WATANZANIA MUOMBEENI RAIS WENU- VIONGOZI WA DINI

Viongozi wa madhehebu mbalimbali ya Dini nchini wamewahasa Watanzania wote kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ili aendelee kuliongoza vyema Taifa la Tanzania ili aweze kudumisha Amani.

Viongozi hao wa Dini wamesema hayo leo Mei 30, 2022 kwenye mkutano wao na waandishi wa habari uliofanyika Mkoani Mbeya ikiwa ni kuelekea kwenye Kongamano la Kuliombea Taifa, Kumuombea Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan pamoja kumpongeza kwa uongozi bora litakalofanyika kesho Mei 31, 2022 katika Ukumbi wa Tughimbe mkoani humo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *