KAMATI TENDAJI KITAIFA ANWANI ZA MAKAZI YAKUTANA DODOMA

Baadhi ya wajumbe wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi wakifuatilia kikao hicho.

Na Mwandishi wetu- Dodoma

Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera,Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu  ameongoza kikao cha tisa cha kamati hiyo.

Kikao hicho kimefanyika Juni 02, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali , Wakurugenzi wa Taasisi na wataalamu ambapo wamejadili hatua zilizofikiwa kuhakikisha zoezi la uwekaji wa anwani katika makazi linakamilika kama lilivyokusudiwa.

Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) (katikati) akiongoza kikao cha Kamati Tendaji ya Kitaifa ya Uratibu wa Operesheni Anwani za Makazi  kilichofanyika Juni 02, 2022 ukumbi wa ofisi hiyo Jijini Dodoma, (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Kaspar Mmuya na wa (kwanza kushoto) ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Clarence Ichwekeleza.

Miongoni mwa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia TAMISEMI Bw. Ramadhan Kailima, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Kaspar Mmmuya, Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA Dkt. Jabiri Bakari, Mtendaji Mkuu Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Bi. Justina Mashiba na Mratibu Anwani za Makazi Zanzibar Bw. Abdalla Dai Abdalla.

Aidha Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni muendelezo wa  maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika 23 Agosti  2022 nchini  ambayo  hufanyika  kila baada ya miaka 10.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *