DC LUDEWA ATOA ONYO KWA WATAKAOVURUGA ZOEZI LA SENSA

Mkuu wa wilaya ya Ludewa Andrea Tsere ametoa onyo kwa mtu yeyote atakayeonekana kuvuruga zoezi la Sensa ya watu na makazi kwa namna yeyote ile ikiwemo kutoa taarifa za uongo, kutokuwepo eneo la makazi yake na kusababisha usumbufu kwa karani wa sensa kuwa atamchukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria ya nchi ikiwemo kulipia faini kiasi cha fedha kisichopungua Ml. 1, jela miezi sita au vyote kwa pamoja.

Kauli hiyo ameitoa katika mikutano ya kutoa elimu juu ya zoezi hilo la Sensa ya watu na makazi iliyofanyika katika kata ya Luilo, Luhuhu pamoja na kata ya Manda huku Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo Isaac Ayengo akisema adhabu hizo zipo kwa mujibu wa sheria kifungu namba 43(3) ambacho kinaeleza makosa ambayo raia hapaswi kuyafanya .

Katika kueneza elimu hiyo kamati ya Sensa ya Wilaya ya Ludewa imejigawa katika makundi matatu na kusambaa katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ambapo kundi la kwanza linaongozwa na mkuu wa Wilaya ya Ludewa Andrea Tsere, la pili likiongizwa na Mkurugenzi wa Halmashauri Sunday Deogratias huku la tatu likiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Wise Mgina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *