RASMI: YANGA WAMSAMEHE AMBUNDO

Na, Fabian Patrick Simbagone

Wakati wapo Kwenye maandalizi ya kuzisaka alama 3 ili watangazwe mabingwa rasmi wa NBC PL, huku wakiwa na matumani ya kuzivuna pointi hizo mbele ya wagosi wa kaya Coastal Union mnamo Juni 15/2022 watakapomenya Kwenye dimba la Benjamin Mkapa, Hatimaye wamefikia maamzi mazuri kwa nyota wao Dickson Ambundo.

Nyota huyo alisimamishwa kabla ya mechi ya nusu fainali ya kombe la Azam sport Federation Cup (FA CUP) kati ya Yanga dhidi ya Simba, kwa kosa la kutoka kambini bila ruhusa Kutoka kwa kiongozi yeyote, Hatimaye uongozi wa Klabu ya Yanga umeamua kumsamehe Dickson Ambundo na kumpa onyo kali ya kutokurudia makosa ya utovu wa nidhamu.

Hivyo Ambundo anatarajia kurejea kambini Hivi karibuni kuungana na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi inayofuata ya ligi kuu Tanzania Bara watakayomenyana dhidi ya Coastal Union.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *