BASHUNGWA AAGIZA KUFANYA MAPITIO BEI YA KODI YA PANGO STENDI YA MAGUFULI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Innocent Bashungwa ametoa siku kumi na nne kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ubungo, Kamati ya fedha na uongozi wa kituo cha Mabasi cha Magufuli kufanya mapitio na kupeleka mapendekezo ya changamoto ya Wapangaji katika kituo hicho ya kulalamikia kiwango kikubwa cha kodi ya pango ambapo wameeleza kwa sasa kiwango cha pango ni shilingi 40,000 kwa mita moja ya mraba.

Bashungwa ametoa maelekezo hayo leo mei 30, 2022 wakati akikagua mradi wa Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli “Magufuli Bus Terminal” kilichopo wilaya ya Ubungo mkoani Dar es salaam.

Pia ameagiza Mkurugenzi huyo kuondolewa kwa Magari yote mabovu yaliyoegeshwa kwa muda mrefu ndani ya kituo hicho ambayo ni zaidi ya 40 yanayosababisha ufinyu wa eneo ili kutoa nafasi kwa magari mengine kupata maegesho ndani ya kituo.

Mwisho ameelekeza Uongozi wa Wilaya hiyo kuendelea kusimamia mpango uliopo kwenye ramani ya kituo hicho kwa kuweka kipaumbele cha kuboresha na kujenga miundombinu ya wafanyabiashara wadogo ili stendi hiyo iwe na manufaa kwa wanaanchi kulingana na Maelekezo ya Mheshimiwa Rais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *