TAIFA STARS KUIVAA NIGER BILA KAPOMBE

Fabian Patrick Simbagone

Wakati maandalizi ya michuano ya kufuzu kombe la mataifa Africa (AFCON) yanaendelea kushika kasi. Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kukiwa kambini kujiandaa na mchezo wao wa kundi F dhidi ya Niger utakaochezwa juni 4 nchini Benini majira ya saa moja za usiku kwa masaa ya hapa kwetu Tanzania.

Taarifa Kutoka kambini zinaripoti kuwa beki wa wa Pembeni wa klabu ya simba sc na timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ Shomari Kapombe ameondolewa Kwenye Kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kinachojiandaa kucheza mchezo wa kufuzu AFCON

Kapombe ameondolewa Kwenye Kikosi cha timu ya Taifa kwa sababu ya kusumbuliwa na majeraha aliyoyapata Kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Geita Gold na nafasi yake imechukuliwa na Lusajo Mwaikenda wa Klabu ya Azam FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *