
NAIBU Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais, Abdallah Hassan Mitawi, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Andrew Komba leo Mei 27, 2022 wamefanya ukaguzi katika mabwawa ya Majitaka ya Mamlaka ya Majisafi na usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA) yaliyopo Chuo cha Dodoma na Hospitali ya Benjamini Mkapa ikiwa maandalizi ya Wiki ya Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.

Viongozi hao waliambatana na Mkuu wa Kitengo cha Mazingira DUWASA, Daniel Mgunda na baadhi ya watendaji wa Hospital ya Benjamini Mkapa ambapo Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu anatarajia kutembelea eneo la mifumo wa kuchakata Majitaka katika hospitali ya Benjamini Mkapa Jumapili Mei 29.
