
YALIYOMO
ORODHA YA MAJEDWALI ……………………………………………… III
VIFUPISHO ………………………………………………………………………. IV
1.0 UTANGULIZI …………………………………………………………….. 1
2.0 MCHANGO WA MALIASILI NA UTALII KATIKA KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO
ENDELEVU ………………………………………………………………… 6
3.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA
KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI,
MALIASILI NA UTALII ……………………………………………. 8
4.0 UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI
KWA MWAKA 2021/2022 …………………………………….. 10
4.1 Ukusanyaji Maduhuli ……………………………………….. 11
4.2 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo …………………… 12
4.3 Mafanikio ……………………………………………………… 13
4.4 Utekelezaji wa Masuala Mtambuka …………………….. 26
4.5 Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara …………………… 33
4.5.1 Sekta ya Wanyamapori ……………………………… 33 4.5.2 Sekta ya Misitu na Nyuki …………………………… 60
4.5.3 Sekta ya Utalii ………………………………………… 77
4.5.4 Sekta ya Mambo ya Kale …………………………… 87
4.6 Miradi ya Maendeleo ……………………………………….. 94
4.7 Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa
Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya
Athari za UVIKO-19 ………………………………………. 103
4.8 Changamoto na Utatuzi …………………………………. 107
5.0 MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA
FEDHA 2022/2023 ………………………………………………. 109
5.1 Ukusanyaji Maduhuli ……………………………………… 111
5.2 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo …………………. 111
5.3 Kazi Zitakazotekelezwa na Wizara na Taasisi
zake ………………………………………………………….. 112
5.3.1 Sekta ya Wanyamapori ………………………………. 112
5.3.2 Sekta ya Misitu na Nyuki …………………………….. 128
5.3.3 Sekta ya Utalii ………………………………………….. 135 5.3.4 Sekta ya Mambo ya Kale …………………………….. 139
5.4 Miradi ya Maendeleo ……………………………………… 142
6.0 SHUKRANI …………………………………………………………….. 144
7.0 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA
2022/2023 ……………………………………………………………. 145
8.0 HITIMISHO …………………………………………………………… 146
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali Na. 1: Maduhuli ya Wizara kwa mwaka 2020/2021 na Makadirio kwa
mwaka wa fedha 2022/2023 …………. 148
Jedwali Na. 2: Idadi ya Watalii Waliotembelea Hifadhi za Taifa na Mapato kuanzia mwaka 2017/2018 hadi
2021/2022 …………………………………. 148
Jedwali Na. 3: Idadi ya Watalii Waliotembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na
Mapato kuanzia mwaka
2017/2018 hadi 2021/2022 …………… 149
Jedwali Na. 4: Mwenendo wa Uwindaji wa Kitalii na Mapato Kuanzia mwaka
2017/2018 hadi 2021/2022 …………… 149
Jedwali Na. 5: Mwenendo wa Upandaji Miti katika Mashamba ya Miti Kuanzia mwaka 2017/2018 hadi
2021/2022 …………………………………. 150
Jedwali Na. 6: Mauzo ya Asali na Nta Nje ya
Nchi kuanzia mwaka wa fedha
2017/2018 hadi mwaka
2021/2022 …………………………………. 151
Jedwali Na. 7: Mwenendo wa Biashara ya Utalii kuanzia mwaka 2017 hadi 2021 ……… 151
Jedwali Na. 8: Idadi ya Wanafunzi Waliodahiliwa katika Vyuo vya Wizara kuanzia mwaka 2017/2018
hadi 2021/2022 ………………………….. 151
Jedwali Na. 9: Idadi ya Wageni Waliotembelea Vituo vya Mambo ya Kale na Mapato kuanzia mwaka
2017/2018 hadi 2021/2022 …………… 152
Jedwali Na. 10: Idadi ya Wageni Waliotembelea Makumbusho ya Taifa na Mapato Kuanzia Mwaka
2019/2020 hadi 2021/2022 …………… 153
Jedwali Na. 11: Muhtasari wa Bajeti ya Matumizi ya Miradi ya Maendeleo kwa mwaka 2022/2023 ………………… 154
Jedwali Na. 12: Namba za Simu za kutoa
Taarifa kuhusu Wanyamapori
Wakali na Waharibifu …………………… 156
Jedwali Na. 13: Muhtasari wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2022/2023 ………………… 156
VIFUPISHO
AfDB – African Development Bank
AserT – Accommodation Services in Tanzania
AWF – African Wildlife Foundation
AWHF – African World Heritage Fund
AU – African Union
BBC – British Broadcasting Corporation
BEVAC – Beekeeping Value Chain
BTI – Beekeeping Training Institute
CAWM-
Mweka – College of African Wildlife Management – Mweka
CBCTC – Community Based Conservation Training Centre
CBS – Columbia Broadcasting System
CCM – Chama cha Mapinduzi
CCTV – Closed Circuit Television
CGTN – China Global Television Network
COCOBA – Community Conservation Banks
CRDB – Cooperative Rural Development Bank
EAC – East African Community
EARTE East Africa Regional Tourism Expo
EPZA Export Processing Zone Authority
ESQR European Society for Quality Research
EU – European Union
EWP – Engineered Wood Products
FAM-Trips – Familiarization Trips
FAO – Food and Agriculture Organization
FITI – Forest Industries Training Institute
FORVAC – Forestry and Value Chain
Development Programme
FTI – Forestry Training Institute
FWITC – Forest and Wood Industries Training
Centre
FZS – Frunkfurt Zoological Society
GDP – Gross Domestic Product
GEF – Global Environmental Facility
GIZ – Deutsche Gesellschaftf Ür
Internationale Zusammenarbeit
GMP – General Management Plan
GPS – Global Positioning System
HAT Hotel Association of Tanzania
ICCROM International Centre for the Study of
Preservation and Restoration of Cultural Property
iCHF – Improved Community Health Fund
ICOM – International Council of Museum
ICOMOS – International Council on Monuments and Sites
ICT – Information and Communication Technology
ILO – International Labour Organisation
IMF – International Monetary Fund
IORA – Indian Ocean Rim Association
ISO – International Organization for Standardization
ITC – International Trade Centre
IUCN – International Union for Conservation of Nature
JWTZ – Jeshi la Wananchi wa Tanzania
KfW – Kreditanstalt für Wiederaufbau (German Development Bank)
KIA Kilimanjaro International Airport
LoRA Long Range
M&E Monitoring and Evaluation
MICE – Meetings, Incentives, Conferences and Exhibitions
MNRT – Ministry of Natural Resources and Tourism
NABAC – National Beekeeping Advisory Committee
NACTE – National Council for Technical Education
NAF – National Antiquities Fund
NAFAC – National Forestry Advisory Committee
NBC – National Broadcasting Company
NCA – Ngorongoro Conservation Area
NCAA – Ngorongoro Conservation Area Authority
NCT – National College of Tourism
NIDC – National Internet Data Center
NMT – National Museum of Tanzania
NORAD – Norwegian Agency for Development Cooperation
NSSF National Social Security Fund
NTAP National Task Force on Anti-poaching
NTDP National Tourism Development Programme
NTPIS – National Tourism Policy
Implementation Strategy
ORM – Online Reputation Management
OR-
TAMISEMI – Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
PAMs – Protected Area Management system
PBS – Public Broadcasting Services
PFP – Private Forestry Plantation
PWTI – Pasiansi Wildlife Training Institute
QR Codes – Quick Response Codes
REGROW – Resilient Natural Resources
Management for Tourism and Growth
SADC
– South African Development Community
SEO – Search Engine Optimization
SHIMIWI – Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali
S!TE Swahili International Tourism Expo
SMT Serikali ya Muungano wa Tanzania
SMZ Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
SOPs – Standard Operating Procedures
SUA – Sokoine University of Agriculture
SWICA – Special Wildlife Investment Concession Area
TaFF – Tanzania Forest Fund
TAFORI – Tanzania Forestry Research Institute
TAHOSSA – Tanzania Heads of Secondary Schools Association
TANAPA – Tanzania National Parks
TATO
– Tanzania Assossiaction of Tour Operators
TAWA – Tanzania Wildlife Management Authorit
TAWIRI – Tanzania Wildlife Research Institute
TBC – Tanzania Broadcasting Coorporation
TCG
TCT –
- Tasking and Coordination Groups
Tourism Confederation of Tanzania
TEHAMA – Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
TFS Tanzania Forest Services Agency
TFS – IIMS Tanzania Forest Service Intergrated Information Management System
TLTO – Tanzania Local Tour Operators
TNBC – Tanzania National Business Council
TOR – Terms of Reference
TPA – Tanzania Ports Authority
TPSF – Tanzania Private Sector Foundation
TRA – Tanzania Revenue Authority
TSEZ – Tourism Special Economic Zone
TTB – Tanzania Tourist Board
TTGA – Tanzania Tour Guide Association
TWPF – Tanzania Wildlife Protection Fund
UAE – United Arab Emirates
UNDP – United Nations Development Programme
UNESCO – United Nations Educational, Scientific and Cultural Organization
UNWTO – United Nations World Tourism Organization
UNWTO-
CAF – United Nations World Tourism
Organization- Commission For Africa
USA – United States of America
USAID – United States Agency for International
Development
VVU – Virusi vya UKIMWI
WCS – Wildlife Conservation Society
WebPR – Web Public Relations
WHC – World Heritage Centre
WMAs – Wildlife Management Areas
WMF – World Monuments Fund
WTTC – World Travel and Tourism Council
WWF – World Wide Fund for Nature
1.0 UTANGULIZI
- Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, ninaomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako Tukufu lipokee na kujadili taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2021/2022. Aidha, ninaomba Bunge lako lijadili na kupitisha makadirio ya mapato na matumizi kwa
mwaka wa fedha 2022/2023. - Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia afya njema na kutuwezesha kuendelea kujenga uchumi na maendeleo endelevu ya nchi yetu. Aidha, ninamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kuwasilisha mbele ya Bunge lako Tukufu, Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Kwa dhati kabisa, nitumie fursa hii kumshukuru Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuniamini na kunipa dhamana ya kusimamia Wizara hii yenye umuhimu mkubwa kwa Taifa na jamii kwa ujumla. Ninaomba niungane na Waheshimiwa Wabunge na Watanzania wenzangu kumuombea kwa Mwenyezi Mungu azidi kumpa nguvu na afya njema ili aendelee kuwatumikia Watanzania.
- Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee, nichukue fursa hii kuwapongeza kwa dhati Mheshimiwa Dkt. Philip Isdori Mpango, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti katika kusimamia maliasili, malikale na kuendeleza utalii. Kupitia miongozo na maelekezo yao mazuri na yenye tija, Wizara imeendelea kutimiza wajibu wake kwa kuimarisha uhifadhi na kuendeleza utalii na hivyo kuchangia katika juhudi za kukuza uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla. Aidha, nikupongeze wewe binafsi, Mheshimiwa Dkt. Tulia Ackson Mwansasu (Mb.), Spika wa Bunge na Mheshimiwa Mussa Azzan Zungu (Mb.), Naibu Spika kwa kuchaguliwa kwa kishindo kuliongoza Bunge letu Tukufu. Imani hiyo imejengeka kutokana na umahiri na weledi mkubwa mliouonesha katika kuliongoza Bunge hili. Vilevile, niwapongeze Wenyeviti wa Bunge kwa kuendesha shughuli za Bunge letu kwa weledi mkubwa.
- Mheshimiwa Spika, kwa dhati, ninaishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Ally Juma Makoa (Mb.), Mbunge wa Kondoa Mjini kwa kujadili, kushauri na kupitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Kwa namna ya kipekee, niseme kuwa Kamati hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuishauri Wizara kupitia maoni na maelekezo yake. Wizara itaendelea kuzingatia maoni na ushauri wa Kamati na Bunge lako Tukufu ili kufanikisha malengo yake.
- Mheshimiwa Spika, naungana na
Waheshimiwa Wabunge wenzangu walionitangulia kumpongeza Mheshimiwa Emmanuel Lekishon Shangai kwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro na Mheshimiwa Shamsi Vuai Nahodha kwa kuteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Aidha, ninaomba nitumie fursa hii adhimu kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge wote kwa juhudi kubwa wanazozifanya katika kusimamia na kuhifadhi maliasili; na kuendeleza utalii. Vilevile, ninawashukuru wananchi wa Mkoa wa Njombe kwa kuendelea kuniunga mkono katika kutekeleza majukumu yangu kama Mbunge na Waziri wa Maliasili na Utalii. Ninapenda kuwahimiza wote kushiriki katika uhifadhi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maendeleo endelevu ya nchi yetu.
- Mheshimiwa Spika, naungana na
- Mheshimiwa Spika, ninapenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa viongozi wenzangu wa Wizara akiwemo Mheshimiwa Mary Francis Masanja (Mb.), Naibu Waziri; Dkt. Francis Kasabubu Michael, Katibu Mkuu; na Ndugu Juma Selemani Mkomi, Naibu Katibu Mkuu kwa ushirikiano wanaonipa katika kutekeleza majukumu yangu. Aidha, nimpongeze mtangulizi wangu Mheshimwa Dkt. Damas Daniel Ndumbaro (Mb.), Waziri wa Katiba na Sheria kwa mchango wake alioutoa katika kufanikisha majukumu mbalimbali ya Wizara. Vilevile, ninawashukuru Watendaji Wakuu na Watumishi wa Wizara; na wadau wote wa Sekta ya Maliasili na Utalii kwa ushirikiano wanaoendelea kutupatia katika kuiongoza sekta hii muhimu kwa maendeleo ya Taifa letu.
- Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee ninaomba kutumia fursa hii kuwashukuru viongozi wote wa Serikali wakiwemo waheshimiwa mawaziri, wabunge na wakuu wa taasisi; pamoja na watumishi, ndugu, jamaa na marafiki kwa jinsi walivyojitoa katika kutufariji na kufanikisha mazishi ya marehemu mama yetu mpendwa Regina Mlowe. Mwenyezi Mungu awabariki sana.
- Mheshimiwa Spika, nitumie nafasi hii kutoa pole kwako, Mheshimiwa Naibu Spika, Waheshimiwa
Wabunge wa Bunge lako Tukufu, ndugu, jamaa, marafiki na watanzania wenzangu kwa kuondokewa na wapendwa wetu: Mheshimiwa Elias Kwandikwa, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu; Mheshimiwa William Tate Olenasha aliyekuwa Naibu Waziri wa Uwekezaji (Ofisi ya Waziri Mkuu) na Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro; Mheshimiwa Khatibu Said Haji aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Konde Zanzibar; na Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Rukwa. Aidha, natoa pole kwa ndugu, marafiki na watumishi wote wa Wizara kutokana na watumishi 10 waliopoteza maisha wakati wakitekeleza majukumu yao. Kwa hakika, watumishi hawa ni mashujaa ambao wamepoteza maisha wakitetea rasilimali za nchi yetu. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu wote mahali pema peponi, Amina. Pia, nitumie fursa hii kutoa pole kwa watumishi waliojeruhiwa wakati wanatekeleza majukumu yao. Sambamba na hilo, ninatoa pole za dhati kwa wananchi ambao wamepata madhara kutokana na wanyamapori wakali na waharibifu na hivyo kujeruhiwa, kupoteza ndugu na kuharibiwa mali zao. - Mheshimiwa Spika, hotuba hii inajumuisha sehemu kuu tano (5) ambazo ni: Utangulizi; Mchango wa Maliasili na Utalii katika kukuza Uchumi na
Maendeleo Endelevu; Maoni na Ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii; Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2021/2022; na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2022/2023.
2.0 MCHANGO WA MALIASILI NA UTALII KATIKA KUKUZA UCHUMI NA MAENDELEO ENDELEVU
- Mheshimiwa Spika, Tanzania imebarikiwa kuwa na rasilimali za maliasili na malikale zenye mchango mkubwa katika uendelezaji utalii, ustawi wa wananchi na ukuaji wa uchumi. Aidha, maeneo ya hifadhi ndiyo vyanzo vikuu vya maji, nishati, makazi ya wanyamapori na viumbe wengine. Pia, maeneo hayo ni muhimu katika uhifadhi wa udongo na ufyonzaji wa hewa ukaa, hali inayopunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. Vilevile, malikale zinatumika kuhifadhi historia na tamaduni zetu.
- Mheshimiwa Spika, maliasili zimeendelea kuchangia katika Pato la Taifa (GDP) na ustawi wa jamii kupitia shughuli za kiuchumi ikiwemo utalii na uuzaji wa mazao ya misitu na nyuki. Mathalan, misitu huchangia asilimia 85 ya nishati yote inayotumika nchini kutokana na matumizi ya miti (mkaa na kuni); na asilimia 90 ya vifaa vya ujenzi na samani zinazotumika majumbani. Kwa upande mwingine, rasilimali za misitu na nyuki huchangia asilimia 3.3 ya Pato la Taifa; asilimia 5.9 ya mapato yatokanayo na biashara ya nje; na ajira takriban milioni 4 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Katika hatua nyingine, asilimia 90 ya umeme unaozalishwa kwa nguvu ya maji unatokana na vyanzo vya maji ambavyo vingi viko katika maeneo yaliyohifadhiwa. Hata hivyo, mchango huo katika GDP haujumuishi thamani ya kifedha na faida nyingine kama vile huduma za kiikolojia na faida nyingine za misitu. Aidha, utalii huchangia asilimia 25 ya fedha za kigeni na huzalisha ajira takriban milioni 1.6 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa mwaka. Kwa upande mwingine, ustawi wa utalii unategemea pamoja na masuala mengine, miundombinu iliyo bora pamoja na uhifadhi wa maliasili, malikale, historia na utamaduni.
- Mheshimiwa Spika, mwenendo wa hali ya uhifadhi unaonesha kuongezeka kwa uharibifu wa maliasili na mazingira katika maeneo mengi nchini. Kiwango cha kutoweka kwa misitu kwa mwaka kimeongezeka kutoka hekta 372,800 kwa makadirio ya mwaka 2015 hadi hekta 469,420 kwa makadirio ya mwaka 2018. Uharibifu huo unasababishwa na ongezeko la idadi ya watu, usafishaji wa mashamba kwa ajili ya kilimo, uchomaji moto holela na matumizi mengine yasiyo endelevu ya rasilimali za misitu. Hali hiyo inachangia kuleta mabadiliko ya tabianchi na athari zake kama vile ukame, kuongezeka kwa joto, mafuriko na mabadiliko ya misimu ya mvua.
- Mheshimiwa Spika, uhusiano bora kati ya uhifadhi na maendeleo una mchango mkubwa katika ustawi na matumizi endelevu ya maliasili, ukuaji wa uchumi, ustawi wa wananchi na usalama wa Taifa. Ninaomba nitumie fursa hii kutoa rai kwa Watanzania wote na wadau wa sekta ya maliasili na utalii nchini, kuendelea kushirikiana na Wizara kuhifadhi maliasili, malikale na kuendeleza utalii, kwa maendeleo ya Taifa letu na dunia kwa ujumla.
3.0 MAONI NA USHAURI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ARDHI, MALIASILI NA UTALII
- Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 04 hadi 05 Mei 2021, Wizara iliwasilisha katika Bunge lako Tukufu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2021/2022, na kupokea maoni na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii pamoja na michango ya Waheshimiwa Wabunge, kwa lengo la kuboresha utekelezaji wa majukumu yake. Vilevile, Wizara imepokea maoni ya Kamati wakati ikiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mpango na bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
- Mheshimiwa Spika, ushauri na maoni ya Kamati yalikuwa ni pamoja na: kutambua, kuendeleza na kutangaza vivutio vya utalii; usimamizi wa maliasili; kujenga na kuimarisha miundombinu iliyomo ndani ya hifadhi; kudhibiti uvamizi katika maeneo ya hifadhi; na kutatua migogoro. Ushauri mwingine ulikuwa kushirikisha Sekta Binafsi; elimu na uhamasishaji; usimamizi na ukusanyaji wa mapato; kuongeza bajeti ya miradi ya maendeleo ya Wizara; kuandaa Mpango kazi mahsusi wa kunufaika na Mjusi dinosaria aliyepo Ujerumani; na kuvuna mamba kwenye mikoa ambayo imekumbwa na matukio mengi ya wananchi kushambuliwa na wanyama hao.
- Mheshimiwa Spika, pia, Kamati ilishauri kuimarishwa kwa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) nchini kwa kuanzisha kampasi kikanda, kupandisha hadhi Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kuwa mamlaka, kufanya utafiti na tathmini ya aina ya miti inayofaa na idadi inayotakiwa kupandwa katika mikoa yote nchini, kuongeza kasi ya kupanda miti kibiashara katika maeneo mengine nchini, na kuanzisha Kampasi ya Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) katika mikoa ya kanda ya kusini mwa nchi.
- Mheshimiwa Spika, naomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Wizara imezingatia maoni na ushauri wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022 na maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka wa fedha
2022/2023.
4.0 UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI KWA
MWAKA 2021/2022
- Mheshimiwa Spika, Wizara ya Maliasili na Utalii ina jukumu la kusimamia uhifadhi wa maliasili, malikale na maendeleo ya utalii. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wizara inasimamia maeneo yaliyohifadhiwa kisheria yenye ukubwa wa kilomita za mraba 307,800 sawa na asilimia 32.5 ya eneo lote la nchi. Maeneo hayo yanajumuisha hifadhi za Taifa 22, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, mapori ya akiba 27, mapori tengefu 26, maeneo ya Jumuiya ya Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) 21, maeneo matatu (3) ya ardhioevu chini ya mkataba wa Ramsar, hifadhi za misitu ya asili 419, hifadhi za misitu ya mazingira asilia 20, mashamba ya miti ya Serikali 24, hifadhi za nyuki 12, maeneo ya malikale 132 na vituo saba (7) vya Makumbusho ya Taifa.
- Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2021/2022 umezingatia miongozo mbalimbali ikiwemo Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/2022 – 2023/2024, Mpango wa Tatu wa
Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 –
2025/2026), Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 – 2025, Sera na Sheria mbalimbali, Mpango Mkakati wa Wizara (2021/2022 –
2025/2026), maagizo mbalimbali ya viongozi wa Serikali na mikataba ya kikanda na kimataifa. - Mheshimiwa Spika, naomba sasa nitoe taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2021/2022.
4.1 Ukusanyaji Maduhuli
- Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara iliidhinishiwa kukusanya maduhuli ya Shilingi 689,345,854,249.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 478,014,580,522.00 zinakusanywa na Wizara kupitia mfumo wa TRA kutoka vyanzo vya
TANAPA, NCAA na TAWA na Shilingi
211,331,273,727.00 zinakusanywa moja kwa moja na Wizara kupitia mfumo wa MNRT Portal kutoka Idara, Mifuko na Taasisi nyingine za Wizara. Hadi kufikia mwezi Aprili 2022, Wizara imekusanya jumla ya Shilingi 397,428,671,967.86 sawa na asilimia 58 ya lengo la makusanyo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 250,985,216,073.86 zimekusanywa kupitia TRA na Shilingi 146,443,455,894.00 zimekusanywa na Wizara kupitia mfumo wa MNRT
Portal.
4.2 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara iliidhinishiwa kutumia jumla ya Shilingi 571,632,424,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida na miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 418,859,544,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi
152,772,880,000.00 ni miradi ya maendeleo. Hadi kufikia mwezi Aprili 2022, Wizara na Taasisi zake ilikuwa imepokea jumla ya Shilingi
416,601,358,591.55 sawa na asilimia 73 ya bajeti iliyoidhinishwa. Kati ya fedha hizo, Shilingi 357,120,042,324.35 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 59,481,316,267.20 kwa ajili ya miradi ya maendeleo.
4.3 Mafanikio
- Mheshimiwa Spika, katika utekelezaji wa majukumu yake kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara imepata mafanikio mbalimbali yakiwemo:
4.3.1 Utangazaji Utalii na Kuvutia Uwekezaji kupitia Programu Maalum ya Tanzania – The Royal Tour
- Mheshimiwa Spika, kipekee kabisa, napenda kuungana na Watanzania wenzangu kumpongeza Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa juhudi zake kubwa za kuitangaza nchi yetu kimataifa kupitia programu ya Tanzania – The Royal Tour. Programu hiyo imewezesha kuitambulisha Tanzania kimataifa kwa kutangaza vivutio vya utalii vya kipekee vya nchi yetu; kuonesha fursa mbalimbali za uwekezaji kwenye sekta ya maliasili na utalii pamoja na kuimarisha nafasi ya nchi katika Jumuiya za kimataifa. Kimsingi, programu hii imehusisha uandaaji wa filamu inayoonesha vivutio na fursa za uwekezaji zilizopo nchini. Pamoja na maeneo mengine, filamu hiyo inaonesha pia vivutio mbalimbali vya utalii katika hifadhi za Taifa, Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, maeneo ya malikale, tamaduni zetu na visiwa vya Zanzibar.
- Mheshimiwa Spika, programu hii ilizinduliwa mwezi Aprili, 2022 katika Jiji la New York na Jiji la Los Angeles nchini Marekani; na kuendelea katika Jiji la Arusha, Dar es Salaam, Dodoma na Zanzibar. Katika uzinduzi uliofanyika nchini Marekani, zaidi ya watu 6,000 walishiriki wakiwemo: viongozi wa kitaifa, viongozi wa majiji husika, watu maarufu, wadau wa utalii na uhifadhi, wawekezaji na wafanyabiashara mbalimbali. Uzinduzi huo pia ulishirikisha vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa vikiwemo: vituo vya televisheni na redio vya CBS, Fox News, NBC, YouTube na PBS – Amazon Prime video.
- Mheshimiwa Spika, programu ya Tanzania – The Royal Tour imeanza kuleta matunda kwa kuvutia watalii na wawekezaji mbalimbali kutembelea nchini. Mathalan, wakala wa utalii zaidi ya 30 kutoka katika masoko ya utalii yakiwemo Marekani, Ufaransa na Lithuania wamehamasika kutembelea nchini ili kujifunza na kujionea vivutio mbalimbali vya utalii kwa lengo la kuvitangaza katika nchi zao. Aidha, wawekezaji kutoka Taifa la Bulgaria wameonesha nia ya kuwekeza nchini kwa kujenga hoteli nne (4) zenye hadhi ya nyota tano (5) katika hifadhi za Taifa Serengeti, Ziwa Manyara na Tarangire; na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Serikali imesaini mkataba wa ushirikiano katika masuala ya utalii, biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Jiji la Dallas Marekani, mwezi Aprili, 2022. Hatua hiyo itafungua fursa za usafiri wa anga kwa kuwezesha safari za moja kwa moja za ndege kutoka Tanzania hadi Dallas, Marekani na hivyo kuongeza idadi ya wageni nchini. Sambamba na hilo, mtandao maarufu wa habari nchini Marekani ujulikanao kama theGrio umetambua juhudi za Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuiongoza vyema sekta ya utalii na uhifadhi nchini, hivyo kuifanya Tanzania kuwa kivutio cha kwanza cha utalii katika Bara la Afrika kwa mwaka 2022. Kwa ujumla, jitihada hizi zitaleta matokeo chanya katika kuongeza idadi ya watalii na hivyo kufikia lengo la watalii milioni 5 na mapato Dola za Marekani bilioni 6 ifikapo mwaka 2025, kama ilivyoelekezwa katika Ibara 67(a) ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020 – 2025.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza programu hiyo, Wizara itaendelea kuimarisha miundombinu mbalimbali ya utalii ikiwemo barabara, viwanja vya ndege na mawasiliano katika maeneo ya hifadhi ili kuhakikisha vivutio vilivyomo vinafikika kwa urahisi. Aidha, Wizara itaboresha huduma za malazi kwa kuongeza idadi ya vitanda na kuvutia uwekezaji; kutangaza vivutio vya utalii; kuibua mazao mapya ya utalii; kuimarisha utoaji mafunzo ya huduma katika sekta ya utalii na ukarimu; kuimarisha ulinzi na usalama wa wageni wanaotembelea maeneo ya hifadhi; na kuimarisha ushirikiano na wadau mbalimbali ikiwemo sekta binafsi.
- Mheshimiwa Spika, napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Waheshimiwa Wabunge na Watanzania kuendelea kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania za kutangaza utalii na kuvutia uwekezaji kwa maslahi mapana ya Taifa na ustawi wa jamii kwa ujumla.
4.3.2 Tanzania kuendelea Kutambulika Kimataifa katika Masuala ya Utalii na Uhifadhi - Mheshimiwa Spika, kufuatia jitihada za Wizara za kutangaza vivutio kwenye masoko mbalimbali na kuboresha huduma za utalii na uhifadhi, Tanzania imeendelea kutambulika kimataifa na kupata tuzo mbalimbali zikiwemo: Hifadhi ya Taifa Serengeti kuwa hifadhi inayoongoza kwa ubora Barani Afrika (Africa’s Leading National Park Attraction) kwa miaka mitatu (3) mfululizo kuanzia mwaka 2019 hadi 2021; na Tanzania kuwa nchi inayoongoza kwa shughuli za utalii Barani Afrika (Africa’s Leading Destination for the Year 2021), tuzo hizi zilitolewa na World Travel Award. Tuzo nyingine ni pamoja na
Travellers’ Choice Destination – National Parks of the World, iliyotolewa na Tripadvisor ambapo Tanzania imeingiza hifadhi nne (4) katika orodha ya hifadhi 25 bora duniani zikiongozwa na Hifadhi ya Taifa Serengeti. Hifadhi nyingine ni Hifadhi za Taifa Kilimanjaro na Tarangire; na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Vilevile, Shirika la Hifadhi za Taifa limetunukiwa Cheti cha Ubora wa Huduma za Kiwango cha Kimataifa cha ISO 9001:2015 kutokana na kuimarishwa kwa utoaji wa huduma bora za utalii. - Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo, TANAPA imepata tuzo ya utoaji wa huduma zenye viwango (European Awards for Quality Achievement – Platinum) iliyotolewa na European Society for Quality Research – ESQR. Aidha, Zanzibar na Jiji la Arusha zimeorodheshwa na Tripadvisor kupitia Travellers’ Choice Destination – Afrika kuwa miongoni mwa maeneo 10 bora ya shughuli za utalii Barani Afrika. Katika hatua nyingine, Hifadhi ya Taifa Serengeti imeibuka kinara kati ya vivutio 10 bora vilivyoorodheshwa na mtandao wa safaribookings.com ulio maarufu duniani kama kivutio kinachofaa kutembelewa katika Bara la Afrika. Aidha, Tanzania imepewa tuzo ya kutambulika kwa ufanisi katika uhifadhi na utalii. Tuzo hii imetolewa na Serikali ya Jamhuri ya Sudan Kusini wakati wa Onesho la Kwanza la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki (East Africa Regional Tourism Expo – EARTE) lililofanyika Jijini Arusha mwezi Oktoba, 2021. Kwa ujumla, tuzo hizi zimekua chachu ya kuvutia na kuwajengea imani watalii kutoka masoko mbalimbali ya utalii duniani hasa katika kipindi hiki cha janga la UVIKO-19.
4.3.3 Kuongezeka kwa Malighafi ya Mazao ya Misitu kwa ajili ya Viwanda
- Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kuongeza upatikanaji wa malighafi ya mazao ya misitu katika mashamba ya miti ya Serikali mita za ujazo 729,000 kwa mwaka 2020/2021 hadi wastani wa mita za ujazo 1,000,000 kwa mwaka 2021/2022. Ongezeko hili la malighafi limeiwezesha Wizara kuingia mikataba 561 ya uvunaji wa mazao ya misitu katika mashamba ya miti ya Serikali na wafanyabiashara wa mazao hayo. Mafanikio haya yametokana na juhudi mbalimbali zikiwemo: kuendeleza mashamba ya miti kwa kupanda miche 29,670,223; na kuanzisha Shamba jipya la Miti la Makere, Mkoa wa Kigoma lenye ukubwa wa hekta 29,827. Juhudi nyingine ni pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu uhifadhi na uanzishwaji wa mashamba ya miti ya taasisi na watu binafsi.
4.3.4 Kuongezeka kwa Matumizi ya Mifumo ya Kielektroniki katika Uendeshaji wa Minada ya Mazao ya Misitu na
Wanyamapori
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeongeza matumizi ya mifumo ya kielektroniki katika kuendesha minada ya mazao ya misitu na wanyamapori. Katika kufanikisha hili, Wizara imeendesha kwa mara ya kwanza minada miwili ya kielektroniki ya kuuza mazao ya misitu. Hatua hii imeongeza uwazi na ushindani ambao umesababisha kuongezeka kwa mapato ya mauzo yatokanayo na minada ya kielektroniki ya misaji na mkurungu kwa asilimia 15 ikilinganishwa na ambavyo ingeuzwa kwa njia ya kiutawala. Aidha, Wizara imefanikiwa kuuza kwa njia ya mnada jumla ya mita za ujazo 989.99 za magogo ya miti aina ya mkurungu ambapo kiasi cha Shilingi 1,686,300,000.00 kimepatikana.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara imefanikiwa kuendesha jumla ya minada saba (7) ya kielektroniki iliyojumuisha vitalu 100 vya uwindaji wa kitalii. Kati ya vitalu hivyo, 64 vimeuzwa na kufanikiwa kukusanya jumla ya Shilingi
18,078,000,000.00 ikilinganishwa na kiasi cha Shilingi 5,023,200,000 ambacho kingekusanywa kwa njia ya kiutawala (administrative allocation). Kwa muktadha huo, mauzo kwa njia ya mnada wa kielektroniki yamewezesha soko kuamua thamani halisi ya vitalu vya uwindaji wa kitalii. Mathalan, kitalu cha daraja la tatu (3) kilichokuwa kinauzwa kwa Dola za Marekani 18,000 kupitia njia ya kiutawala, kimenunuliwa kwa Dola za Marekani 255,000 ikiwa ni ongezeko la asilimia 1,317. Pamoja na ongezeko la mapato, matumizi ya mifumo hii imeendelea kuongeza uwazi na kurahisisha ufanyaji biashara katika mazao ya misitu na wanyamapori.
4.3.5 Kushiriki kikamilifu katika Miradi ya Kimkakati
- Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imefanikiwa kukamilisha kazi ya kusafisha eneo la ekari 274,608 kwa ajili ya Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme la Julius Nyerere. Aidha, Wizara imeendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika eneo la mradi. Sambamba na hatua hiyo, Wizara imeshiriki katika zoezi la kufanya tathmini ya athari za kimazingira katika eneo la Mradi wa Ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania lenye urefu wa kilomita 1,443. Lengo la tathmini hiyo ni kuhakikisha kuwa maliasili na malikale zilizopo katika eneo la mradi zinaendelea kuhifadhiwa. Kukamilika kwa miradi hii kutaongeza tija katika kuvutia uwekezaji katika Sekta ya Maliasili na Utalii na sekta nyingine za kiuchumi.
4.3.6 Kuendeleza Utalii Ikolojia katika Hifadhi za Misitu za Mazingira Asilia
- Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa mazao ya utalii nchini, Wizara imeendelea kuboresha miundombinu ya utalii ikolojia katika hifadhi za misitu ya mazingira asilia zikiwemo hifadhi za Amani, Pugu Kazimzumbwi, Kalambo, Rungwe, Magamba na Ziwa Duluti. Baadhi ya juhudi zilizofanyika ni ukarabati wa barabara zenye urefu wa kilomita 66.7, njia za watembea kwa miguu kilomita 163.2 na ujenzi wa kambi tano (5) za kitalii. Sambamba na hilo, Wizara imeandaa na kurusha vipindi 105 vya redio, 48 vya televisheni, makala 72, video clips 87 na vipeperushi 21,200 vya kutangaza vivutio vilivyopo katika maeneo hayo; na kuendesha programu mbalimbali za uhifadhi na utalii wa ndani.
4.3.7 Sekta ya Utalii Kuendelea kuwa Stahimilivu (Resilient) katika kipindi cha UVIKO-19
- Mheshimiwa Spika, pamoja na changamoto ya uwepo wa janga la UVIKO-19, sekta ya utalii nchini imeendelea kuwa stahimilivu ambapo idadi ya watalii na mapato yameendelea kuongezeka. Mathalan, katika mwaka 2021, Tanzania imefanikiwa kupokea jumla ya watalii wa kimataifa 922,692 ikiwa ni ongezeko la asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 kwa mwaka 2020. Aidha, mapato yatokanayo na watalii wa kimataifa yameongezeka kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 hadi Dola za Marekani milioni 1,310.34 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 82. Mafanikio hayo yamechochewa na juhudi mbalimbali zilizofanywa na Wizara zikiwemo: kufanikisha Onesho la Kwanza la Kimataifa la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki; na uzinduzi wa programu maalum ya Tanzania – The Royal Tour. Juhudi nyingine ni pamoja na kutumia mabalozi wa hiari wa utalii, ziara za mafunzo (FAM – trips) na utekelezaji wa Mwongozo wa Kuendesha Shughuli za utalii katika kipindi cha kukabiliana na janga la UVIKO – 19.
4.3.8 Kukua kwa Utalii wa Ndani
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuhamasisha utalii wa ndani kupitia kampeni na programu mbalimbali. Hatua hizi zimeongeza idadi ya watalii wa ndani waliotembelea maeneo ya hifadhi, vituo vya malikale na makumbusho kutoka watalii 562,549 mwaka 2020 hadi 788,933 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 40.2. Ongezeko la idadi ya watalii limechangiwa na juhudi mbalimbali zikiwemo: Kampeni ya kutangaza utalii wa faru katika Hifadhi ya Taifa Mkomazi; programu maalum ya Onesho la Mchango wa Mwanamke katika Kuhifadhi Mila na Utamaduni wa Mtanzania; Kampeni Maalum ya Uhamasishaji wa Kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru; matukio mbalimbali ya utalii wa michezo; maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani; na maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani 2022 ambapo takriban wanawake 680 walitembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Sambamba na hilo, Wizara imeendelea kushirikiana na vyombo vya habari kutangaza na kuhamasisha utalii wa ndani.
4.3.9 Kupungua kwa Ujangili na Uvunaji Haramu wa Maliasili
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuongeza jitihada za kuimairisha ulinzi na uhifadhi wa rasilimali za maliasili kwa kudhibiti ujangili, biashara haramu ya nyara, uvunaji haramu wa mazao ya misitu na nyuki na uvamizi wa maeneo yaliyohifadhiwa. Jitihada hizo zinadhihirishwa na matokeo ya sensa ya wanyamapori iliyofanyika mwaka 2021 ambapo idadi ya tembo imeongezeka kwa asilimia 30 katika Mfumo Ikolojia Ziwa Natron – West Kilimanjaro. Aidha, katika Mfumo Ikolojia Ruaha – Rungwa, idadi ya nyati imeongezeka kwa asilimia 80; pundamilia asilimia 36; na palahala asilimia 65 ikilinganishwa na sensa iliyofanyika mwaka 2018. Pia, idadi ya faru weusi ambao wako hatarini kutoweka imeongezeka kwa asilimia 27.5 ikilinganishwa na idadi yao kwa mwaka 2018. Ongezeko la wanyamapori hao ni kiashiria cha kuimarika kwa ulinzi na usimamizi wa maeneo ya hifadhi.
- Mheshimiwa Spika, mafanikio hayo yamechangiwa na juhudi za Serikali ikiwa ni pamoja na kufanya doria ambapo jumla ya siku doria 434,371 zimefanyika na kuwezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 7,719 pamoja na nyara za Serikali na magogo yenye ujazo wa mita 1,218. Juhudi nyingine ni kufanya operesheni maalum za kiintelijensia zilizowezesha kuzuiwa kwa matukio 66 ya ujangili; kukamatwa kwa silaha mbalimbali zikiwemo bunduki 135 na kuvunjwa kwa mitandao ya ujangili; na kuimarisha Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu kwa kutoa mafunzo ya kijeshi, upelelezi, uchunguzi na usimamizi wa kesi kwa watumishi mbalimbali. Pamoja na juhudi hizi natoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na Wizara kulinda na kutunza rasilimali zilizopo kwa maslahi ya kizazi cha sasa na vijavyo.
4.3.10 Kupandishwa Hadhi Maeneo ya Hifadhi
- Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kupandisha hadhi mapori tengefu matatu (3) na WMA moja (1) kuwa mapori ya akiba Luganzo – Tongwe, Msima, Igombe na Wami – Mbiki. Hatua hii imeongeza idadi ya Mapori ya Akiba kutoka 22 hadi 27. Lengo la jitihada hizi ni kuimarisha ulinzi na matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo katika maeneo hayo. Aidha, upandishwaji hadhi wa maeneo hayo unalenga kuchochea uhifadhi na uwekezaji katika shughuli za utalii wa picha na uwindaji.
4.3.11 Kuimarika kwa Utalii wa Urithi wa Utamaduni na Malikale
- Mheshimiwa Spika, Wizara imefanikiwa kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea vituo vya malikale na makumbusho kutoka 349,264 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia 582,080 mwezi Machi 2021/2022 sawa na ongezeko la asilimia 167. Ongezeko hilo limechochewa na juhudi mbalimbali zikiwemo: kuanzisha programu maalum za kuhamasisha makundi mbalimbali katika jamii kutembelea vivutio vya malikale na makumbusho; kufanya matamasha ya utamaduni katika maeneo mbalimbali nchini; kuanzisha jarida maalum la makumbusho; na kufanya mikutano maalum na wahariri wa vyombo vya habari. Katika hatua nyingine, Wizara imeimarisha miundombinu katika maeneo ya malikale na makumbusho kwa kujenga nyumba 12 zinazoonesha tamaduni za jamii ya Wangoni, Wakinga, Wasafwa na Wasukuma kwa kufuata ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam; kukarabati jengo la kihistoria la Soko la Watumwa; na jengo alilokuwa anafikia Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere – Mikindani, Mtwara katika kipindi cha harakati za uhuru.
4.4 Utekelezaji wa Masuala Mtambuka
4.4.1 Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi Katika Maeneo Yaliyohifadhiwa
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutatua migogoro ya ardhi baina ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa. Baadhi ya kazi zilizofanyika ni pamoja na kuhakiki mipaka ya hifadhi yenye urefu wa kilomita 33,107; kusafisha kilomita 5,743; na kuweka vigingi 1,219 na mabango 1,096 katika maeneo ya hifadhi za misitu na wanyamapori. Katika hatua nyingine, Wizara imeendelea kushiriki na kutoa ushirikiano kwa Kamati ya Kitaifa ya Mawaziri nane (8) yenye lengo la kutatua migogoro ya ardhi nchini. Pia, Wizara imeendelea na zoezi la uhakiki wa mipaka ya maeneo ya malikale na urithi wa utamaduni kwa kupima maeneo ya vituo vya Kalenga, Tembe la Kwihara, Ujiji Kigoma, Tongoni, Amboni na Kunduchi; na kuendelea na taratibu za kupata hati za umiliki za maeneo hayo. Aidha, Wizara imeendelea kutoa elimu kwa wananchi pamoja na kamati mbalimbali katika ngazi za mkoa na wilaya kuhusu umuhimu wa kulinda maeneo yaliyohifadhiwa.
4.4.2 Ushirikishaji wa Wadau katika Uhifadhi na Uendelezaji Utalii
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana na wananchi, sekta binafsi, washirika wa maendeleo na wadau wengine katika kutekeleza majukumu yake. Katika kufanikisha hilo, Wizara imepanda miti 13,000,000 katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mashambani, maeneo yaliyoathiriwa na uharibifu wa mazingira pamoja na kandokando ya vyanzo vya maji. Kati ya miche hiyo, miche 690,000 ilipandwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dodoma kama jitihada za kuendeleza kampeni ya Dodoma ya Kijani. Aidha, katika kuendelea kuhamasisha jamii kushiriki katika uhifadhi na kunufaika na rasilimali za maliasili, Wizara imegawa mizinga ya nyuki 2,133; madawati 111; na kugawa vifaa vya ujenzi kama vile saruji mifuko 305, mbao 2,423 na vifaa mbalimbali vya michezo. Kwa upande mwingine, Wizara imejenga soko la samaki, Kilombero; jengo la utawala na maktaba katika Shule ya Sekondari ya Mwambesi, Pwani; ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi ya Ihefu, Mufindi; na ukarabati wa soko katika Kijiji cha Sange, Ileje.
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa jamii na wadau wengine wanapata elimu kuhusu uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za maliasili na shughuli za Utalii, Wizara imeendelea kutoa elimu ya uhifadhi wa rasilimali za wanyamapori, misitu na nyuki kwa viongozi wa Wilaya, Kata, vijiji, kamati za maliasili za vijiji, madiwani, wanafunzi na vikundi vya ufugaji nyuki kwa kufanya mikutano 16,046 katika vijiji 2,107. Aidha, elimu ya uhifadhi wa malikale imetolewa katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani, Mwanza na Tabora. Vilevile, Wizara imewezesha jamii kuanzisha na kutangaza hifadhi za misitu na nyuki za vijiji zenye ukubwa wa hekta 541,562.97 katika wilaya za Liwale, Handeni, Tunduru, Kilwa, Mpwapwa na Kilosa. Pia, Wizara imeendelea kushirikiana na wadau katika kuwaelimisha kuhusu miongozo ya uendeshaji wa biashara za utalii nchini, uendelezaji wa mazao ya utalii ikiwemo utalii wa utamaduni na fukwe. Kwa upande mwingine, Wizara imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mbinu za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuhamasisha jamii katika masuala ya uhifadhi wa mila na utamaduni wa mtanzania, jamii ya wenyeji wa mikoa ya Njombe (Wakinga) na Mbeya (Wasafwa) zimefanikiwa kujenga kaya zenye jumla ya nyumba saba (7) katika Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam. Aidha, Wizara imewezesha uanzishaji wa
Makumbusho ya Wairaq katika Wilaya ya Karatu; Makumbusho ya Benki ya CRDB, Dar es Salaam; na uboreshaji wa Makumbusho ya Bujora na kituo cha Utamaduni Dofa, Karatu. Vilevile, Katika jitihada za kukabiliana na moto kichaa, Wizara kwa kushirikiana na wadau imetoa elimu kwa wananchi 1,731 kutoka katika vijiji 333 vinavyopakana na hifadhi za Taifa Kilimanjaro, Burigi – Chato, Udzungwa na Mto Ugalla; na maeneo ya hifadhi za misitu na nyuki.
4.4.3 Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
- Mheshimiwa Spika, Tanzania ilipewa heshima ya kuwa nchi pekee ya Kanda ya Afrika kushiriki mdahalo maalum wa mawaziri kuhusu masuala ya kisera ya uendelezaji utalii katika maeneo ya vijijini yaani Ministerial Debate on Policies to Foster
Tourism for Rural Development. Mdahalo huo ulifanyika wakati wa Mkutano Mkuu wa 24 wa Shirika la Utalii Duniani Jijini Madrid, Uhispania mwezi Desemba, 2021 ambapo Tanzania ilishiriki na ilisisitiza uimarishaji wa uhifadhi na utalii endelevu. Aidha, Tanzania ilipongezwa kwa mkakati wake wa kuendeleza utalii wa utamaduni na vyakula kupitia zao jipya la Swahili Tourism. Katika hatua nyingine, Wizara ilishiriki Mkutano wa 64 wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Utalii Kamisheni ya Afrika uliofanyika nchini Cabo Verde mwezi Septemba, 2021; na maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani yaliyofanyika Jijini Abidjan, Ivory Coast mwezi Septemba, 2021. - Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara imeshiriki mikutano mbalimbali katika Sekta ya Maliasili na Utalii ikiwemo: Mkutano wa 13 wa Kamati ya Uongozi wa Mkataba wa Lusaka katika kukabiliana na ujangili na usafirishaji haramu wa mazao ya wanyamapori na mimea uliofanyika Jijini Livingstone, Zambia mwezi Machi 2022; Mkutano wa 23 wa nchi wanachama wa Mkataba wa UNESCO wa mwaka 1972 unaohusu ulinzi na uhifadhi wa maeneo ya Urithi wa Dunia uliofanyika Paris, Ufaransa mwezi Novemba, 2021; na Mkutano wa Umoja wa Afrika kuhusu urejeshwaji wa urithi wa utamaduni ulio nje ya Bara la Afrika uliofanyika Dakar Senegal mwezi Novemba, 2021. Vilevile, Wizara ilishiriki Jukwaa la Uhifadhi wa Wanyamapori Afrika uliofanyika Gaborone, Botswana mwezi Novemba, 2022; Mkutano wa masuala ya uwindaji wa kitalii uliofanyika Las Vegas, Marekani mwezi Januari, 2022; na Mikutano ya Mkataba wa Kimataifa Unaosimamia Biashara ya Wanyamapori na Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES) iliyofanyika Mwezi Machi, 2022 nchini Ufaransa.
- Mheshimiwa Spika, Sambamba na hilo, Wizara imeshiriki Mkutano wa Nne (4) wa Tume ya Pamoja ya Ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya uliofanyika Jijini Nairobi nchini Kenya mwezi Agosti, 2021. Aidha, Wizara imeshiriki mkutano wa ushirikiano baina ya Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika sekta za maliasili, malikale na utalii uliofanyika Zanzibar mwezi Septemba, 2021 ili kuboresha ushirikiano katika uhifadhi wa maliasili, malikale na uendelezaji wa utalii. Vilevile, Wizara imeendesha mafunzo ya kujengea uwezo watalaam wa Afrika ili kuwawezesha kuandaa maeneo ya kuingizwa katika Orodha ya Urithi wa Dunia. Mafunzo hayo yalifanyika Jijini Dar es Salaam mwezi Desemba, 2021 na yalishirikisha nchi 10 ambazo ni Msumbiji, Zimbabwe, Ethiopia, Kenya, Uganda, Afrika Kusini, Zambia, Rwanda, Algeria na Mwenyeji Tanzania. Katika hatua nyingine, Wizara imeratibu na kushiriki mikutano mingine ya kikanda na kimataifa ikiwemo SADC, EAC, IORA, UAE, Tripatite ya AU – SADC – EAC pamoja na mikutano ya Tume za Ushirikiano kati ya Tanzania na nchi mbalimbali.
4.4.4 Utawala na Uendelezaji Rasilimaliwatu
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha utendaji kazi, Wizara imehuisha muundo wake ambapo majukumu ya kiutendaji ya Idara ya Utalii yamehamishiwa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na majukumu ya kiutendaji ya Idara ya Mambo ya Kale kwenda Shirika la Makumbusho ya Taifa (NMT). Aidha, muundo mpya wa Wizara umejumuisha Kitengo cha Uratibu wa Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu. Katika hatua nyingine, Wizara imeendelea kuboresha mazingira ya kazi ambapo nyumba na ofisi 25 zimejengwa pamoja na ununuzi wa mitambo 43, magari 74, pikipiki 33, samani na vitendea kazi vya ofisi. Sambamba na hilo, watumishi 144 wamepatiwa mafunzo ya muda mrefu na 630 ya muda mfupi ili kuwajengea uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Vilevile, Wizara imeajiri watumishi 389 wa kada mbalimbali na kupandisha vyeo watumishi 1,343. Pia, Wizara imeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kuanza ujenzi wa jengo la makao makuu ya Wizara katika eneo la Mji wa Serikali – Mtumba, Jijini Dodoma.
- Mheshimiwa Spika, ili kuimairisha afya za watumishi na kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, Wizara imeendelea kuhamasisha na kuwezesha watumishi kushiriki mazoezi mbalimbali baada ya saa za kazi na siku za mapumziko ya wiki. Aidha, Wizara kupitia taasisi zake imeshiriki mashindano ya SHIMUTA na SHIMIWI yaliyofanyika Mjini Morogoro mwezi Oktoba na Novemba, 2021 mtawalia, na maadhimisho ya Mei Mosi yaliyofanyika Jijini Dodoma mwezi Mei, 2022 na kufanikiwa kupata tuzo mbalimbali. Kwa upande mwingine, Wizara imeendelea kusimamia maslahi, maadili, ustawi na afya za watumishi ikiwa ni pamoja na kuwawezesha watumishi waliojitokeza wanaoishi na VVU na Ukimwi kupata lishe bora. Vilevile, katika kuendelea na juhudi za kupambana na janga la UVIKO-19, Wizara imetoa vifaa kinga kwa watumishi.
4.5 Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara
4.5.1 Sekta ya Wanyamapori
- Mheshimiwa Spika, Sekta ya Wanyamapori ina jukumu la kuhifadhi, kusimamia, kutoa mafunzo na kufanya tafiti za wanyamapori ndani na nje ya maeneo ya hifadhi. Utekelezaji wa majukumu hayo unaongozwa na Sera ya Taifa ya Wanyamapori ya mwaka 2007 na kusimamiwa na Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori Sura 283, Sheria ya Hifadhi za Taifa Sura 282, Sheria ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro Sura 284 na Sheria ya Kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania Sura 260. Aidha, majukumu haya yanatekelezwa kupitia Idara ya Wanyamapori, TANAPA, NCAA, TAWA, TAWIRI, TWPF, Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – Mweka (CAWM), Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori – Pasiansi (PWTI) na Kituo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii – Likuyu Sekamaganga (CBCTC).
4.5.1.1 Masuala Mahsusi ya Sekta ya Wanyamapori
(i) Utatuzi wa Migogoro baina ya Binadamu na Wanyamapori Wakali na Waharibifu
- Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na migogoro baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu, Wizara imeendelea kutekeleza Mkakati wa Kitaifa wa Utatuzi wa Migogoro baina ya Wanyamapori na Binadamu (2020 – 2024). Mkakati huu unalenga kuweka njia bora na endelevu za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu, kupunguza madhara ya wanyamapori kwa jamii na kuhakikisha kuwa wananchi wanaoishi karibu na maeneo ya hifadhi wanapata elimu ya namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
- Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza mkakati huo, Wizara imeendelea kutoa elimu ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu kwa jamii zinazoishi karibu na maeneo ya hifadhi na kutumia teknolojia ya kufuatilia nyendo za wanyamapori hao kwa kuwafunga vifaa maalum vya kusukuma mawimbi ili kurahisisha ufuatiliaji. Katika kufanikisha zoezi hilo, jumla ya tembo 107 (Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, mfumo ikolojia Tarangire – Manyara na Selous – Mikumi; mapori ya akiba Maswa na Ikorongo – Grumeti; na Pori Tengefu Longido); mbwa mwitu saba (7) na faru 64 (Mfumo Ikolojia Serengeti); nyumbu 10 (mifumo ikolojia ya Tarangire na Serengeti) na simba 21 (Mifumo Ikolojia ya Serengeti na Ruaha – Rungwa) waliofungwa mikanda ya mawasiliano (GPS collar) wameendelea kufuatiliwa mienendo yao.
- Mheshimiwa Spika, hata hivyo Wizara imetoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu hususan tembo katika wilaya 21 na kujenga vizimba viwili (2) vya mamba Ziwa Rukwa katika Wilaya ya Songwe kwa ajili ya kuwakinga wananchi na madhara ya mamba. Katika hatua nyingine, Wizara imeanzisha utaratibu wa mawasiliano wa namba za simu za kiganjani za bure kwenye kanda ili kuwezesha wananchi kutoa taarifa za wanyamapori wakali na waharibifu kwa ajili ya kupata msaada wa haraka inapotokea matukio. Vilevile, Wizara imeanzisha vikosi maalum vya mwitikio wa haraka vinavyojumuisha askari wahifadhi na askari wa vijiji hususan katika maeneo yenye matukio mengi ya wanyamapori wakali na waharibifu katika wilaya za Lindi Mjini, Tunduru, Bunda, Manyoni, Meatu, Itilima, Bariadi na Ngorongoro.
Aidha, mamba waliokuwa wanatishia uhai wa watu katika Mto Ruvu na Ziwa Victoria wamevunwa. - Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kuimarisha jitihada za kupunguza madhara yatokanayo na wanyamapori wakali na waharibu kwa wananchi. Katika mwaka wa fedha 2021/2022 Wizara imetenga fedha kiasi cha Shilingi 1,230,000,000 kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa vituo 11 vya askari wa kuzuia wanyamapori wakali na waharibifu katika wilaya 11 nchini. Vituo hivyo vinaendelea kujengwa katika Kijiji cha Malwilo Wilaya ya Meatu; Kijiji cha Kijereshi Wilaya ya Busega; Kijiji cha Milola Wilaya ya Mchinga; Kijiji cha Milonde Wilaya ya Tunduru; Kijiji cha Kwakoa Wilaya ya Mwanga; Kijiji cha Itunundu Wilaya ya Iringa; Kijiji cha Udinde Wilaya ya Songwe; Kijiji cha Ndala Wilaya ya Nzega; Kijiji cha Lubungo Wilaya ya Mvomelo; Kijiji cha Ilangali Wilaya ya Chamwino; na Kijiji cha Mtera Wilaya ya Mpwapwa.
- Mheshimiwa Spika, hatua nyingine zilizochukuliwa na Wizara ni pamoja na kuendelea kulipa kifuta jasho na kifuta machozi kwa wananchi walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu. Hadi kufikia mwezi Aprili 2022, jumla ya Shilingi 790,721,500.00 zimetolewa kwa wahanga 3,598 walioathiriwa na wanyamapori wakali na waharibifu katika wilaya 36. Aidha, Wizara itaendelea kushirikiana na wananchi na wadau mbalimbali katika jitihada za kukabiliana na wanyamapori hao.
(ii) Udhibiti wa Mimea Vamizi katika Maeneo ya Hifadhi
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kufanya tafiti na kutumia mbinu mbalimbali za kukabiliana na mimea vamizi katika maeneo ya hifadhi. Katika kutekeleza hili, Wizara imefanya tathmini katika hifadhi za Taifa nane (8) ambazo ni Serengeti, Arusha, Saadani, Mkomazi, Mikumi, Katavi, Nyerere na Ibanda – Kyerwa; na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Tathmini imebaini uwepo wa spishi 33 za mimea vamizi ikiwemo Bidens schimperi, Gutenbergia
cordifolia na Tagetes minuta kwenye eneo la ukubwa wa hekta 35,331. Wizara imeendelea kudhibiti mimea hiyo kwa kutumia mbinu mbalimbali ikiwemo matumizi ya moto mpango, kung’oa na kufyeka ambapo jumla ya hekta 10,668.88 imedhibitiwa.
4.5.1.2 Idara ya Wanyamapori
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ulinzi, usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za wanyamapori, Wizara imekamilisha Kanuni na Amri za Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu. Kukamilika kwa kanuni hizi kumewezesha utekelezaji wa mfumo na majukumu ya jeshi hilo katika kulinda rasilimali za maliasili. Sambamba na hilo, Wizara imefanya mapitio ya Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Wanyamapori (2014 – 2019) na rasimu ya Mkakati mpya wa miaka 10 (2022 – 2032) iko katika hatua ya kupata maoni ya wadau kwa hatua zaidi. Aidha, ili kuboresha mazingira ya uwekezaji na utoaji huduma kwa wateja, Wizara imefanya mapitio ya Kanuni za Utalii wa Picha za mwaka 2016; Kanuni za Uwekezaji Mahiri ya mwaka 2021; Kanuni ya Mashamba ya Wanyamapori ya mwaka 2020; na Kanuni za Biashara ya Nyara ya mwaka 2010. Vilevile, taratibu za usajili wa magari ya Jeshi la Uhifadhi kutoka namba za kiraia kwenda namba za kijeshi zimekamilika ambapo magari 1,338 kati ya 1,699 yamepata usajili huo.
- Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuimarisha uhifadhi wa wanyamapori nchini, Wizara imefanya tathmini ya mapori tengefu 18 na kuandaa mpango na vipaumbele vya maeneo matano (5) yatakayopandishwa hadhi kuwa mapori ya akiba na kukamilisha Mtaala wa mafunzo ya kijeshi. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na OR – TAMISEMI pamoja na wadau wengine imeendelea na zoezi la uhakiki wa shoroba za Kwakuchinja, Selous – Niassa na Upper – Kitete kwa lengo la kuweka alama ili kuzihifadhi. Kwa upande mwingine, Wizara inakamilisha taratibu za kuingiza nchini faru weupe 30 kutoka Afrika Kusini kwa lengo la kuboresha uhifadhi na utalii katika Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro; na hifadhi za Taifa Burigi – Chato na Mikumi.
4.5.1.3 Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania –
TANAPA
- Mheshimiwa Spika, Shirika lina jukumu la kusimamia uhifadhi na uendelezaji utalii kwenye hifadhi za Taifa 22. Katika kutekeleza jukumu hilo, Shirika limeendelea kuboresha mahusiano kati ya hifadhi na jamii ambapo elimu ya uhifadhi imetolewa kwa vijiji 477 vinavyopakana na hifadhi za Taifa. Aidha, Shirika limeongeza wigo wa kutoa elimu ya uhifadhi katika shule za msingi na sekondari kwa kuanzisha programu maalum za elimu ya uhifadhi katika shule 147 zinazopakana na Hifadhi za Taifa za Saadani, Mikumi, Udzungwa, Kitulo, Katavi, Gombe, Mahale, Rubondo, Ibanda-Kyerwa na Rumanyika – Karagwe. Vilevile, Shirika limetoa mafunzo ya kuanzisha benki za kijamii za shughuli za uhifadhi (COCOBA) kwa wanachama 649 wa vikundi 43 ili kujikwamua kiuchumi na kupunguza utegemezi wa mazao ya maliasili.
- Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha mifumo ya kiikolojia, Shirika limeendelea kudhibiti maambukizi ya magonjwa kati ya wanyamapori na mifugo. Katika kutekeleza hili, Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limetoa chanjo 63,005 dhidi ya ugonjwa wa mapafu kwa ng’ombe, kondoo na mbuzi. Chanjo hii imetolewa katika vijiji 12 vinavyopakana na hifadhi za Taifa Mkomazi na Tarangire. Aidha, chanjo dhidi ya kichaa cha mbwa imetolewa kwa mbwa 2,683 na paka 55 katika vijiji 12 vinavyopakana na hifadhi za Taifa Mkomazi na Tarangire. Hatua hii inalenga kuzuia milipuko na kusambaa kwa magonjwa yanayoweza kuathiri wanyamapori ambao kutokana na mienendo yao kwa nyakati tofauti hufika katika maeneo yaliyo nje ya hifadhi.
- Mheshimiwa Spika, ili kuboresha nyanda za malisho, kudhibiti magonjwa na moto kichaa pamoja na kuongeza mawanda ya shughuli za utalii, Shirika limeendelea kutekeleza programu za moto mpango katika hifadhi za Taifa 11 ambapo jumla ya hekta 1,935,621 zimechomwa moto. Aidha, barabara za kukinga moto zenye urefu wa kilomita 162.9 zimetengenezwa ili kuzuia moto kuunguza maeneo ya hifadhi. Katika hatua nyingine, Shirika limeendelea kuboresha miundombinu ya utalii kwa kujenga madaraja mawili (2) katika hifadhi ya Taifa Tarangire na Ruaha; kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 3,157 katika hifadhi 16; na kutengeneza mwongozo wa uendelezaji na usimamizi wa viwanja vya ndege katika hifadhi za Taifa. Vilevile, Shirika limekarabati viwanja vya ndege 12 katika hifadhi za Taifa za Ruaha, Serengeti, Nyerere, Tarangire, Saadani, Mikumi na Mkomazi.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuimarisha huduma za malazi na kuvutia uwekezaji wa utalii, Shirika limetoa maeneo 41 yenye uwezo wa kubeba vitanda 2,250 kwa wawekezaji kwa ajili ya kujenga miundombinu ya huduma za malazi kwa watalii. Aidha, jumla ya maeneo mapya 103 yenye uwezo wa vitanda 5,500 yameainishwa katika hifadhi za Taifa Nyerere, Mto Ugalla, Burigi – Chato, Rubondo, Ruaha, Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Mikumi, Saadani, Mkomazi na Arusha. Aidha, Shirika limeainisha maeneo maalum 11 ya uwekezaji katika hifadhi za Taifa Nyerere, Burigi – Chato, Katavi, Mto Ugala na Ruaha; na kujenga “cottages” 13 zenye jumla ya vitanda 79 katika hifadhi za Taifa Kilimanjaro, Burigi – Chato, Rubondo, Saanane, Mikumi na Mkomazi ili kuwezesha huduma ya malazi kwa watalii wa ndani na nje ya nchi.
- Mheshimiwa Spika, katika kuongeza mazao mapya ya utalii na wigo wa ukusanyaji mapato, Shirika limeanzisha utalii wa faru katika hifadhi za Taifa Mkomazi na Serengeti. Aidha, Shirika limeendelea kukamilisha taratibu za awali za uanzishwaji wa mazao ya utalii wa uvuvi wa samaki na uendeshaji baiskeli katika Hifadhi ya Taifa Katavi, utalii wa boti katika Hifadhi ya Taifa Ruaha na utalii wa kupiga kasia (canoeing) katika hifadhi za Taifa Tarangire na Ziwa Manyara. Aidha, Shirika limejenga viwanja vya michezo vya mpira wa miguu, mpira wa wavu na mchezo wa tennis katika Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa lengo la kuchochea utalii wa michezo.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua ya kutangaza utalii kidijitali, Shirika limeandaa na kusambaza video fupi 83 na mabango ya kielektroniki 139 yenye jumbe mbalimbali kuhusu vivutio vya utalii vinavyopatikana katika hifadhi za Taifa. Aidha, Shirika limeendelea kuhamasisha utalii kupitia michezo ikiwemo michezo ya Wabunge wa mabunge ya Afrika Mashariki, mashindano ya mbio na matamasha yaliyoanzishwa katika hifadhi na mikoa mbalimbali nchini. Vilevile, Shirika limeendelea kutangaza vivutio vyake katika vyombo vya habari vya ndani na vya kimataifa vikiwemo BBC, CCTV na CGTN. Sambamba na hilo, Shirika limeendelea kupanua wigo wa matumizi ya teknolojia kutangaza na kuhamasisha utalii kwa kutengeneza QR codes za vipeperushi vya lugha za Kifaransa, Kiingereza na Kihispaniola ambavyo vimesambazwa katika Ofisi 44 za Balozi za Tanzania nje ya nchi. Pia, Shirika limewezesha kufanyika kwa ziara tisa (9) za mafunzo kwa makundi mbalimbali ya kimkakati wakiwemo: wakala wa biashara za utalii, wahariri wa vyombo vya habari, wawekezaji na watu mashuhuri kutoka ndani na nje ya nchi. Pia, Shirika limeendelea kushiriki maonesho mbalimbali ya utalii ndani na nje ya nchi.
- Mheshimiwa Spika, ili kurahisisha mazingira ya kufanya biashara na utoaji wa huduma katika maeneo ya hifadhi za Taifa, Shirika limeboresha miundombinu ya TEHAMA kwa kutengeneza mfumo endeshi utakaowezesha kampuni za utalii kuwasilisha maombi ya awali ya nafasi za maeneo ya kupiga kambi za kitalii kwa wageni. Aidha, Shirika limeanzisha dawati mtandao la kutolea msaada na usajili wa matukio mbalimbali. Vilevile, mifumo ya teknolojia na mawasiliano ya huduma ya mtandao imeboreshwa ili kupanua huduma katika malango mapya matatu (3) yaliyofunguliwa katika hifadhi za Taifa Ziwa Manyara, Rubondo na Mkomazi.
- Mheshimiwa Spika, Shirika limeendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi kwa kukamilisha ujenzi wa nyumba za watumishi 28 katika hifadhi za Taifa Ruaha (10), Serengeti (2), Burigi – Chato (6), Mto Ugalla (5), Mahale (2) na Ibanda – Kyerwa (3). Aidha, Shirika linaendelea kukamilisha ujenzi wa nyumba 17 katika hifadhi za Taifa Nyerere (7) na Ruaha (10). Vilevile, Shirika kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limenunua boti moja (1) kwa ajili ya kuimarisha doria katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara; na magari sita (6) kwa ajili ya kuimarisha shughuli za utalii na uhifadhi.
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ulinzi na usalama wa hifadhi, Shirika limeendelea kutumia vifaa mbalimbali vya kiteknolojia vikiwemo vifaa vya mawasiliano ya mtandao mpana (LoRa Transmitters), trimble GPS, vifaa vya kuwezesha kuona usiku pamoja na kamera maalum (hand held thermal image camera) ili kufuatilia usalama wa wanyamapori. Sambamba na hilo, Shirika limeendelea kujiimarisha katika kutumia mbinu za kisasa za kufanya doria zinazoongozwa na taarifa za kiintelijensia. Kwa kutumia mbinu hizo, Shirika limeweza kufanyika kwa jumla ya siku doria 216,663 zilizowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 4,217 waliochukuliwa hatua mbalimbali za kisheria. Aidha, nyara za Serikali pamoja na silaha zikiwemo bunduki aina ya shortgun (7), rifle (2) na magobore (33) zilikamatwa. Jitihada hizi zimewezesha kudhibiti ujangili, hususan wa tembo na faru katika maeneo ya hifadhi za Taifa. 4.5.1.4 Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania – TAWA - Mheshimiwa Spika, Mamlaka ina jukumu la kusimamia uhifadhi na kuendeleza utalii katika mapori ya akiba 27, maeneo ya mifumo ya ikolojia manne (4), mapori tengefu 26 na maeneo matatu (3) ya ardhioevu. Aidha, Mamlaka ni mwangalizi na mshauri wa shughuli za uhifadhi katika maeneo 21 ya Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori, mashamba 34, bustani 30, ranchi sita (6) na Kituo kimoja (1) cha kulelea wanyamapori wenye matatizo mbalimbali.
- Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza majukumu hayo, Mamlaka imetoa jumla ya leseni 36 za ufugaji wa wanyamapori kwa wawekezaji wa bustani, mashamba na ranchi za wanyamapori; na leseni 34 kwa ajili ya kuendesha biashara ya nyamapori. Aidha, Mamlaka imeendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji ambapo jumla ya maeneo saba (7) yametolewa kwa wawekezaji chini ya utaratibu wa uwekezaji mahiri katika mapori ya akiba na tengefu. Maeneo hayo ni mapori ya akiba Ikorongo (1), Grumeti (1), Maswa (3) na Selous (1); na Pori Tengefu la Ziwa Natron (1). Uwekezaji huo umeiwezesha Mamlaka kuongeza mapato yatokanayo na shughuli za uwindaji wa kitalii kutoka Shilingi 4,294,512,390.00 kwa mwaka 2021 hadi Shilingi 22,109,585,590.00 mwezi Aprili, 2022.
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ulinzi na usalama wa rasilimali za wanyamapori kwenye mapori ya akiba na tengefu, ardhioevu na maeneo ya wazi, Mamlaka imefanya jumla ya siku doria 104,678 zilizowezesha kukamatwa kwa nyara mbalimbali za Serikali, majangili 2,389, bunduki 102 na mitego ya nyaya 1,314. Jitihada hizo zimechangia kupunguza idadi ya mifugo inayovamia maeneo ya vitalu vya uwindaji kutoka mifugo 9,248 mwaka wa fedha 2020/2021 hadi mifugo 7,267 mwaka wa fedha 2021/2022. Kupungua kwa mifugo, kumewezesha kuongezeka kwa umiliki wa vitalu kutoka asilimia 63 hadi asilimia 70.4. Aidha, Mamlaka imetoa mafunzo kwa watumishi 1,863 kuhusu Kanuni na Amri za Jumla za Jeshi la Uhifadhi. Vilevile, Mamlaka imetoa mafunzo ya utayari ya Jeshi la Uhifadhi la Wanyamapori na Misitu kwa watumishi 150 kwa lengo la kuimarisha nidhamu na ufanisi wa utendaji kazi.
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeendelea kuboresha miundombinu ya utalii kwa kujenga lango la wageni, vituo saba (7) vya kukusanya mapato, kambi nne (4) za wageni, kituo kimoja (1) cha kutolea taarifa kwa wageni, jengo moja (1) la kupumzikia wageni, ofisi tano (5), karakana mbili (2) na vituo viwili (2) vya askari katika mapori ya akiba ya Maswa, Pande, Rukwa, Wami – Mbiki, Kijereshi, Mkungunero, Lukwika/Lumesule, Swagaswaga na Moyowosi; mapori tengefu ya Kilombero na Ziwa Natron; Kituo cha Urithi wa Dunia cha Kilwa Kisiwani na Songo
Mnara; Eneo la Bustani ya Wanyamapori Tabora; na Ofisi ya Kanda ya Kati na Magharibi. Katika hatua nyingine, Mamlaka imefungua na kujenga barabara zenye urefu wa kilomita 321.5 kwa kiwango cha changarawe na madaraja mawili (2) katika mapori ya akiba 11 ya: Wami – Mbiki (km 25),
Mpanga/Kipengele (km 16), Mkungunero (km 89.5), Swagaswaga (km 20), Liparamba (km 20), Maswa (km 40), Pande (km 12), Igombe (km 37), Kijereshi (km 22) na Lukwika/Lumesule (km 40) na madaraja makubwa (2) katika Pori la Akiba Liparamba na Mpanga/ Kipengele. - Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa masoko ya uwindaji wa kitalii, Mamlaka imeshiriki maonesho mbalimbali ya biashara ya kimataifa ikiwemo Safari Club International Convention, Marekani. Kupitia maonesho hayo, Mamlaka iliweza kutangaza fursa za uwekezaji na kuhamasisha wafanyabiashara kuwekeza katika shughuli za utalii na uwindaji. Aidha, Mamlaka imeandaa mfumo wa kidijitali unaotoa taarifa kwa wageni kuhusu vivutio vya utalii vilivyopo katika maeneo yanayosimamiwa na TAWA. Aidha, Mamlaka imeanzisha ranchi sita (6) katika mikoa ya Manyara (2), Kilimanjaro (1), Pwani (2) na Simiyu (1); mashamba ya wanyamapori 27; na bustani za wanyamapori 24 ili kurahisisha upatikanaji wa nyamapori kwa wananchi.
4.5.1.5 Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro – NCAA
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka ina jukumu la kusimamia shughuli za uhifadhi wa maliasili na malikale, uendelezaji wa utalii na ustawi wa jamii zinazoishi ndani ya eneo la hifadhi. Katika utekelezaji wa jukumu hilo, Mamlaka imeendelea kuimarisha ulinzi wa maliasili na malikale zilizopo ndani ya Hifadhi kwa kufanya siku doria 28,980 zilizofanikisha kukamatwa kwa watuhumiwa 44 wa makosa ya ujangili wa wanyamapori. Aidha, Mamlaka imeboresha ulinzi wa faru kwa kuwawekea alama maalum za utambuzi na mifumo ya kielektroniki kwa ajili ya ufuatiliaji. Vilevile, Mamlaka imeboresha mazingira ya utendaji kazi kwa kukarabati vituo sita (6) vya askari katika maeneo ya Lemala, Makhoromba, Ndutu, Kakesio, Endamagha na Masamburai. Pia, ujenzi wa vituo vipya vya askari katika maeneo ya Lositete na Lemala unaendelea. Sambamba na hatua hizo, Mamlaka imeendelea kutoa mafunzo ya amri za jumla na kanuni za kudumu za Jeshi la Uhifadhi kwa watumishi 718 na semina kuhusu maadili kwa watumishi 136. Mafunzo haya yamesaidia kuimarisha nidhamu na utendaji kazi wa watumishi katika ulinzi na uhifadhi wa maliasili na malikale zilizopo hifadhini.
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeimarisha miundombinu ya utalii ndani ya hifadhi kwa kukamilisha ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 4.2 inayoshuka kreta ya Ngorongoro kwa kiwango cha tabaka gumu la mawe; na ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 15 kutoka Ndutu hadi Kakesio kwa kiwango cha changarawe. Sambamba na hilo, Mamlaka imekarabati barabara zenye urefu wa kilomita 472 ndani ya Hifadhi; na miundombinu ya viwanja vya ndege vya Ndutu na Ngorongoro. Aidha, katika kuhamasisha uwekezaji wa shughuli za utalii, Mamlaka imefungua barabara zenye urefu wa jumla ya kilomita 19 kuelekea maeneo ya uwekezaji yaliyo jirani na Kreta ya Empakai. Vilevile, Mamlaka imeendelea kukarabati miundombinu ya umeme, vyoo na mifumo ya maji ndani ya Hifadhi ili kuboresha huduma za utalii na kuvutia uwekezaji. Sambamba na hilo, Mamlaka imenunua mitambo mizito mitano (5) na malori matano (5) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa barabara ndani ya hifadhi. Pia, upembuzi yakinifu wa ujenzi wa barabara kuu yenye kilomita 83 kutoka lango kuu la Loduare hadi Golini kwa kiwango cha tabaka gumu umekamilika.
- Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kuongeza mapato na muda wa mtalii kukaa hifadhini, Mamlaka imeendelea kuibua mazao mapya ya utalii ikiwemo utalii wa usiku (night game drive), utalii wa kutembea kwenye miti (canopy walkways), utalii wa kutembea na farasi, utalii wa baiskeli na utalii wa puto ndani ya hifadhi. Katika hatua nyingine, Mamlaka imeendelea kushiriki maonesho ya utalii ndani na nje ya nchi. Vilevile, Mamlaka imeendelea kutangaza mubashara vivutio vya utalii katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Mathalan, kupitia onesho la
Dubai Expo 2020, washiriki kutoka mataifa mbalimbali waliweza kuona mubashara vivutio vilivyopo hifadhini. - Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha uwepo wa maji safi na salama, Mamlaka imekamilisha kwa asilimia 65 ujenzi wa mradi wa maji ujulikanao kama Mama Hhawu Water Treatment Plant wenye uwezo wa kutibu maji lita milioni 1,500,000 kwa siku. Mradi huo unahusisha ujenzi wa mtambo wa kuchuja maji, ukarabati wa banio na matanki mawili (2) yenye uwezo wa lita 105,000 kwa ajili ya kuhifadhi maji na ujenzi wa kituo cha uendeshaji wa mtambo. Mradi huu pamoja na kuwanufaisha wageni wanaoingia Hifadhini, pia utawanufaisha wananchi 5,000 wanaopakana na Hifadhi ikiwa ni pamoja na hospitali teule ya Wilaya ya Karatu.
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka imeendelea na jukumu la kuendeleza jamii ya wenyeji waishio ndani ya Hifadhi. Katika kutekeleza jukumu hili, Mamlaka imetoa ufadhili kwa wanafunzi 2,163 wa jamii ya wenyeji katika ngazi ya shule za msingi, sekondari, vyuo vya kati na vyuo vikuu. Aidha, Mamlaka imegawa mizinga 1,878 kwa vikundi 94 vya wafugaji nyuki katika wilaya za Ngorongoro, Karatu, Monduli na Meatu. Vilevile, Mamlaka imewezesha utoaji wa huduma za afya kwa wenyeji katika Zahanati ya Ngorongoro; kuwapatia wenyeji 1,300 kadi za bima ya afya ya jamii iliyoboreshwa (iCHF); na kutoa chanjo kwa jumla ya mifugo 2040. Sambamba na hatua hizo, Mamlaka imefanya mikutano 183 yenye jumla ya washiriki 34,803 kwa lengo la kutoa elimu ya uhifadhi na namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
- Mheshimiwa Spika, ili kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto za matumizi mseto ya ardhi ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro, Mamlaka imefanya uhamasishaji kupitia vikao na mikutano ya majadiliano baina ya Serikali na wadau mbalimbali wakiwemo wenyeji waishio ndani ya eneo la Hifadhi. Kupitia jitihada hizo, jumla ya kaya 278 zenye wakazi 1,439 walikua wamejiandikisha kuhama kwa hiari kutoka hifadhini. Pia, Wizara imebainisha maeneo mbadala ya Handeni, Tanga na Kitwai, Manyara kwa ajili ya makazi kwa wananchi watakaohama kutoka Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Kwa upande wa Handeni, Mamlaka imebainisha eneo lenye ukubwa wa hekta 112,239 kwa ajili ya matumizi ya makazi na huduma za jamii. Hadi kufikia mwezi Aprili 2022, Wizara ilifanikiwa kupima eneo lenye ukubwa wa hekta 73,528.73 lililogawanywa kwa ajili ya matumizi mbalimbali yakiwemo: makazi (hekta 10,080.4), kilimo (hekta 13,628.48), malisho (hekta 22,176.06), ujenzi wa taasisi za elimu ya juu na vyuo (hekta 1,329.37), ushoroba wa wanyamapori (hekta 26,314.42) na hifadhi ya misitu (hekta 6,082.72). Zoezi la upimaji na upangaji wa matumizi ya ardhi katika eneo lililobaki pamoja na eneo la Kitwai lenye ukubwa wa hekta 409,416 linaendelea.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara kwa kushirikiana na Uongozi wa mikoa ya Arusha na Tanga imekamilisha ujenzi wa nyumba 103 katika eneo la Handeni ambazo ni awamu ya kwanza ya ujenzi wa nyumba 500 kwa ajili ya wananchi wenyeji waishio ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro ambao wameridhia kuhama kwa hiari. Sambamba na ujenzi wa nyumba hizi, maeneo haya yatakuwa na miundombinu muhimu ya kijamii ikiwemo barabara zenye urefu wa kilomita 2,880, umeme, maji, zahanati 25, vituo vya afya vitatu (3), shule za msingi 25, shule za sekondari nne (4), ofisi nne (4) za vijiji, ofisi 11 za kata, ofisi moja (1) ya tarafa, ofisi moja (1) ya mahakama na kituo kimoja (1) cha polisi na mahakama. Wizara inaendelea na juhudi za kukamilisha miundombinu muhimu pamoja na kuhamasisha na kuelimisha jamii ili waweze kuhama kwa hiari kwa manufaa ya uhifadhi na maendeleo ya jamii.
- Mheshimiwa Spika, katika kuboresha nyanda za malisho na kudhibiti mimea vamizi, jumla ya ekari 7,000 zimechomwa kwa kutumia njia ya moto mpango. Aidha zoezi la kung’oa/kufyeka magugu vamizi limefanyika katika eneo lenye jumla ya ekari 2,500. Jitihada hizi zimesaidia kuboresha nyanda za malisho na makazi ya wanyamapori sambamba na kupunguza mgongano baina ya wanyamapori na mifugo. Katika hatua nyingine, Mamlaka imeotesha jumla ya miche ya miti 460,000 ambapo miche 54,460 imegawiwa kwa jamii zinazozunguka eneo la Hifadhi.
- Mheshimiwa Spika, Katika kuimarisha uwekezaji wa kitalii ndani ya Hifadhi, Mamlaka imetenga jumla ya maeneo mapya sita (6) kwa ajili ya uwekezaji wa kimkakati yenye uwezo wa jumla ya vitanda 480. Maeneo haya yatatolewa kwa wawekezaji wa kimkakati kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya huduma za malazi ya hadhi ya juu ili kuvutia wageni wenye hadhi kutembelea Hifadhi. Aidha Mamlaka imetenga maeneo mawili (2) katika eneo lililokuwa likitumika kama makao makuu kwa ajili ya kujenga hosteli ili kutoa huduma za malazi ya gharama nafuu mahsusi kwa watalii wa ndani.
4.5.1.6 Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori – TAWIRI
- Mheshimiwa Spika, Taasisi ina jukumu la kuratibu na kufanya tafiti za wanyamapori nchini. Katika kutekeleza jukumu hilo, Taasisi imeidadi wanyamapori katika mifumo ikolojia ya Ruaha – Rungwa na Katavi – Rukwa; maeneo ya mtawanyiko; na shoroba zilizomo katika mifumo ikolojia hiyo. Matokeo ya sensa katika mfumo ikolojia wa Ruaha – Rungwa yanaonesha kuwa kuna tembo 15,608, nyati 20,911, swala pala 8,643, pundamilia 10,552, palahala 6,636 na kongoni 4,017. Aidha matokeo hayo yakilinganishwa na yale ya mwaka 2018 yanaonesha kuimarika kwa idadi ya tembo sambamba na ongezeko la nyati kwa asilimia 80, pundamilia asilimia 36, na palahala asilimia 65.
- Mheshimiwa Spika, matokeo ya sensa katika Mfumo Ikolojia wa Katavi – Rukwa yameonyesha kuwa kuna tembo 3,089, nyati 24,405, pundamilia 3,339, kongoni 3,356 na twiga 1,295. Matokeo haya yakilinganishwa na sensa iliyofanyika mwaka 2018 yanaonyesha ongezeko la asilimia mbili
(2) kwa tembo; na idadi ya wanyamapori wengine wakiwemo nyati, pundamilia, kongoni na twiga haikubadilika kwa kiwango kikubwa. Matokeo hayo pia yanaonesha kupungua kwa shughuli za kibinadamu katika mifumo ikolojia hiyo. Aidha, matokeo ya sensa katika Mfumo Ikolojia Ziwa Natron – West Kilimanjaro yameonesha kuwa kuna ongezeko la idadi ya tembo kutoka 169 mwaka 2018 hadi 219 mwaka 2021; na ongezeko la wanyamapori wengine wakiwemo pundamilia na nyumbu. Vilevile, matokeo ya sensa katika eneo la West Kilimanjaro ni pundamilia 3,651, swala granti 1,284, nyati 18, swala thomi 553 na twiga 1,030. Hata hivyo, idadi ya nyati imepungua kwa asilimia 19 na swala thomi kwa asilimia 16. Matokeo hayo yanasababishwa na ongezeko la mifugo hususan ng’ombe ambao wameongezeka kwa asilimia 337 kutoka 80,344 mwaka 2018 hadi 350,881 mwaka 2021. Kwa ujumla, takwimu zinaonesha maoneo yaliyohifadhiwa yamezidi kuimarika. - Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kutatua migongano baina ya binadamu na wanyamapori, Taasisi ilihamisha wanyamapori 278 (nyumbu 180 na pundamilia 98) kutoka maeneo ya Mto wa Mbu kwenda Hifadhi ya Taifa Tarangire; na simba 13 waliokuwa wanahatarisha maisha ya binadamu katika wilaya za Bunda na Serengeti kwenda Hifadhi ya Taifa Burigi – Chato. Aidha, katika kutatua migogoro baina ya binadamu na wanyamapori, Taasisi imefunga mikanda ya mawasiliano kwa ajili ya kufuatilia mienendo ya wanyamapori. Jumla ya makundi ya tembo 107 katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro; Pori la Akiba Maswa na mapori tengefu ya Longido na Ziwa Natron; makundi ya Mbwa mwitu 7 katika Mfumo Ikolojia Serengeti; na makundi ya simba 21 katika mifumo ikolojia Serengeti na Ruaha – Rungwa wamefungwa mikanda ya mawasiliano kwa ajili ya ufuatiliaji wa nyendo zao. Kwa upande mwingine, Taasisi ilitoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na migongano baina ya binadamu na wanyamapori (simba na tembo) kwa waelimishaji 610 katika wilaya 21 watakaotoa mafunzo kwa jamii ya namna ya kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu. Katika hatua nyingine, Taasisi iliandaa Kongamano la 13 la
Kisayansi la Kimataifa lililofanyika Jijini Arusha, mwezi Desemba 2021 kwa lengo la kutoa matokeo ya tafiti mbalimbali kuhusu uhifadhi. Washiriki katika Kongamano hilo walikuwa 436 toka nchi 18 duniani na mada 177 ziliwasilishwa.
4.5.1.7 Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – CAWM Mweka
- Mheshimiwa Spika, Chuo kina jukumu la kutoa mafunzo katika ngazi za Cheti cha Msingi, Astashahada, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili. Aidha, Chuo kinafanya tafiti na kutoa ushauri wa kitaalam kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na uendeshaji utalii. Katika kutekeleza hili, mwaka 2021/2022, Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 834 katika ngazi za Astashahada, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili. Aidha, jumla ya wanafunzi 433 walihitimu na kutunukiwa vyeti katika ngazi ya Astashahada, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili. Aidha, Chuo kimetoa mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 22 juu ya mbinu ya kukamata na kuhamisha nyoka katika eneo la Bulyankulu, Mkoa wa Shinyanga na mafunzo kwa waongoza watalii wapatao 1,060 kutoka katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.
- Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na kupitia mitaala 10 iliyopo; kuandaa mitaala nane (8) mipya; na kuboresha Kitengo cha TEHAMA kwa kununua vitendea kazi mbalimbali vya kuimarisha utendaji kazi. Aidha, ili kuboresha utoaji wa mafunzo, Chuo kimejenga kumbi mbili (2) za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 250 kila moja katika kampasi kuu ya Mweka (1) na eneo la Mafunzo kwa Vitendo
Kwakuchinja (1). Vilevile, Chuo kimekamilisha ujenzi wa hosteli yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 294 katika kampasi kuu ya Mweka na kununua magari mawili (2) kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo.
4.5.1.8 Taasisi ya Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori Pasiansi
- Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Taaluma ya Usimamizi wa Wanyamapori Pasiansi ina jukumu la kutoa mafunzo ya uhifadhi wa wanyamapori na himasheria katika ngazi ya Astashahada. Katika kutekeleza jukumu hilo, Taasisi imedahili wanafunzi 410 katika fani za uhifadhi wanyamapori na himasheria, uongozaji watalii na usalama kwa ngazi ya Astashahada na Astashahada ya awali. Aidha, Taasisi imetoa mafunzo ya utayari wa Jeshi la Uhifadhi kwa watumishi wapya 43 wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania. Katika hatua nyingine, Taasisi imetoa mafunzo ya muda mfupi kuhusu usimamizi wa rasilimali za wanyamapori kwa wanavijiji 140 kutoka wilaya za Tanganyika, Mpanda, Nsimbo, Serengeti, Uvinza, Kigoma, Simanjiro na Karatu. Vilevile, Taasisi inaendelea kuboresha mitaala yake ili kuendana na mahitaji ya kila siku katika uhifadhi wa wanyamapori na utalii. Pia, Taasisi ipo katika hatua za mwisho za ujenzi wa maktaba ya kisasa yenye uwezo wa kubeba watu 400 kwa wakati mmoja pamoja na uchimbaji wa kisima kirefu cha maji safi katika eneo la mafunzo Forti Ikoma.
4.5.1.9 Kituo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii, Likuyu-
Sekamaganga - Mheshimiwa Spika, Kituo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii, Likuyu – Sekamaganga kina jukumu la kuzijengea uwezo jamii zinazoishi jirani na maeneo yaliyohifadhiwa ili zishiriki katika uhifadhi na matumizi endelevu ya maliasili. Katika kutekeleza jukumu hilo, Kituo kimetoa mafunzo kwa wanafunzi 204 ambapo Askari Wanyamapori wa Vijiji 20 wamepata mafunzo ya usimamizi wa rasilimasili za maliasili; askari 34 wamepata mafunzo ya kuongoza watalii; na askari 150 wa TAWA wamepata mafunzo ya utayari wa Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu. Vilevile, Kituo kimetoa ushauri wa kitaalam kwa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori tano (5) za Mbarang’andu, Kimbanda na Kisungule (Namtumbo); na Chingoli na Nalika (Tunduru). Katika hatua nyingine, Chuo kimefanya mapitio ya mitaala ya kozi za Astashahada ya Awali ya Utalii na Waongoza watalii, Askari Wanyamapori wa Vijiji, Viongozi wa Wajumbe wa Kamati za Maliasili za Vijiji pamoja na kuandaa mitaala mipya ya kozi za Astashahada na Stashahada ya utalii na waongoza watalii.
4.5.1.10 Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania – TWPF - Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania una jukumu la kuwezesha uhifadhi wa wanyamapori ndani na nje ya maeneo yaliyohifadhiwa. Katika kutekeleza jukumu hilo, Mfuko umeendelea kuwezesha operesheni maalum za kuzuia ujangili; utekelezaji wa kazi za Kikosi Kazi cha Taifa cha kupambana na ujangili (NTAP); na Jeshi la Uhifadhi. Aidha, Mfuko umewezesha kufanyika kwa uhakiki wa matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu katika wilaya 36 zilizoathirika pamoja na kufanya malipo ya Shilingi 790,721,500.00 kwa wahanga 3,598 walioathiriwa na wanyamapori hao. Kwa upande mwingine, Mfuko umewezesha zoezi la kupandisha hadhi mapori tengefu matatu (3) kuwa mapori ya akiba. Vilevile, Mfuko umewezesha kufanyika kwa mapitio ya Kanuni mbalimbali za Sekta ya Wanyamapori; kufanya tathmini ya utendaji wa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori; kuandaa mpango mkakati wa kuongoa shoroba; na kuwezesha upatikanaji wa silaha za Jeshi la Uhifadhi. 4.5.2 Sekta ya Misitu na Nyuki
- Mheshimiwa Spika, Sekta ya Misitu na Nyuki ina jukumu la kusimamia uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki. Utekelezaji wa jukumu hilo unaongozwa na Sera ya Taifa ya Misitu (1998) na Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki (1998). Aidha, utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekta hizi unasimamiwa na Sheria ya Misitu Sura 323, Sheria ya Ufugaji Nyuki Sura 224 na Sheria ya kuanzisha Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania Sura 277. Vilevile, jukumu la uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za misitu na nyuki hutekelezwa kupitia Idara ya Misitu na Nyuki, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI), Chuo cha Misitu Olmotonyi (FTI), Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) Moshi, Chuo cha Ufugaji Nyuki (BTI) Tabora na Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF).
4.5.2.1 Masuala Mahsusi ya Sekta ya Misitu na Nyuki
(i) Kuongeza Thamani ya Mazao ya Misitu na Nyuki
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa mazao ya misitu na nyuki yanayozalishwa hapa nchini yanaongezwa thamani, Wizara imeendelea kutoa elimu, kuhamasisha na kuwezesha wadau mbalimbali kujenga viwanda vya kuongeza thamani ya mazao ya misitu na nyuki. Juhudi hizi zinalenga kuhakikisha viwanda vilivyopo na vitakavyojengwa vinazalisha bidhaa mbalimbali zitokanazo na mbao pamoja na mazao ya nyuki ili kuongeza thamani na mapato yatokanayo na bidhaa hizo. Pamoja na juhudi hizo, Wizara imeandaa Mkakati wa Kitaifa wa Mazao ya Mbao Yaliyohandisiwa (National Engineered Wood Sector Development Framework 2021 – 2031) pamoja na Mpango kazi wa utekelezaji wake utakaowezesha uanzishaji na uendelezaji wa viwanda vya mazao ya misitu. Pia, Wizara imekamilisha ujenzi wa viwanda vitano (5) na ukarabati wa kiwanda kimoja (1) cha kuchakata mazao ya nyuki katika wilaya za Kibondo, Nzega, Sikonge, Bukombe, Mlele na Tabora Mjini.
(ii) Kuboresha Mazingira ya Kibiashara katika Sekta za Misitu na Nyuki
- Mheshimiwa Spika, ili kuboresha mazingira ya kibiashara na kuendelea kuvutia wawekezaji katika sekta za Misitu na Nyuki, Wizara imeendelea kufanya maboresho ya tozo mbalimbali na kuandaa miongozo ya kuratibu biashara ya mazao na huduma za misitu na nyuki. Wizara imefanya maboresho ya Kanuni ya Tozo za Misitu Na. 627 ya mwaka 2020 na kuandaa Kanuni mpya iliyotolewa katika Tangazo la Serikali Na. 59 la mwaka 2022. Katika hatua nyingine, Wizara imeandaa Mwongozo na kanuni za kuratibu biashara ya hewa ukaa (carbon trading) na mwongozo wa kutumia makundi ya nyuki kwa ajili ya kutoa huduma ya uchavushaji wa mimea. Maboresho hayo yamechochea uwekezaji na ukuaji wa biashara ya mazao na huduma katika sekta za misitu na nyuki.
4.5.2.2 Idara ya Misitu na Nyuki
- Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha maandalizi ya Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Misitu 2021 – 2031; Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ufugaji Nyuki 2021 – 2031; Mkakati wa Kitaifa wa Mazao ya Mbao
Yaliyohandisiwa wa mwaka 2021 – 2031; Taarifa ya Misitu ya Jamii (PFM Facts and Figures) ya mwaka 2022; na Mpango kazi wa Usimamizi wa Misitu ya Jamii wa mwaka 2022. Aidha, Wizara imeandaa Mwongozo wa Uanzishwaji na Usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na Manzuki wa mwaka 2021; Mwongozo wa Usimamizi na Matumizi Endelevu ya Misitu ya Mikoko wa mwaka 2021; Taratibu za Kitaifa za Mafunzo na Elimu ya Ugani ya Ufugaji Nyuki za mwaka 2021; Mwongozo wa kufanya utafiti wa misitu na nyuki nchini wa mwaka 2022; Mwongozo wa kutumia makundi ya nyuki kwa ajili ya kutoa huduma ya uchavushaji wa mimea wa mwaka 2022; na Agizo la Kiufundi Na. 1 (Technical Order No. 1) la mwaka 2021 kuhusu uzalishaji, ubora na tija ya mazao ya misitu. Katika hatua nyingine, Wizara imefanya tathmini ya Sheria na Kanuni ya Misitu ili kuboresha ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi. Miongozo hii inalenga kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za misitu na nyuki pamoja na kuongeza mapato ya
Serikali. - Mheshimiwa Spika, Wizara imekamilisha kazi ya tathmini ya mchango wa sekta ya misitu na nyuki katika pato la Taifa. Tathmini hiyo imebaini kuwa sekta ya misitu na nyuki kwa sasa inachangia asilimia 3.3 ya pato ghafi la Taifa. Aidha, tathmini imebainisha maeneo yenye mchango mkubwa katika kuongeza mapato na maeneo mengine mapya ambayo yanahitaji msukumo ili kuweza kuongeza uchangiaji wa sekta ya misitu na nyuki katika uchumi wa Taifa.
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha usimamizi na uendelezaji wa rasilimali misitu na nyuki, Wizara imekamilisha Andiko la Kuanzisha Mamlaka ya Usimamizi wa Misitu na Nyuki Tanzania na hatua inayofuata ni kupitisha katika mamlaka mbalimbali za maamuzi. Katika hatua nyingine, Wizara imeratibu mikutano miwili (2) ya Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Misitu – NAFAC; mikutano mitatu (3) ya Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa Ufugaji Nyuki – NABAC; na vikao vitatu (3) vya wadau wa misitu kupitia Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za misitu na nyuki. Sambamba na hilo, Wizara imeanza utekelezaji wa mradi wa kuboresha mnyororo wa thamani wa mazao ya ufugaji nyuki (BEVAC). Mradi huu pamoja na manufaa mengine utaimarisha usimamizi wa manzuki na hifadhi za nyuki, kuunganisha wazalishaji wa mazao ya nyuki na masoko, kuimarisha uwezo wa taasisi zilizo kwenye mnyororo wa thamani wa ufugaji nyuki ili ziweze kutoa huduma stahiki katika ukuzaji wa sekta ya ufugaji nyuki nchini, pamoja na kuwajengea uwezo makundi mbalimbali wakiwemo wanawake kushiriki shughuli mbalimbali za ufugaji nyuki.
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa jamii inaendelea kuelimishwa na kuhamasishwa kushiriki katika uhifadhi wa rasilimali za misitu na nyuki, Wizara imeratibu maadhimisho ya Siku ya Nyuki Duniani yaliyofanyika Mkoa wa Ruvuma tarehe 29 Julai, 2021; na maadhimisho ya siku ya misitu Duniani na upandaji miti Kitaifa yaliyofanyika Mkoa wa Mwanza tarehe 23 Machi, 2022. Aidha, Wizara imesajili na kuingiza taarifa za wafugaji nyuki 1,026 kwenye kanzidata ya Misitu na Nyuki iliyounganishwa na Mfumo wa MNRT – Portal. Vilevile, Wizara kwa kushirikiana na Shirika la Chakula Duniani imeratibu Mkutano wa Pili wa Kimataifa wa Kikundi kazi cha Misitu ya Nyanda Kame uliofanyika Jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 17 hadi 18 Novemba, 2021.
4.5.2.3 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania – TFS - Mheshimiwa Spika, Wakala umepewa jukumu la kusimamia, kuhifadhi na kuendeleza rasilimali za misitu na nyuki zilizo chini ya Serikali Kuu. Katika kutekeleza jukumu hilo, Wakala unasimamia misitu 463 iliyohifadhiwa kisheria. Misitu hiyo inajumuisha: mashamba ya miti 24, misitu ya mazingira asilia 20, misitu ya hifadhi ya asili 419 na hifadhi za nyuki 12. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wakala umehakiki mipaka ya misitu 120 yenye urefu wa kilomita 160; kusafisha mipaka yenye urefu wa kilomita 1,112; kuweka vigingi 589 na mabango 204; na kuchimba mashimo 48 yanayoonesha uelekeo wa mpaka. Aidha, Wakala umejenga barabara zenye urefu wa kilomita 49, kalavati nane (8) na daraja moja (1) katika mashamba ya miti 14 ya Buhindi, Kiwira, Longuza, Meru, North Kilimanjaro, Rondo, Rubare, Sao Hill, Shume, Mpepo, Ukaguru, West Kilimanjaro, Wino na North Ruvu. Vilevile, Wakala umekarabati kilomita 906 za barabara, kalvati 18 na madaraja nane (8) katika misitu ya mazingira asilia ya Amani, Pugu – Kazimzumbwi, Magamba na Mlima Rungwe; na mashamba ya miti 24. Katika hatua nyingine, mipango 48 ya usimamizi na uendelezaji wa misitu yenye ukubwa wa hekta 1,157,134 imeandaliwa. 100. Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha ulinzi wa rasilimali za misitu na nyuki, Wakala umeendesha jumla ya siku doria 84,050 ambazo zimewezesha kukamatwa kwa watuhumiwa 726. Aidha, doria zimewezesha kukamatwa kwa mazao mbalimbali ya misitu ikiwemo magunia 19,934 ya mkaa, magogo yenye ujazo wa mita 1,218.19, kuni zenye mita za ujazo 180, nguzo 5,239, mbao 3,761 pamoja na fremu za milango na madirisha 802. Kwa upande mwingine, mafunzo kuhusu usimamizi shirikishi wa misitu; athari na namna ya kukabiliana na moto kichaa; na upandaji na utunzaji wa miti yametolewa kupitia mikutano 297 katika vijiji 236. Pia, Wakala umetoa elimu ya biashara ya mazao ya misitu na nyuki kwa wadau 532.
- Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuendeleza mashamba 24 ya Serikali yenye ukubwa wa hekta 510,000 Wakala umetekeleza kazi mbalimbali ikiwemo kuzalisha tani 11.35 za mbegu bora za miti; kupanda miche 9,795,687 katika eneo lenye ukubwa wa hekta 7,833; kupalilia hekta 19,601; kupogoa miti hekta 10,137; na kupunguza miti katika eneo la hekta 1,559. Aidha, misitu yenye ukubwa wa hekta 121,100 imehifadhiwa kisheria. Kadhalika, ili kuendeleza ulinzi wa mashamba ya miti; kilomita 596 za njia za kuzuia moto zilisafishwa, kukarabati minara 16 ya kubaini matukio ya moto pamoja na kutoa mafunzo kwa watumishi 236 wanaofanya kazi ya kukabiliana na moto kwenye mashamba. Katika hatua nyingine, Wakala umeandaa Mpango Mkakati wa miaka 30 wa kusimamia na kuendeleza mashamba ya miti ambao utawezesha kuanzishwa na kuongeza wigo wa mashamba ya miti ya kibiashara kama vile mianzi, utomvu, mpira na miti ya dawa kama vile Prunus africana inayotumika kutengeneza madawa ya kutibu saratani.
- Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kuimarisha shughuli za utalii ikolojia na malikale, Wakala umekarabati kilomita 66.7 za barabara za ndani ya hifadhi za misitu asilia, kilomita 163.2 za njia za kutembea watalii na kambi tano (5) za kupumzikia. Aidha, Wakala umeandaa na kurusha vipindi 173 vya
Tanzania ya Kijani katika televisheni na redio vyenye maudhui ya uendelezaji wa utalii; uhifadhi wa misitu na ufugaji nyuki; matumizi ya nishati mbadala; na kukabiliana na matukio ya moto. Vilevile, Wakala umeandaa na kusambaza vipeperushi 20,622 na makala moja (1) ya vivutio vya utalii ilirushwa kwenye televisheni na programu sita (6) zilizorushwa kupitia redio mbalimbali nchini. Kwa upande mwingine, Wakala umeendelea kuelimisha Umma kuhusu uhifadhi na huduma mbalimbali zinazotolewa na Wakala kupitia matamasha na maonesho mbalimbali ndani na nje ya nchi. Pia, katika kuendeleza utalii wa malikale, Wakala umefanya ukarabati wa ofisi, ujenzi wa banda la utalii, ujenzi wa camping – site yenye uwezo wa kubeba wageni 20 na kukarabati kituo cha kutolea taarifa katika Kituo cha Malikale cha Kolo (Kondoa)”. Vilevile, Wakala umejenga banda la kupumzikia wageni katika kituo cha malikale cha Kaole. Ili kuongeza ufanisi katika uhifadhi na ukusanyaji wa maduhuli, Wakala umeboresha mfumo wa Forest Resources Management Information System (FREMIS) na kuunda mfumo fungamanishi mpya ujulikanao kama TFS Intergrated Information Management System (TFS – IIMS). Vilevile, mafunzo maalum yametolewa kwa wataalam watano (5) wanaotoa huduma za kiufundi kuhusu mfumo huo. - Mheshimiwa Spika, katika jitihada za kusimamia na kuendeleza ufugaji nyuki, Wakala umezalisha tani 12.4 za asali na tani 0.3 za nta kutoka kwenye manzuki 182. Aidha, Wakala umeanzisha mashamba mawili (2) maalum ya kufuga nyuki (bee
farm) ya Kondoa – Manyoni na Mwambao – Handeni. Wakala umetengeneza mizinga 2,500 na kuongeza mashine za kutengeneza mizinga katika kiwanda cha Wakala kilichopo Kondoa. Vilevile, ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa jamii, Wakala umetoa mafunzo ya mbinu bora za ufugaji na uzalishaji wa mazao ya nyuki kwa vikundi 49 vyenye wafugaji 896 na kugawa mizinga 416 kwa jamii katika wilaya za Mvomero, Lindi, Nyasa na Songea. Kwa upande mwingine, Wakala umekusanya sampuli 70 za asali kutoka katika wilaya 29 na kuzipeleka kwenye maabara ya kimataifa iliyopo nchini Ujerumani kwa lengo la kupima ubora wa asali inayozalishwa hapa nchini. Matokeo yanaonesha kuwa asilimia 99 ya sampuli hizo zimekidhi viwango vya ubora wa kimataifa na hivyo kutoa fursa kwa asali ya Tanzania kuendelea kuuzwa katika masoko mbalimbali duniani. - Mheshimiwa Spika, Wakala umeendelea kuboresha ustawi wa watumishi kwa kuweka mazingira wezeshi ya kufanyia kazi. Katika kutekeleza hilo, Wakala umejenga ofisi 12 na kukarabati majengo 46 katika Ofisi za Kanda ya Ziwa, Kanda ya Kasikazini, Kanda ya Magharibi, Kanda ya Kusini, Kanda Mashariki na mashamba ya miti ya West Kilimanjaro, Ukaguru, Sao Hill, Rubare, Rondo, Kawetire na Buhindi. Aidha, Wakala umenunua magari 26 na pikipiki 33 ili kuwezesha usimamizi na ufuatiliaji wa shughuli za uhifadhi wa misitu na nyuki. Vilevile, Wakala umetoa mafunzo ya utayari ya kijeshi kwa watumishi 498 na mafunzo ya Kanuni na Amri za Jeshi la Uhifadhi kwa watumishi 161. Mafunzo haya yamesaidia kuimarisha nidhamu na utendaji kazi kwa watumishi katika kulinda na kusimamia rasilimali za misitu, nyuki na malikale.
4.5.2.4 Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania – TAFORI
- Mheshimiwa Spika, Taasisi ina jukumu la kufanya na kuratibu utafiti wa misitu na ufugaji nyuki na kutoa ushauri wa kitaalamu katika nyanja za misitu na ufugaji nyuki. Katika kutekeleza majukumu yake, Taasisi kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu imefanya utafiti kuhusu moto wa misituni kwa kutumia Satellite na kubaini kuwa eneo la kilomita za mraba 95,793 liliungua na moto kwa kipindi cha mwaka 2021/2022. Aidha, maeneo ambayo yameathirika zaidi na moto ni mikoa ya Lindi (kilomita za mraba 13,066), Morogoro (kilomita za mraba 11,539) na Katavi (kilomita za mraba 10,878). Pia, utafiti umebaini uwepo wa maeneo yaliyoathirika na matukio ya moto katika maeneo ya hifadhi kama vile Hifadhi za Taifa (kilomita za mraba 32,652), mapori ya Akiba (kilomita za mraba 26,733), Hifadhi za Misitu (kilomita za mraba 11,725) na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro (kilomita za mraba 267). Vyanzo vikuu vya moto huo ni pamoja na ufunguaji mashamba kwa ajili ya kilimo, uvunaji asali usiotumia zana za kisasa, majangili na moto mpango. Ili kupambana na moto kichaa Wizara itaendelea kushirikiana na wadau kutoa elimu kwa jamii kuhusu vyanzo, athari na mbinu za kukabiliana na moto katika maeneo ya hifadhi. Sambamba na hilo, TAFORI kwa kushirikiana na
Mfuko wa Uhifadhi wa Milima ya Tao la Mashariki (EAMCEF) imetengeneza mfumo wa utoaji wa taarifa za uhalifu ikiwemo moto ili kuwezesha jamii kukabiliana na matukio ya moto kwa wakati. - Mheshimiwa Spika, Taasisi imeendelea kushirikiana na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) katika kufanya utafiti juu ya uvunaji wa utomvu kwenye miti ya misindano ili kubaini umri sahihi wa kuvuna utomvu, madhara yake kwenye ukuaji wa miti na ubora wa mbao. Matokeo ya awali ya utafiti yanaonesha kuwa ugemaji wa utomvu unaathiri miti yenye umri wa kati ya miaka mitano (5) hadi 20. Wastani wa ukuaji wa kipenyo cha mti unaogemwa hupungua kwa asilimia 16 ukilinganisha na mti usiogemwa. Hivyo, ili kupunguza athari ya ukuaji wa miti inashauriwa kuwa uvunaji wa utomvu ufanyike kwa miti yenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.
- Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kubaini mchango wa rasilimali za misitu kwa jamii, Taasisi imefanya utafiti wa uzalishaji na biashara ya mazao yatokanayo na mti wa Mlonge. Matokeo ya utafiti yanaonesha kuwa mti wa mlonge hupandwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwemo mikoa ya Iringa, Pwani, Morogoro, Tanga, Dar es Salaam na Dodoma. Mti huu hutumika kuzalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo dawa, lishe na mafuta. Aidha, utafiti unaonesha kuwa kwa mwaka mkulima hupata wastani wa Shilingi 2,054,944.41 kupitia uuzaji wa mbegu za mlonge na Shilingi 572,365.00 kupitia uuzaji wa majani ya mlonge. Kutokana na fursa hiyo, inashauriwa kuwa jamii iendelee kutunza na kupanda miti ya milonge ili kuweza kuongeza kipato cha kaya na Taifa kwa ujumla.
- Mheshimiwa Spika, Katika hatua nyingine, Taasisi imefanya utambuzi na utafiti wa miti iliyopandwa katika mikoa ya Iringa, Njombe, Mbeya, Morogoro na Ruvuma. Lengo la utafiti huu ni kutambua aina na kiwango cha miti iliyopo katika mikoa hiyo kwa lengo la kutoa taarifa kwa wawekezaji. Matokeo ya utafiti yamebaini uwepo wa spishi kuu tatu (3) ambazo ni misindano, mikaratusi na miwato. Aidha, spishi hizo zipo katika eneo la ukubwa wa hekta 203,172.35 ambapo kwa mikoa ya Iringa na Morogoro ni hekta 72,347; Mkoa wa Njombe hekta 115,391.04; Mkoa wa Mbeya hekta 14,140.21; na Mkoa wa Ruvuma hekta 1,294.10. Matokeo hayo yanaonesha kuwa rasilimali za misitu zilizopo katika maeneo hayo ni toshelevu kwa wawekezaji kuwekeza viwanda vya kuchakata na kuongeza thamani ya mazao ya misitu. Hata hivyo, ili kuwa na uwekezaji endelevu katika sekta ya misitu, inashauriwa kuendelea na usimamizi na kuongeza mashamba mapya ya miti katika mikoa hiyo.
- Mheshimiwa Spika, Taasisi imefanya utafiti wa kutambua aina na kiwango cha miti inayotumika kama miti dawa kwa mikoa ya Tabora, Shinyanga, Mwanza, Mara na Kagera. Matokeo ya utafiti yamebainisha uwepo wa aina (spishi) tano (5) za miti inayotumika kama miti dawa katika mikoa hiyo. Aina
ya miti hiyo ni Nengonengo (Securidaca longipenduculata), Ng’watya (Zahna africana), Msana (Combretum zeyheri), Mlungulungu (Zantoxylum chalybeum) na Mzima (Terminalia serícea). Spishi hizi za miti hutumika kutibu magonjwa mbalimbali yakiwemo athma, homa kali, magonjwa ya zinaa, matatizo ya tumbo, matatizo ya kibofu cha mkojo, upungufu wa damu na matatizo ya njia ya mfumo wa upumuaji. Hata hivyo, uwepo na mtawanyiko wa spishi hizi hutofautiana kati ya spishi moja (1) na nyingine. Aidha, TAFORI kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta ya misitu imetengeneza teknolojia ya kuoanisha aina za miti na maeneo ya kupanda (Site – Species Matching Tool, SSMT) kwa ajili ya kurahisisha upandaji wa miti nchini ikiwa ni njia ya kusaidia mkulima kutambua aina ya miti na mahali inapostahili kupandwa. Ili kuhakikisha uwepo endelevu wa aina ya miti hii muhimu, Wizara itaendelea kuelimisha jamii na kuanzisha programu maalum ya kutunza na kuendeleza miti dawa.
4.5.2.5 Vyuo vya Taaluma ya Misitu na Ufugaji Nyuki
- Mheshimiwa Spika, Vyuo vya taaluma ya misitu na ufugaji nyuki vinajumuisha Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki (BTI); Chuo cha Viwanda vya Misitu (FITI) na Chuo cha Misitu Olmotonyi (FTI). Vyuo hivi vimepewa jukumu la kutoa mafunzo ya uhifadhi, usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na nyuki katika ngazi ya Astashahada na Stashahada. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki kimedahili wanafunzi 378 pamoja na kutoa elimu ya ufugaji nyuki wenye tija kwa wafugaji nyuki 130 katika wilaya za Sikonge, Mlele na Mpanda. Aidha, Chuo kimeendelea kuboresha miundombinu ya kufundishia kwa kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mazao ya nyuki, kukarabati jengo la utawala na kuanza ujenzi wa karakana ya kufundishia. Vilevile, Chuo cha Viwanda vya Misitu kimedahili wanafunzi 286, kuendesha programu ya mafunzo kazini kwa wahitimu 20 katika viwanda vitano (5) vya kuchakata magogo katika mikoa ya Iringa na Njombe; na kukarabati bwalo la chakula la wanafunzi. Katika hatua ya kuendelea kusogeza huduma kwa jamii, Chuo kimepata eneo lenye ukubwa wa hekta 150 katika eneo la Shamba la Miti Sao Hill kwa ajili ya kuanzisha Kampasi. Pia, Chuo cha Misitu Olmotonyi kimedahili wanafunzi 892 wa ngazi ya Astashahada na Stashahada. Sambamba na hilo, Chuo kimeanza zoezi la mapitio ya mitaala ya kozi tano (5) ambapo kazi hii itakamilika mwishoni mwa mwezi Juni, 2022.
4.5.2.6 Mfuko wa Misitu Tanzania – TaFF
- Mheshimiwa Spika, Mfuko una jukumu la kuwezesha shughuli za uhifadhi, usimamizi na uendelezaji rasilimali za misitu. Katika kuendeleza jitihada za kuongoa maeneo yaliyoharibiwa, Mfuko umetoa ruzuku kwa miradi 60 inayoendelea na miradi mipya 63 ya uanzishaji wa vitalu vya miti na upandaji miti shuleni katika wilaya 36 za mikoa nane (8) inayopatikana katika maeneo ya Nyanda Kame ikiwemo Dodoma, Singida, Shinyanga, Simiyu na Manyara. Pia, Mfuko umetoa ruzuku maalum kwa miradi minne (4) inayotekelezwa na Taasisi za Serikali ambapo miradi mitatu (3) inahusu uanzishaji na uendelezaji wa mashamba ya miti ya kupandwa katika mikoa ya Kigoma na Morogoro; na mradi mmoja (1) ni ujenzi wa kituo cha kukusanya mazao ya nyuki katika Wilaya ya Mlele. Aidha, kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Mfuko umegharamia ununuzi wa mashine za kuchakata na kufungasha mazao ya nyuki kwa ajili ya viwanda vinne (4) katika Halmashauri za Wilaya ya Kibondo, Bukombe, Sikonge na Mlele. Vilevile, Mfuko umetoa ruzuku kwa miradi 12 ya uhifadhi na uendelezaji misitu na miradi 92 ya ufugaji nyuki inayoendelea kutekelezwa na wadau. 112. Mheshimiwa Spika, kwa upande mwingine, Mfuko umetoa ruzuku kwa miradi 11 ya ufugaji nyuki kwa vikundi 40 vya vijana na wanawake katika mikoa ya Kigoma, Tabora, Songwe, Lindi, Katavi, Mbeya na
Morogoro. Aidha, Mfuko umewezesha Kamati ya Kitaifa ya Ushauri wa masuala ya Misitu na Kamati ya Kitaifa ya Ushauri ya Ufugaji Nyuki kutekeleza majukumu yake. Kwa kuzingatia jitihada hizo, Mfuko uliweza kupata tuzo ya Taifa ya utendaji bora ya mifuko na programu za uwezeshaji wananchi kiuchumi kwa kuwa mshindi wa pili kitaifa kati ya mifuko 21 iliyoshindanishwa.
4.5.3 Sekta ya Utalii
- Mheshimiwa Spika, Sekta ya Utalii ina jukumu la kusimamia, kuendeleza na kutangaza utalii nchini. Utekelezaji wa jukumu hilo unaongozwa na Sera ya Taifa ya Utalii ya mwaka 1999, usimamiaji wa Sheria ya Utalii Na. 29 ya mwaka 2008 na Sheria ya Bodi ya Utalii Tanzania Sura 364. Vilevile, jukumu hilo hutekelezwa kupitia Idara ya Utalii, Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Wakala wa Chuo cha Taifa cha
Utalii (NCT).
4.5.3.1 Suala Mahsusi katika Sekta ya Utalii
(i) Kukuza Utalii wa Mikutano na Matukio
- Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza juhudi za kukuza utalii na kuimarisha uhifadhi, Wizara kwa kushirikiana na Jumuiya ya Afrika Mashariki iliandaa Onesho la Kwanza la Kimataifa la Utalii la Jumuiya ya Afrika Mashariki lililofanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 09 hadi 16 Oktoba, 2021. Onesho hilo lilijumuisha waoneshaji 185 kutoka nchi mbalimbali na wanunuzi wa kimataifa 41 kutoka nchi 22 ndani na nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. Aidha, pamoja na onesho hilo kufanyika katika kipindi cha UVIKO-19, jumla ya wageni 2,733 walishiriki na wadau kutoka maeneo mbalimbali duniani walipata fursa ya kufuatilia makongamano ya kitaalamu kwa njia ya mtandao.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara ilishiriki Mkutano wa 64 wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Kanda ya Afrika (64th UNWTO Commission For Africa – CAF) uliofanyika kuanzia tarehe 02 hadi 04 Septemba, 2021 katika Kisiwa cha Cabo Verde, ambapo Tanzania ilichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mwenyeji wa Mkutano ujao wa 65 wa UNWTO – CAF. Mkutano huo utafanyika Jijini Arusha tarehe 05 hadi 07 Oktoba, 2022 na maudhui yake ni kujenga upya utalii stahimilivu wa Afrika kwa maendeleo jumuishi ya kijamii na kiuchumi yaani Rebuilding Africa’s Tourism Resilience for Inclusive Socio-Economic Development.
4.5.3.2 Idara ya Utalii
- Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya biashara ya utalii nchini, Wizara imefanya mapitio ya Sheria ya Utalii Sura 365 na kutangaza maboresho kupitia Tangazo la Serikali Na. 41 la mwaka 2021. Maboresho hayo yamewezesha kuondoa mamlaka ya Bodi ya Leseni katika kutoa leseni za wakala wa biashara za utalii nchini ambazo kwa sasa zinatolewa kupitia mfumo wa kielektroniki wa MNRT Portal. Hatua hiyo imeongeza tija katika utoaji huduma ikiwemo kurahisisha mchakato wa utoaji wa leseni za biashara za utalii na hivyo kupunguza gharama, muda na kuongeza wigo wa ushiriki wa wananchi na wawekezaji mbalimbali katika biashara hizo.
- Mheshimiwa Spika, katika kusimamia na kuimarisha ukusanyaji wa maduhuli, Wizara imefanya kaguzi za biashara za utalii katika maeneo mbalimbali nchini. Maeneo hayo ni pamoja na: malango ya kuingilia wageni katika hifadhi za Taifa za Tarangire, Ruaha, Mikumi na Ziwa Manyara; na Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro ambapo jumla ya Shilingi 994,593,250.00 zimekusanywa kutokana na kaguzi hizo. Aidha, Wizara imeendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi – Dawati la Utalii na Diplomasia kubaini na kuwachukuliwa hatua wafanyabiashara wa utalii wasiofuata sheria, kanuni na taratibu za kuendesha shughuli hizo.
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kusajili wakala wapya wa biashara za utalii nchini ambapo hadi kufikia Aprili, 2022 jumla ya wakala wapya 252 wamesajiliwa. Aidha, Wizara imetambua na kuhakiki huduma za malazi katika mikoa 26 Tanzania bara ambapo imeongeza idadi ya huduma zilizopaswa kukusanya tozo ya kitanda siku kutoka 1,815 mwaka 2020 hadi 8,681 mwaka 2021 sawa na ongezeko la asilimia 378. Sambamba na hilo, Wizara imepanga huduma za malazi nne (4) katika daraja za ubora wa nyota zilizopo katika mikoa ya Arusha, Dar es Salaam, Pwani na Kigoma. Vilevile, Wizara imeimarisha mfumo wa kielektroniki wa kupanga huduma za malazi katika viwango vya ubora wa nyota – AserT unaowezesha watoa huduma za malazi kujitathmini wenyewe kabla ya huduma zao kupangwa katika daraja za ubora. Lengo ni kuhakikisha huduma hizo zinakuwa na ubora unaostahili pamoja na kukidhi mahitaji ya soko la utalii.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza mazao ya utalii ya kimkakati, Wizara imepata eneo lenye ukubwa wa ekari 22.44 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Kimataifa cha Utalii wa Mikutano na Matukio katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Jijini Dar es Salaam. Aidha, Wizara imepokea nyaraka za umiliki pamoja na ramani za eneo hilo. Hatua inayoendelea ni kumpata Mtaalam Elekezi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu wa mradi. Katika kuendeleza zao la utalii wa fukwe nchini, Wizara imebaini maeneo yenye fursa za uwekezaji wa shughuli za utalii pembezoni mwa Bahari ya Hindi katika mikoa ya Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi na Mtwara. Lengo ni kuyasajili maeneo hayo kama Kanda Maalum za Kiuchumi za Utalii kupitia Mamlaka ya Maeneo ya Uzalishaji kwa Mauzo ya Nje – EPZA. Aidha, Wizara ilifanya mkutano na wadau Jijini Dar es Salaam mwezi Februari, 2022 kwa lengo la kujadili uendelezaji wa maeneo hayo. Hatua hii itachochea ukuaji na uendelezaji wa shughuli za utalii wa fukwe, meli na michezo ya kwenye maji katika maeneo ya fukwe nchini.
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kushirikiana na wadau wa utalii nchini ambapo katika mwaka wa fedha 2021/2022, Wizara ilifanya jumla ya vikao sita (6) Jijini Arusha. Vikao hivyo vilihusisha vyama mbalimbali vya wadau katika sekta ikiwemo TATO, TLTO, TCT, TTGA, HAT na TPSF. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyojadiliwa kupitia vikao hivyo ni pamoja na fursa za uwekezaji, utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta na uendelezaji na utangazaji wa mazao ya utalii nchini.
4.5.3.3 Bodi ya Utalii Tanzania – TTB
- Mheshimiwa Spika, Bodi ya Utalii ina jukumu la kutangaza utalii wa Tanzania ndani na nje ya nchi. Katika kutekeleza jukumu hilo, Bodi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeratibu ushiriki wa Tanzania katika maonesho mbalimbali ya kitaifa na kimataifa. Maonesho hayo ni pamoja na FITUR 2022 na InvesTour ya nchini Uhispania; National Tour Association Annual Convention (NTA Travel Exchange), nchini Marekani; road show iliyohusisha nchi za Ujerumani, Austria, Switzerland, Swedeni na Denmark; na Africa Tourism Leadership Forum 2021, nchini Rwanda. Aidha, Bodi iliratibu ushiriki wa Wizara katika onesho la dunia la Expo 2020 Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu, na uzinduzi wa Programu ya The Royal Tour. Katika onesho hilo, nchi yetu ilipewa heshima ya pekee ya kuwa na siku maalum ambapo mnara maarufu duniani wa Burj Khalifa ulipambwa kwa rangi za bendera ya Tanzania; na vivutio vya utalii vilivyopo nchini vilioneshwa mubashara.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza jitihada za kutangaza vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji nchini, Bodi iliandaa ziara za mafunzo (FAM – trips) tisa (9) zenye jumla ya washiriki 66 kutoka makundi ya wakala wa biashara za utalii, wawekezaji, waandishi wa habari na watu mashuhuri. Wageni hao walitoka katika nchi 23 zikiwemo Algeria (4), Marekani (24), Poland (3), Georgia (8), Canada (5), Nigeria (1), Macedonia (3) na Qatar (18) na kutembelea vivutio mbalimbali nchini ikiwemo hifadhi za Taifa Serengeti na Ziwa Manyara; Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro; na Zanzibar. Aidha, Bodi imeendelea kusambaza nyenzo za kutangaza utalii na kufanya vikao na wakala wa biashara za utalii pamoja na mabalozi wa nchi mbalimbali zikiwemo Marekani, China, Urusi, Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Israel, Qatar, Kuwait, Sweden, India, Japan, Afrika Kusini, Nigeria, Namibia, Algeria na Rwanda. Juhudi hizo zinalenga kuvutia makundi mbalimbali ya watalii na wawekezaji kutembelea nchini. Mathalan, Tanzania imepokea makundi sita (6) yenye jumla ya watalii 1,924 kwa pamoja kutoka nchi ya Israel.
- Mheshimiwa Spika, kwa kutambua fursa mbalimbali za kuwatumia mabalozi wa hiari wa utalii, Bodi imekamilisha mwongozo wa vigezo vya kuchagua na kuainisha majukumu ya mabalozi. Aidha, Wizara imefanya uteuzi wa mabalozi mbalimbali wa hiari akiwemo Bwana Mamadou Sakho, Raia wa Ufaransa ambaye ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kimataifa wa Ufaransa; Bi. Rawan Dakik, aliyeweka rekodi ya kuwa mwanamke Mtanzania wa kwanza kupanda na kufika kwenye kilele cha Milima Everest, ambao ni mrefu zaidi duniani; Mtoto Sharon Ringo ambaye pia amepewa heshima ya kuwa Balozi wa Utalii katika Jumuiya ya Afrika Mashariki; na Bi. Isabella Mwampamba ambaye amekuwa akifanya shughuli mbalimbali za kuhamasisha na kutangaza utalii.
- Mheshimiwa Spika, Bodi imeendelea kutumia teknolojia mbalimbali katika kutangaza utalii ndani na nje ya nchi. Katika kutekeleza hilo, Bodi inatumia Kituo cha Kielektroniki cha Kutoa Habari (Digital Command Centre) ambacho hutangaza na kufuatilia mwenendo wa masuala ya utalii wa Tanzania katika mitandao ya kijamii ya Facebook, Twitter, Instagram na YouTube, Search Engine
Optimization (SEO), Email marketing, Affiliate
Marketing, Online Reputation Management (ORM) na WebPR. Katika hatua nyingine, Wizara imeendelea kuhamasisha utalii wa ndani kupitia matamasha na matukio mbalimbali yakiwemo: Kili Marathon 2022; Rock City Marathon; Serengeti Marathon; BurigiChato Marathon; Tabora Marathon; Majimaji
Serebuka; Majimaji Festival; Bagamoyo Cultural Festival – TaSuBa; Dodoma Wine Festival; Maonesho ya Utalii Mkoani Tanga; Senene Festival; Arusha Marathon; Zinj Day; East Africa Trade Fair; Siku ya Utalii Duniani 2022; Maonesho ya Biashara – Chato; Mbeya Tulia Marathon 2022; Karibu Dodoma Festival; Karibu Kilifair Summit; na Maonesho ya Biashara na Utalii ya Afrika Mashariki – Mwanza. Matamasha na maonesho hayo yametoa fursa mbalimbali za kutangaza utalii na kuendeleza wigo wa mazao ya utalii nchini. - Mheshimiwa Spika, katika juhudi za kutangaza mazao la utalii, Bodi imeratibu ushiriki wa Wizara katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) ambapo vivutio vya utalii vimetangazwa na elimu ya uhifadhi imetolewa. Kwa upande mwingine, Bodi imeendelea kuimarisha vituo vya kutolea taarifa za utalii katika Kanda kwa kuwapatia nyenzo za kutangaza utalii. Vilevile, Bodi imeendelea kushirikiana na vyombo mbalimbali vya habari kwa ajili ya kutangaza utalii.
4.5.3.4 Chuo cha Taifa cha Utalii – NCT
- Mheshimiwa Spika, Chuo cha Taifa cha Utalii kimepewa jukumu la kutoa mafunzo katika ngazi ya Astashahada na Stashahada katika fani ya utalii, ukarimu na uratibu wa matukio. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Chuo kimedahili jumla ya wanafunzi 1,127 katika ngazi ya Astashahada na Stashahada. Aidha, Chuo kimekarabati miundombinu ya kutolea mafunzo katika kampasi za Bustani, Arusha na Temeke; na kununua na kusimika mifumo ya TEHAMA, vitendea kazi na vifaa mbalimbali vya kutolea mafunzo na kujifunzia katika kampasi za Mwanza, Temeke, Bustani na Arusha. Vilevile, Chuo kimenunua eneo lenye jumla ya ekari 32.2 kwa ajili ya ujenzi wa Kampasi ya Mwanza. Katika kuboresha mafunzo ili kuendana na mahitaji ya soko, Chuo kimefanya mapitio ya mitaala tisa (9) na kuandaa mitaala mipya minne (4) katika fani za ukarimu na utalii. Katika hatua nyingine, Chuo kimeanza kuongezeka majengo ya mafunzo katika Kampasi ya Arusha. Kazi zilizofanyika ni pamoja na kufanya Tathmini ya Mazingira na Athari za Kijamii, kuandaa michoro ya majengo yanayotarajiwa kujengwa kwa kushirikiana na Chuo cha Ufundi – Arusha.
- Mheshimiwa Spika, Chuo kimeendelea kutoa mafunzo kwa kutekeleza programu za kimkakati za kukuza ujuzi ikijumuisha Uanagenzi na Utarajali. Katika kutekeleza hilo, mafunzo ya uanagenzi yametolewa kwa washiriki 216; na mafunzo ya Utarajali (Internship Program) kwa wahitimu 135.
Aidha, Chuo kimetoa mafunzo ya muda mfupi kwa wadau 220 katika mnyororo wa utalii. Vilevile, Chuo kimefanya utafiti na kutoa ushauri kuhusu namna ya uendeshaji wa hoteli zinazomilikiwa na Mfuko wa Taifa la Hifadhi za Jamii (NSSF). Katika hatua nyingine, Chuo kimetoa mafunzo kwa wataalam 44 wa Sekta ya Umma na Binafsi ya kupanga huduma za malazi katika daraja za ubora wa nyota (hotel assessors). Vilevile, Chuo kimetoa mafunzo maalum kwa watoa huduma 1,072 kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Mwanza na Mara ili kuwajengea uwezo na kuimarisha ubunifu wa huduma.
4.5.4 Sekta ya Mambo ya Kale
- Mheshimiwa Spika, Sekta ya Mambo ya Kale ina jukumu la kusimamia uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za malikale na urithi wa utamaduni. Sekta hii inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia Sera ya Malikale ya mwaka 2008; Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 na Sheria ya Makumbusho ya Taifa Sura 281. Sekta ya malikale inajumuisha Idara ya Mambo ya Kale na Shirika la Makumbusho ya Taifa (NMT).
4.5.4.1 Suala Mahsusi katika Sekta ya Mambo Kale
Kuenzi falsafa za Baba wa Taifa Hayati Mwl.
Julius Kambarage Nyerere
- Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuenzi falsafa za Baba wa Taifa, Wizara imezindua Mpango wa Miaka 10 wa Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Mpango huu unalenga kuweka utaratibu endelevu utakaohakikisha kuwa urithi na falsafa za Mwalimu Nyerere zinaenziwa, kuhifadhiwa na kuendelezwa. Katika kutekeleza mpango huo, Wizara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imeratibu Adhimisho la Kumbukizi ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Mwl. Nyerere lililofanyika Mwitongo, Butiama – Mkoa wa Mara tarehe 13 Aprili, 2022. Tamasha hilo lilihusisha matukio mbalimbali yakiwemo msafara wa mbio za baiskeli za Twende Butiama kutoka Msasani, Dar es Salaam hadi Mwitongo, Butiama; programu za kielimu kuhusu Urithi wa Mwalimu Nyerere kwa wanafunzi wa sekondari na shule za msingi; midahalo na makongamano, maonesho maalum ya sekta mbalimbali kuhusu mchango wa Mwalimu Nyerere, uzinduzi wa nembo maalum ya miaka 100 ya Mwalimu Nyerere; matembezi ya miguu kwa vijana kutoka Mwanza hadi Butiama pamoja na sanaa za jukwaani. Pia, jamii ilishiriki katika kuenzi falsafa za Mwl. Nyerere kwa kupanda miti na kushiriki katika maonesho ya bidhaa za utalii na utamaduni.
4.5.4.2 Idara ya Mambo ya Kale
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha malikale na urithi wa utamaduni vinalindwa, Wizara imekamilisha rasimu ya marekebisho madogo ya Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 na Sheria ya Makumbusho Sura 281 na kuwasilisha kwenye Mamlaka husika kwa hatua zaidi. Aidha, Wizara imekamilisha zoezi la kutafsiri Sheria hizo kwa lugha ya Kiswahili kwa lengo la kutoa uelewa kwa Umma.
- Mheshimiwa Spika, ili kuimarisha uhifadhi katika maeneo ya malikale, Wizara imehakiki na kupima mipaka katika vituo vya: Magofu ya Kunduchi, Dar es Salaam; Mapango ya Amboni na Magofu ya Tongoni, Tanga; Tembe la Kwihara, Tabora; Makumbusho ya Kumbukizi ya Mkwawa – Kalenga,
Iringa; Makumbusho ya Kumbukizi ya Dkt. Livingstone Ujiji, Kigoma; na Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa, Songea. Kufuatia hatua hiyo, Makumbusho ya Mkwawa Kalenga, Iringa imepata hati miliki ya ardhi. Aidha, taratibu za upatikanaji wa hati kwa maeneo mengine zinaendelea. - Mheshimiwa Spika, katika kuendelea kuhifadhi urithi wa historia ya nchi na kutangaza utalii, Wizara imekusanya taarifa ya maeneo mbalimbali ya kihistoria ikiwemo: jengo la iliyokuwa Kamati ya Ukombozi ya Bara la Afrika lililopo Dar es Salaam; makambi ya wapigania uhuru ya Masonya Ruvuma, Dakawa na Mazimbu Morogoro na Kongwa Dodoma; kituo cha redio Tanzania (RTD) kilichotumika kurusha matangazo wakati wa harakati za ukombozi wa nchi za kusini mwa Bara la Afrika; na Chuo cha Diplomasia Dar es Salaam kilichotumika kutoa mafunzo ya wapigania uhuru. Maeneo mengine ni pamoja na eneo lenye asili ya Mkoa wa Dodoma lililopo Kikuyu, Mapango ya Nang’oma ya Kipatimo Lindi na Mji wa Kihistoria Pangani. Sambamba na hilo, Wizara imeendelea kutoa vibali 10 kwa watafiti wa ndani na nje kwa ajili ya kufanya utafiti wa malikale katika maeneo mbalimbali yakiwemo Tendaguru, Bonde la Olduvai, Ziwa Eyasi, Kilwa na Isimila. Tafiti hizi zinasaidia kubaini maeneo ya malikale yenye sifa za kutangazwa kuwa Urithi wa Taifa.
4.5.4.3 Shirika la Makumbusho ya Taifa Tanzania – NMT
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha utekelezaji wa shughuli za Makumbusho, Shirika limeandaa sera ya ndani inayotoa mwongozo wa utafiti, ukusanyaji, uhifadhi na utoaji elimu kwa wadau juu ya urithi wa Taifa. Aidha, katika kuhakikisha mila na tamaduni za Watanzania zinaendelea kuhifadhiwa, Shirika limekusanya mikusanyo 54 kutoka kwa jamii ya watu wa Songea na mikusanyo 25 kutoka kwa jamii ya watu wa Rukwa. Vilevile, Shirika limekusanya mikusanyo na taarifa kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo Idara ya Maelezo na Shirika la Habari Tanzania (TBC). Pia, zoezi la ukusanyaji wa taarifa za kumbukumbu za Marais wastaafu linaendelea ambapo Hotuba 79 zinazohusu ukombozi, maendeleo, uchumi, utamaduni na siasa zimekusanywa. Aidha, Kitabu cha wasifu wa Hayati Benjamini Mkapa; picha za Marais; na vifaa mbalimbali vimekusanywa na kuhifadhiwa. Kwa upande mwingine, Shirika limetengeneza mfumo wa kidigitali wa kusajili na kuhifadhi mikusanyo na limejiunga na Datasaver ya National Internet Data Center (NIDC) ili kuhifadhi taarifa za mikusanyo kwa usalama zaidi. Katika hatua nyingine, Shirika kwa kushirikiana na Goethe Insitut limewajengea uwezo watumishi 24 kuhusu uhifadhi wa mikusanyo kidijitali. Aidha, Shirika limeweka onesho la kudumu la tembo katika Makumbusho ya Elimu Viumbe – Arusha; na usimikaji wa taswira za wanyamapori wakiwemo nyati, tembo, twiga, faru na kiboko. Kwa upande mwingine, Shirika limefanikiwa kupata Kiwanja hekari 19 katika eneo la Mkonze, Dodoma ambapo jengo la Makumbusho ya Marais litajengwa.
- Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha utendaji kazi kwenye vituo vya malikale na makumbusho, Shirika limefanya ukarabati wa jengo la kihistoria la soko la watumwa na kufungua ofisi katika Mji Mkongwe Mikindani. Aidha, Shirika limeanza kusimamia na kuendesha Kituo cha Makumbusho ya Dkt. Rashid Mfaume Kawawa. Sambamba na hatua hizi, Shirika limeendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu makumbusho na urithi wa utamaduni kwa kuandaa na kurusha vipindi 24 vya redio, 52 vya televisheni na matangazo 40 kwenye mitandao ya kijamii. Vilevile, Shirika limeendelea na kampeni ya
Twenzetu Makumbusho na pragramu za KijijiSoko, Museum Art Explosion na Mkole kwa lengo la kuendelea kuhamasisha jamii kuhifadhi na kuendeleza tamaduni zetu. Pia, Shirika limefanya warsha iliyowahusisha wahariri 20 kutoka vyombo vya habari 10 na ya wadau wa elimu ya sekondari jijini Dar es Salaam. Aidha, Shirika limeendesha programu 40 za uelimishaji katika maeneo ya Madaba, Tunduru na Songea; na kuanzisha klabu 35 za historia na uzalendo katika mikoa ya Tanga na Morogoro. - Mheshimiwa Spika, Shirika limefanya utafiti wa tafsiri ya malikale zinazohusiana na biashara ya utumwa huko Mikindani (Mtwara) na Pangani (Tanga) na utafiti wa masoko ya utalii wa Makumbusho Tanzania. Aidha, mikusanyo 1,290 ya akiolojia imekusanywa kutokana na utafiti uliofanyika eneo la Laetoli lenye nyayo za Zamadamu. Kupitia tafiti hizo, jumla ya machapisho sita (6) yamezalishwa ikiwemo kitabu kinachoainisha na kuchambua Makumbusho zilizopo nchini. Machapisho hayo yametoa ushauri na mapendekezo ya namna ya kuhifadhi mikusanyo na maeneo ya malikale. Sambamba na hilo, Shirika limefanya utafiti kwa kukusanya vipepeo 5,361 katika eneo la Usambara Mashariki kwa lengo la kubaini umuhimu wake na namna ya kuhifadhi. Matokeo yanaonesha uwepo wa familia nne (4) zenye jumla ya spishi 110 ambazo zinachangia katika uchavushaji wa mimea na utunzaji wa mazingira. Kupitia matokeo hayo, Shirika limeanzisha bustani za vipepeo kwa ajili ya kuhifadhi na kutoa elimu kwa jamii. Aidha, tafiti kuhusu masalia ya mjusi wa dinosaria katika eneo la Tendaguru zimeendelea kufanyika kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es Salaam na Makumbusho ya Elimu Viumbe ya Ujerumani, ambapo masalia ya mjusi huyu yameendelea kupatikana. Sambamba na hilo, utafiti umefanyika wa kuainisha thamani ya kiutamaduni ya eneo hilo kwa lengo la kuandaa mpango wa usimamizi na uhifadhi.
4.5.4.4 Mfuko wa Mambo ya Kale
- Mheshimiwa Spika, Mfuko huu ulianzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 kwa lengo la kutekeleza majukumu ya uhifadhi na utafiti wa malikale. Katika mwaka 2021/2022, Mfuko umewezesha maandalizi ya Mpango wa miaka 10 wa Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Vilevile, Mfuko umewezesha ukarabati wa jengo alilofikia Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wakati wa kudai uhuru lililopo Manispaa ya Mikindani, Mtwara; kuandaa mpango mkakati wa miaka mitano (2021/2022 hadi 2025/2026) wa Mfuko wa Mambo ya Kale; kufanya tathmini ya Sera ya Malikale ya 2008; na kuwezesha uandaji wa rasimu ya uwekezaji katika maeneo ya malikale.
4.6 Miradi ya Maendeleo
137. Mheshimiwa Spika, katika Mwaka
2021/2022, Wizara ilitengewa jumla ya Shilingi 152,772,880,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ya Wizara na Taasisi. Fedha hizo zinajumuisha Shilingi 113,893,184,000.00 fedha za ndani na Shilingi 38,879,696,000.00 fedha za nje. Hadi kufikia Aprili, 2022 Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 59,481,316,267.20 kwa ajili ya miradi ya maendeleo ambapo Shilingi 33,567,915,783.20 ni fedha za ndani na Shilingi 25,913,400,484.00 ni fedha za nje. Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo iliyo chini ya Idara za Wizara ni kama ifuatavyo:-
(i) Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kusini (Resilient Natural Resources Management for Tourism and
Growth – REGROW)
- Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Benki ya Dunia. Kwa mwaka wa fedha 2021/2022, Shilingi 33,701,696,000.00 ziliidhinishwa. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa mitambo nane (8) kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu katika Hifadhi ya Taifa Nyerere na kukamilisha taratibu za ununuzi wa malori 17, boti za upepo (airboat) mbili (2) na magari mawili (2) ya kuoneshea sinema. Kazi nyingine ni kufanya usanifu na tathmini ya athari za kimazingira kwa ajili ya ujenzi wa barabara (km 2,051); njia za utalii wa miguu (km 132.5) majengo (80); madaraja na viwanja vya ndege 14 katika hifadhi za Taifa Mikumi, Ruaha, Nyerere na Udzungwa; na Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asilia Kilombero.
- Mheshimiwa Spika, katika kutangaza utalii, Wizara imeandaa mkakati wa kutangaza utalii kusini, mwongozo wa mafunzo ya utalii wa nyuki (Api-
tourism) na kukamilisha maandalizi ya ujenzi wa Kituo cha Utafiti wa Wanyamapori, Iringa. Aidha, Wizara imefanya utafiti wa wanyamapori na kukusanya takwimu za mtawanyiko wa wanyamapori katika hifadhi za Taifa Nyerere na Ruaha. Vilevile, miongozo ya kushughulikia migogoro baina ya wanyamapori na binadamu imefanyiwa mapitio; mafunzo ya utalii wa nyuki na matumizi bora ya ardhi yametolewa katika hifadhi za Taifa Nyerere na Ruaha. - Mheshimiwa Spika, shughuli nyingine zilizofanyika ni uwezeshaji wa shughuli za kiuchumi kwa jamii zinazopatikana katika eneo la mradi kwa lengo la kuimarisha uhifadhi na kuwaongezea kipato. Aidha, Wizara imetoa mafunzo ya maendeleo ya jamii na usimamizi wa ushirika kwa watumishi 18 wa mradi, wawezeshaji wa jamii 15, maafisa watendaji wa vijiji 15 na wasimamizi saba (7) wa wilaya za Chamwino, Iringa, Kilolo, Morogoro, Mvomero, Kilosa na Ifakara zinazotekeleza mradi. Kwa upande mwingine, skimu ya umwagiliaji ya majaribio ya Madibira imeendelea kuboreshwa; na ujenzi na ufungaji wa miundombinu ya kupimia maji na utandazaji wa mifereji unaendelea.
(ii) Mradi wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara (Support to Combating Wildlife Crime and Advancing Conservation)
- Mheshimiwa Spika, Mradi unatekelezwa na Wizara kwa ufadhili wa Mfuko wa Mazingira wa Kimataifa (Global Environmental Facility – GEF) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (United Nations Development Programme – UNDP). Kwa mwaka 2021/2022, Mradi uliidhinishiwa kiasi cha Shilingi 2,000,000,000.00 kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali zikiwemo: kutoa mafunzo ya mbinu za kukabiliana na ujangili na biashara haramu ya nyara kwa watumishi 110 kutoka Kikosi Kazi cha Taifa Dhidi ya Ujangili (NTAP) na Kanda 10 za Kiikolojia za Kupambana na Ujangili (TCG); na kuandaa Mwongozo wa Utendaji wa Kikosi Kazi cha Taifa Dhidi ya Ujangili. Kazi nyingine ni kufanya tathmini ya uwezo na mahitaji ya NTAP na TCG; kuondoa vifaa vya mawasiliano (GPS Collars) kwa tembo 16 katika ikolojia ya Ruaha – Rungwa; kuwezesha doria za kiintelijinsia katika ikolojia ya Ruaha – Rungwa; kuhuisha Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara; na ununuzi wa magari 10 kwa ajili ya TCGs.
(iii) Mradi wa Panda Miti Kibiashara (Private Plantation and Value Chain in Tanzania)
- Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatekelezwa kwa ubia baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ufini. Kwa mwaka 2021/2022, Mradi uliidhinishiwa Shilingi 328,000,000.00. Kazi zilizotekelezwa ni pamoja na: kuwezesha vikundi 64 vya wakulima wa miti wapatao 3,995 kusajiliwa katika ngazi ya wilaya na kuwezesha mikutano 26 katika ngazi ya kijiji na kuvijengea uwezo; kutoa huduma za ugani kwa vikundi 80 vya wakulima wa miti ili kuviimarisha viweze kutoa huduma kwa wanachama wake wapatao 9,662; na kuwezesha utunzaji wa mashamba 15 ya mbegu bora za miti. Sambamba na hilo, viongozi wa vikundi vya wapanda miti na wakulima wa miti 327 wamepatiwa mafunzo ya uanzishaji, upandaji na utunzaji wa miche katika vitalu vya miti.
- Mheshimiwa Spika, kazi nyingine zilizofanyika ni kukusanya taarifa za mashamba ya miti 1,557 yenye jumla ya eneo la hekta 1,188.98 yanayomilikiwa na wakulima 1,324; na kuandaa mipango 1,206 ya namna ya kutunza mashamba ya miti. Aidha, mashamba darasa 56 yameanzishwa; kuwezesha utoaji wa hati miliki za kimila za mashamba ya miti 869 katika kijiji cha Ibaga; na kuwezesha uandaaji wa mipango ya matumizi bora ya ardhi 12 katika vijiji 12 katika wilaya za Njombe (2), Ludewa (4), Mufindi (4) na kilolo (2). Katika hatua nyingine, mafunzo ya kupambana na moto kichaa yametolewa kwa wasimamizi 42; kuwezesha ununuzi wa pikipiki 19 kwa ajili ya maafisa ugani wa halmashauri; na kuwezesha wajasiriamali 674 wadogo na wakati kushiriki katika mafunzo ya uchakataji magogo na wajasiliamali zaidi ya 180 kuhusu namna ya kuandaa mipango ya biashara.
- Mheshimiwa Spika, Wizara imenunua mashine na vifaa maalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa vitendo kwa mfumo wa darasa linalotembea (mobile training unit); na kuboresha miundombinu ya kufundishia katika Kituo cha Mafunzo ya Misitu na Viwanda vya Misitu (FWITC), Mjini Mafinga. Kwa upande mwingine, Wizara imewezesha uandaaji wa maandiko ya mradi pamoja na kuchapisha nakala 9,000 za Mwongozo kuhusu usimamizi na utunzaji wa mashamba ya miti. Vilevile, Wizara imewezesha utafiti wa uzalishaji wa mkaa mbadala; kuwezesha maonesho ya uwekezaji katika sekta ya Misitu yaliyofanyika Mkoa wa Iringa, mwezi Novemba 2021; na kuwezesha uandaaji wa andiko la kuimarisha vituo vya mafunzo vya FITI, FTI na FWITC.
(iv) Mradi wa Kuongeza Thamani kwa Mazao ya
Misitu (Forestry and Value Chain
Development Programme (FORVAC)
- Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Ufini. Katika mwaka 2021/2022, jumla ya Shilingi 2,000,000,000.00 ziliidhinishwa. Kazi zilizofanyika ni pamoja na: kuandaa na kuidhinisha mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 29; na kutenga eneo lenye jumla ya hekta 123,462 za misitu. Aidha, Wizara imenunua sare 432 na pikipiki 20 kwa ajili ya wanakamati wa maliasili wa vijiji katika vijiji 25 viliyoko katika kongani za Tanga, Lindi na Ruvuma; na ununuzi wa pikipiki 16 kwa Halmashauri za wilaya kwa ajili ya maafisa misitu na maafisa nyuki wilaya. Katika hatua nyingine, Wizara imeandaa Mipango ya Usimamizi ya misitu ya vijiji 30 katika eneo la misitu ya vijiji la hekta 269,024; kutangaza kisheria Misitu ya Hifadhi ya vijiji 16 yenye hekta 146,064 katika Tangazo la Serikali Na. 454 la mwaka 2021; na kuandaa mipango ya uvunaji endelevu wa misitu 40 ya vijiji. Sambamba na hilo, Wizara imeanzisha viwanda vinavyotembea vya kuchakata magogo (mobile sawmills) katika wilaya za Ruangwa na Songea; kununua mitambo ya kukausha mbao kwa kutumia nishati ya jua kwa wilaya za Liwale na Ruangwa; kufadhili miradi ya biashara 60 za wajasiriamali wadogo wadogo 630; na kutoa mizinga 1,592 katika wilaya za Handeni, Mbinga na Liwale.
- Mheshimiwa Spika, Wizara imeanzisha vikundi 19 vya kukopeshana na kuweka akiba vyenye wanachama 801 katika kongani za Tanga, Lindi na Ruvuma; na kupanda miche ya miti 553,620 kwenye hekta 470 katika vijiji vya Mkali A, Mkali B, Liuli na Lipingo katika Wilaya ya Nyasa. Aidha, Wizara imetoa mafunzo kuhusu dhima na majukumu ya Serikali za Vijiji na Kamati za Maliasili, ufugaji na uchakataji wa mazao ya nyuki kwa viongozi, wataalam wa ngazi ya wilaya na vijiji katika mikoa ya Lindi, Ruvuma na Tanga. Vilevile, vijiji vitano (5) vya Chiseyo, Ikuyu na Litemo (Mpwapwa), Mnkonde (Kilindi) na kwamwande (Handeni) vimewezeshwa kutenga hifadhi za nyuki za vijiji zenye jumla ya hekta 5,069.73. Katika hatua nyingine, Wizara imewezesha uchapishaji wa nyaraka mbalimbali zikiwemo: mikakati ya utekelezaji wa Sera za Taifa za Misitu na Nyuki, Mkakati wa Mazao ya Mbao Yaliyohandisiwa (2021 – 2031) na Mpango kazi wake, Mwongozo wa Takwimu za uhalisia wa Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa misitu na Mwongozo wa Uanzishaji na Usimamizi wa Hifadhi za Nyuki na Manzuki Tanzania.
(v) Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki – BEVAC
- Mheshimiwa Spika, Mradi huu unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya. Katika mwaka 2021/2022, jumla ya Shilingi
1,000,000,000.00 ziliidhinishwa kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali ikiwemo: kukamilisha taratibu za tathmini kwa ajili ya ununuzi wa vifaa vya
Maabara ya Utafiti wa Ufugaji Nyuki katika Kituo cha Utafiti wa Ufugaji Nyuki, Njiro – Arusha; na kukamilisha taratibu za ujenzi na maboresho ya miundombinu ya chuo hicho ikihusisha bweni, maktaba na maabara ya mafunzo. Kazi nyingine ni kufanyika kwa tathmini kuhusu mahitaji ya soko na mtazamo wa wanunuzi wa bidhaa za nyuki katika masoko ya kikanda ya Ulaya, Uingereza na Mashariki ya Kati. Aidha, tathmini imefanyika katika maeneo machache ya mradi kwa ajili ya kuelewa uwezo uliopo na kutambua wadau tarajali katika mnyororo wa thamani. - Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, ukarabati wa ofisi kuu ya mradi iliyopo Tabora umefanyika; na kununua magari matatu (3), pikipiki 20, samani na vifaa vya TEHAMA kwa ajili ya ofisi kuu ya uratibu wa mradi Tabora. Sambamba na hilo, vikao vitano (5) vya uratibu vilifanyika Tanzania bara (3) na Zanzibar (2); na warsha ya uzinduzi wa mradi ilifanyika. Kwa upande mwingine, mafunzo yametolewa kwa mashirika mawili (2) ya Api – Support na Honey Exporters Association yanayojihusisha na biashara ya mazao ya nyuki. Mafunzo hayo yalilenga kujenga uwezo wa mashirika kwa ajili ya kuanzisha kamati ya utetezi wa maslahi ya biashara na sera za biashara katika ngazi ya kitaifa na kimataifa.
4.7 Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya Athari za UVIKO-19
- Mheshimiwa Spika, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19. Katika kutekeleza mpango huo, Wizara ya Maliasili na Utalii iliidhinishiwa jumla ya Shilingi 90,202,345,530.00 Hadi kufikia mwezi Aprili, 2022, Wizara ilipokea jumla ya Shilingi 83,037,216,335.51 sawa na asilimia 92.1 ya fedha zilizoidhinishwa. Mpango huo unatekelezwa na Idara ya Utalii, Kitengo cha Utafiti na Mafunzo, Kitengo cha TEHAMA na taasisi za TANAPA, TAWA, NCAA, TFS, NMT, TTB, CAWM – MWEKA na NCT.
- Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza Mpango huu, Wizara inaendelea na ukarabati wa barabara ambapo jumla ya kilometa 1,164.3 kati ya kilometa 2,383.12 za barabara na vivuko viwili (2) vimekamilika katika maeneo yaliyohifadhiwa, ujenzi wa viwanja vya ndege (airstrips) vitano (5) na njia za kutembea kwa miguu zenye urefu wa kilomita 110. Aidha, Wizara inaendelea na ujenzi wa madaraja matano (5), malango 12, vituo vya kutolea taarifa vitano (5), campsite nne (4), picnic site sita (6), ujenzi wa vyoo sita (6), vituo vitano (5) vya kukusanyia mapato na maeneo ya kutua helikopta (helipads) matano (5). Shughuli hizo zinatekelezwa katika Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro; hifadhi za Taifa tisa (9), mapori ya akiba 10, mapori tengefu mawili (2), hifadhi za misitu ya mazingira asilia 11 na bustani ya wanyamapori moja (1). Maeneo hayo ni pamoja na: hifadhi za Taifa Kilimanjaro, Gombe, Serengeti, Tarangire, Saadani, Mkomazi, Mahale, Nyerere na Katavi; mapori ya akiba Rungwa, Swagaswaga, Mkungunero, Kijereshi, Wami – Mbiki, Liparamba, Lukwika/Lumesule, Mpanga Kipengere, Igombe na Maswa; mapori tengefu Ziwa Natron na Kilombero; Bustani ya Wanyamapori ya Ruhila; na hifadhi za misitu ya mazingira asilia za Magamba, Pugu – Kazimzumbwi, Nilo, Chome, Essimingor, Mlima Hanang, Mlima Rungwe, Kalambo Falls, Uluguru, Amani na Matogoro.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara inaendelea na ujenzi wa vituo vya taarifa vitatu (3) katika maeneo ya Tendaguru – Lindi, Lindi Manispaa na Kigamboni – Dar es Salaam. Aidha, Wizara imefanya ukarabati wa Jengo la Kihistoria la Watumwa, Mikindani; na magofu ya Kimbiji na Mbua Maji, Kigamboni – Dar es Salaam na Kua – Mafia. Vilevile, Wizara inaendelea na ujenzi wa onesho la tembo katika Kituo cha Elimu Viumbe, Arusha; na nyumba za asili za kaya tatu (3) za jamii ya Wairaq, Wasukuma na Wazanaki katika Kijiji cha Makumbusho – Dar es Salaam. Vilevile, Wizara inaendelea na ujenzi wa miundombinu ya vyoo katika Kituo cha Majimaji, Songea; na mfumo wa ulinzi katika makumbusho za Mwalimu Nyerere, Butiama na Elimu ya Viumbe, Arusha. Kwa upande mwingine, Wizara imekamilisha taratibu za manunuzi kwa ajili ya vitendea kazi mbalimbali vikiwemo: magari 10, malori 19, wheel excavator tano (5), motor grader sita (6), water bowser sita (6), compactor tano (5), low bed nne
(4), back hoe loader moja (1), concrete mixer moja (1), mahema 529, mtambo mmoja (1) maalum kwa ajili ya kuchimba visima vya maji na boti tatu (3). - Mheshimiwa Spika, katika kuimarisha huduma za utalii na kukabiliana na janga la UVIKO19, Wizara imetoa mafunzo kwa wadau wa utalii 4,698 katika mikoa 26 nchini kuhusu miongozo ya kukabiliana na janga la UVIKO-19 pamoja na kutoa chanjo kwa hiari kwa wadau 354. Aidha, mafunzo kwa wataalam wa ndani ya kupanga huduma za malazi katika daraja za ubora wa nyota (hotel assessors) yametolewa kwa wataalam 43 wa Serikali na Sekta Binafsi. Vilevile, Wizara imetoa mafunzo maalum kwa watoa huduma 1,072 kutoka mikoa nane (8) ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe, Iringa, Mbeya, Mwanza na Mara ili kuwajengea uwezo na kuimarisha ubunifu wa huduma. Katika hatua nyingine, Wizara imetoa mafunzo kwa waongoza watalii 1,060 ikijumuisha mafunzo maalum kwa wanawake 89. Mafunzo haya yalihusisha waongoza watalii kutoka Serikali ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Aidha, Wizara imenunua vifaa kinga vya kukabiliana na UVIKO-19 ikiwemo vitakasa mikono 14,285 vyenye ujazo wa mililita 500 kila moja na barakoa makasha 50 yenye jumla ya barakoa 2,800 kwa ajili ya wadau wa utalii kupitia vyama vyao.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua za kutangaza utalii hasa katika masoko ya kimkakati, Wizara imeshiriki maonesho mawili (2) ya kimataifa ambayo ni FITUR 2022 na InvesTour nchini Uhispania na Expo 2020 Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu. Aidha, programu endeshi (software) kwa ajili ya mfumo wa ufuatiliaji na utoaji wa taarifa za utangazaji utalii katika mitandao ya kijamii kupitia Digital Command Centre imenunuliwa. Katika hatua nyingine, Wizara kwa mara ya kwanza inaendelea na utafiti wa watalii wa ndani (stand – alone domestic tourism survey) kwa ajili ya kupata mchango wa Sekta ya Utalii katika Pato la Taifa. Sambamba na hilo, Wizara imeandaa Mfumo wa Kielektroniki wa Ufuatiliaji na Tathmini ya Miradi; na kuboresha mfumo wa MNRT Portal; na Mfumo wa kielektroniki wa tathmini ya upangaji wa huduma za malazi na chakula katika daraja za ubora – AserT.
4.8 Changamoto na Utatuzi
4.8.1 Changamoto
- Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka 2021/2022, Wizara imekabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uwepo wa ugonjwa wa UVIKO-19 duniani ambao umeathiri kwa kiasi kikubwa sekta ya utalii na hivyo kupungua kwa mapato yanayotokana na sekta hiyo. Aidha, kumekuwa na ongezeko la migogoro kati ya binadamu na wanyamapori ambao umesababisha uharibifu wa mali na vifo. Changamoto nyingine ni; uwepo wa matukio ya moto katika maeneo ya hifadhi; uvamizi wa hifadhi za wanyamapori, misitu na malikale kwa shughuli za kibinadamu; utegemezi mkubwa wa misitu kwa ajili ya nishati; na uwepo wa mimea vamizi katika baadhi ya maeneo ya hifadhi hali inayosababisha kuathirika kwa uoto wa asili na kupungua kwa malisho ya wanyamapori. 4.8.2 Utatuzi wa Changamoto
- Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na changamoto hizo, Wizara imeweka mikakati mbalimbali ikiwemo: kutoa elimu kwa wadau wa utalii juu ya namna bora ya kutumia Mwongozo wa
Uendeshaji wa Shughuli za Sekta ya Utalii – SOPs; na kuendelea kutekeleza Mpango wa Kuirejesha Sekta ya Utalii nchini katika hali ya awali kabla ya kuathiriwa na UVIKO-19 ambao umeweka mkazo katika njia mbadala za utangazaji utalii, kuboresha miundombinu ya utalii, kuimarisha mazao ya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani. Mikakati mingine ni kujenga vituo vya askari katika maeneo yenye changamoto kubwa ya matukio ya wanyamapori wakali na waharibifu; kutumia mbinu za kielektroniki za kufuatilia mienendo ya makundi ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa kuwafunga vifaa maalum hususan katika maeneo yenye matukio mengi; kutoa elimu ya namna ya kujikinga na wanyamapori wakali na waharibifu kwa kutumia mbinu mbalimbali za kitaalamu na asili; na kuimarisha doria za kupambana na ujangili na biashara haramu ya nyara. Aidha, Wizara itaendelea kutoa elimu ya namna ya kuzuia na kukabiliana na moto kichaa katika maeneo ya hifadhi; kuweka alama na mabango katika maeneo ya mipaka ya hifadhi; kuwezesha jamii inayopakana na maeneo ya hifadhi kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao; kuhimiza wananchi kupanda miti katika maeneo yao kwa ajili ya kupata nishati na matumizi mbalimbali; na kuwezesha miradi mbalimbali ya jamii ikiwemo ufugaji nyuki kwa lengo la kuwapatia kipato. Kwa upande mwingine, Wizara itaendelea kufanya tafiti za namna bora ya kukabiliana na mimea vamizi pamoja na kuendeleza operesheni za kung’oa na kuteketeza mimea hiyo.
5.0 MPANGO NA BAJETI KWA MWAKA WA FEDHA 2022/2023
- Mheshimiwa Spika, Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2022/2023 umezingatia miongozo mbalimbali ikiwemo Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa mwaka 2022/2023 – 2024/2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/2022 – 2025/2026), Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya 2020 – 2025, Sera mbalimbali, Mpango Mkakati wa Wizara (2021/2022 – 2025/2026), maagizo mbalimbali ya viongozi wa Serikali na mikataba ya kikanda na kimataifa.
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara itaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia vipaumbele mbalimbali vya sekta ambavyo ni pamoja na: kukuza utalii wa ndani, kuongeza kasi ya utangazaji utalii kitaifa na kimataifa kwa kuendeleza programu ya The Royal Tour, na kuibua masoko mapya ya utalii; kukarabati na kuimarisha miundombinu katika maeneo ya hifadhi; na kuibua na kuendeleza mazao ya utalii ya kimkakati ikiwemo utalii wa fukwe, mikutano na matukio, meli za kitalii, michezo na utamaduni. Vipaumbele vingine ni: kuendelea kuishirikisha jamii katika mbinu za kujikinga dhidi ya wanyamapori hatarishi; kuimarisha shughuli za upandaji miti, ufugaji nyuki na mnyororo wa thamani wa mazao yake; kuimarisha mnyororo wa thamani wa mazao ya misitu; kuimarisha mfumo wa utoaji huduma za utalii ili kukidhi viwango vya kimataifa; kuboresha ulinzi na usalama wa rasilimali za maliasili na malikale; kuendelea kuimarisha tafiti pamoja na mifumo ya takwimu na ukusanyaji wa mapato ya Serikali yatokanayo na Sekta ya Maliasili na Utalii; na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na kuendeleza rasilimaliwatu.
5.1 Ukusanyaji Maduhuli
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, makadirio ya maduhuli yatakayokusanywa kutokana na sekta ya maliasili na utalii ni jumla ya Shilingi 670,856,583,921.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 469,364,418,596.00 zitakusanywa na Wizara kupitia mfumo wa TRA kutoka vyanzo vya
TANAPA, NCAA na TAWA. Aidha, Shilingi 201,492,165,325.00 zitakusanywa moja kwa moja na Wizara kupitia mfumo wa MNRT Portal kutoka Idara, Mifuko na Taasisi nyingine za Wizara.
5.2 Matumizi ya Kawaida na Maendeleo
- Mheshimiwa Spika, Wizara kwa mwaka
2022/2023 inakadiria kutumia jumla ya Shilingi
624,142,732,000.00. Kati ya fedha hizo, Shilingi 443,706,567,000.00 zitagharamia Matumizi ya Kawaida na Shilingi 180,436,165,000.00 ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Makadirio ya Matumizi ya Kawaida yanajumuisha makadirio ya Mishahara Shilingi 175,884,707,000.00 na makadirio ya Matumizi Mengineyo Shilingi 267,821,860,000.00. Fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Shilingi 109,879,593,000.00 fedha za ndani na Shilingi 70,556,572,000.00 fedha za nje. - Mheshimiwa Spika, Fedha za Matumizi ya Kawaida zinajumuisha Shilingi 22,974,824,000.00 kwa ajili ya Wizara na Shilingi
420,731,743,000.00 kwa ajili ya taasisi zilizo chini ya Wizara. Kati ya fedha za Wizara, Shilingi 7,537,783,000.00 ni Mishahara na Shilingi 15,437,041,000.00 ni matumizi mengineyo. Fedha za taasisi zinajumuisha Shilingi 168,346,924,000.00 za mishahara na Shilingi 252,384,819,000.00 fedha matumizi mengineyo.
5.3 Kazi Zitakazotekelezwa na Wizara na Taasisi zake
5.3.1 Sekta ya Wanyamapori
5.3.1.1 Idara ya Wanyamapori
- Mheshimiwa Spika, Wizara inatarajia kupandisha hadhi mapori tengefu Lake Natron, Kilombero, Loliondo, Lolkisale, Longido, Muhuwesi, Umba River, Mto wa Mbu, Simanjiro, Ruvu Masai, Ruvu Same na Kalimawe; na misitu ya Litumbandyosi na Gesimazoa kuwa mapori ya akiba. Aidha, Wizara itatenga na kurasimisha maeneo ya shoroba za wanyamapori na kuimarisha usimamizi wa maeneo ya mifumo ikolojia inayovuka mipaka ya nchi. Sambamba na hilo, Wizara itaendelea kutoa elimu ya mbinu za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu na kutoa kifuta jasho na kifuta machozi kwa waathirika wa matukio ya wanyamapori hao. Vilevile, Wizara itaandaa mkakati wa kutekeleza Sera ya
Wanyamapori na kufanya Mapitio ya Sheria na Kanuni mbalimbali zinazosimamia sekta ndogo ya Wanyamapori. Kwa upande mwingine, Wizara itaendelea kuratibu utekelezaji wa mikataba ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa na kushiriki katika maonesho mbalimbali ya kitaifa, kikanda na kimataifa; na kuimarisha mikakati ya kupambana na ujangili na Jeshi la Uhifadhi. - Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea kuratibu utatuzi wa migogoro ya ardhi baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi. Sambamba na hilo, Wizara itatoa mafunzo ya uongozi na upandishwaji vyeo kwa watumishi wanaounda mfumo wa kijeshi na itaendelea kutoa elimu kwa wananchi na vyombo vingine vya ulinzi na usalama kuhusu uwepo wa Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu.
5.3.1.2 Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania – TANAPA
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Shirika litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuwezesha uandaaji wa Mipango ya Matumizi Bora ya Ardhi katika vijiji 30 vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa Nyerere na vijiji 18 vinavyozunguka Hifadhi ya Taifa Serengeti. Shirika pia litachimba mabwawa mapya nane (8); na kukarabati mabwawa matano (5) kwa matumizi ya wanyamapori katika hifadhi za Taifa za Mkomazi, Tarangire, Mikumi, Katavi, Ruaha, Saadani, na Serengeti; kuandaa na kufanya mapitio ya mipango ya ujumla ya usimamizi minne (4) ya hifadhi za Burigi – Chato, Tarangire, Saadani na Kitulo; na kutengeneza mipango sita (6) ya usimamizi wa moto katika hifadhi za Taifa Nyerere, Burigi-Chato, Ibanda-Kyerwa, Mto Ugalla, RumanyikaKaragwe na Kigosi. Pia, Shirika litaboresha maeneo ya malisho ya wanyamapori kwa kudhibiti mimea vamizi katika eneo lenye ukubwa wa hekta 30,331 katika hifadhi za Taifa Nyerere, Saadani, Serengeti, Arusha,
Ibanda – Kyerwa, Mto Ugalla, Mikumi, Mkomazi na Katavi. Vilevile, Shirika litaotesha miti ya asili 100,000 katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro. - Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kuimarisha ulinzi na usimamizi wa hifadhi kwa kuboresha matumizi ya sayansi na teknolojia kwa kununua vifaa 20 vya mawasiliano ya mtandao mpana (LoRa Transmitters), ndege tatu (3) zisizo na rubani na kuweka mfumo wa redio za kidijitali katika vituo vitano (5) katika Kanda ya Magharibi; na hifadhi za Taifa za Nyerere, Ruaha, Udzungwa na Mikumi. Pia, Shirika litanunua vitendea kazi mbalimbali ili kuwezesha operesheni za doria kufanyika kwa tija na ufanisi zaidi.
- Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kushirikisha jamii zinazoishi jirani na hifadhi katika shughuli za uhifadhi kwa kuimarisha vikundi 28 vya ulinzi shirikishi, vikundi 12 vya COCOBA na vikundi vitatu (3) vya klabu za mazingira. Vilevile, elimu ya uhifadhi itaendelea kutolewa katika vijiji 864 vinavyozunguka hifadhi zote za Taifa na kuwezesha vijiji 11 kunufaika na miradi 11 ya ujirani mwema. Pia, Shirika litawezesha ununuzi wa mizinga ya nyuki 800 kwa vikundi 24 vya jamii katika vijiji 24. Katika hatua nyingine, Shirika litaendelea kudhibiti majanga ya moto kwenye hifadhi kwa kutengeneza mipango sita (6) ya usimamizi wa moto kichaa katika hifadhi za Taifa Nyerere, Kigosi, Mto Ugalla, Burigi – Chato, Ibanda – Kyerwa na Rumanyika – Karagwe.
Sambamba na hilo, Shirika litatekeleza Mipango ya Usimamizi wa Moto na kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kwa ajili ya kukabiliana na moto kichaa. - Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kupanua wigo wa uwekezaji kwenye hifadhi za Taifa kwa kutenga maeneo mapya 58 ya ujenzi wa loji na kambi za kitalii kwa ajili ya huduma za malazi zenye vitanda 3,330 katika hifadhi za Taifa Nyerere, Mto Ugalla, Burigi – Chato, Rubondo, Ruaha, Serengeti, Tarangire, Ziwa Manyara, Mikumi, Saadani, Mkomazi na Arusha. Pia, Shirika litajenga malazi ya gharama nafuu yenye jumla ya vitanda 308 kwa ajili ya watalii wa ndani katika hifadhi za Taifa Mikumi, Kilimanjaro, Mkomazi, Rubondo na Nyerere.
- Mheshimiwa Spika, katika kupanua wigo wa utalii na mapato, Shirika litaanzisha utalii wa faru weupe katika hifadhi za Taifa Burigi – Chato na Mikumi. Aidha, Shirika litawezesha kuanza rasmi kwa uwekezaji katika maeneo ya utalii maalum katika Hifadhi ya Taifa Ruaha. Vilevile, Shirika litashiriki maonesho ya utalii katika masoko 19 ya nchi za India, Brazil, Argentina, Qatar, Uholanzi, Ufini, Poland, Urusi, Uswisi, Ujerumani, Israel, Ubelgiji, Marekani, Uhispania, Uingereza, Ufaransa, China, Korea ya
Kusini na Italia. - Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kuboresha miundombinu ya huduma za utalii kwa kujenga barabara mpya zenye urefu wa kilomita 2,500 katika hifadhi za Taifa Arusha, Burigi – Chato, Gombe, Katavi, Kilimanjaro, Kitulo, Mahale, Udzungwa, Manyara, Rubondo, Rumanyika – Karagwe, Ruaha, Mikumi, Nyerere na Serengeti. Aidha, Shirika litajenga njia za utalii zenye urefu wa kilomita 251 na barabara za kutembea kwa miguu zenye urefu wa kilomita 342.5. Vilevile, Shirika litakarabati barabara zenye urefu wa kilomita 6,500; na viwanja vya ndege 17 katika hifadhi za Taifa Ruaha, Mikumi, Nyerere, Saadani, Tarangire, Mkomazi na Serengeti. Pia, Shirika litajenga nyumba 77 za makazi ya watumishi katika hifadhi za Taifa Kigosi, Mto Ugalla, Nyerere, Gombe, Serengeti na Ruaha. Vile vile Shirika litaanzisha Kikosi Kazi cha Ujenzi kwa ajili ya kuhudumia miundombinu ya shirika na iliyo nje ya shirika kibiashara. Kazi nyingine zitakazotekelezwa ni pamoja na ununuzi wa magari tisa (9), seti mbili (2) za mitambo ya kutengeneza barabara, boti moja (1), injini za boti tatu (3) na pikipiki nane (8). Katika hatua nyingine, Shirika litaanza kurusha mubashara (Live streaming) shughuli na matukio ya vivutio vilivyopo katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. 5.3.1.3 Mamlaka ya Usimamizi wa
Wanyamapori Tanzania – TAWA - Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Mamlaka itaendelea kuimarisha ulinzi na usimamizi wa hifadhi kwa kufanya siku doria 284,460 katika mapori ya akiba, mapori tengefu, maeneo ya ardhioevu na Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori. Aidha, watumishi 330 watapatiwa mafunzo ya ukakamavu na utayari ya Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu. Kwa upande mwingine, Mamlaka itanunua trekta moja (1), magari 14 na pikipiki 45 kwa ajili ya doria na shughuli za utawala. Vilevile, Mamlaka itajenga madaraja matano (5) katika Pori la Akiba Lukwati/ Piti, mabwawa mawili (2) katika Pori la Akiba Swagaswaga, vibanda viwili (2) vya walinzi na ujenzi wa miundombinu maalum ya mawasiliano katika Pori la Akiba Maswa na Kanda ya Ziwa.
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka itaendelea kutangaza zao la uwindaji wa kitalii katika maonesho mbalimbali ya kimataifa, hususan katika masoko makubwa ya Marekani, Ufaransa, Uingereza, Ubelgiji, Japan, Falme za Kiarabu na Afrika Kusini; na masoko yanayochipukia ya China na Urusi na nchi za Mashariki ya Mbali. Aidha, Mamlaka itabuni mbinu mbalimbali za kuhakikisha vitalu vya uwindaji wa kitalii vinapata wawekezaji ikiwa ni pamoja na kuanzisha vifurushi kwa bei maalum. Sambamba na hilo, Mamlaka itaendelea kutangaza maeneo ya uwekezaji mahiri (SWICA) ili kuvutia wawekezaji katika maeneo hayo.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Mamlaka itaweka mifumo ya umeme wa jua kwenye miundombinu ya utalii iliyopo katika mapori ya akiba ya Mpanga/Kipengere, Wami – Mbiki, Swagaswaga na Mkungunero. Aidha, Mamlaka itaweka mifumo ya maji kwenye mapori ya akiba ya Mpanga Kipengere, Lukwati/ Piti, Wami – Mbiki, Lukwika/ Lumesule na Maswa; Eneo la Urithi wa Dunia la Kilwa; na jengo la kupumzikia watalii katika Pori la Akiba Mpanga Kipengere. Vilevile, Mamlaka itajenga makasha maalum matano (5) kwa ajili ya kutunzia wanyamapori wakubwa kwenye Pori la Akiba Pande; malango mawili (2) katika mapori ya akiba ya Pande na Ikorongo/ Grumeti; picnic site moja (1) katika Pori La Akiba Liparamba; uzio katika Pori la Akiba Pande, Bustani ya Wanyamapori Ruhila na Pori Tengefu la Ziwa Natron. Pia, Mamlaka itajenga kilomita 37.95 za barabara za utalii katika mapori ya akiba ya Kijereshi na Maswa.
- Mheshimiwa Spika, katika kuvutia uwekezaji na kuimarisha uwindaji wa kitalii ikiwa ni pamoja na kuendeleza programu ya Tanzania – The Royal Tour, Mamlaka itaendelea kutangaza maeneo ya uwekezaji mahiri ili maeneo hayo yapate wawekezaji. Vilevile, Mamlaka itaendelea kuhamasisha ufugaji wa wanyamapori ili watu, makampuni na Mashirika binafsi waweze kuanzisha ranchi, bustani na mashamba ya wanyamapori. Sambamba na hilo, Mamlaka itaanzisha kitengo maalum kwa ajili ya kuwezesha ukamataji wa wanyamapori wa mbegu ili kufanyika kitalaam na kwa gharama nafuu.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Mamlaka itaandaa mipango ya usimamizi ya jumla (GMP) ya mapori mapya ya Maswa, Moyowosi na Rungwa kwa lengo la kuimarisha usimamizi wa mapori hayo. Aidha, Mamlaka itakarabati kiwanja cha ndege katika Pori la Akiba Moyowosi; ofisi ya Kanda ya Kaskazini; nyumba moja ya mtumishi Kunduchi; na ujenzi wa vimbweta vinne (4) katika Pori la Akiba Pande. Vilevile, Mamlaka itaandaa mpango wa maendeleo ya utalii; mpango wa masoko ya utalii; mwongozo wa utoaji wa quota za uwindaji; na viwango vya miundombinu ya utalii ndani ya mapori ya akiba. Aidha, Mamlaka itaondoa magugu maji kwenye eneo la ekari sita (6) katika Pori la Akiba Uwanda; na kusafisha kilomita 460 za barabara kwenye mapori ya akiba Maswa, Igombe, Inyonga, Moyowosi na Rungwa.
- Mheshimiwa Spika, katika kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza tija, Mamlaka itaanza ujenzi wa ofisi ya Makao Makuu Jijini Dodoma; kujenga ofisi mbili (2) kwa ajili ya mapori ya akiba Msanjesi na Igombe; maghala matano (5) ya silaha; nyumba 13 za watumishi katika mapori ya akiba Mpanga/ Kipengere (1), Selous (2), Maswa (2), Igombe (4) na Rukwa (4). Aidha, Mamlaka itajenga vituo vya askari vitano (5) katika mapori ya akiba ya Wami – Mbiki (2), Swagaswaga (1), Ugalla (1) na Pori Tengefu Lunda – Mkwambi (1); na karakana tatu (3) katika Kanda ya Kaskazini na mapori ya akiba ya Maswa na Rukwa.
5.3.1.4 Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro – NCAA
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Mamlaka itaendelea kuimarisha ulinzi na uhifadhi wa maliasili na malikale kwa kufanya siku doria 36,000; operesheni maalum sita (6); kutoa mafunzo kwa watumishi 300; na kununua vitendea kazi mbalimbali kwa ajili ya kuimarisha ulinzi katika eneo la hifadhi. Katika hatua nyingine, Mamlaka itaendelea kuimarisha ushirikiano na jamii zinazopakana na Hifadhi kwa kufanya mikutano 175 ya ujirani mwema kwa lengo la kutoa elimu ya uhifadhi na kutatua migogoro. Vilevile, Mamlaka itaendelea kuwezesha miradi ya maendeleo kwa halmashauri zinazopakana na eneo la hifadhi.
- Mheshimiwa Spika, Mamlaka itaendelea kuboresha nyanda za malisho kwa kudhibiti mimea vamizi kupitia moto mpango, kung’oa, kufyeka na kuwezesha utafiti. Zoezi hili litafanyika katika eneo lenye ukubwa wa hekta 5,000 lililoathirika zaidi katika maeneo ya Ndutu na Kreta ya Ngorongoro. Katika hatua nyingine, Mamlaka itaotesha miche ya miti 460,000 ambayo itapandwa katika maeneo yaliyoathirika na ukataji miti na mingine itagawiwa kwa jamii inayozunguka Hifadhi. Sambamba na hilo, Mamlaka itasafisha mpaka wenye urefu wa kilomita 200 na kusimika vigingi 50 kwenye eneo hilo kwa lengo la kuzuia moto kichaa na uvamizi wa maeneo ya hifadhi. Aidha, katika eneo la Oldeani, Mamlaka itaweka uzio wa umeme rafiki kwa mazingira wenye urefu wa kilomita 30 kwa lengo la kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu.
- Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza na kukuza utalii, Mamlaka itajenga barabara zenye jumla ya kilomita 55.5. Kati ya hizo, kilomita 29.5 zitajengwa kutoka Loduare hadi Golini kwa kiwango cha tabaka gumu la zege, kilomita 25 kutoka Ndutu hadi Endulen kwa kiwango cha changarawe na kilomita moja (1) kutoka makutano ya Seneto na Kreta ya Ngorongoro kwa kiwango cha tabaka gumu la mawe. Katika hatua nyingine, Mamlaka itaendelea kufanya ukarabati wa mara kwa mara kwenye mtandao wa barabara zenye jumla ya kilomita 554 ndani ya hifadhi.
- Mheshimiwa Spika, katika kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama kwa matumizi ya wageni na askari, Mamlaka itajenga mfumo wa maji safi katika eneo la Ngoitoktok; na kukarabati mifumo ya maji katika vituo vya askari vya Mbulumbulu, Endamagha, Lemala, Oloirobi, Seneto, Makoromba na Lerai. Vilevile, Mamlaka itaendelea na soroveya itakayowezesha uchimbaji wa visima vitano (5) vya maji katika maeneo ya Jiwe la Nasera, Olduvai, Ndutu, Laetoli na Bonde la Faru. Katika jitihada za kuvutia uwekezaji wenye tija, Mamlaka itaendelea kubainisha maeneo ya uwekezaji wa Loji zenye hadhi ya kimataifa. Mpango huu unatarajiwa kuongeza vitanda zaidi ya 480. Aidha, Mamlaka itaendelea kushiriki katika matukio na maonesho mbalimbali ya utalii na uhifadhi ndani na nje ya nchi. Vilevile, Mamlaka itaendelea kuboresha na kutumia njia za kidigitali ikiwemo Ngorongoro live streaming kutangaza mubashara vivutio na matukio mbalimbali kutoka hifadhini.
- Mheshimiwa Spika, katika kuongeza thamani ya vituo vya malikale na idadi ya wageni wanaovitembelea, Mamlaka itakarabati njia za watembea kwa miguu katika vituo vya Laetoli, Amboni Tanga na Olduvai na kuboresha makumbusho katika vituo vya Olduvai, Kimondo cha Mbozi, Laetoli na Mary Leakey. Aidha, Mamlaka itaendesha mafunzo katika vyuo vitano (5), shule tano (5) za sekondari na shule tano (5) za msingi katika wilaya za Karatu, Monduli, Mbozi na Tanga Mjini ili kutoa elimu na kutangaza utalii wa miamba na malikale. Katika kuboresha huduma na maisha ya wananchi waishio ndani ya eneo la hifadhi, Mamlaka itaendelea kutekeleza programu za kuelimisha na kuhamasisha wenyeji waishio ndani ya Hifadhi kuhama kwa hiari kwenda kwenye maeneo ya nje ya Hifadhi yakiwemo maeneo maalum yaliyotengwa. Aidha, Mamlaka itaendelea na ujenzi wa ofisi za makao makuu katika eneo la Kemyn, Wilaya ya Karatu. Vilevile, Mamlaka itanunua gari maalum litakalowezesha kubeba wastani wa watalii 30 wakati wa kutembelea vivutio ndani ya Hifadhi.
5.3.1.5 Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania – TAWIRI
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Taasisi itaendelea kuboresha miundombinu yake ikiwemo: kujenga jengo la makao makuu na nyumba tatu (3) za watumishi, kununua magari matatu (3) na vifaa vya maabara na kukarabati nyumba tatu (3) za watumishi na maabara ya Kituo cha Utafiti Serengeti. Aidha, Taasisi itaendelea kutekeleza tafiti za kimkakati zinazohusu migongano baina ya binadamu na wanyamapori, mimea vamizi katika maeneo yaliyohifadhiwa, chura wa Kihansi katika eneo lake la asili, utalii na maisha ya jamii Kusini mwa Tanzania, magonjwa ya wanyamapori na yanayoambukiza wanyama na binadamu, mimea tiba pamoja na nyuki na mazao yake.
- Mheshimiwa Spika, Taasisi itafanya sensa tatu (3) za wanyamapori katika maeneo ya Mfumo Ikolojia Nyerere – Selous – Liparamba – Mikumi, Mfumo Ikolojia Saadani – Wami Mbiki na Pori la Akiba Swagaswaga. Aidha, Taasisi itaendelea kutoa elimu na kusambaza matokeo ya tafiti zinazofanywa na Taasisi. Sambamba na hilo, Taasisi itaratibu kongamano la Kisayansi la 14 la Kimataifa, itatoa elimu ya mbinu rafiki za kukabiliana na migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu pamoja na elimu ya mbinu bora za ufugaji nyuki. Vilevile, Taasisi itachapisha matokeo ya tafiti mbalimbali katika majarida ya kisayansi.
5.3.1.6 Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori – CAWM Mweka
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Chuo kitaendelea kutoa mafunzo katika ngazi ya Cheti cha Msingi, Astashahada, Stashahada, Shahada na Stashahada ya Uzamili katika fani ya uhifadhi wanyamapori na utalii pamoja na mafunzo ya muda mfupi. Aidha, Chuo kitakamilisha ujenzi wa jengo la mafunzo na kujenga nyumba mbili (2) za watumishi. Vilevile, Chuo kitakarabati nyumba 10 za watumishi, hosteli saba (7) na kuweka samani na heater za umeme 21 katika hosteli. Sambamba na hilo, Chuo kitajenga maegesho ya magari, uzio wa ukuta wenye urefu wa mita 600, vyoo, madarasa na kuweka miundombinu ya maji katika maeneo ya mafunzo kwa vitendo Kwakuchinja, Wilaya ya Babati na Arash, Wilaya ya Ngorongoro.
5.3.1.7 Kituo cha Mafunzo ya Uhifadhi wa Maliasili kwa Jamii, Likuyu-
Sekamaganga
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Kituo kitaendelea kutoa mafunzo kwa wanafunzi 162 wakiwemo Askari Wanyamapori wa Vijiji (80), Waongoza Watalii (50) na Viongozi na wajumbe wa Kamati za Vijiji (32). Aidha, kitaanzisha kozi ya Astashahada ya Utalii na Waongoza Watalii (NTA 5). Vilevile, Kituo kitarabati jengo la utawala, nyumba moja (1) ya watumishi na bweni moja (1). Sambamba na hilo, Kituo kitatoa ushauri wa kitaalam kwa Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori kuhusu masuala mbalimbali ya uhifadhi wa wanyamapori.
5.3.1.8 Taasisi ya Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi - Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Taasisi itadahili wanafunzi 400 katika fani za uhifadhi wa wanyamapori, himasheria na uongozaji wa watalii na usalama. Aidha, Taasisi itakamilisha taratibu za kuhuisha usajili wake NACTE, kuandaa mtaala kwa ajili ya uanzishwaji wa kozi ya Stashahada katika Fani ya Uhifadhi wa Wanyamapori, Uongozaji Watalii na Usalama; na kuweka samani katika maktaba. Vilevile, itakamilisha ujenzi wa uzio wa chuo, kuboresha miundombinu ya TEHAMA na kuanzisha shamba la wanyamapori ili kuongeza mapato pamoja na kuimarisha utoaji mafunzo kwa vitendo.
5.3.1.9 Mfuko wa Kuhifadhi Wanyamapori Tanzania – TWPF
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Mfuko utaendelea kuwezesha operesheni maalum za kuzuia ujangili, uhakiki na ulipaji wa kifuta machozi na kifuta jasho; utatuzi wa migogoro kati ya wananchi na maeneo yaliyohifadhiwa na upandishwaji hadhi wa mapori tengefu matano (5) kuwa mapori ya akiba. Aidha, Mfuko utaendelea kuwezesha utoaji wa elimu na vitendea kazi kwa wilaya tano (5) zenye matukio mengi ya wanyamapori wakali na waharibifu; mapitio ya Sera, Sheria na Kanuni za Sekta ya wanyamapori; kujenga uwezo wa watumishi; uratibu na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Wanyamapori ya mwaka 2000; na kuwezesha Jeshi la Uhifadhi wa Wanyamapori na Misitu pamoja na kudhibiti ujangili. 5.3.2 Sekta ya Misitu na Nyuki
5.3.2.1 Idara ya Misitu na Nyuki
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara itaandaa mipango kazi ya kutekeleza Sera za Taifa za Misitu; na Ufugaji Nyuki. Aidha, Wizara itaandaa mikakati ya Taifa ya Upandaji na Uendeshaji wa Miti ya Mianzi; Kilimo Mseto; Nishati ya Mkaa; Upandaji Miti; na Uwekezaji katika Sekta ya Misitu na Ufugaji Nyuki. Aidha, Wizara itaandaa Mwongozo wa Usimamizi wa Misitu ya Asili na Mashamba ya Miti; na Mwongozo wa Usimamizi wa Nyuki wasiouma. Vilevile, Wizara itafanya mapitio ya mwongozo wa Uvunaji endelevu na Biashara ya Mazao ya Misitu; Sheria ya Misitu Sura 323; na Sheria ya Ufugaji Nyuki Sura 224. Kwa upande mwingine, Wizara itaendelea kufanya tathmini ya mchango wa Sekta ya Misitu na Ufugaji Nyuki katika pato la Taifa kwa kutumia mfumo wa Uchumi wa Kijani (green accounting). Vilevile, Wizara itatafsiri kwa lugha ya Kiswahili na kusambaza miongozo mbalimbali ya Sekta ya Misitu na Ufugaji Nyuki ili kutoa uelewa mpana kwa umma kuhusu miongozo hiyo.
- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa jamii inaendelea kushiriki kwenye uhifadhi na uendelezaji wa rasilimali za misitu na nyuki, Wizara itaandaa mkutano mmoja (1) wa wadau wa misitu na nyuki; kuwezesha uanzishaji wa hifadhi za nyuki za vijiji vitano (5); kutoa mafunzo ya mbinu bora za ufugaji nyuki kwa vikundi vitano (5) vya wafugaji nyuki; kuandaa jukwaa la wataalam wa fani ya ufugaji nyuki; na kuwezesha vyama vya ushirika wa wafugaji nyuki kuandaa mikataba ya ufugaji nyuki katika maeneo ya hifadhi. Aidha, Wizara itafanya ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya misitu na nyuki inayotekelezwa na Wizara. Vilevile, Wizara itaratibu vikao vinne (4) vya Kamati ya Ushauri wa Misitu – NAFAC, vikao vitatu (3) vya Kamati ya Ushauri wa Ufugaji Nyuki – NABAC na vikao vinne (4) vya Kamati Endeshi ya utekelezaji wa mpango kazi wa mazao ya misitu yaliyohandisiwa. Pia, Wizara itaratibu Siku ya Upandaji Miti Kitaifa, Siku ya Misitu Duniani na Siku ya Nyuki Duniani.
5.3.2.2 Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wakala utaandaa Mipango ya Usimamizi wa Misitu 57 yenye ukubwa wa hekta 1,703,202 na kufanya mapitio ya Mipango ya Usimamizi wa misitu ya hifadhi 111. Vilevile, Wakala utaendesha jumla ya siku doria 212,400 na operesheni maalum 355 katika maeneo ya hifadhi za misitu na nyuki. Katika hatua za kuimarisha ulinzi na kutatua migogoro katika hifadhi za misitu na nyuki, Wakala utapima mipaka ya misitu 133 na kuhakiki mipaka yenye urefu wa kilomita 33,107; kusafisha mipaka yenye kilomita 5,746 na njia za kuzuia moto zenye urefu wa kilomita 6,000; kuweka vigingi 1,369 na mabango 2,133; na kujenga minara miwili (2) mipya ya kubaini matukio ya moto na kukarabati mingine 11. Aidha, Wakala utapandisha hadhi maeneo ya ardhi huria tisa (9) kuwa misitu ya hifadhi ya Taifa.
- Mheshimiwa Spika, Wakala utakarabati kilomita 356.5 za njia za watalii na kilomita 157.3 za barabara za msituni; na kuandaa ramani za vivutio vya kiikolojia katika misitu ya hifadhi. Aidha, ili kuvutia utalii ikolojia, Wakala utajenga ofisi moja (1), mabanda nane (8) ya kupumzika watalii, malango matatu (3) na vyoo 15; na kukarabati barabara yenye urefu wa kilometa 210 kwa ajili ya ulinzi wa misitu na michezo ya kitalii. Aidha, Wakala utakarabati miundombinu katika vituo sita (6) ikiwemo kilometa
10.5 ya njia za kutembea kwa miguu, mageti matatu (3) na mabenchi ya kukalia 60 katika vituo vya Michoro ya Miambani Kolo – Kondoa, Mji Mkongwe – Bagamoyo, Tembe la Kwihara – Tabora, Magofu ya Tongoni – Tanga na Kaole – Bagamoyo. - Mheshimiwa Spika, kutokana na mahitaji makubwa ya malighafi ya mazao ya misitu nchini, Wakala utaongeza uzalishaji wa mbegu za miti nchini kwa kuongeza vyanzo vipya vya mbegu vitatu (3) na kuzalisha tani 24 za mbegu na miche ya miti 33,156,000. Aidha, Wakala utapanda miti katika eneo lenye ukubwa wa hekta 7,636 na kurudishia miti iliyokufa kwenye eneo la hekta 2,019. Aidha, Wakala utapalilia eneo lenye hekta 32,677, kupogolea hekta 11,421 na kupunguzia miti kwenye hekta 3,331. Katika hatua nyingine, Wakala utaanzisha upandaji wa miti aina ya mpira katika Shamba la Miti Rondo na kuandaa Mipango ya Usimamizi wa mashamba ya miti 18 yenye jumla ya ukubwa wa hekta 418,119. Vilevile, katika kuhakikisha usimamizi thabiti wa mashamba ya miti ya Serikali na upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu nchini, Wakala utakamilisha maandalizi na kuanza utekelezaji wa Mkakati wa Usimamizi na Uendelezaji wa Mashamba ya Miti ya Serikali wa miaka 30 (2021 – 2051).
- Mheshimiwa Spika, Wakala utatoa elimu ya kupambana na kuzuia moto kwa jamii katika vijiji 54 pamoja na kuanzisha bustani ya miti iliyo hatarini kutoweka katika eneo la Chamwino. Aidha, Wakala utaendelea kulinda hekta 158,100 za hifadhi za mikoko na kupanda miche katika eneo la hekta 83. Vilevile, Wakala utatatua migogoro ya mipaka katika hifadhi za misitu 13 na kuwezesha kuandaa mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 40. Pia, Wakala utaendeleza mashamba ya nyuki mawili (2); kuanzisha shamba jipya moja (1) la ufugaji nyuki la Kipembawe katika Wilaya ya Chunya lenye ukubwa hekta 21,790; kuendeleza viwanda vitatu (3) vya nyuki; kutoa elimu kwa wafugaji nyuki 848; kuzalisha tani 49 za asali, tani 2.9 za nta na kilo 50 za chavua; na kuchonga mizinga ya nyuki 1,200.
- Mheshimiwa Spika, Wakala utaboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi wa kazi kwa kununua magari 34, pikipiki 46, basi moja (1), malori matatu (3), boti mbili (2), mtambo mmoja (1) na kujenga majengo nane (8) ya ofisi. Aidha, Wakala utawezesha watumishi 70 kupata mafunzo ya muda mrefu na watumishi 493 kupata mafunzo ya muda mfupi. Vilevile, Wakala utaendeleza jitihada ya kuboresha shughuli za kijeshi ambapo utatoa mafunzo ya uongozi wa kijeshi kwa watumishi 300.
5.3.2.3 Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania – TAFORI
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Taasisi itajenga jengo la Kituo cha Utafiti cha Tabora; kukarabati majengo mawili (2) ya Vituo vya Utafiti vya Kibaha na Malya; na vifaa vya maabara. Aidha, Taasisi itafanya tafiti za kimkakati sita (6) zenye lengo la kutathmini rasilimali za misitu zilizopo; kubaini mchango wa sekta ya misitu kwenye pato la Taifa kwa kutumia Uchumi wa Kijani; na kutathmini miti ya asili inayotumika kibiashara iliyo hatarini kutoweka na kubaini namna ya kuizalisha, kuipanda na kuitunza. Aidha, Taasisi itasimamia uboreshaji wa Mfumo wa Taarifa za Usimamizi wa Misitu na Nyuki (Forest and Beekeeping Management Information System) ili kuongeza takwimu zitokanazo na miradi na programu mbalimbali za utafiti nchini. Sambamba na hilo, Taasisi itaratibu Kongamano la Kisayansi la tatu (3) la Kimataifa na kuchapisha matokeo ya tafiti mbalimbali katika majarida ya kisayansi.
5.3.2.4 Vyuo vya Taaluma ya Misitu na Ufugaji
Nyuki
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Chuo cha Viwanda vya Misitu kitadahili wanafunzi 400 wa mafunzo ya muda mrefu kwa ngazi ya Astashahada na Stashahada; na kuendesha mafunzo ya ufundi sanifu na ufundi stadi wa teknolojia ya viwanda vya misitu. Aidha, Chuo kitajenga bweni; kukarabati madarasa, ofisi na nyumba za watumishi; na kitanunua vifaa vya mafunzo na magari. Kwa upande mwingine, Chuo cha Mafunzo ya Ufugaji Nyuki kitadahili wanafunzi 450 wa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya Astashahada na Stashahada; na kuendelea kuimarisha miundombinu ya kufundishia kwa kujenga jengo la maabara, maktaba, kununua kompyuta na kuendelea na awamu ya pili ya ujenzi wa uzio wa Chuo. Pia, Chuo kitaanzisha Utalii wa Nyuki (Api-tourism) katika manzuki za Chuo na kuimarisha karakana kwa kununua vifaa na mashine. Katika hatua nyingine, Chuo cha Misitu Olmotonyi kitadahili wanafunzi 900 wa mafunzo ya muda mrefu katika ngazi ya
Astashahada na Stashahada. Aidha, Chuo kitakarabati mabweni sita (6), nyumba za wakufunzi 10; na kununua magari mawili (2) na kompyuta 50.
5.3.2.5 Mfuko wa Misitu Tanzania – TaFF
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Mfuko utaendelea kuwezesha utekelezaji wa miradi 209 inayoendelea na miradi mipya 180 ya uanzishwaji wa vitalu vya miti; upandaji miti mashuleni; ufugaji nyuki; ruzuku maalum kwa ajili ya kuendeleza mashamba ya miti; na miradi ya utafiti yenye lengo la uhifadhi, usimamizi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali za misitu na kuongeza thamani ya mazao ya misitu na nyuki. Vilevile, Mfuko utawezesha TAFORI kufanya na kuratibu tafiti sita (6) za kimkakati zenye lengo la kuendeleza sekta ya Misitu na Nyuki. Pia, Mfuko utawezesha ununuzi wa magari mawili (2) kwa ajili ya kuboresha ukusanyaji wa mapato yatokanayo na mazao ya misitu na nyuki; na kuwezesha kazi ya mapitio ya sheria ya misitu kwa ajili ya kuweka vifungu vya kuimarisha Mfuko ikiwemo kuingiza suala la ufugaji nyuki. Aidha, Mfuko utawezesha kufanyika kwa vikao vya Kamati ya Ushauri wa Misitu – NAFAC; na vikao vya Kamati ya Ushauri wa Ufugaji Nyuki – NABAC. 5.3.3 Sekta ya Utalii
5.3.3.1 Idara ya Utalii
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka fedha 2022/2023, Wizara itakamilisha Mkakati wa Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Utalii ya Mwaka 1999; na kuandaa Programu ya Maendeleo ya Utalii nchini. Katika hatua za kuendeleza mazao ya utalii nchini, Wizara itabainisha maeneo ya fukwe katika maziwa makuu ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa kwa ajili ya uwekezaji na uendelezaji wa shughuli za utalii. Katika hatua nyingine, Wizara itaendelea kupanga huduma za malazi katika daraja za ubora katika mikoa ya Kilimanjaro, Mbeya na Mwanza. Vilevile, Wizara itaendelea kutoa mafunzo kwa wadau wa utalii kuhusu matumizi ya mfumo wa kielektroniki wa kupanga huduma za malazi katika daraja za ubora (AserT) pamoja na kufanya ukaguzi kwa watoa huduma za utalii nchini. Sambamba na hilo, Wizara itabaini vivutio vya utalii na fursa za uwekezaji wa shughuli za utalii nchini katika mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Morogoro na Tanga. Aidha, Wizara itafanya mikutano mitatu (3) ya wadau yenye lengo la kuhamasisha wadau kuwekeza na kuendeleza mazao mbalimbali ya utalii. Aidha, Wizara itaratibu maadhimisho ya Siku ya Utalii Duniani pamoja na kuendelea kushiriki katika matukio mbalimbali ya utangazaji na uendelezaji utalii ndani na nje ya nchi.
5.3.3.2 Bodi ya Utalii Tanzania – TTB
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Bodi ya Utalii Tanzania itaandaa mkakati wa uendelezaji wa utalii wa mikutano na matukio ambao unalenga kuvutia matukio mbalimbali ya kimataifa kufanyika nchini. Aidha, Bodi itaandaa onesho la sita (6) la Swahili International Tourism Expo (S!TE); na kuratibu Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Kanda ya Afrika utakaofanyika tarehe 05 hadi 07 Oktoba, 2022 Jijini Arusha. Matukio hayo yatatoa fursa za kutangaza na kuendeleza utalii, kuvutia uwekezaji na kukutanisha wadau wa utalii wa ndani na nje ya nchi kupitia mikutano ya kibiashara.
- Mheshimiwa Spika, Bodi itaratibu ziara maalum 15 za mafunzo kwa ajili ya makundi maalum ya wadau ikiwemo wakala wa biashara za utalii, waandishi wa habari, watu mashuhuri, mabalozi wa hiari wa utalii na wawekezaji katika masoko mbalimbali ya utalii. Katika juhudi za kutangaza utalii ndani na nje ya nchi, Bodi itaendelea kuandaa na kusambaza nyenzo za utangazaji utalii pamoja na kutumia mbinu za kidigitali na mitandao ya kijamii. Aidha, Bodi itaendeleza programu ya utalii wa utamaduni na kutangaza mazao ya utalii ikiwemo uwindaji wa kitalii, utalii ikolojia na utalii wa malikale. Sambamba na hilo, Bodi itaendelea kushirikiana na vituo mbalimbali vya habari katika kuandaa na kurusha vipindi maalum na makala za utangazaji utalii.
- Mheshimiwa Spika, Bodi itaendelea kutekeleza Mkakati wa Utangazaji Utalii Kimataifa wa mwaka 2020 – 2025 kwa kushiriki katika maonesho ya utalii ya kimataifa na road show za utalii. Juhudi hizo zinalenga kuitangaza Tanzania katika masoko ya utalii ya msingi, kimkakati na yale yanayoibukia kwenye mabara ya Amerika, Ulaya, Afrika, Mashariki ya Kati, Asia na Pasifiki. Aidha, Bodi itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kuratibu na kushiriki katika matukio yanayohusisha utangazaji utalii ndani ya nchi. Hatua hizi zinalenga kuendeleza utangazaji wa vivutio vya utalii ndani na nje ya nchi, sambamba na kuendeleza juhudi zilizoanzishwa kupitia programu ya Tanzania – The Royal Tour.
5.3.3.3 Chuo cha Taifa cha Utalii – NCT
- Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Chuo kitadahili wanafunzi 1,537 katika ngazi ya Astashahada, Stashahada pamoja na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa wadau 437 katika mnyororo wa utalii. Aidha, Chuo kitanunua vitendea kazi mbalimbali na kufanya ukarabati wa miundombinu ya kutolea mafunzo katika Kampasi ya Bustani, Temeke na Arusha. Vilevile, kitafanya tafiti na kutoa ushauri katika fani ya utalii, ukarimu na uratibu matukio. Katika hatua nyingine, Chuo kitajenga jengo lenye madarasa, ukumbi na jiko la kujifunzia katika Kampasi ya Arusha pamoja na kuanza ujenzi wa Kampasi Mpya ya Mwanza. Pia, Chuo kitatekeleza programu za kimkakati za kukuza ujuzi ikijumuisha uanagenzi, utarajali na urasimishaji wa ujuzi uliopatikana katika mfumo usio rasmi (recognition of prior learning). Aidha, Chuo kitaanzisha shahada ya kwanza katika fani ya Utalii na Ukarimu na kuanzisha lugha za kigeni kama Kichina, Kihispania na Kijerumani. 5.3.4 Sekta ya Mambo ya Kale
5.3.4.1 Idara ya Mambo ya Kale
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara itafanya tathmini ya utekelezji wa Sera ya Malikale ya mwaka 2008 na kuandaa mkakati wa utekelezaji; na kufanya mapitio ya Sheria ya Mambo ya Kale Sura 333 na Sheria ya Makumbusho ya Taifa Sura 281. Aidha, Wizara itaandaa kanuni na miongozo ya uhifadhi na utafiti wa maeneo ya malikale; vigezo vya kutambua rasilimali za Urithi wa Utamaduni kuwa Urithi wa Taifa; na mpango wa kitaifa wa usimamizi na uendelezaji wa rasilimali za urithi wa utamaduni. Katika hatua nyingine, Wizara itafanya ufuatiliaji wa hali ya uhifadhi kwa vituo na maeneo ya malikale; na kukagua maeneo ya urithi wa utamaduni wa Taifa yaliyopo katika mikoa ya Mbeya, Iringa, Morogoro, Dodoma na Kilimanjaro kwa ajili ya kuboresha orodha ya kitaifa ya maeneo ya Urithi wa Utamaduni wa Taifa.
- Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine, Wizara itapima maeneo saba (7) ya malikale kwa lengo la kupata hati miliki na kupunguza migogoro ya mipaka; na kutengeneza mfumo wa maombi ya vibali vya utafiti. Aidha, itashiriki mikutano na maonesho ya Kikanda na Kimataifa inayohusiana na uhifadhi na uendelezaji wa malikale; Vilevile, itafanya vikao vitano (5) vya wadau kuhusu uhifadhi wa malikale na urithi wa utamaduni.
5.3.4.2 Shirika la Makumbusho ya Taifa – NMT
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Shirika litafanya tathmini ya Uhifadhi, kuainisha thamani za kitamaduni; na kufanya ukarabati wa majenzi ya kale 22 katika maeneo ya Pangani – Tanga, Kua – Mafia, Mikindani – Mtwara na Kigamboni – Dar es Salaam. Aidha, Shirika litaweka Onesho la Kudumu la Historia katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Dar es Salaam. Vilevile, Shirika litaendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba za asili kwa kufuata ramani ya Tanzania katika Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam ambapo nyumba za kaya tatu (3) zitajengwa. Katika hatua nyingine, litaendelea kuimarisha mifumo ya TEHAMA katika shughuli za utafiti, uhifadhi na maonesho. Pia, Shirika litaendelea kutekeleza Mpango wa Miaka 10 wa Kuenzi na Kusherehekea Urithi wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
- Mheshimiwa Spika, Shirika litaendelea kutangaza vivutio vya malikale na Makumbusho kidigitali na kuhamasisha utalii wa ndani kwa kutumia maonesho tano (5) na matamasha saba (7).
Sambamba na hilo, Shirika litafanya tafiti nne (4) na kukusanya na kuhifadhi mikusanyo ya asili na kiutamaduni 220. Vilevile, Shirika litaendelea kuhamasisha, kusimamia na kushauri kuhusu uanzishwaji wa makumbusho mpya za watu na taasisi binafsi. Pia, Shirika litaendelea kufanya programu mbalimbali za kujenga uelewa kwa vizazi vya sasa kuhusu uzalendo, uhifadhi na uendelezaji wa tamaduni na urithi wa Asili katika mikoa ya Mara, Simiyu na Singida.
5.3.4.3 Mfuko wa Mambo ya Kale – NAF
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2022/2023, Mfuko utawezesha ufuatiliaji wa mikusanyo na malikale ndani na nje ya nchi; kukusanya taarifa za maeneo mapya ya malikale katika mikoa ya Katavi, Simiyu, Njombe, Dodoma, Kigoma na Lindi. Aidha, Mfuko utawezesha ufuatiliaji wa taarifa za kiutafiti katika maeneo ya malikale; uandaaji wa miongozo ya uanzishaji wa Makumbusho nchini, mpango wa uhifadhi wa mji wa kihistoria wa Bagamoyo na Pangani na mpango wa uhifadhi na usimamizi wa njia ya kati ya biashara ya utumwa na vipusa. Vilevile, Mfuko utawezesha utoaji wa elimu kwa wadau kuhusu uhifadhi na uendelezaji wa malikale.
5.4 Miradi ya Maendeleo
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara inakadiria kutumia Shilingi 180,436,165,000.00 kutekeleza Miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 109,879,593,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 70,556,572,000.00 ni fedha za nje. Fedha za maendeleo Shilingi 180,436,165,000.00 zinajumuisha Shilingi 71,684,572,000.00 kwa ajili ya kutekeleza miradi tisa (9) ya Idara na Vitengo viliyo chini ya Wizara; Shilingi 108,751,593,000.00 za Miradi itakayotekelezwa na Taasisi (TANAPA, NCAA, TAWA na NCT).
- Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara itatekeleza miradi ya maendeleo kama ifuatavyo: –
i. Mradi wa Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (Resilient Natural Resources Management for Tourism and Growth Project – REGROW);
ii. Mradi wa Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public Finance Management and Reform Programm VI);
iii. Mradi wa Kukabiliana na Ujangili na Biashara
Haramu ya Wanyamapori (Support to Combat
Poaching and Illegal Wildlife Trade in Tanzania);
iv. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Maeneo ya Hifadhi, Mapori ya Akiba na Kikosi Dhidi Ujangili;
v. Mradi wa Panda Miti Kibiashara (Private Plantation and Value Chain in Tanzania);
vi. Mradi wa Kujenga Uwezo wa Taasisi na Mafunzo ya Misitu na Ufugaji Nyuki (Capacity Building in Forestry and Beekeeping);
vii. Mradi wa Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki (Support to Beekeeping Value
Chain Programme – BEVAC); na
viii. Mradi wa Uendelezaji wa Utalii wa Mikutano na Matukio (MICE Tourism Development Project).
6.0 SHUKRANI
- Mheshimiwa Spika, ninapenda kutumia nafasi hii tena kukushukuru wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika na Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge kwa ushirikiano mnaotoa katika kuliongoza Bunge letu Tukufu. Pia, ninawashukuru wadau wote kwa ushirikiano wao katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Kipekee, nizishukuru nchi marafiki, washirika wa maendeleo, mashirika ya kimataifa, taasisi za kiserikali pamoja na wadau wengine wakiwemo sekta binafsi kwa ushirikiano wao katika kuendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii na uchumi wa nchi kwa ujumla. Nachukua fursa hii kutaja baadhi yao kama ifuatavyo: Serikali za Canada, China, Falme za Kiarabu, Korea Kusini, Marekani, Morocco, Namibia, Norway, Ubelgiji, Ufaransa, Ufini, Ujerumani, Uswisi na Jumuiya ya Umoja wa Nchi za Ulaya. Mashirika na taasisi za Kimataifa ni pamoja na: AfDB, AWF, AWHF, FAO, FZS, GEF, GIZ, ICCROM, ICOM, ICOMOS, ILO, IMF, ITC, IUCN, KfW, NORAD, PAMS Foundation, Trade Aid, UNDP, UNESCO, UNWTO, USAID, WCS, WHC, WTTC, World Bank, Wild Aid, WMF na WWF. Aidha, ninapenda kuwashukuru wananchi wote walioshiriki kikamilifu katika shughuli za uhifadhi wa maliasili, malikale na uendelezaji utalii. Nitumie fursa hii kuwaomba wadau wote kuendelea kutoa ushirikiano kwa Wizara ili iweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.
7.0 MAOMBI YA FEDHA KWA MWAKA 2022/2023
- Mheshimiwa Spika, ninaomba Bunge lako
Tukufu liidhinishe jumla ya Shilingi
624,142,732,000.00 kwa matumizi ya Fungu 69 –
Wizara ya Maliasili na Utalii kwa mwaka wa fedha 2022/2023. Kati ya fedha hizo, Shilingi 443,706,567,000.00 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Shilingi 180,436,165,000.00 ni za miradi ya maendeleo. - Mheshimiwa Spika, fedha za matumizi ya kawaida zinajumuisha Shilingi 175,884,707,000.00 za mishahara na Shilingi 267,821,860,000.00 za matumizi mengineyo. Aidha, fedha za miradi ya maendeleo zinajumuisha Shilingi 109,879,593,000.00 fedha za ndani na Shilingi 70,556,572,000.00 fedha za nje.
8.0 HITIMISHO
- Mheshimiwa Spika, napenda kuhitimisha kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwako wewe na Waheshimiwa Wabunge wote kwa kunisikiliza. Aidha,
Hotuba hii inapatikana pia katika tovuti ya Wizara ya
Maliasili na Utalii: www.maliasili.go.tz - Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
ORODHA YA MAJEDWALI
Jedwali Na. 1: Maduhuli ya Wizara kwa mwaka 2020/2021 na Makadirio kwa mwaka wa fedha 2022/2023
Na. Taasisi Makadirio na Makusanyo kwa Mwaka 2021/2022
(hadi Aprili, 2022) Makadirio kwa mwaka
2022/2023
Makusanyo kwa mwaka
2020/2021 Makadirio kwa mwaka
2021/2022 Makusanyo hadi Aprili, 2022 %
(i) (ii) (iii) (iv) (vi) (vii)
A: Maduhuli yaliyokusanywa kupitia Mfumo wa MNRT Portal
- Wizara 22,657,242,000 22,657,242,000 6,168,830,213 27 9,507,352,000
- Taasisi 172,136,947,241 181,051,970,727 135,812,770,980 75 184,397,895,325
- Mifuko 23,752,412,851 7,622,061,000 4,461,854,701 59 7,586,918,000
JUMLA 218,546,602,092 211,331,273,727 146,443,455,894 69 201,492,165,325 B: Maduhuli yaliyokusanywa kupitia Mifumo ya TEHAMA ya Wizara kwenda TRA - TANAPA 363,899,596,000 253,704,221,522 140,231,422,143.61 55 257,524,745,788
- NCAA 162,663,179,000 162,663,179,000 73,843,062,100 45 148,000,000,000
- TAWA 58,063,935,590 61,647,180,000 36,910,731,830.25 60 63,839,672,808
Jumla 584,626,710,590 478,014,580,522 250,985,216,073.86 53 469,364,418,596
JUMLA KUU 803,173,312,682 689,345,854,249 397,428,671,967.86 58 670,856,583,921
Jedwali Na. 2: Idadi ya Watalii Waliotembelea Hifadhi za Taifa na
Mapato kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022
Na. Mwaka Watalii Mapato (Shilingi)
Nje Ndani Jumla
- 2017/2018 670,144 409,119 1,079,263 254,794,242,000
- 2018/2019 743,248 494,254 1,237,502 282,426,174,846
- 2019/2020 658,250 394,693 1,052,943 252,194,833,476
- 2020/2021 153,389 358,500 511,889 56,979,796,789
- 2021/2022* 347,040 511,860 858,900 140,231,422,143.61
Jumla 2,572,071 2,168,426 4,740,497 986,626,469,254.61
- Hadi Aprili, 2022
Jedwali Na. 3: Idadi ya Watalii Waliotembelea Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro na Mapato kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022
Na. Mwaka wa Fedha Watalii wa Nje Watalii wa Ndani Jumla ya Watalii Mapato
- 2017/2018 372,732 271,423 644,155 128,973,748,000
- 2018/2019 430,616 270,094 700,710 143,949,144,000
- 2019/2020 412,244 294,807 707,051 123,858,764,000
- 2020/2021 72,632 118,982 191,614 31,426,077,258
- 2021/2022* 184,767 162,561 347,328 73,843,062,100
Jumla 1,472,991 1,117,867 2,590,858 502,050,795,358
- Hadi Aprili, 2022

Jedwali Na. 4: Mwenendo wa Uwindaji wa Kitalii na Mapato Kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022
Na. Mwaka Idadi ya Watalii Mapato
Wawindaji Watazamaji (Observers) Jumla
- 2017/2018 473 291 764 29,870,663,155
- 2018/2019 444 360 804 25,771,163,424
- 2019/2020 484 483 967 22,384,414,381
- 2020/2021 355 255 610 24,945,979,320
- 2021/2022* 494 381 875 23,657,308,675.09
Jumla 2,250 1,770 4,020 126,629,528,955.09
- Hadi Aprili, 2022 Jedwali Na. 5: Mwenendo wa Upandaji Miti katika Mashamba ya Miti
Kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022
Jina la
Shamba Ukubwa
wa msitu 2017/
2018 2018/ 2019 2019/2 020 2020/2 021 2021/2 022 Jumla
- Buhindi 21,880 771 846 357 495 504 2,973
- Kawetire 5,182 263 145 47 62 78 595
- Kiwira 2,820 104 162 99 87 136 588
- Korogwe 10,276 64 215 129 108 0 516
- Longuza 7,067 48 117 168 133 223 689
- Mbizi 23,824 410 322 311 209 123 1,375
- Meru 8,195 291 553 357 180 258 1,639
- Mtibwa 16,109 653 306 125 97 166.5 1,348
- North
Kilimanjaro 8,069 260 190 249 155 201 1,055 - Rondo 31,930 196 209 126 154 207 892
- Rubare 2,979 458 438 309 36 1,241
- Rubya 6,374 209 304 234 72 76 895
- North Ruvu 1,926 81 110 100 170 42 503
- Sao Hill 135,903 2,758 2,525 2,616 2,793 2,761 13,453
- Shume 4,863 169 120 144 174 161 768
- Ukaguru 3,127 270 434 303 230 210 1,447
- West
Kilimanjaro 7,632 223 256 239 160 144 1,022 - Wino 39,400 883 453 420 428 509 2,693
- Morogoro 12,950 50 161 283 263 220 977
- Silayo 69,756 446 523 888 825 1200 3,882
- Mpepo 20,905 200 500 500 500 0 1,700
- Iyondo Msimwa 2,935 220 120 200 175 101 816
- Buhigwe 1,383 70 206 143 130 126 675
- Makere
Kusini 65,178 N/A N/A N/A 173 334 507
Jumla (ha) 510,663 9,097 9,215 8,347 7,773 7,817 42,249*
- Hadi Aprili, 2022
Jedwali Na. 6: Mauzo ya Asali na Nta Nje ya Nchi kuanzia mwaka wa
fedha 2017/2018 hadi mwaka 2021/2022
Na. Mwaka Asali Nta
Tani Thamani Tani Thamani
- 2017/2018 806 8,062,842,500 338 6,598,782,597
- 2018/2019 608 4,860,834,400 179 1,437,865,600
- 2019/2020 2,032 13,413,721,200 251 3,865,400,000
- 2020/2021 1,988 19,878,220,000 393 6,489,999,500
- 2021/2022
- 1,201.98 12,019,766,000 747.56 14,951,148,000
Jumla 6,635.98 58,235,384,100 1,908.56 33,343,195,697 - Hadi Aprili, 2022
Jedwali Na. 7: Mwenendo wa Biashara ya Utalii kuanzia mwaka 2017 hadi 2021
Mwaka 2017 2018 2019 2020 2021
Idadi ya watalii wa kimataifa 1,327,143 1,505,702 1,527,230 620,867 922,692
Watalii wa Hotelini 1,163,752 1,404,672 1,353,279 563,779 848,936
Mapato (US $ million) 2,258.96 2,595.59 2,604.46 714.5 1,310.34
Wastani wa siku za Mtalii kukaa nchini 10 10 13 10 10
Wastani wa matumizi ya fedha kwa mtalii kwa siku (US $) Package Tour 410 331 379 312 364
Non-
Package
Tour 139 135 216 115 141
Jedwali Na. 8: Idadi ya Wanafunzi Waliodahiliwa katika Vyuo vya
Wizara kuanzia mwaka 2017/2018 hadi 2021/2022
Chuo Wanyamapori Utalii Misitu na Nyuki
CAWM- PWTI – Likuyu NCT – FITI – BTI – FTI – Jumla
Mweka Pasiansi Seka – Utalii Moshi Tabora Olmotonyi
Mwaka magang
a
2017/2018 551 441 97 228 133 201 672 2,323
2018/2019 600 441 140 556 180 266 803 2,986
2019/2020 846 300 298 550 250 400 825 3,469
2020/2021 929 343 162 1,087 224 408 867 4,020
2021/2022 834 410 204 1,082 286 378 892 4,086
Jumla 3,760 1,935 901 3,503 1,073 1,653 4,059 16,884
Kuu
Jedwali Na. 9: Idadi ya Wageni Waliotembelea Vituo vya Mambo ya Kale na Mapato kuanzia mwaka
2017/2018 hadi 2021/2022
Kituo 2017/2018 2018/2019 2019/2020 2020/2021 2021/2022
(hadi Aprili, 2022)
Wageni Mapato Wageni Mapato Wageni Mapato Wageni Mapato Wageni Mapato
Magofu ya Kaole 10,458 27,242,000 19,724 42,525,000 34,226 70,863,000 21,259 39,857,800 31,101 15,080,000
Zama za Mawe Isimila 1,445 8,167,000 2,634 11,469,000 2,392 10,214,000 6,823 14,866,924.5 7,490 18,972,916
Mji Mkongwe, Bagamoyo 6,798 24,324,000 11,302 32,845,200 18,392 50,793,624 9,573 21,162,000 18,848 6,113,000
Makumbusho ya Mkwaw
- Kalenga a 1,501 2,105,000 2,408 4,601,000 1,655 3,267,300 3,672 5,966,730 4,737
7,173,150
Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara 1,083 10,439,000 2,990 18,738,000 3,740 40,538,000 4,040 27,563,500 4,870 27,742,750
Kimondo cha Mbozi 1,368 3,039,000 3,604 6,596,000 2,705 5,061,440 3,726 11,252,480 1,692 4,211,160
Mapango ya Amboni 21,662 19,377,000 11,086 21,271,000 8,308 17,789,240 8,434 18,692,280 12,494 25,053,760
Magofu ya Tongoni 104 792,000 470 1,098,000 345 984,000 192 373,000 164 186,000
Dkt. Livingstone Ujiji, Kigoma 2,606 6,224,000 3,742 8,547,180 3,198 7,786,000 3,027
6,876,475
3,551
7,793,390
Tembe la Kwihara 361 902,000 407 828,000 506 919,000 392 338,000 365 600,000
Michoro ya Miambani
Kondoa, Kolo 1,766 12,550,000 1,959 16,662,000 2,765 17,543,000 2,316 9,407,000 4,376 7,848,000
Makumbusho ya Caravan Serai, Bagamoyo 1,814 4,246,000 4,283 9,374,000 3,028 6,250,880 2,190
3,478,000
4,254
7,585,000
Nyumba Kumbukizi ya
Mwl. Nyerere –
Magomeni 302 608,000 195 494,000 0** 0** 181
283,000
1,128
1,864,400
Jumla 51,268 120,015,000 64,804 175,048,380 81,260 232,009,484 65,825 160,117,189.5 95,070 130,223,526
**Kituo kilifungwa kwa ajili ya ukarabati mkubwa
Jedwali Na. 10: Idadi ya Wageni Waliotembelea Makumbusho ya Taifa na Mapato Kuanzia
Mwaka 2019/2020 hadi 2021/2022
KITUO
TAKWIMU ZA WAGENI NA MAPATO
2019/2020 2020/2021 2021/2022 (Hadi Aprili, 2022)
Nje Ndani Jumla Mapato Nje Ndani Jumla Mapato Nje Ndani Jumla Mapato
Nyumba ya
Utamanduni
11,391 13,198 24,589 200,914,700 4,011 17,588 21,599 151,187,860 3,657 39,995 43,652 192,587,487
Kijji cha
Makumbusho
2,281 5,115 7,396 74,029,200 497 234,345 234,842 125,218,267 1061 481,254 482,315 148,258,533
Azimio la Arusha
291 4,235 4,526 14,961,400 52 2,395 2,447 8,702,950 123 3,314 3,437 17,666,300
Vita ya
Majimaji
99 3,271 3,370 5,964,500 21 10,083 10,104 7,363,800 21 2,312 2,333 49,541,900
Mwalimu J. K
Nyerere
62 8,809 8,871 11,231,500 15 6,285 6,300 13,633,000 15 5,353 5,368 13,192,000
Elimu Viumbe 1,995 4,173 6,168 49,071,250 379 7,768 8,147 32,137,350 640 4,124 4,764 19,859,500
Dkt. Rashid Kawawa
– – –
– –
- 4 360 364 1,005,500
Mji Mkongwe Mikindani
– – –
–
- 2 943 945 1,107,000
JUMLA 16,119 38,801 54,920 356,172,550 4,975 278,464
283,439 338,243,227 5,523 537,655 543,178 443,218,220
Jedwali Na. 11: Muhtasari wa Bajeti ya Matumizi ya Miradi ya Maendeleo kwa mwaka 2022/2023
Na. Na. ya Mradi Jina la Mradi Fedha zinazoombwa kwa mwaka 2022/2023 (Sh.)
Fedha za Ndani Fedha za Nje Jumla Mhisani
(i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii)
1003 Sera na Mipango
- 5203 Usimamizi wa Maliasili na Kuendeleza Utalii Ukanda wa
Kusini (REGROW) 141,000,000 61,184,930,496 61,325,930,496 WB / GoT - 6251 Five year Medium Term Strategic
Plan for Public Finance Management Reform Programme
(PFMRP) 0 145,750,000 145,750,000 Finland
Jumla Ndogo 141,000,000 61,330,680,496 61,471,680,496
2001 Wanyamapori - 4810 Kujenga Uwezo wa Maeneo ya Hifadhi, Mapori ya Akiba na
Kikosi Dhidi Ujangili 188,000,000 0 188,000,000 GoT - 4812 Kuzuia na Kupambana na Ujangili na Biashara Haramu ya Nyara 0 2,916,531,100 2,916,531,100 UNDP
Jumla Ndogo 188,000,000 2,916,531,100 3,104,531,100
3001 Misitu na Nyuki - 4647 Panda Miti Kibiashara 0 3,360,500,000 3,360,500,000 Finland
- 4648 Kujenga Uwezo wa Taasisi na Mafunzo ya Misitu na Ufugaji Nyuki 141,000,000 0 141,000,000 GoT
- 4651 Kuwezesha Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya Nyuki
(BEVAC) 0 2,948,860,404 2,948,860,404 EU
Na. Na. ya Mradi Jina la Mradi Fedha zinazoombwa kwa mwaka 2022/2023 (Sh.)
Fedha za Ndani Fedha za Nje Jumla Mhisani
Jumla Ndogo 141,000,000 6,309,360,404 6,450,360,404
4001 Utalii - 4816 Uendelezaji wa Utalii wa
Mikutano na Matukio (MICE) 658,000,000 0 658,000,000 GoT
Jumla Ndogo 658,000,000 0 658,000,000
Taasisi za Wizara - 4813 Miradi ya TANAPA 60,646,469,000 0 60,646,469,000 GoT
- 4814 Miradi ya NCAA 29,340,231,000 0 29,340,231,000 GoT
- 4817 Miradi ya TAWA 15,944,893,000 0 15,944,893,000 GoT
- NCT 2,820,000,000 0 2,820,000,000 GoT
Jumla Ndogo 108,751,593,000 0 108,751,593,000
JUMLA KUU 109,879,593,000 70,556,572,000
Jedwali Na. 12: Namba za Simu za kutoa Taarifa kuhusu Wanyamapori Wakali na Waharibifu
Na. TAASISI/KANDA FREE TOLL NUMBER NAMBA YA TTCL
- Wizara – Dodoma 0800110076 0734986511
- Ngorongoro 0800110087 0734986512
- TAWA – Manyoni 0800110089 0734986513
- TAWA – Iringa 0800110090 0734986514
- TAWA – Morogoro 0800110093 0734986515
- TAWA – Dar es Salaam 0800110098 0734986516
- TANAPA – Mikumi 0800110099 0734986517
- TANAPA – Mbarali 0800110068 0734986518
- TAWA – Masasi 0800110067 0734986519
- TANAPA – Bunda 0800110059 0734986520
- TAWA – Tunduru 0800110054 0734986521
- TAWA – Tabora 0800110048 0734986522
- TANAPA – Mkomazi 0800110046 0734986523
- TAWA – Arusha 0800110027 0734986524
Jedwali Na. 13: Muhtasari wa Bajeti ya Wizara kwa mwaka 2022/2023
Na. Bajeti Kiasi (Shilingi)
I Matumizi ya Kawaida
Mishahara 175,884,707,000
Matumizi Mengineyo (O.C) 267,821,860,000
Jumla Ndogo 443,706,567,000
II Miradi ya Maendeleo
Fedha za Ndani 109,879,593,000
Fedha za Nje 70,556,572,000
Jumla Ndogo 180,436,165,000
JUMLA FUNGU 69 (I +II) 624,142,732,000
