DTB FC YABADILISHWA JINA KUWA SINGIDA BIG STARS

Na, Fabian Patrick Simbagone

Katika muendelezo wa kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao, timu ya DTB FC iliyopanda daraja msimu huu kwa kushika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Championship ikivuna alama 66 sawa na Ihefu tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ndio ikaamua bingwa wa Championship.

Timu hiyo leo 30/5/2022 imethibitisha kubadili jina lake kutoka kuitwa DTB FC yani DIAMOND TRUST BANK na kuitwa SINGIDA BIG STARS, jina hilo ndio jina litakalotumika katika ligi kuu Tanzania Bara kuanzia msimu ujao pamoja na mashindano mengine yakiwemo Azam Sport Federation Cup (ASFC).

DTB zamani ambayo kwa sasa ni Singida Big Stars FC imehamia mkoani Singida na itakuwa inatumia uwanja wa Iliti ambao zamani ulikuwa unaitwa (Namfua) kama uwanja wake wa nyumbani, pia uwanja huo ulikuwa unatumiwa na Singida United FC.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *