Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi na wadau mbalimbali wa michezo katika hafla ya kupokea Kombe la Dunia (World Cup) litakaloshindaniwa katika Mashindano ya Mpira wa miguu nchini Qatar, iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Kombe la Dunia kutoka kwa Balozi wa Kombe hilo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano BellettiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa na Balozi wa Kombe la Dunia kutoka (FIFA) mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano Belletti katika picha ya pamoja na wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan, akipokea zawadi yenye mfano wa Kombe dogo la Dunia kutoka kwa Balozi wa Kombe hilo kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Brazil Juliano BellettiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akinyanyua juu Kombe la Dunia (World Cup) litakalo shindaniwa katika Mashindano ya Mpira wa miguu yatakayo fanyika nchini Qatar katika hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.Wadau mbalimbali wa Michezo pamoja na Viongozi wakiwa kwenye hafla ya mapokezi ya Kombe la Dunia Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 31 Mei, 2022.