
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Sophia Mjema amekabidhi pikipiki nne(04) kwa Maafisa ushirika kwa ajili ya kurahisisha utendaji wa majukumu katika kuhudumia Wananchi wa mkoa wa Shinyanga
Akizungumza baada ya kukabidhi pikipiki hizo ambazo zimenunuliwa kutoka Tume ya maendeleo ya ushirika iliyo chini ya wizara ya Kilimo ikiwa ni mahususi kwa ajili ya shughuli za vyama vya ushirika amesema kupatikana kwa pikipiki hizo kutasaidia katika kuondoa changamoto ambayo walikuwa wakiipata Maafisa wa ushirika hasa kwa kushindwa kuwafikia wakulima kwa wakati kutokana na changamoto ya usafiri ilivyokuwa ikiwakabili lakini kwa Sasa changamoto hiyo haitowasumbua tena baada ya pikipiki ambazo wamekabidhiwa kwa ajili ya majukumu yao
Hata hivyo ameongeza kwa kuwaasa Maafisa hao kuwa makini katika matumizi ya vyombo hivyo walivyokabidhiwa siku ya Leo kwani kama visipotumiwa vizuri, kwa umakini na uangalizi baada ya muda sio mrefu tatizo Hilo halitakuwa limetatuliwa bali itarudi kama ilivyokuwa awali lakini vikitunzwa na kuendeshwa kwa umakini basi vitadumu na kuzidi kuwa imara wakati wote
Mheshimiwa Sophia Mjema ametoa wito kwa Wananchi wote wa Mkoa wa Shinyanga kuwatumia vizuri Maafisa hao wa ushirika katika kuhakikisha wanahudumiwa na kutatuliwa shida na matatizo yao kwa wakati kwani kwa Sasa watakuwa wakifikiwa kwa ukaribu

Kwa upande wake Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika Mkoa wa Shinyanga Bi Hilda Boniface amemshukuru Mkuu wa mkoa Mheshimiwa Sophia Mjema kwa kukabidhi pikipiki hizo ambazo zitaenda kuondoa changamoto kwa Wananchi hususani wakulima ambao kwa asilimia kubwa wapo wakulima wa Pamba pamoja na Tumbaku
Ambapo amemuhakikishia Mkuu wa mkoa pikipiki hizo ambazo zimetolewa siku ya Leo zitagawanywa kwa kila Maafisa wa wilaya ili ziweze kuwasaidia katika majukumu yao ya kuwahudumia vizuri na kwa ukaribu katika kutatua changamoto kwa wilaya zote zilizopo Shinyanga.
