PABLO YANGA NI BORA, NABI TUTASHINDA KWA NIDHAMU YETU, KAPOMBE TUNAITAKA FAINALI

Fabian Patrick Simbagone

Kuelekea katika mchezo wa nusu fainali ya Azam Sport Federatim Cup kati ya timu ya soka ya Yanga SC dhidi ya Simba SC ambayo itapigwa hapo kesho katika uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza, kikosi cha Yanga kipo kambini mkoani Shinyanga na leo kimefanya mazoezi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo, huku kikosi cha Simba sc kikiwa kambini jijini Mwanza na wao wamefanya mazoezi ya mwisho katika dimba la Nyamagana.

Leo mchana makocha wa timu zote mbili pamoja na baadhi ya wachezaji wameongelea maandalizi ya timu zao yalivyo hadi sasa kuelekea kwenye derby ya kesho.

Kocho wa Yanga sc Nasreddine Nabi amesema wamekuwa na maandalizi mazuri pia amekuwa akiwambia wachezaji wake kujituma kuanza kwenye mazoezi hadi kwenye mechi.

“Tunaendelea na maandalizi kitu muhimu nimewambia wachezaji ni kujituma kuanzia kwenye maandalizi mpaka kwenye mechi, tumekuwa tukishinda kwa nidhamu yetu kama timu”

“Tunajua mchezo utakuwa mgumu na tunawaheshimu SimbaSC na tutaingia kwa tahadhari katika mchezo wa kesho”

Kwa upande wa Pablo Franco ambae ni kocha mkuu wa Simba SC amesema kuwa lengo lao ni kutwaa kombe la ASFC kwani ndio kombe walilobaki wakishindania

“Mashindano haya ndio tunategemea kupata taji, tunatarajia kupata upinzani mkubwa na mechi itakuwa ngumu lakini tupo tayari kwa mapambano”

“Tupo kwenye hatua ya nusu fainali ni mchezo wa derby lazima uwe wa msisimko lakini tupo tayari kwa mapambano”. Pablo ameongeza kwa kukiri kuwa wapinzani wao ni bora. “Yanga wataingia kwenye mchezo wa kesho wakiwa na kiwango bora zaidi yetu lakini tunahitaji sana kupata ushindi katika mchezo wa kesho”.

Beki wa pembeni wa simba Shomari Kapombe amesema mchezo wa kesho dhidi ya yanga ni tegemeo pekee walilobaki nalo la kuhakikisha wanatwaa kombe muhimu msimu huu “ni mchezo pekee ambao sisi tunauangalia kwa macho mawili”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *