Fahamu mbinu bora za ukaushaji wa zao la Pilipili Kichaa


Unaweza kutumia njia hizi zinazo pendekezwa.
1. Ukaushaji wa kutumia Jua (Kaushio hili hujengwa mfano wa kichanja cha chekecheke chenye matundu madogo yatakayoruhusu mzunguko wa hewa)

2. Ukaushaji wa kutumia makaushio ya Sola, Gesi au Umeme. Makaushio haya hutengezwa kwa utaalamu unaoleta joto la wastani ndani ya kaushio.

Faida za kufuata mbinu bora za ukaushaji wa pililili:

1. Kupunguza uwezekano pilipili kuharibika (rejects).
2. Kuongeza ubora wa pilipili baada ya kuvuna mfano kubakiza rangi halisi ya pilipili.
3. Kuhifadhi virutubisho vya zao husika (hii ni kutokana na kukaushwa kwa njia bora).
4. Kutunza uzito halisi wa zao (moisture content).
5.Kuongeza uwezo wa kutunzika katika maghala.