MBUNGE LUDEWA, ATINGA MRADI WA CHUO CHA VETA

Mbunge wa jimbo la Ludewa, Joseph Kamonga ametembelea mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa katika kata ya Lugarawa Wilayani Ludewa Mkoani Njombe kitakacho gharimu kiasi cha zaidi ya Sh. Bilion 5.

Akiwa katika mradi huo Kamonga Amesema wananchi wa Ludewa na mkoa wa Njombe kwa ujumla wanauhitaji mkubwa wa chuo hicho na ndiomaana akakisemea bungeni ili aweze kupata fedha za kuendeleza ujenzi huo.

“Chuo hiki kilianzishwa kujengwa mwaka 2005, lakini hakikuendelea na kikaishia kuchimbwa msingi hivyo wananchi walivyonipa dhamana ya kuwaongoza nikaone nianze na vipaumbele vyao ikiwemo Chuo hiki cha Veta”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *