengineyo (Sh.)Jumla (Sh.)
6001 – 26311266  Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) 729,852,000242,289,000972,141,000
6005-26311352Bodi      952,708,000246,000,0001,198,708,000
6005 – 26311267 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)931,108,000234,000,0001,165,108,000
6005 – 26311234 Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA)539,346,0001,500,000,0002,039,346,000
6005 – 26311130 Taasisi ya Sanaa na Utamaduni1,151,956,000204,000,0001,355,956,000
Bagamoyo (TaSUBa)   
6004 – 26311273 Baraza la Michezo la Taifa (BMT)570,591,000422,289,000992,880,000
6004 – 6311346 Chuo             cha Maendeleo        ya Michezo-Malya210,000,000210,000,000
Jumla4,875,561,0003,058,578,0007,934,139,000
JUMLA KUU8,201,882,00011,392,949,00019,594,831,000

Kiambatisho Na.9C

c) Miradi ya Maendeleo

Na.Jina la MradiMakisio ya Bajeti 2022/23
Idara ya Maendeleo ya Utamaduni
1.  6293 – Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika515,000,000
2.  6502     – Mfuko wa Utamaduni na Sanaa Tanzania – Maandalizi ya Ujenzi wa Jengo la Ofisi    2,000,000,000 400,000,000
3.  6521 – Kuimarisha Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na Kukiuza   Kiswahili Kikanda na Kitaifa300,000,000
Jumla ya Idara3,215,000,000
Idara ya Maendeleo ya Michezo
4.6385 – Ujenzi wa Chuo cha Michezo Malya – Ukarabati na Uendelezaji wa Akademia ya Michezo600,000,000 700,000,000
5.6503 – Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dodoma100,000,000
6.6504 – Ujenzi wa Vituo vya Mazoezi na Kupumzika Wananchi – Ujenzi wa Sports Arena (Dar es Salaam na Dodoma)6,966,160,000 200,000,000
7.6523 – Ujenzi wa Eneo Changamani la Michezo Dar es Salaam1,500,000,000
86527 – Ujenzi na Uimarishaji wa Miundombinu ya Michezo katika Shule    Maalumuza Michezo2,000,000,000
Jumla ya Idara12,066,160,000
Idara ya Maendeleo ya Sanaa
9.4353 – Ukarabati wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo Kuratibu Tamasha la Kimataifa la Sanaa na Utamaduni la Bagamoyo Ununuzi na Ufungaji wa Mitambo ya TV Ununuzi na Ufungaji wa Mitambo ya Redio250,000,000 100,000,000 150,000,000 50,000,000
Jumla ya Idara550,000,000
JUMLA KUU YA DEV.15,831,160,000
JUMLA KUU YA FUNGU 96 (PE+OC+DEV)35,425,991,000

Viongozi wakuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa Kongamano la Idhaa za Kiswahili Duniani tarehe 14-18 Machi, 2022 Jijini Arusha.

Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Omary Mchengerwa (Mb.) akipiga ngoma kuashiria uzinduzi wa utoaji wa Tuzo za Muziki tarehe 28 Januari, 2022  Jijini Dar es salaam.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.)

(katikati) pamoja na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Philip Gekul (Mb.)

(wa kwanza kushoto) wakishiriki mbio za kilomita tano wakati wa kilele cha mashindano ya riadha ya Mbeya Tulia Marathon yaliyofanyika tarehe 7 Mei, 2022 Jijini Mbeya.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *