BASHUNGWA: TOENI ELIMU KWA JAMII UTUNZAJI WA MAZINGIRA NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Angela Msimbira OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amewaagiza maafisa mazingira hao nchini kuelimisha wananchi kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Ametoa maagizo hayo leo 3 Juni, 2022 jijini Dodoma wakati akizungumza na maafisa mazingira wa Mikoa, Wilaya na Halmashauri zote nchini uliokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na kukumbushana kuhusu suala la utunzaji mazingira na namna ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Waziri Bashungwa amesema jamii haiwezi kuwa bora kama wataharibu mazingira hivyo ni muhimu wakahakikisha wananchi wanapata elimu juu ya utunzaji,uhifadhi na kuendeleza mazingira nchini.

Amesema ni wajibu wa maafisa mazingira nchini kuhakikisha wanapeleka uelewa kwa wananchi ili waweze kujua umuhimu utunzaji mazingira na si jukumu laSerikali pekee hivyo wajiwekee mikakati endelevu itakayoendana na maendeleo na uchumi wa nchi, ili liwe jambo la watanzania.

“Nchi yetu inakabiliwa na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababishwa na shughuli za kibinadamu , zisizozingatia uhifadhi wa mazingira, hivyo ni wajibu wa maafisa Mazingira kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii kuhusu uhifadhi na utunzaji wa mazingira” amesema Bashungwa

Amefafanua kuwa Serikaliimechukua hatua mbalimbali kwa lengo lakukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo kuandaa sera mpya ya Taifa ya mazingira ya mwaka 2021 ambayo ilizinduliwa Februari,2022 inayotoa muongozo wa kusimamia masuala ya mazingira nchini.

WaziriBashungwa amesema kwa sasa Serikali inaangalia namna mabadiliko ya tabia nchi yanavyoathiri mazingira na uhitaji wa jamii ili kuangalia suala la maendeleo ya nchi yanaendane na mazingira.

“Sio jambo jepesi, ni suala ambalo ni lazima ukae utulize kichwa kwa sababu linahitaji miji kukua, kujenga uchumi wa viwanda, kuongeza tija kwenye kilimo lakini imputs ambazo tunahitaji kuweka tija ambapo vyote hivi vinapaswa kwenda sambamba na suala la utunzaji mazingira,”amesema Bashungwa.

Bashungwa ameshauri kuwepo na mpango wa kuwajengea uwezo wataalam hao ili wanapojifunza wakafundishe na wengine kwa sababu mabadiliko ya tabia nchi yanabadilika hivyo waendele kujifunza kutoka kwenye maeneo mengine dunia ili waweze kuendana na kasi ya mabadiliko.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Muungano na Mazingira Mary Maganga alisema lengo la warsha hiyo ni kukumbushana majukmu na wajibu kwa upande wa usimamizi na utekelezaji wa masuala ya mazingira kwa ujumla.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *