KAMATI KUZUIA UHALIFU BAHARINI YAKUTANA DODOMA

Kamati ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilina na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na  Maziwa Makuu imekutana na kufanya kikao  cha dharura kwa lengo la kujadili mkataba wa ununuzi wa boti ya doria litakalosaidia kukabiliana na vitendo hivyo nchini.

Kikao hicho kimesimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu katika ukumbi wa ofisi hiyo  Mei 30, 2022 jijini Dodoma  kikihusisha Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali na wadau wa maendeleo.

Miongoni wa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na  Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdallah Kirungu, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo Bw. Sergio Valdini na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania Bw. Tabuchi Tomoyoshi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *