SIMBACHAWENE AONGOZA KIKAO CHA MAWAZIRI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe.George Simbachawene (katikati) akiongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi  (wa kwanza kushoto) ni  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye na mwisho ni Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene ameongoza kikao cha Mawaziri kwa lengo la kujadili taarifa ya Utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za makazi.

Kikao hicho kimefanyika Mei 27, 2022 katika Ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dodoma ambapo kilihudhuriwa na mawaziri wakiwemo  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Nchi Ofisi wa Makamu wa Pili wa Rais, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Hamza Hassan Juma na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula.

Kikao hicho kimefanyika kama sehemu ya maandalizi ya zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti  2022 nchini  ambapo itakuwa Sensa ya Sita tangu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964 na  sensa ya watu na makzi hufanyika  kila baada ya miaka 10.

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.Dkt. Angelina Mabula akichangia hoja wakati wa kikao cha mawaziri cha  kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Innocent Bashungwa akifafanua jambo wakati wa kikao hicho.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye akieleza jambo katika kikao cha mawaziri cha  kujadili taarifa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mawasiliano  Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi. Clarence Ichwekeleza akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi katika kikao cha Mawaziri kilichofanyika  Mei 27, 2022 Ofisi ya Waziri Mkuu  Jijini Dodoma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *